Benjamin William Mkapa nimjuaye...

Benjamin William Mkapa nimjuaye...

Shuhuda zipo mimi naona Mkapa alijitahidi sana kuiwekea nchi heshima ya juu haswa katika kukuza pato la taifa na kuzima mfumuko wa bei,maisha ya mtanzania ni ya kawaida sana kwa hiyo raisi anapoweza kumuwezesha kila mtanzania angalau kula mlo mmoja bila maumivu makubwa tunasema aliweza.

Aliikuta nchi iko pabaya sana alikuwa na ziada yakutufanyia watanzania tuwe na mwelekeo wa kiuchumi ili kuwa kazi ya taabu sana kwa hiyo panapostahili tumpe sifa.

Jk makundi yanamchanganya sana anapigana vita tatu wanompinga serikalini,wanompinga katika chama chake,na wananchi na wapinzani wote wamemkalia koo,yeye mwenyewe alikosea sana kuingia kwa njia ya mtandao na kutumia vyombo vya habari kumkandia,ndio maana yamemrudia na anapoteza umaarufu kwa haraka sana
Mkapa ni Mwandishi wa Habari anajua kuwa akianza kujibu mapigo ndio utakuwa mwisho wake. Lakini anajua kuwa yeye ndiye aliyemsaidia Jk kuingia madarkani. Labda sisi wanaJf tusubiri kipindi cha Kampeni atapewa jukumu la kuendesha Kampeni ili Jk awe rais. Mimi nawambieni Ipo siku Hapa tanzania atakuja kiongozi na yeye atakuwa Chizi atawafunga wote hata huyu Jk kwa kufanya mambo kinyume cha Sheria za Nchi. Mbona Zambia na Malawi yanatokea mambo haya?? Ipo Siku inakuja
 
Pamoja na matatizo yote ya Mkapa, kuna mtu anaweza kutupa walau mambo 10 tu ambayo rais wetu mpendwa JK amelifanyia taifa hili tunapoelekea kufikisha mwaka wa tano?

Binafsi nasema JK is a failure compared to Mkapa. Hata kina Mpendazoe ambao Phillemon Mikael anawakandia wanatumiwa na JK kumwandama Mkapa ili kuficha mapungufu ya JK.

Nipende au nichukie lakini binafsi sifurahishwi na utendaji wa serikali ya JK ambayo ilikuwa inatafuta namna zote za kumpunguza Magufuli lakini Mungu wa Israel na Mungu wa Yakobo bado anamsimamia mtumishi wake Pombe Magufuli.

Mambo mazuri ya JK.
1. Anapenda sana kusafiri kwenda Ulaya na Marekani kuomba misaada badala ya kutafuta namna ya kujikomboa kutoka kwenye huu umasikini unaolikabili Taifa letu.

2. Anaendesha Serikali kiushkaji badala ya kuwa strict na kupambana na UFISADI.

3. Ndio president peekee ambaye ameshindwa kuwawajibisha walitafuna pesa za EPA.

4...
 
hapo mzee unayejihita "Good post kaniki".Kwa nini sofia simba ndo chaguo la mwisho?.nadhani ni mwenyekiti wa wanawake za vigogo.Tupe picha yake tafadhali
 
Yapo mazuri katenda na yapo mabaya katenda. Mzani unaangukia wapi?
 
Hoja hii imefunikwa na pazia la UDINI. Mengine msemayo kanyaboya. Tazama inavyomaliziwa 'Mnaomsema vibaya mshindwe ka kulegea'. Mwanzilishi acha UDINI.
 
BWM is a bulldozer, with too much confidence in himself. Intellectually he is, of course, shoulder higher than JK. And he took his job much more seriously.

I believe his over confidence made him ignore Nyerere's edict that Ikulu is a sacred abode. He abused Ikulu. He converted it into a den of hungry, ruthless, ammoral speculators, local and foreign, determined to carve out the natural resources of our land between themselves, to the exclusion of the helpless valid owners, the wananchi of Tanzania. This was sacrilege.

He ignored pleas, local and foreign, that Tz was too poor to afford purchasing that sophisticated radar and the ultra-modern presidential plane; instructing his Minister to arrogantly and impudently tell us that we may have to feed on grass so that the equipment will be bought. That was an insult I will never forget. Indeed it has now come to pass, that a large number of Tanzanians are now even hungrier than they were during his era, and are in for grass because of the scarcity of food!

BWM bulldozed the giving away of government houses meant for its employees, for peanuts, as though on his retirement, government would wound up! Worse still, he arrogated to himself, his family and friends, the government-owned US$ 4 billion Kiwira Coalfields for a mere US$ 700,000 and decided to pay only US$ 70,000 as first and only installment. It is a relief to fair-minded patriotic Tanzanians that J.K.'s Government is planning to revoke this dirty, uncouth deal and repossess Kiwira Coalfields.

It is true that BWM exercised his powers to make some aspects of our economy grow somewhat. But prabably prodded by a partner-in-life with insatiable appetite for wealth and riches, he erred in a deplorable manner; and for this, he is personally accountable. For this, the Constitution and the law must take their course.
 
Wewe na mimi hatuwezi kujua labda mahakama ndio mwenye uwezo wa kujua na kusafisha Mkapa
 
No, Mizengo Kayanza Peter Pinda ameshatoa huku nini tena,
keshasema hana kisima cha pesa nje wala ndege....vp atakuwa fisadi?
 
Mahakama Huru na za kutafiti kujua kuwa kama kweli ana makosa au Kamati ya Bunge, Bunge Letu hawawezi kusafisha madudu haya wala nini. Lipo upande wa Mkapa kwa kazi yake nzuri katika Taifa lakini ukweli ni kwamba ana tuhuma za kujibu kwa Watanzania hivyo ni yeye mwenyewe ndio wa kusema.
 
Mimi sikatai wala sikubali kuwa BWM ana tuhuma za kujibu. Sikatai kwa kuwa nasikia kwenye mawimbi tu kuhusu tuhuma hizo.

Haya sasa, wenye tuhuma kwanini hawachukui hatua ya kwanza ili haki itendeke? Ni nani anaetuhumu? Je, ni nani asietenda sahihi kwa taifa, mwenye tuhuma au mjua tuhuma na kukaa nazo bila kuchukua hatua na kubaki kupika majungu?

Mtu hatahukumiwa kwa yale aliyoyafanya tu, bali pia kwa aliyoacha kuyafanya, hasa akijua kuwa kuyatekeleza ni kutimiza haki. Kama BWM ni mkosefu, wale wote wanaomtuhumu mitaani wana hatia pia kwa kutochukua hatua stahili, hasa wakizijua hatua za kuchukua ili haki itendeke.

Miaka 10 kama kiongozi wa Taifa masikini kama hili lenye matatizo chungu mzima, kila hatua ya kutatua matatizo hayo ni lazima iwe na risk ya lawama. Kama binadamu ni lazima alikosea na wakati mwingine atakuwa alikosea sana. Ila alitimiza wajibu wake na akalifikisha Taifa alipoliachia likiwa na heri kuliko awali. Hata kama angekuwa hajafanya yote yanayosemwa kayafanya, bado matatizo yangetafutwa ili alaumiwe.

Mbona sasa Taifa linatikisika na hakuna anaetaka waliopo madarakani washitakiwe? Au halijatikisika na kuliwa vya kutosha?
 
Mimi nakubaliana na wewe kabisa, maana kama kweli huyu jamaa ana tuhuma lakini amefanya mambo mengi sana katika Taifa letu kwa ujumla hata kufikia kuona na kuona mambo mengi sana tumeweza kwasababu yake. hivyo watu wajitokeze kwa ajili ya kumpeleka mahakamani. siyo kinga yake au Katiba, Ni katiba ya Tanzania yenye matatizo
 
Kwani wewe ufahamu kuwa Mazuri mia moja yanaweza kuharibiwa na baya moja tu. Itashangaza sana kama Mkapa hata shtakiwa mahakamani. Ametafuna sana pesa zetu sisi tunaolopa kodi, Yeye ndio aliye introduce PAYE ili aweze kutafuna kwa urahisi zaidi pesa za walala hoi. Lakini hakuwa peke yake alikuwa na wenzake kama kina Mramba, Balali n.k
 
JF nini kumetokea??

takribani Miaka 2 iliyopita nilimtetea sana Mkapa ,humu ndani waumini wengi walinishambulia sana ati sikitakii kizazi cha watanzania yaliyo mema kwa kumtetea fisadi na tena hadi wakuu wakafikia kufananisha jina hili langu na la mkapa .

Sasa leo nauliza nini kinatokea? Siamini kuona watetezi wameongezeka kiasi hiki.
 
LOL! ulikuwa kama nabii usiyekubalika kwenu!

Tulikuwa pamoja mkuu, roho zenu hazikuungana, wengine ofcourse wanaona hali halisi ya sasa na wanafunguka macho, that man was the LEADER! not just leader!

Mkapa atakumbukwa tu piga ua!
 
Ni kweli kabisa na pia kuna haja ya kuanzisha Mahakama ya jinai kuhusu viongozi
 
Ni nchi ya Kusadikika tu ambako kina Majivuno wako juu ya sheria, lakini sio Bongo wala Tanganyika. Kwa wale wanaotaka sheria zetu ziwe na macho ya kuchagua wahalifu, laana iwe juu yao wao na vizazi vyao.
 
Back
Top Bottom