Benjamin William Mkapa nimjuaye...

Amini usiamini Mkapa alikuwa ni mtu sahihi kabisa kuchukua nchi ile ktk wakati sahihi na kwa mda muafaka.

Nakumbuka sana enzi hizo kabla ya Mkapa amini usiamini mishahara wafanyakazi ilikuwa miezi mitatu ama zaidi ndio unapata ,ndicho kipindi serikali ilistop kufundisha waalimu na kuajili walimu angalia hii BOGUS asingetokea Mkapa .

mimi nafikiri ni ujuha tu kwamba mtu kama Mkapa lazima angetenda mema tuu mwanzo hadi mwisho ,binadamu yeyote anatamani,ana mapungufu ila nafikiri kinachotakiwa kufanyika ni kuangalia Binadamu huyo ana nia gani juu ya binadamu wezake.

Tumesimuliwa ktk hadithi,ijili nk mfano Musa ,Abrahamu ,Daudi ,Samsoniwalivyokuwa wanaongea na Mungu moja kwa moja na kutumwa kuchunga kondoo lakini pamoja na sauti hiyo ya Mungu kuna wakati walikuwa wanawatelekeza kondoo na kufanya mambo yao,ije kwa poor Mkapa??
 
Hatukatai kwamba Mkapa alifanya mambo fulani mazuri wakati akiwa madarakani. Lakini uzuri wote aliuharibu kwa kuinajisi IKULU kwa kufanya biashara yeye na mkewe na kutumia madaraka yake vibaya kujiuzia Kiwira. Kuna kashfa nyingi za ufisadi katika utawala wake ambazo zinamhusisha moja kwa moja. Kama alivyosema yule Mbunge Mpendazoe, huyu ni wa kushitakiwa, na wale wote wanaomtetea kama vile akina Pinda waende wakamtetee huko. Nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria.
 
Benjamin William Mkapa alivyochaguliwa kuwa rais mtoto wake mwenyewe wa kumzaa ambaye alimjua kuliko sisi alisema "Watanzania ndio mmemchagua huyu kuwa rais? Mmekwisha".

Nilikuwa na reservations kuhusu Mkapa, lakini pia nilifikiri huyu kijana alikuwa anazidisha chumvi.

Baada ya baba yake kumaliza utawala wake sasa nimeelewa zaidi maana ya maneno ya huyu kijana.

Mkapa is an arrogant policy wonk who thought he could get away with anything because nobody was smarter than him, especially after Nyerere's death.
 
Nyie vipi?

Hivi nani kasema Kikwete hapa? Hapa tunamjadili Mkapa. Kubadilisha mada na kuanza kusema Kikwete ni UPUUZI WA HALI YA JUU. Si umeona kabisa kichwa cha habari ni Mkapa, sasa wamleta Kikwete wa nini hapa?

Tukija kwa Kikwete nitasema kwa ufupi " Mungu airehemu Tanzania..." Kama Watz walipotea katika kuchagua basi sasa tumerudia tena makosa ya kumuweka Mwinyi madarakani. Kikwete issue hata huwezi kuzijadili. Mtu aliyeingizwa kwa hela za EPA, DEEPGREEN, MAPANKI, nk unategemea nini? Mtu anayechaguliwa viongozi wake na Rostam Aziz? Ila faida moja ya Kikwete ni kuwa HUWA ANACHEKA SAAANA.

Mkapa tulikuwa na imani naye sana. Alilipwa na analipwa hadi leo na bado kaja kuiba hadi inatia kinyaa. Huwezi kuiba hadi unaleta RAHA ndani ya moyo.

Mkapa lazima apande KIZIMBANI. Inamsaidia hiyo Kinga yake tu ambayo inabidi wabunge waiondoe na yeye apande Kizimbani. Kikwete na yeye siku ikifika atapanda kizimbani tu. Sasa hivi kumuongelea Kikwete ni kupoteza muda kwani jamaa ana kinga moja nzito sana na kikatiba na ile ya nje ya katiba yaani Wabunge Mafisadi.

Siku ikifika, nyie mnaomtetea, muwe mwataka au hamtaki, jamaa atashitakiwa na kuhukumiwa jela kwa kuhujumu uchumi wa Tanzania. That day is comig too soon.
 
Hatukatai kwamba Mkapa alifanya mambo fulani mazuri wakati akiwa madarakani. Lakini uzuri wote aliuharibu kwa kuinajisi IKULU kwa kufanya biashara yeye na mkewe na kutumia madaraka yake vibaya kujiuzia Kiwira. Kuna kashfa nyingi za ufisadi katika utawala wake ambazo zinamhusisha moja kwa moja. Kama alivyosema yule Mbunge Mpendazoe, huyu ni wa kushitakiwa, na wale wote wanaomtetea kama vile akina Pinda waende wakamtetee huko. Nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria.

Review hiyo sentensi, naona kama ni wishful thinking!
 
Ukweli unabaki palepale kuwa Mkapa alikuwa makini kuzidi Jk
Jamani tuache yote ila mkapa huwezi kumlinganisha na JK.Alifanya mambo yaliyoonekena.Ingawa ana mapungufu yake ila hayazidi mazuri alofanya.Hata ndani ya familia baba hawezi kufanya yote mazuri.Mkapa ndo mwanga tulionao sasa wa TZ

Nani kawalinganisha?
Hata wangekuwa ndugu bado wangetofautiana. Hata wangekuwa baba na mwana bado wangetofautiana kwani Mungu ameumba kila binadamu kwa mfano wake mywenyewe, yaani hakuna binadamu wawili watakao kuwa sawa.

Nadhani watu wameeleza au wameanika mabaya au negative zake baada ya Kaniki kumsifia sana utadhania ni Nabii!
Mkapa ndo mwanga tulionao sasa wa TZ
???????....mmmmmhhhhh....
 
Mkapa hana maana yeyote ile, huyu anastahili kunyongwa, yeye ndo kafilisi nchi. Hii serikali inatabia ya kulinda watu wake lakini hata ishi kufaidi wizi wake, lazi auwawe. Yani huyu mzee ni mshenzi kabisa.
 
mimi nasema hivi mkapa ni mwanaume mtake msitake....huwezi kumlinganisha na huyu kikwete
BWM is a bulldozer, with too much confidence in himself. Intellectually he is, of course, shoulder higher than JK. And he took his job much more seriously., ..... But prabably prodded by a partner-in-life with insatiable appetite for wealth and riches, he erred in a deplorable manner; and for this, he is personally accountable. For this, the Constitution and the law must take their course.
.....Tumeburuzwa wee vya kutosha, uongozi wa JK na nvyombo vyao vya hbari wametulazimisha tumseme mkapa kwa muda wa miaka minne-JUST IMAGINE 4 YRS WATU WANAMSEMA MKAPA, 4 YEARS HAKUNA REMARKABLE CHANGES ZA UONGOZI WA SASA , 4YRS JK hana kitu........
Mkapa hoyeee!..
JK ziiii!!!!!!
Shuhuda zipo mimi naona Mkapa alijitahidi sana ...Jk makundi yanamchanganya sana .....
Hata mimi Binafsi sijafurahishwi na Jk hata kidogo, amekuwa anaficha sana uhalisi wake na pia hata utendaji wake tofauti sana na BEN, Ben alikuwa makini japo madudu yake. Jk is freaking with his ambitions....
.. ..na kikwete hakumtaka......kikwete alitakiwa kumuweka pinda uwaziri mkuuu kama compromise kati ya watu wa mkapa, nationalists [wataifa]....!
...ila napata sana wasiswasi na Jk maana sijaelewa sana itikadi yake..!! Hana sana tamaa ya madaraka sana Pinda labda aje kubadilika baadae sana.
Mkapa alikuwa Hodari na Kiongozi makini hata kuliko mzee mzima wa kaya Jk, huwezi kumfananisha na Jk hata kidogo, .. lakini Mkapa alikuwa kiongozi mzuri.Labda hii ndio janja ya Mzee mzima wa kaya kwa kufanya watu waseme Ben ni mbaya na kuona yeye ni safi
....JK anaonekana kutofanya kitu kwa sababu mapengo yanayohitaji kuonekana kama yamefanywa na kiongozi yalizibwa tayari na Mkapa.....
Pamoja na matatizo yote ya Mkapa, kuna mtu anaweza kutupa walau mambo 10 tu ambayo rais wetu mpendwa JK amelifanyia taifa hili tunapoelekea kufikisha mwaka wa tano?....
Anayeongelewa ni huyu:
Benjamin William Mkapa nimjuaye...(kama kielezavyo kichwa cha habari) kuna mijadala lukuki ya JK, kwanini na huu tuupeleke kwa JK?

1.Alivunja hosia wa J.K.Nyerere kwa kumpa uwaziri EL.
2. Alijijengea ikulu binafsi huko Lushoto, Tanga.
3. Alijijengea Hotel ya Kitalii huko Lushoto, Tanga.
4. Alizembea na kuruhusu mtandao katika kugombe Urais 2005......n.k. endelea.............................
Shairi ungeanza:-
Akawapa Wajanja kiwanja cha ndege cha KIA kwa bei ya dola 1,000/ kwa mwaka.
Je kuna ukweli hapa?....$1,000 kwa mwaka???
 
Kwani kosa ni lako basi...!

Hujui mwanga kama hujaona giza. kwenye shairi lako hukumalizia vizuri, kuwa ulishawahi kula chakula cha mchana kwake...!

Pale umaandika njaaaaa tu mshikaji...!

Unahitaji fimbo kama mtoto wa shule,

Ebo......!
 
shairi ungeanza:-

aliuza mashirika yote ya tanzania.

Akajipa mgodi wa kiwira.

Akajipa nyumba za serikali.

Akawapa wazungu migodi yetu na ardhi ya bure wachimbe madini.

Akauza kilimanjaro hotel mara tatu na huku sasa twalipa fidia wale wawili wa mwanzo.

Akawapa wajanja kiwanja cha ndege cha kia kwa bei ya dola 1,000/ kwa mwaka.
Aka-epa hela zetu bale bot.

Aka deepgreen hela zetu.

Aka meremeta hela zetu na madini.

Kama hiyo haitoshi, akaanza kushirikiana na wajanja wachache kuuza silaha ili majirani zetu wachinjane huku akilitumia jwtz na usalama wa taifa. Akitumia jwtz, alinunua radar kwa bei ya juu kuliko inavyotakiwa. Akajinunulia na dege bofu bofu.

Alim-fisadisha mzindakaya ili a-shut up.

Na hii yote na yote uliyoandika na yale yote hatukuyaandika, alilipwa mshahara wa walipa kodi. Makonde siku moja atakiona cha ntema kuni njomba.

...............lol
 
Mtanisamehe kwa kujibu hoja zenu wakuu this time. I only get here at night TZ time....pse understand...thanks
 
Good post kaniki.

Unajua ninachofurahi ni kuwa huyu jamaa anayelaumia yupo, anaishi, anadunda, vongozi waliokuwa wamkamat kaa amekosea wapo nao wanaishi!

Tutaendelea kulalamika na kulaumu tu hapa, TUNA RAIS YUPOYUPO TU KAMA SANAMU, watu watasubiri kumlaumu akitoka kwenye uongozi.

JK huwazi ku-mquote kila siku anatoa pumba
JK hana unaloweza kujivunia kuwa tuna kiongozi

IQ ya JK is remotely far lower than BMW.

KWA MIMI MTANZANIA MMOJA, NINAPOONA KUWA WATANZANIA WENZANGU WALIMWEKA JK! then MTU AKANIPA NAFASI YA KU-COMPARE KATI YA HAWA WAWILI, MKAPA KWAMWACHA MBALI SANA JK!

Kuhusu kuuzwa viwanda kosa lilifanyika na akina Mwinyi kukubali globalisation!

