Bendera za Uamsho zashushwa Zanzibar nzima

Bendera za Uamsho zashushwa Zanzibar nzima

Kifo cha uhamsho kimeshafika na Pumzi imeshaanza kutolewa huku ndugu zao wakiwawekea Oxygen wapate kupuma uzur maana hali yao ni mbaya......Katika hatua nyngne ambayo SMZ imeonesha kidogo makucha yake imeendesha msako mkali wa Bendera za Uhamsho na kuzishusha na kuondoka nazo, SMZ kutumia jeshi la polisi limekamata DVD zote na CD zinaonesha mambo ya Uhamsho.......tukio hili lilitokea pale Mlandege gari ya polisi ilpofka na kubeba kila kitu katka duka moja la wakala mkuu wa CD hizi maana ufanya biashara na kuuzwa nchi za Kiarabu na ulaya......Ulinzi umeimarishwa Visiwani muda wote Jeshi la polisi linaonesha nguvu yake ambayo muda mrefu waliwalea Uhamsho sababu hawakupewa Ruksa....na mkakati uliopo ni kufutwa kabisa Uhamsho katka ramani ya Tanzania sababu ni Taasisi ya Kidini lakini inaingilia mamlaka ambayo si yake na kujenga chuki baina ya watu......Ahsante SMZ maana waliwadharau sababu hamkuwapa CHAI

Tunashukuru kwa info, mkuu kwani UAMSHO ilikuwa imesajiliwa kama ilikuwa bado kushajiliwa waliwezaje kuwa na ubavu wa kupeperusha bendera?

Mimi nashauri SMZ ibebe na harddrive zote hata zile zilizofutwa, kuna utaalamu wa kusoma kilicho kuwa mle hata kama wamefuta.
 
Si wanasema jamaa ni chizi!!

SAM_2542.JPG
 
naunga mkono SMZ na bara nao wafanye hivyo kwani UHAMSHO ni upuuzi watu tuna njaa tunatafuta suluhu wengine wanatuletea chuki za kidini ambazo hazina msingi........tena ikiwezekana mihandara yote na maongezi kuhusu dini zingine ipigwa marufuku kabisa nchini
 
kifo cha uhamsho kimeshafika na pumzi imeshaanza kutolewa huku ndugu zao wakiwawekea oxygen wapate kupuma uzur maana hali yao ni mbaya......katika hatua nyngne ambayo smz imeonesha kidogo makucha yake imeendesha msako mkali wa bendera za uhamsho na kuzishusha na kuondoka nazo, smz kutumia jeshi la polisi limekamata dvd zote na cd zinaonesha mambo ya uhamsho.......tukio hili lilitokea pale mlandege gari ya polisi ilpofka na kubeba kila kitu katka duka moja la wakala mkuu wa cd hizi maana ufanya biashara na kuuzwa nchi za kiarabu na ulaya......ulinzi umeimarishwa visiwani muda wote jeshi la polisi linaonesha nguvu yake ambayo muda mrefu waliwalea uhamsho sababu hawakupewa ruksa....na mkakati uliopo ni kufutwa kabisa uhamsho katka ramani ya tanzania sababu ni taasisi ya kidini lakini inaingilia mamlaka ambayo si yake na kujenga chuki baina ya watu......ahsante smz maana waliwadharau sababu hamkuwapa chai
safiii safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Na radio Nuur hapa zanzibar pia imefungiwa nayo ilikua inaongoza kwa uchochezi huko Tanganyika poleni kama radio imani inaendelea kuwakera huku full burdani sasa. mr zaifu bado anacheka cheka tu huko, nahisi harufu ya Mwamunyage Davis kuongoza nchi.

Dah!huku mkuu mzee bado anacheka 2,tusubiri tuone
 
Duuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!! walikuwa washajitangazia kajamhuri kao
 
Naifikiri suala hapo sio bendera, ni ile dhana yao kwa watu nafikiri kuna ambao wameupokea ujumbe na wapo tayari kwa lolote...ikibidi hata kufa kuutetea uhamsho...hii ni hatari...nilikuwa najiuliza siku nyingi kuwa watu wamelala mpaka waamshwe?

Halafu kwamba ni chizi hapana ni wajanja wachache wanataka kumkwepesha na mkono wa sheria chizi ataongozaje watu wenye akili...huyo ni fyonso...
 
Naifikiri suala hapo sio bendera, ni ile dhana yao kwa watu nafikiri kuna ambao wameupokea ujumbe na wapo tayari kwa lolote...ikibidi hata kufa kuutetea uhamsho...hii ni hatari...nilikuwa najiuliza siku nyingi kuwa watu wamelala mpaka waamshwe?

Amani haitarudi mpaka Zanzibar iwe huru...Vinginevyo ni kujidanganya tu , Watanganyika.
 
Dr. Shein ni mbara, mtanganyika,mzanzibari, muunguja au mpemba?

Wagawe, upate kuwatawala vizuri.

shein ni Mbara muunguja hana itikadi za kipemba shein ameandaliwa bongo acha hizo ujampata mpemba asilia ww........na kama Karume angekuwepo asingetawala mtu sababu jamaa alkuwa hawataki hata kidogo anayejua ataungana mkono na mm si kwamba natungahapana na wala si kwamba nawachukia hawa jamaa ila nasema yalyosemwa na Karume
 
Hawa ni balaa nyekundu ndani ya Nchi yetu!
Nani aliwapa ruksa ya kupeperushaga bendera?

Ama Tendwa nini??
 
Cuf+ccm=alshabab,boko haram , alquaida,uamsho n.k


‘Siasa bila dini ni uendawazimu'
Na Lilian Nyenza


Kanisa halitaacha kutoa mwongozo kwa watu wake hata kwa mambo ya kisiasa ukiwamo uchaguzi kwa kuwa, siasa bila dini ni sawa na uendawazimu.
Aidha, imedaiwa kuwa tabia ya kuwalaghai vijana kuwa ni taifa la kesho, ndiyo inayowadumaza kiakili na kuwafanya watumiwe na wanasiasa kufanya fujo, badala ya kujitokeza kuongoza kwa kufuata taratibu za nchi.


Mkurugenzi wa chama cha kifamilia cha Undugu Association Tanzania, Padri Baptiste Mapunda, alitoa kauli hiyo katika sherehe za kuuaga mwaka 2004 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2005, zilizofanyika katika ukumbi wa Parokia ya Mt. Yosefu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo wa UNDUGU ASSOCIATION TANZANIA alisema kuwa, Tanzania imeanza kuonesha dalili mbaya za machafuko kutokana na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa kuweka mbele ubinafsi.


"Tukikaa kimya huku mambo yanaharibika katika jamii; eti tuwaachie wanasiasa wafanye watakavyo, tutakuwa hatutendi wajibu wetu na hivyo, Kanisa halitaacha kusema ukweli kwa maslahi ya umma hata kama unamkera mtu. Hii ni kwa kuwa tunajua wazi kuwa siasa bila dini, ni uendawazimu ambao mtu hajui akifanyacho kwa kuwa akili yake haijatimia kiroho." alisema.


Aliitaka jamiii ya Kitanzania ijifunze thamani ya amani na siasa safi kutokana na hali ya amani na usalama katika nchi jirani za Rwanda na Burundi ambayo ni hatari na inasikitisha.


Alisema vita na mauaji yanayoendelea katika nchi hizo, yanasababishwa na uroho wa madaraka wa watu wachache ambao hawajali utu wa wengine.
Aliongeza kuwa, "Siku zote tunapaswa kukumbuka kuwa, amani na mapendo ambayo Mungu ametujalia, tunapaswa kuyaenzi sisi sote kwa kuwa siasa bila dini, ni sawa na uendawazimu."


Padri Mapunda aliiasa jamii kuendelea kumuomba Mungu ili azidi kuwajalia amani,upendo na utulivu uliopo sasa, kuwa uwepo hata baada ya Uchaguzi Mkuu kupita.
Amewataka Waamini kuwaombea viongozi wanyanyasaji kama Herode, wabadilike na hivyo, kuongoza nchi kwa haki na akawasihi Watanzania kuyashinda maovu kwa kutenda yaliyo mema.


Hata hivyo, Padri Mapunda amewatahadharisha vijana kujiepusha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa siasa, kwa nia ya kufanya fujo katika uchaguzi.
"Vijana mara nyingi wamekuwa wepesi wa kurubuniwa na vijizawadi vidogo vidogo, ili wafanye kile wanachokitaka wanasiasa wabinafsi. Sasa mimi nasema mkae chini na mlitafakari hilo kwa makini. Mtakao angamia ni ninyi na si wao," alitahadharisha.


Alisema vijana ni Taifa la leo na Taifa bila vijana limekufa, hivyo aliwasihi kuwaheshimu wazazi na walezi ili wapate kuishi maisha marefu na yenye heri duniani, kama walivyojaliwa kuuona mwaka huu mpya.


Naye Mwenyekiti wa Umoja huo, Bw. Benjamini Komba alisema, lengo la Shirika la Undugu, ni kuiunganisha jamii, ikiwa ni pamoja na kuimarisha Ukristo katika kupata hamasa katika kazi ya umisionari, ili ijengeke roho ya umisionari wa kweli nchini Tanzania.


Bw. Komba alisema kuwa, Shirika limekuwa na mchango mkubwa kwa jamii, kwa kuwa ni chombo cha kuelimisha jamii na kuendeleza mawasiliano na wamisionari wa Afrika ambao wapo ndani na nje ya nchi kwa lengo la kusukuma mbele kurudumu la Injili katika Taifa hili.
Umoja huo haujishughulishi na mambo ya siasa na hauna ubaguzi wa dini, rangi, imani wala itikadi.
Katika sherehe hizo, Wanaundugu na watu wengine walialikwa na kuhudhuria pamoja na familia zao.
 
Back
Top Bottom