Ubabaishaji wa Benki ya NBC kwenye kutoa mikopo

senkoP

Senior Member
Aug 28, 2017
161
174
Bank ya NBC ni wababaishaji sana kuhusu utoaji wa mikopo. Sijui tatizo ni nini? Mtu anaomba mkopo taratibu zote zimesha kamilika mpaka makato tayari lakini hawaingizi mkopo. Kuna jamaa ameomba mkopo NBC yapata mwezi sasa umekwisha mkopo hawaingizi na anakatwa.

Amefatilia kwa Afisa Mikopo kamwambia yeye kashamaliza sehemu yake bado sehemu sijui ya mtu gani uko anayehusika kuapprove.

Kwakweli hii bank ni tatizo huduma zake haziriziki sishauri mtu hata siku moja kama ana uhitaji wa fedha kwa dharura aende NBC hakika utakwamishwa bila hata sababu za msingi. Kama kuna mdau anajua tatizo la kucheleweshewa mkopo atuambie.
 
Mbona wako poa na wanaunafuu, jana wamenipa m30 kwa kutumia watumishi portal fasta tu! We taja tawi husika liliokuzingua sio General Nbc! Benki yetu ya Taifa hii usiogope, Mbona Chongolo kamwaachia uwanja Bashite kiroho safi tu!
 
Kwanini niende kwa hawa mnaowaita wanyanyaji na si huko?

1. Benki nyingi zina uzee mwingi.
Mimi mtumishi wa umma na dhamana yangu ni mshahara pamoja na bosi wangu sasa kwanini mutake vielelezo vingi kana kwamba najaza form ustawi wa jamii kuomba msaada?

2. Hizi benki au microfinance kama Banc ABC au Finca wako chap na wadanyakazi/madalali wao wako anxious sana , very charming.

Lakini nenda NMB kaombe mkopo utaona unavyodharaulika. Toa salary slip yako isome singe digit , namaanisha mshahara chini ya Million Moja utaona wanavyoishika.
Mimi siangalii nakatwa sh. Ngapi , naangalia nahitaji sh. ngapi kwa kazi ipi .
Kwisha
 
Mbona wako poa na wanaunafuu, jana wamenipa m30 kwa kutumia watumishi portal fasta tu! We taja tawi husika liliokuzingua sio General Nbc! Benki yetu ya Taifa hii usiogope, Mbona Chongolo kamwaachia uwanja Bashite kiroho safi tu!
Cha kushangaza hata ukipiga simu huko General Bank unakosema hakuna msaada wowote.....ni tatizo..hata customer care yao very hovyo

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom