TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.
Apumzike kwa Amani.
Michango ya Watz wengi humu JF inaonyesha wengi kutoguswa na Msiba huu Mkubwa wa Kitaifa kama ilivyokuwa mingine. Nakumbuka majuzi tu tulipopata ule wa Mh Mahiga wengi waliguswa sana.
Kwanini kwa Mzee wetu huyu ushabiki umekuwa mwingi??
Kuna jambo la kufikirisha hapa hasa kwetu sisi tulio hai juu ya matendo yetu na namna tunavyoishi.

Kwa upande wa wale wenye nafasi za Uongozi basi nao watambue kuwa hata uwe na mamlaka kiasi gani hata uwe na kiburi kiasi gani hata uwe na ulinzi wa namna gani haitokusaidia kukuwekea kinga ya KIFO kwenye maisha yako.
Mwenye mamlaka na nguvu ya kweli kwenye maisha yetu ya hapa Duniani ni Mungu pekee.

Kifo ni fumbo hakuna ajuae kisho yake.
 
Meseji ya kwanza mtandaoni ya msiba. Pumzika kwa amani ya Yesu mh Mkapa. Kuishi ni Kristo kufa ni faida.
 
Huzuni Kwa taifa na familia yake.Mungu awatie nguvu Wanafamilia wote Apumzike Kwa amani mzee wetu.
 
Raha ya milele umpe eeh bwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom