Benki ipi nzuri kukopa kati ya Absa, NBC, NMB, na CRDB?

mwanyaluke

JF-Expert Member
Jan 22, 2015
473
1,448
ipo hivi mimi ni mwalimu, mfanyabishara na mkulima , mimi ni mkopaji mzuri sana , nilikuwa na mkopo kupitia salary nilikopa 2019 NMB, nimekuwa na mkopo wa biashara nimekopa CRDB, kwa sasa nimemaliza deni nadaiwa na bodi tu ya mikopo, nina uhitaji tena wa pesa kama milioni mia moja tu.

Nipeni ipi bank nzuri nikope. Ushauri wako uandane na uhalisia na vigezo.
 
Sasa mwalimi si uende kwenye hizo benki husika ili ukapate ABC!!

Na kama ni mkopo wa biashara, ni lazima uwe umekopa na kurejesha kwa muda mrefu + mzunguko mkubwa wa biashara, ndiyo utakuwa na uhakika wa kupata mkopo mkubwa.

Mkopo wa wafanyakazi, ni lazima uwe na mshahara mkubwa kazini. Hivyo vigezo unavyo?
 
Najaribu kupiga mahesabu:-
Maximum- miaka 8
8 x 12 x 1,500,000 (rejeshio kwa mwezi)=144,000,000/=
Sidhani kama mshahara wako unaruhusu kukatwa milioni 1.5 kwa mwezi?

Kama unataka utumie biashara kukopea, inawezekana muhimu hiyo biashara iwe na akaunti yake kwa jina la biashara, na iwe na mtiririko mzuri wa pesa kuingia na kutoka, pia uwapelekee mpango biashara waweze kuutathmini.
Ndivyo viwanda vya pamba ukopa mabilioni kwa njia hiyo.
Bank nzuri kwa mazingira hayo ni CRDB.​
 
Sasa mwalimi si uende kwenye hizo benki husika ili ukapate ABC!!

Na kama ni mkopo wa biashara, ni lazima uwe umekopa na kurejesha kwa muda mrefu + mzunguko mkubwa wa biashara, ndiyo utakuwa na uhakika wa kupata mkopo mkubwa.

Mkopo wa wafanyakazi, ni lazima uwe na mshahara mkubwa kazini. Hivyo vigezo unavyo?
ni mteja wa CRDB kitambo nawaza kuwabadili
 
Mkuu si unakuta ana vyanzo vingine.kusomea fani fulani sio kuwa ndio kipimo chako Cha hela ama utajiri wako wa hapo baadaye. Doto biteko,majaliwa pm,jpm,Samia, NYERERE,marwa ryoba mp Serengeti,mwita weitara mp Tarime wote hao walikuwa Ni walimu. Ukiwa mdogo unajua ukiwa daktari ama, Engineer,lawyer ndio hela nyingi utapata. Mafanikio huja pale unapokuwa na uwezo wa kuupanda shilingi ikazaa shilingi ama hata Senti moja ama thumuni ndicho nilichokiona mpaka umri huu.
Kuna walimu wangapi wanamiliki biashara kubwa hapa mjini. Yaani salary Ni mbegu unayopewa utajua alone uile uipande ama uhonge Bata Ni wewe Ila sio kuwa salary ndio uwezo wa mtu wa kipesa. Kama ana biashara anazomiliki around turnover ya 400M kwa mwaka je, Kuna watu wanakifanya kitu Kama passion na sio kujipatia salary.
Pia wanajiongeza ama Kuna biashara za familia wanasimamia.akadai mwenyewe kuwa Ni mkulima mfanyabiashara na mwalimu yaani pia na mfugaji unadhani utalingana Naye unategemea single income ya 3M kwa mwezi ingawa yeye salary yake Ni 500k-1.2M.

Ila watu sema Ni asili ya brain tuliyopewa na mother nature
 
Sina uelewa sana ila nilisikia fomula wanayotumia crdb na nmb katika kucalculate deni inautofauti,crdb hua wanacalculate deni na kuweka interest kwa kutumia kiwango ulichokopea hata kama umeanza kulipa ila nmb hutumia kiwango ambacho bado unadaiwa endapo utakua umeanza kulipa.
 
Back
Top Bottom