TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.
Watu wamekosa hekima kisa siasa..inasikitisha sana kushindwa kutofautisha siasa na maisha ya kawaida ya kinaadamu.
Ni vizuri sana kuwa na busara ya kuacha kutumia vifo vya watu wengine kwa malengo ya kijenga hoja za kisiasa bila uthibitisho wake. Wote tunatembea na vifo vyetu viganjani mwetu. Tusubiri facts kwanza halafu ndipo tuzichambue
"Amevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo ameumaliza, BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe na Apumzike kwa amani"
 
Usifanaize Mungu na binaadamu dhaifu anakwenda chooni
Shida ipo maana unadhani basi wema ukitendwa kwa watu hawatakuwepo wa kukusema vibaya.

Ilihali unajua fika hata Mungu ainyeshapo mvua kuna mama mjamzito anatembea kwenda hospitalini pasipokuwa na mwamvuli.

Salaam.
 
Shida ipo maana unadhani basi wema ukitendwa kwa watu hawatakuwepo wa kukusema vibaya.

Ilihali unajua fika hata Mungu ainyeshapo mvua kuna mama mjamzito anatembea kwenda hospitalini pasipokuwa na mwamvuli.

Salaam.

Hoja yako ni nini hapa, hebu tuanzie hapo ili nijue mwelekeo.
 
Binafsi pamoja na mazuri mengine mengi aliyoyafanya nitamkumbuka zaidi katika utawala wake alivyodhiditi mfumoko wa bei. Bidhaa mbalimbali katika utawala wake hazikupanda hata kidogo na hata baadhi kushuka bei. Thamani ya fedha ilionekana.
Pumzika kwa amani mzee wetu.

Ana mazuri mengi kwa kweli. Apumzike kwa amani.
 
Benjamin Wiliam Mkapa nakuombea heri njema uendapo katika Safari yako ya Uvuli upate heri, raha na upumzike kwa Amani katika ardhi nzuri. Poleni sana Familia, Pole Tanzania.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom