Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 22, 2021. Mahakama yatupilia mbali hoja tatu za utetezi. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 23, 2021

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Leo tarehe 22/11/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea baada ya kuahirishwa siku siku ya Ijumaa, tarehe 18 Novemba, 2021.

Kujua kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 18, 2021. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 22, 2021

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

=========

UPDATES:

JAJI AMEINGIA MAHAKAMANI


Kesi imetajwa..

Wakili wa Serikali Pius Hilla Anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali

Esther Martin
Nassoro Katuga
Jenitreza Kitali
Tulimanywa Majige
Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi

Nashon Nkungu
John Malya
Dickson Matata
Seleman Matauka
Sisty Aloyce
Maria Mushi
Khadija Aron

Jaji anaita Majina ya Washtakiwa wote wanne,

Wanaitika

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Shauri limekuja kwa ajili ya Kupokea Uamuzi na Tupo tayari Kuendelea na Shauri..

Kibatala: sisi pia Mh Jaji Shauri lilikuwa kwa ajili ya Uamuzi Mdogo kwa Ruhusa yako tupo tayari Kuendelea na Shauri

Jaji anaandika Kidogo

Jaji: tarehe 18 November Mahakama hii ilihairisha Kesi hii wakati Shahidi akiwa anatoa Ushahidi Wake

Mahakama inatoa Uamuzi kama ninavyosoma Sasa. Wakati Wa Shauri Hili Dodo Shahidi alikuwa anatoa Ushahidi Kuhusu Kuchukuliwa Maelezo ya Onyo

Shahidi aliomba kutoa Kielelezo ambacho ni Detention Register ambayo alitumia Siku anawapokea Watuhumiwa Namba 2 na Namba 3. Walipo fikishwa kwake na Shahidi namba 1 na Shahidi namba 4. Kwa Maana ACP KINGAI na ASP Jumanne, Wakati anakitoa, Upande wa Utetezi walipinga

Kwamba 1. palikuwa hakuna Disposal Order 2. Mahakama ilikuwa inazuia kwa sababu ilishakijadili Functus Officio 3. KWA issue Estoppel Kwamba Jambo ambalo Limeshajadilowa Mahakamani Upande wa Mashitaka Wanazuiwa Kurudisha tena Mahakamani

Upande wa Utetezi waliwakilishwa na Jeremiah Mtobesya na Peter Kibatala, Kwa Upande wa Mashtaka Waliwakilishwa na Abdallah Chavula na Pius Hilla. Kwa Kutokurudia Mahakama itazungumza Kwa pamoja Hoja zote.

Jaji: Kwa kuanza Upande wa Utetezi walisema Kwamba Hakuna Disposal Order Kwa kupitia Kifungu cha 353, Wakasema Kwamba Kwa Mahakama Kutoa Kielelezo ni Njia Pekee ya DISPOSAL ORDER, Na Kwamba Kielelezo ambacho Kinaombwa Kuingia kilishatolewa Mahakamami na Kutolewa

Na Kwamba Jaji alikwepo au aliyemrithi hakuna Sehemu yoyote ambayo wametoa Mahakamani Disposal Order, Na Kwamba suala la Kutoa Kielelezo Mahakamani linatakiwa Kuwa Shirikishi na Lifuate Taratibu za Utawala na tatu lazima Utoaji wa Disposal Order Ufanyike kwenye Mwenendo wa Wazi

Naibu Msajili Kutoa Kielelezo pasipo Amri ya Mahakama, Ni Kukiuka Misingi na wakaomba basi Mahakama Isipokee. Wakasema haitoshi Palipaswa kuwa na Register Ya DISPOSAL Ambapo kwa Mujibu wa Muongozo wa Jaji Mkuu Unavyosema. Na Mahakama iangalie Katika Muongozo Katika Sehemu ya 4:4

Jaji: Na Hoja ya Pili kuhusu Mahakama Kuwa Funtus officio, Wakiomba kwamba Kwa sababu Mahakama Ilisha toa Maamuzi, Katika kesi Ndogo ndani ya Shitaka Kubwa basi Mahakama Ione kwamba pale ambapo Mahakama Ilisha toa a Maamuzi awezi Tena Kujadili Kuhusu Kielelezo hicho

Na Kwa sababu Mahakama Ilisha letewa Kielelezo hicho na ikakikataa, Na Kwamba Shahidi Namba Moja Alisha letewa na Kwa ajili ya a Utambuzi haijalishi, Wakaomba Mahakama ireje Kesi mbalimbali, Theresia Zackaria Vs Oscar Ukurasa wa Nne, NBC & IMMA ADVOCATE Vs....ya Mahakama ya Rufaa

Issue ya Estoppel Kwamba waliomba Mahakama ione kwamba Upande wa Mashtaka Hauwezi Kuleta Jambo hilo Kisheria, Estoppel Asili yake ni Madai lakini iliingizwa Kwenye a kesi za Jinai, Kwa kesi ISSA TOJO Mbele ya Jaji Mkuu wa wakati huo Jaji Samata,

Alisema Kwamba Kanuni ya Estoppel Ni sehemu za Sheria zetu. Na wakasisitiza Kupitia kesi ya JULIUS MICHAEL Vs JAMHURI. Ambapo Mahakama Ilipolewa na Kufanya Maamuzi. Ambapo Mahakama ili Ombwa Kurejea Kurasa wa 6 Mpaka 9. Waliomba Mahakama Ione kwamba Swala la Upoowa

Detention Register Lilishajadiliwa na alitakiwi Kuletwa Tena Mahakamani. Lengo la Kanuni hiyo ni Kufanya Mfumo wetu wa Jinai Kuwa Mfumo uliokamilika. Na Kwamba Mshtakiwa asiitwe tena Mahakamani. Kulinda Heshima Ya Mahakama na suala la Uchumi..

Kwa Maana hiyo wakaomba Mahakama Kuona kwamba Kanuni ya Estoppel Inaizuia Kuleta tena Mahakamani, Wakaomba Mahakama is Ipokee Detention Register, Na Upande wa Mashtaka Na wao walianza kwa Kupinga, Kwamba Mapingamizi yaliyoletwa yamekosewa yametafsiriwa Vibaya

Jaji: Kwamba suala la Upokelewaji wa Kielelezo ni Vigezo Vitatu vinatumika. Vya Relevance, Competence and Materiality. Kwa Upande wa Mashtaka walisema Kwamba Shahidi alisema wazi ni wapi alipotoa Kielelezo hicho. Hata Maamuzi ya Mahakama Ya wakati huo yalihusu Shahidi Kutokujenga

Misingi na Kwamba Kielelezo Hicho akijawahi Kitamkwa Kwamba ni Incompetent. Hoja ya Pili ilikuwa ni Detention Register ilikuwa inatolewa kwa ajili ya a Utambuzi wakati sasa Kinatolewa Kwa ajili ya Kielelezo. Kuhusiana na Maamuzi ya a kesi ya OSCAR na THERESIA wamesema hawana

Shida na Maamuzi hayo na Kwamba Maamuzi hayo kwenye kesi hii ni Distinguishable. Kwamba Mahakama Iliamua Kanuni ya Funtus Officio ni Kanuni iliyokuwa Inatumika Kwenye Sheria kesi. Kama Kesi ya KAMURI Vs JAMHURI ambapo Kwa Maoni yao wanasema Mashauri hayo ya natengeneza Kanuni kwa

Jinsi gani Kanuni ya Funtus Officio inaweza Kutumika ambapo ni Mashauri yanayo kuwa yamekwishamalizika. Wakaomba turejee Kesi ya THERESIA kuwa Distinguishable. Na tukija Issue Estoppel Walikiri kwamba ni Kanuni za Sheria zetu na Wakapinga kwamba ipo tofauti Kwenye kesi hii..

Wakasema issue Estoppel Inaweza Kutumika Pale ambapo Kesi iliyopo inafanana kabisa na Kesi iliyokwisha, Kwenye Uamuzi wa Mahakama Hii wanasema ujikite katika Shahidi Kushindwa Kujenga Misingi. Na Kwamba Shauri linapswa Kufika Mwisho.. Na Kwa Shauri hili bado haijafika Mwisho

Kwamba Detention Register Ilikataliwa kwenye Shauri hili hili, Na Kwamba Sababu ya a Kukataa Detention Register Ilikuwa haijafika Mwisho na Kwamba Khakuna namna ambapo Shauri Dogo litatengenishwa na Kesi Mama. Issue Estoppel Kama Swala la Kisheria lina Kosa asifa kwa Sababu

Shauri Halikufika Mwisho. Pia haliweI Kuwepo Sababu hata Malengo ya Kwa nini ilikataliwa mara ya kwanza ni tofauti na Sasa. Na suala la Tatu kuhusiana na DISPOSAL ORDER Kama Ilivyo kuwa imesemwa na Upande wa Utetezi..

Jaji: Wamesema Kwamba Amri ya kuachia Kielelezo inatolewa baada ya Shauri Kufika Mwisho. Na Kwamba Kielelezo hakikuombwa Kurudishwa Kwa wenyewe Bali Malengo yalikuwa ni Kukirudisha Mahakamani. Kwamba Malengo yake yameandikwa kwenye Barua hiyo na Naibu Msajili

Na Kwamba wanaomba Mahakama Ione kwamba Kanuni inayohitaji Kuwepo Kwa Amri ya Kuachia Kielelezo Haiwezi Kutumika Katika Shauri hili. Kwa Mujibu wa Kesi ya KONDO GEDE Vs JAMHURI. Inaelezea kwamba Mahakama inaweza Kutumia suala la Mdomo.

Wakaomba Mahakama Ipokee Kielelezo Kwa sababu ambazo wamezieleza. Kuhusiana na Ukweli Kwamba Naibu Msajili hana Uwezo wa Kutoa Kielelezo, Shahidi ameeleza namna gani alipata Kielelezo. Wakaomba Mahakama imuamini Shahidi. Kwa sababu Shahidi anaaminika.

Uombwaji wa Kielelezo Uliombwa Kwa Makusudi Ya Kurudi Mahakamani na Siyo Kurudi kwa Mwenyewe. Kama rejea Ya Kesi ya GANDI, Mahakama itumie Sheria kesi hii. Kwamba Maombi yalikuwa ni Upokelewaji wa Kielelezo. Mahakama ijikite Katika Kanuni za Upokelewaji Wa Kielelezo ambazo ni Competence, Relevance na Materiality. Na Kwamba Maamuzi ya a Mahakama ya lisema kwamba Kielelezo kinaweza Kuna mbwa kwa Njia ya Utawala. Kwa Upande wa Utetezi walipata Muda wa Kufanya Rejoinder. Wakasema Kwamba Kesi Ndogo iliyopo katika kesi Kubwa inajitegemea Kabisa.

Jaji: Kwa Sheria na Utaratibu uliopo pale ambapo Mahakama Unahitaji Kufanya Kesi Ndogo, inaondoka Kabisa katika Kesi Kubwa. Mwenendo Wa Kesi Ndogo katika kesi kubwa ni Suala la Factual Exercise, Suala la Kutafuta ukweli. Kwamba Suala la Kuthibitisha kwamba Maelezo ya Mshtakiwa yalichukuliwa kwa Njia halalali ni Wajibu wa Upande wa Mashtaka Na Upande wa Utetezi wanao Wajibu pia.

Jambo la Tatu ni kwamba Mahakama Ilishawahi Kufanya Kesi Ndogo kwa Mshtakiwa Wa Pili. Na Kwamba Swala la Amri kama ambavyo inatajwa katika Kifungu cha 353 ni Jambo la Msingi katika Kueleza Mnyororo kama. Ulifuta Utaratibu, Wakiendelea Kueleza tofauti kati ya Kesi Ndogo katika kesi Kubwa, na wakaeleza Namna ambavyo Mashahidi wanapewa Utambulisho tofauti. Na Kwamba Kwa Sababu ni Kesi tofauti basi Waliomba Kesi tofauti.

Wakaomba Mahakama ifuatilie na Kusoma Guidelines ambayo imewekwa na Mahakama kuhusu Kushughulika na Kielelezo hicho. Mahakama isome Mwanzo hadi Mwisho Namna ya Mahakama Kushughulika na Kielelezo Hiko..

Jaji: Kwamba Quorum Ya Exhibit Register Inapaswa Amri ya Mahakama Ione Imetolewa na Imetolewa na nani. Na Kwamba Kesi ya DEGE ni Irrelevant. Upande wa Mashtaka Wameangalia Kama Jambo la Kielelezo tu lakini wao wanaangalia Admissibility. Na Kwamba Mahakama inabanwa Kuendelea Kushughulika na suala hilo kupitia Funtus officio. Issue Siyo Conclusivity ya kesi Bali hata Jambo ambalo Lipo Mbele ya Mahakama. Kesi ya Gandhi haihusiani na Kutoa Kielelezo kinyemela na Kesi hiyo ni Distinguishable.

Kwamba Kesi ya Julius Michael na wenzake ndiyo Inajielezea yenyewe, Mahakama Ione inabanwa na Maamuzi yake, Wakaendelea Kusema Hoja walizoleta kwamba Kukosekana kwa Amri ya a Mahakamani, Funtus Officio na Issue Estoppel Kwa sababu hizo Wakaomba Mahakama Ikatae Kielelezo hiko

Na Hizo ndiyo zilikuwa Hoja za pande zote mbili, Na Hoja zote zimenisaidia Kufikia Uamuzi. Siku ya tarehe 19 Mwezi wa September Wakati anatoa Ushahidi Wake Mahakamani aliomba Kutoa Ushahidi Wake Mahakamani. Aliomba Kutoa Kielelezo hicho.

Jaji: Shahidi Aliomba Kutoa Kielelezo hicho, Maombi hayo yalikuwa yamekataliwa. Na Hoja zilikuwa kwamba Shahidi Hakuwa amejenga Misingi wa Namna gani ambapo Kielelezo Kimemfikia. Na namna kilivyotunzwa.

Mahakama Ilitoa Uamuzi wa Kukubali Pingamizi na Kwamba Mahakama Uliona Kweli Shahidi Hakuwa amejenga Misingi. Na Kwamba Mahakama Uliona Kwamba Kielelezo hicho hakikikuwa kimetolewa na Utawala na Njia Nyingine za Kuleta Kielelezo

Kielelezo hicho Kilikataliwa Mahakamani. Ambapo Upande Wa Mashtaka Wakaomba Kielelezo hicho Kwa Ofisi ya naibu Msajili. Naibu Msajili aliwapatia Kielelezo hicho. Na Kwa sababu Shahidi aliomba kutoa Kielelezo Ndiyo Kikapingwa na Upande wa Utetezi.

Jaji: Hoja ya Funtus Officio inaweza Kuathiri Maamuzi ya Mahakama. Na Kwa sababu hiyo naanza na Jambo hili. Kwa sababu hii na Tizama Maamuzi na hoja zilizoletwa. Na rejea Mashauri yote yaliyoletwa Mbele Ya Mahakama.

Maamuzi ya KISOPO MEDARD dhidi ya Waziri wa Ardhi Maamuzi yanakubali kuwa Yanatumika katika Mfumo wetu wa Sheria, Mahakama Imeombwa Irejee eneo linalosomeka hivi, Kwenye Mambo ya Mwenendo Wa Mahakama Kama Maamuzi yalishajulikana basi Inazuiwa Kuyajadili tena.

Na kesi ya OSCAR RWECHUNGURA kama ambavyo nimekwisha Kusema Kwamba Mahakama Ilikuwa Inazuiwa na Kanuni hiyo ya Funtus Officio, kwa hiyo siyo Sawa Hakimu Mkazi Kukubali Kupokea suala hilo katika Mahakama ya Wilaya.

