Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Kwa hali nchi ilipofikishwa na Jk ikulu kufanywa pango la wanyang'anyi.Sehemu yakufanyia biashara ya uwaziri nalazimika kukumbuka kauli ya Mzee Mkapa kwamba tutamkumbuka.

Japokuwa Mh.Mkapa alikuwa na mapungufu yake lkn hakuwa dhaifu kama huu.

Mkapa alipokea nchi kutoka kwa dhaifu wa kukusanya kodi na alipokuwa anatoka akamwachia dhaifu wa kufuja kodi zetu.

Jk hakumbuki kuwa Mh. Mkapa alituambia tufunge mikanda na akasahau kutuambia tuifungue mpaka leo.
Tulikubali kufunga mkanda akajenga barabara, bunge la kisasa ambalo wassira na komba wanachapa usingizi,uwanja wa mpira wa kisasa,majengo pacha ya benki kuu, jk airport,ndege ya rais,rada,daraja la Mkapa n.k

Alirudisha heshima ya mfanyakazi iliyokuwa imepotea kipindi cha ruksa

Leo hii ni MAJANGA. Sio serikalini sio chamani kote kumekuwa kama familia ya MAPANYA .baba mwizi, mama,watoto,shangazi, mjomba,wajukuu wote wezi.

kwa shingo upande nalazimika kumkumbuka Mzee Mkapa pamoja na madhaifu yake.

teeh teeh, kaka nimecheka hadi nimejamba. Kweli nchi hii mwinyi aliiuguza, Mkapa akaitibisha na ikapona, Kikwete ameibebenda na afya ya nchi imezorota kama mtoto mwenye kwashiorkor, imedumaa na huenda ikafariki kabisa.
 
at least ben alikua anauma anapuliza,huyu wa sasa anachota tu wala hana habari na chochote zaidi ya safari yaani anaponda raha na familia yake mpaka hiyo miaka 10 iishe siijui tutakuwa wapi:disapointed:

Kuna mtu humu ndani alisema huyu baba (kikwete) asipojua kuendesha ndege mwaka huu b asi atakuwa anakichwa kigumu sana.
 
Mwizi tu huyu! hajajibu tuhuma mbali mbali zinazomkabili ikiwemo kufanya biashara akiwa Ikulu, kuhusiana na ufisadi wa Rada, ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi, wizi wa Kiwira, kuuza nyumba na Serikali kwa bei ya kutupa, wizi wa mabilioni ya EPA, Meremeta, Kagoda ambavyo vilifanyika akiwa madarakani. Kuwaleta Net Group na kuwakabidhi management positions za TANESCO na kuwalipa mabilioni chungu nzima pamoja na kuwa hawakujua lolote lile kuhusu umeme kisha kuwashinikiza kusaini mkataba na kampuni yake ya wizi ya kiwira wa shilingi bilioni 326. Angekuwa china angepata habari yake.

BAK you are right, ila tunachofanya hapa tunamliganisha Ben with chinese prof. Ben was like a dad who will buy 5kgs of beef and he will eat 2kgs and bring 3kgs to the kids. The chinese prof. is buying only 1 kgs and borrows another 1 kg from the butcherman but eats both 2kgs alone. Kids do not get anything. In that regard Ben was better.
 
Watu si mlichagua sura........kuleni sura yake sasa tuone kama mtafika.Mzee mchonga alivyopindua matokeo dodoma mwaka 1995 alimaanisha kwa kuona mbali.
Ila kwa kuwa alikuwa anaongea na taifa la watu maamuma hatukuliona hilo tangu mwanzo alipofanya upheaval na watu mkaja na tafsiri zenu za hovyo hovyo eti huyu mda wake bado.
Leo inajidhihirisha kuwa kwa nini alizunguka kila meza kuyaelimisha majitu yasoyojitambua (NEC) kubalisha msimamo.
Haya sasa oneni.......uchumi wa nchi ka Zimbabwe mwenye vikwazo.
Rushwa,wizi,ufisadi na urasimu vyote vimetamalaki......
 
Yeye na sumaye waliiba sana,japo walibana vyombo vya habari kutokuandika habari chafu za serikali mfno kashifa ya makaa ya mawe,tanzanati na sumaye,lkn kikwete ameweka kila kitu wazi watu wameona na watu wanasema,lkn wanaojua wasema wizi uliofanyika kipindi cha mkapa ni zaidi ya kikwete,tutamkumbuka nyerere sio yeye .
 
Yeye na sumaye waliiba sana,japo walibana vyombo vya habari kutokuandika habari chafu za serikali mfno kashifa ya makaa ya mawe,tanzanati na sumaye,lkn kikwete ameweka kila kitu wazi watu wameona na watu wanasema,lkn wanaojua wasema wizi uliofanyika kipindi cha mkapa ni zaidi ya kikwete,tutamkumbuka nyerere sio yeye .
Mijitu mijinga kama wewe Kanone ndiyo kikwazo cha maendeleo yetu. Ukisoma kichwa cha mada hii kinaongelea jinsi awamu ya nne ilivyonunua vyombo vya habari na kuwapumbaza wananchi waamini kuwa Mkapa amejimilikisha mgodi na kufanya biashara ikulu. Na kwa akili zenu finyu mukabaki muna amini hivyo. Wenye akili wengi wameelewa kuwa ilikuwa propaganda ya kuwapoteza mubaki mukimjadili Mkapa wakati wao wanahangaika kujipanga waanze na lini.
 
Kikwete ni raisi wa hovyo kabisa kuwahi kutokea duniani. Yeye ni safari tu, hajui hata alipewa ukuu wa nxhnchi afanye nini
 
Mijitu mijinga kama wewe Kanone ndiyo kikwazo cha maendeleo yetu. Ukisoma kichwa cha mada hii kinaongelea jinsi awamu ya nne ilivyonunua vyombo vya habari na kuwapumbaza wananchi waamini kuwa Mkapa amejimilikisha mgodi na kufanya biashara ikulu. Na kwa akili zenu finyu mukabaki muna amini hivyo. Wenye akili wengi wameelewa kuwa ilikuwa propaganda ya kuwapoteza mubaki mukimjadili Mkapa wakati wao wanahangaika kujipanga waanze na lini.

Mkuu wew ndo Ben nin ,eti propaganda ? Kweli hapo kuna propaganda?
 
Kuna kale ka wimbo heri baba Nyerere, kawimbo kanaendea kwa kumtaja Mwinyi na Mkapa...
Kakimalizia Watanzania watamlilia Mungu.

Sijui ni kwaya/kundi gani waliimba hayo!
 
Kumfananisha kikwete na mkapa ni kumtukana mkapa. Kikwete hafai hata kuwa DC
 
Back
Top Bottom