Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Now the wise one or the stupid one? Kwanini hakusema haya yote kipindi yupo madarakani? Kwanini hakuyasema kipindi cha chaguzi zilizopita?
Aliwahi sema haya huko Davos akiwa president - zama hizo akiomba msaada wa neti:

"Now for our own, let me say: I don't want to be putting the developed countries on the dock. We [Africans] also have a task, we also have a challenge; because we also have a capacity to some extent of funding the war on poverty ourselves: organizing our economies, organizing our revenue collection systems, organizing our own budgeting, being more accountable and transparent. Those we can undertake. A combination of those reforms I think would see a tremendous, truly predictable advance in the war against poverty."

Anyway! Kuna nyakati hawa viongozi wanaongea kwa akili zao, ila mara nyingi kwenye maamuzi, uwezo wa yule mwovu hutawala.
 
Ametupa zawadi ya kitabu ili tujielimishe masuala ya uongozi kwa kusoma kazi zake, kuzitafakari na kujipima tulipotoka, tulipo na tuendako tunapoitizama Tanzania ya leo na ile aliyoiongoza miaka 24 iliyopita.

Tunakupongeza kwa kuweka kumbukumbu ya kazi zako na uongozi wako kwenye maandiko ili tukujue, tujifunze na kujielimisha kutoka kwenye mkusanyiko wa hadithi ya maisha yako kama raia na pia katika nafasi ya kulitumika taifa kama Rais kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

Kupitia kitabu chako cha My life My Purpose, Maisha yangu , Makusudi yangu, umetuonyesha ulipotoka, ulipotembea, ulipo na ushauri kwa nchi yako ambayo umeipenda na kuendelea kuipigania hata sasa unapostaafu lakini si kwenye kuwatumikia Watanzania.

Tunaamini kitabu cha Mkapa kitasomwa iwe kwenye shule za msingi na hata kwenye taasisi za elimu ya juu. Ni Imani yatu kuwa kuwa Rais John Magufuli, wakati akikizindua anawashauri wadau kukitafsiri kwa Kiswahili ili kisomwe na wengi.

Tunaamini kitasomwa na wengi na kufuatiliwa na Watanzania wa aina mbalimbali kwa kuwa kina ujumbe na maudhui yanayowagusa vijana, wanasiasa, wasomi, wanahabari na kwa ujumla kila mmoja popote alipo.
Kitabu hiki kama ambavyo majumuisho yake yametolewa kwa ufupi na Mkuu wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Rwekaza Mukandala, kinaelezwa kuwa ni kitabu cha kwanza kuandikwa na kiongozi wa nchi kuhusu maisha yake binafsi.

Hongera, kwa kiongozi wetu ambaye kitabu chake kitaendelea kubaki kuwa tunu ya taifa na zaidi ya sana tutakitumia kujifunza kupitia kwake fikira na falsafa yake ikiendelea kuishi kwenye mawazo yetu.
Mkapa katika andiko lake ametukumbusha mengi kubwa ni kulipenda na kuhimiza watu kulisimamia taifa letu. Ametukumbusha kuwa na mshikamano na kukumbuka kuwa daima hatutakuwa na maendeleo kama hatutajitegemea.
Rais mstaafu anasema kama nchi ni lazima tuondokane na utegemezi tujitegemee na kutumia rasilimali zetu kwa maendeleo yetu wenyewe.

Lakini, pia anatukumbusha kuwa nchi yetu inapita katika harakati ambazo tunahitaji sana kuwa na uadilifu na uzalendo. Mkapa anatuonya kuwa kuna baadhi ya watu kwa nia zao wanaweza kukwamisha maendeleo ili kutimiza azma zao.
Anatueeleza jinsi ambavyo aliingizwa mkenge kwenye masuala ya fedha za akaunti ya madeni ya nje (EPA) ambayo mtihani wake uliishia kuwa kashfa ya EPA ambayo wengi wanaifahamu, lakini la msingi hapa si kulaumiana ila ni kuonyesha jinsi hamu ya kupata tija binafsi inavyoweza kuliangusha taifa.