BWM alikuwa mkweli , mchapakazi na ailsimamia maamuzi yake hii ndio sifa ya kiongozi, hatukuona ujinga wa kujadili mahakama ya kadhi au ya kikristo hakuwa ana muda huo

Tutatukana na kusema lolote, tukubali kuwa sisi wenyewe watanzania ndio tuna makosa SASA KAMA MTU ALIONA MKAPA ANA MATATIZO NDIO MKAMKWEKA JK KUREKEBISHA?????????????????????LOL!

Tujadili mzizi wa matatizo, system zetu, sheria zetu lakini kwa yeyote mwenye akili BWM hatasahaulika kwa mazuri aliyotenda TZ. Na kama kuna mabaya mimi siamini mpaka aende jela! ndio nitaamini


VIZAZI VIJAVYO VIKITUULIZA KUWA ETI MKAPA ALIIBA?? TUTASEMA NDIO?? NA WAKITUUULIZA JE WALE VIONGOZI WALIOKUJA BAADA YAKE WALIFANYA NINI walimshtaki?? kimya!!!!! bado mnalaumu wezi

Mtanzania bila aibu anasema eti aombe msamaha! haya mawazo ya kifisadi pia! eti MKAPA KAMA KWELI ALIIBA AKIOMBA MSAMAHA BASI IS OK! bado tunasema tatizo ni viongozi hapa?? watz siku zote wajuaji tunamuhitaji MKAPA MWINGINE!

Unaweza ukampa MAXIMO cheo cha urais na akafanya vizuri zaidi kuliko JK!

Tatizo sisi, mwakani JK anaweza akasema hagombei tunaweza kumpa urais Sofia Simba! sisi!

Super!.....substance tupu
 
Mimi naamini alikuwa rais mstaafu...amefanya alichofanya kibaya kizuri lets go ahead!!!
Tuongelea JK...and coming 2010 president, too late too little we can do for this guy now??? twende mbele JK atuambie anavyo solve hizo problem kwani ni chama chao CCM ndiyo imeyafanya chini ya Mstaafu wao!Tumshataki JK 2010; apigwe chini!
 
nafikiri tufuate ushauri wa Sikonge, kuwa anayejadiliwa hapa ni Mkapa hivyo kuleta issue za Mrisho kikwete ni kupoteza malengo, hivyo naomba wote au sisi sote tumjadili huyo Nkapa kwa mazuri na mabaya yake. na kama alivyo sema Choveki? Aliyo fanya mkapa ni saswa sawa na kubaka mtoto kwa nguvu , hivyo amepoteza sifa zake za kuwa binadamu muungwana . Leo hii fikiria unakutana na mtu mzuri, kwa kila kitu muadilifu kazini, anaakili za shule etc etc, then siku moja anadakwa kwa kosa la kunajisi mtoto, watu wote wata guna ahh, yule baba, mbona mtaratibu, mnamsingizia etc etc yaani inakuwa vigumu watu kuamini kwa fulani bin fulani ndio kafanya hivyo, lakini mwisho ya yote tunabidi tukubali ukweli huo, kwamba Benjamini mwana wa William Bin Mkapa aliinajisi ikulu na kuibaka tanzania kwa faida ya wageni na marafiki/mashemeji zake at the expenses of the majority of tanzanians angalia watu wa geita walivyo dhulumiwa dhahabu yao, angalia watu wa buzwagi, nzega, kilwa na gesi yao, Mererani na Tanza nite yao, Tipper, Reli, ATCL, Tanesco na hata kwenye mabarabara ambapo inflation of the cost ni jambo la kawaida, nyumba za serikali kuuzwa kwa wachache at the expense of majority, kwani leo hiii ina i-cost alot serikali kuwapa makazi watu wanao stahili. ingekuwa anataka kusaidia raia wa tanzania kupata nyumba zao ili wasi dhalilike wanapo retire ilikuwa ni kuanzisha mortgage finance, maaana mtanzania waleo awe huyo mfanyakazi atapata wapi nyumba ya kuishi wakati nyumba zote wamejiuzia? au je sera hii ya kuuza nyumba za serikali kwa wafanyakazi inamsaidia vipi mfanyabiashara au mkulima ambao ndio majority of tanzanians? Huku ni kukosa akili ndogo tu ambazo mzee wa kizaramo ambaye hakwenda shule anaielewa na angejua cha kufanya, eg Sea Man Mzee wetu Marehemu Sheik Amri Abeid Karume na Nyumba za Michenzani?, huyu ndio kiongozo mwenye kujali watu wakena upeo ingwa shule yake si kama ya Mkapa.
 
