Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Hii sasa ni total desperation. Mkapa anakumbukwa kwa "mema"? Hakuna mtu asiye na mema kabisa hapa duniani. Hata Mobutu, Idd Amin na Hitler walikuwa na mema yao. Vigezo pekee vya kumkumbuka rais mstaafu ni uongozi thabiti (sio udikteta), uadilifu, uzalendo na kusimamia katiba na haki za binadamu kikamilifu. Muhimu zaidi ni rais ambaye akiondoka anaiacha nchi ikiwa kwenye mwelekeo bora wa maendeleo.

Hakuna rais anayeweza kuwa na sifa hizo huku akisimamia mfumo wa kifisadi unaozingatiwa kikamilifu na chama chake cha siasa. Mkapa ni mwana-CCM kamili na hana tatizo kabisa na jinsi chama hicho kilivyo. Yeye ndiye muumin mkuu wa mwenendo wa kuukabidhi uchumi kwa wawekezaji wa nje kama ndiyo mkakati pekee wa maendeleo. Dharau yake kwa wazawa ilikuwa wazi kabisa bila hata ya kujaribu kuonyesha ni jinsi gani anavyoweza kubadili huo "uduni" wa wananchi wake wawe na uwezo zaidi wa kufikiri na kutenda.

Kwa mtu aliyesimamia ufisadi mkubwa wa rasilimali za taifa na kutishia waliojaribu kuhoji na kisha kurithisha mwenendo huo kwa aliyemfuatia sioni haja ya kumkumbuka kwa chochote; labda waliofadhiliwa kibinafsi wakumbuke. Kwamba aliyefuatia ndio ovyo zaidi si hoja ya maana ya kumkumbuka aliyetangulia katika uozo huohuo. Fisadi ni fisadi tu. You may hate JK, but BM is just another side of the same coin. They play the same game in differing styles.
 
Baada ya vyombo vya habari vilivyokuwa vimenunuliwa na genge la mtandao kumsakama sana kwa habari nyingi za kumponda. Mkapa aliwahi sema maneno machache sana kuwa Watanzania tutamkumbuka.

Kwa kweli hali ya nchi iliyopo saizi hakika jamaa tutamkumbuka tu, tutake tusitake. Nchi kila kitu kinaenda hovyo, na wanaonufaika ni wachache waliokuwa vinara wa hilo genge. Hakika sipati picha itakapofika 2014 hali itakuwaje. Saizi hela haina thamani kabisa, naamini soon BOT itaprint note zingine za elfu 20 na elfu 50. Ki ukweli buku 10 haina thamani tena. Ukishachenji imeisha.

Nchi huwa haiongozwi kwa blabla bali inahitaji commitment ya hali ya juu sana.

Kila la kheri.....

Yeye na wajanja wezake kugawana nyumba za Serikali.
 
hyu muendeleza mada asisahau haya:-

=================================
Mwizi tu huyu! hajajibu tuhuma mbali mbali zinazomkabili ikiwemo kufanya biashara akiwa Ikulu, kuhusiana na ufisadi wa Rada, ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi, wizi wa Kiwira, kuuza nyumba na Serikali kwa bei ya kutupa, wizi wa mabilioni ya EPA, Meremeta, Kagoda ambavyo vilifanyika akiwa madarakani. Kuwaleta Net Group na kuwakabidhi management positions za TANESCO na kuwalipa mabilioni chungu nzima pamoja na kuwa hawakujua lolote lile kuhusu umeme kisha kuwashinikiza kusaini mkataba na kampuni yake ya wizi ya kiwira wa shilingi bilioni 326. Angekuwa china angepata habari yake
 
Mwaka 2005 wakati rais mstaafu wa awamu ya 3 akiondoka madarakani aliaga kwa msemo huu "MTANIKUMBUKA WATANZANIA"

Nilikuwa napata picha hasa za kiuchumi kwa kauli yake lakini nimekuja gundua kumkumbuka kwa nengi na hasa hili la udini ambalo limemwingiza Ikulu hasa alipo mchafua mwenzake kwenye kinyang'anyiro cha urais ndani ya Chama mwaka 2005 ikiwa ni miaka kumi toka aambiwe haujakuwa na mzee ila kwa fikra za vijana wakajua bado mtoto kumbe hafai.

Sasa kauli ya baba wa taifa kuwa ukila nyama ya mtu huachi ndo hii inaonekana waneshaonja na ni tamu kwao na Mungu wao sasa wanafanya ni kitoweo.

TUNAKWENDA WAPI??
 
Kwa mwendo huu hata Kikwete mtamkumbuka tu.

Your bar is already low. With the passage of time, nostalgia is inevitable. Especially if the current trend of non-meritorious ascent continues, as it is bound to due to its steep roots.

Mgojeni mpate Pinda type apinde mambo mpaka Kikwete aandikiwe kitabu "The Genius of Msoga and The Art of Propaganda"
 
Namkumbuka kwa machafuko yaliyopo, na jeshi kutumiwa kisiasa
 
Kwa hali nchi ilipofikishwa na Jk ikulu kufanywa pango la wanyang'anyi.Sehemu yakufanyia biashara ya uwaziri nalazimika kukumbuka kauli ya Mzee Mkapa kwamba tutamkumbuka.

Japokuwa Mh.Mkapa alikuwa na mapungufu yake lkn hakuwa dhaifu kama huu.

Mkapa alipokea nchi kutoka kwa dhaifu wa kukusanya kodi na alipokuwa anatoka akamwachia dhaifu wa kufuja kodi zetu.

Jk hakumbuki kuwa Mh. Mkapa alituambia tufunge mikanda na akasahau kutuambia tuifungue mpaka leo.
Tulikubali kufunga mkanda akajenga barabara, bunge la kisasa ambalo wassira na komba wanachapa usingizi,uwanja wa mpira wa kisasa,majengo pacha ya benki kuu, jk airport,ndege ya rais,rada,daraja la Mkapa n.k

Alirudisha heshima ya mfanyakazi iliyokuwa imepotea kipindi cha ruksa

Leo hii ni MAJANGA. Sio serikalini sio chamani kote kumekuwa kama familia ya MAPANYA .baba mwizi, mama,watoto,shangazi, mjomba,wajukuu wote wezi.

kwa shingo upande nalazimika kumkumbuka Mzee Mkapa pamoja na madhaifu yake.
 
Ukweli ulio wazi Mkapa ni bora kuliko kikwete katika uongozi japo wote ni mafisadi

Msemo wa Nyerere hii nchi inahitaji raisi kama mvuta bangi
 
Kweli tutakukumbuka kwa Mauwaji ya Watu wasio na hatia Kule Zanzibar na Tanganyika
 
Kweli tunakukumbuka kwa kujimilikisha mgodi wa Kiwira, benki M, mauwaji ya Bulyankulu,
 
Kweli tanganyika watu wamekwisha wamebaki machizi na ndo hao wanapewa uwaziri, nkamia & mwigulu haya c majanga. Mkapa is the best
 
Atakumbukwa kifo cha Baba wa Taifa mikononi mwake, kajipa Kiwira, kauza nyumba za serikali, Mgodi wa Tanzanite, Geita, Mwadui, North Mara, Tanesco netgroup, TTCL kuzalisha airtel ambayo si ya serikali, kuuza NBC kwa bn 15 na ufisadi mwengne.
 
Atajumbukwa kwa mengi
1.Rais wakwanza kutoa ushaidi wa wizi mahakamani
2.Ni rais pekee aliyemwacha mkewe na familia yake kufanya biashara ikulu
3.Ni rais pekee aliyeuza nyumba za serikali bila uchungu
4.Ni rais pekee aliyeacha Bot watu wajichukulie fedha
5.Pia ni rais pekeee aliyekuwa na maamuzi magumu
 
Back
Top Bottom