Mkapa katika andiko lake anatushauri kuwa na sera na mipango ya kusaidia vijana. Anaeleza kuwa wako vijana wengi mno, lakini kama taifa hatujawa na sera za kuwaendeleza na kuwafanikisha ili wawe na maisha bora.
Rais huyu mstaafu hajawaacha wanasiasa, anawakumbusha kuwa inavyoelekea kila mtu anayejitumbukiza kwenye siasa ana lake jambo. Wapo wanaotaka kupata safari za ughaibuni, lakini pia kuna wafanyabiashara wanaolenga kujinufaisha na kupata mafanikio ya biashara zao.

Yote haya Mkapa anatukumbusha kuyatazama. Anasema ni vyema pia kuwa na baraza la kisheria la kitaalamu kupitia mikataba yetu ya kimataifa ili kuweka mambo kwa uwazi na kwa manufaa ya taifa letu.
Ni maoni yetu kuwa Mkapa ametufundisha na kutushauri, hivyo basi tuzingatie yote mema anayotushauri kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu.



Chanzo: Nipashe
 
Hivi kuna mtu alikuwa mbishi kama cha Mkapa kweli? Huyu mzee alikuwa asikii manake hata Jiwe akitoka atakwambia huu ujazz band wakati watu wanayaona na kupiga kelele lakini hawasikii kabisa.
 
Apart from everything.. Nahisi kila Mkuu amepewa jukumu la kuhakikisha atakapotoka madarakani chama chao kinabakia madarakani! Kwaio akuna anaetaka imfie.. Kinda like Mu7's type of things lakini siyo.. So, kijiti anacho mkulu.. and he is doing his things :(
 
kuna mambo mengine hata utubu hayafutiki, ni lazima ukayajibu tu kwa pirato!! kwa mfano damu za wale wadai haki 21 zile ndizo zinamlilia na kumsumbua sana.

Watawala wakizungukwa na wapembe wao na ma mitutu ya bunduki huwa wanasahau kabisa kwamba hapa duniani hatujajileta kuna siku ni lazima ukayajibu mashtaka kulingana na matendo yako.
 
Hapo ni wajibu sasa wa vyama vya upinzani kuungana kudai tume huru kwa hoja nzito na ushawishi mkubwa ili watawala waelewe maana ya tume huru.Tena kabisa ikiwezekana machapisho ya kutosha yachapishwe kwenye mitandao kila mtanzania mwenye access ya kuperuzi kwenye mitandao asome japokua pengine inaweza ikatafsiriwa kua ni uchochezi.

kwa sababu kutegemea tume huru chini ya CCM na utawala huu ni sawa na kusubiria embe chini ya mnazi. kwa sababu ccm ilishajiona kwamba bila yenyewe hakuna Tanzania
 
Miaka themanini naa uzee umetaradadi kufa kupo njiani mali alizojilimbikizia ataziacha sasa sio kitu tena ila toba, haoni umehimu wa mali ila kumrudia Muumba, amejua kiburi ni kama nazi haishindani na jiwe yani kifo. Atulie tu atakutana ma mhusika siku ya mwisho sisi hatuwezi kusamehe na ikawa faraja kwake.
Kaka umeandika maneno mazito, umeupa huzuni moyo wangu.
 
Sitashangaa hata huyu wa sasa akitoka akaandika kitabu na kusema haya haya, they talk what they can't stand and live
 
Return Of Undertaker,
Why did His Excellency Ben Mkapa fail to give hiyo "TUME HURU YA UCHAGUZI" ; kwa sababu he had all the tools and powers at his exposal to do that! Is His Excellency regretting or trying to push the ball in someone else's court?
 
Back
Top Bottom