Mimi naamini alikuwa rais mstaafu...amefanya alichofanya kibaya kizuri lets go ahead!!!
Tuongelea JK...and coming 2010 president, too late too little we can do for this guy now??? twende mbele JK atuambie anavyo solve hizo problem kwani ni chama chao CCM ndiyo imeyafanya chini ya Mstaafu wao!Tumshataki JK 2010; apigwe chini!
huku ni kukimbia tatizo, nyerere alisema mtoto akililia wembe mpe, akijikata atelewa wembe si kitu cha kuchezea, hivyo hato rudia kosa au mtoto akita kugusa sufuria la moto, unakumbuka biology mambo ya voluntary and involuntary reaction/reflex action? basi baaada ya hapo atakuwa anaogopa kitu cha moto.
na yanayoweza kufanywa
mosi kufuta Pension yake
pili kumfunga
tatu kufilisi mali zake hususana alizopata kwa njia isiyo stahili
na nyingine kama itakavyo onekana ina faa
 
Huyu bwana alikuwa kiongozi mzuri ila aliruhusu au kujiingiza kwenye rushwa ambayo inamfanya aonekane hakufanya kitu. Inawezekana uongozi uliopo ulitumia weakness hiyo kuhakikisha akipindisha mambo bila ya wao kuchaguliwa, wangemrudi baada ya kukihama chama na kueleza yote yaliyofanyika nyuma ya pazia kwa wananchi na akaogopa.Kwa yeye alivyo, sidhani kama angelikuwa ni mtu wa kudharau zile dosier za nani ni nani zilizoletwa mbele ya meza ya CC yao kabla ya uchaguzi kule dodoma. Pengine anastahili kuyapata anayoyapata kwa kuruhusu mianya ya viongozi kufanya madudu
 
Eeeh! Kiumbe umesifu kama anayesifu mbingu.

Hata watakatifu Duniani hupatikana baada ya Devil's advocate kusema mabaya yooote na yakashindwa na mema. Sasa wewe unasifu tuuuu. Naona kwako huyu alikuwa Malaika.
 
[/COLOR] [/SIZE][/FONT] Mnaomsema vibaya mshindwe ka kulegea. Hamna shukrani. Ni kiongozi ambaye wanaokumbuka, tunamshukuru sana.

Mkuu Mkapa didn't do Tanzania any favors kwa hiyo ukitaka umtetemekee wewe mwenyewe. Mkapa aliomba kura mwenyewe na kuitaka kazi. Alipo pata uraisi tukamfidia kazi zote alizofanya kwa kumuwekea security detail, mshahara usiyo punguzwa kodi, makazi ya bure, usafiri wa bure etc. Mkapa didn't do Tanzania any favors. Kama kuna mafanikio yote kaleta ni kwa sababu katimiza wajibu na hakuna haja ya kutoa asante za kurembana kwa umtu kutimiza wajibu wake.
Kuna baadhi ya mafanikio yake umetaja they are open to debate and they are not a matter of fact.
Hiyo ndege bora iligundulika ina matatizo na thamani yake siyo bei serikali iliyo lipia. Tena ni ndege hiyo hiyo ambao wananchi tuliambiwa hata tule majani itanunuliwa.
Wewe kama una urafiki au undugu na Mkapa au kama unataka kujimuvuzisha kwake sawa ila usije na a very opinionated thread halafu uipresent as if it's proven facts & fugures.
 
Back
Top Bottom