Na katika Kesi ya IMMA ADVOCATE Pia, Kesi ya MWIGURO COSMAS, Pia Kesi ya MAHURI dhidi Ya JAMHURI. Ambapo Iliamua kwamba Katika Mazingira hayo inajitokeza ni Wakati gani Hakimu anakuwa Funtus officio na hawezi Kuendelea na Shauri Mbele yake.

Jaji: Ambapo Iliamua kwamba Katika Mazingira hayo inajitokeza ni Wakati gani Hakimu anakuwa Funtus officio na hawezi Kuendelea na Shauri Mbele yake. Pia Mahakama ya Tanzania SELEMAN Vs SMZ Mahakama Ilisema Kwamba Mahakama Inakuwa Funtus Officio

Maamuzi yote haya ni nayo ya rejea ni wazi kuwa ni Mashauri ambayo imefikisha Mahakama Mwisho. Kwa Upande wa Utetezi Wamesema Siyo lazima Kesi iwe imefika Mwisho. Nakubalina nao lakini inategemea ni Jambo gani.

Jaji: Kwa sababu hiyo Mahakama hii inajiuliza kwamba Je Jambo la Kuijadili Register Ilikuwa inafikisha Mahakama Mwisho? Jibu ni Hapana.. Kielelezo Kinaweza Kutolewa Mahakamani Kwa ajili ya Utambuzi.. Na Inapotolewa kama Utambuzi basi ni tofauti inapopokelewa kwa ajili ya Ushahidi

Kielelezo kinapoitwa kwa ajili ya Utambuzi Kimakosa hadhi ya Mahakama Kutumia kama Kielelezo. Katika mazingira Mengi ambapo Mahakama Imepokea Kielelezo anapokuwa Shahidi ambaye ni Competent anakitumia.

Mahakama Inaona kwamba suala La Kutolewa Kielelezo na Shahidi Hakuwa inafikisha Mahakama Mwisho. Kwa Sheria Kesi nilizozitaja hapo Juu ili Mahakama Iwe Funtus Officio Mambo haya lazima yatimie.

Jaji: MAHAKAMA inakuwa Funtus officio Ikithibitika kwamba Jambo Lililopo Mbele ya Mahakama limesha zungumzwa na Kutolewa Maamuzi. Kwamba Jambo hilo linatakiwa liwe limeimaliza Kesi Kwa Kumkuta Mshtakiwa Ana hatia au Kuitisha Jambo lolote.

Amri hiyo ambayo inakuwa imeinyima Mahakama, inatakiwa iwe na Matokeo ya kufikisha Kesi Mwisho. Ukiangalia Kimantiki Kielelezo mbacho Kimetolewa Baada ya Kielelezo hicho Kukataliwa Kilikuwa Katika suala la Utambuzi Na kwamba Upokelewaji wake siyo Wa Mwisho basi hata Kupokelewa kwake siyo Jambo la Msingi, Hoja ya FUNTUS OFFICIO naitupilia mbali kwa Sababu nilizo eleza.

Jaji: Suala Zima La ISSUE ESTOPPEL ni sehemu ya Sheria zetu, nakubaliana na Maamuzi ya Mahakama kuu. Kwamba ilikusudi ziweze Kutumia ya Issue Estoppel Lazima Mambo haya yawepo

Pale ambapo Jambo limesha amriwa na Mahakama, Maamuzi yalifikiwa kwa manufaa ya Mshtakiwa, Kwamba Maamuzi yakifikisha Mahakama Mwisho. Kwa sababu hiyo ndiyo inatengeneza Falsafa ya Issue Estoppel.

Ni Kuhakikisha kwamba Mshtakiwa Haitwi tena, Pili Kulinda Mfumo unaotambulika katika Mfumo jinai. Kulinda Hadhi ya Taasisi na suala la Kiuchumi. Kama ambavyo imeelezwa Mwanzo. Suala la Detention Register Ilishaletwa Mahakamani na Mahakama ikaikataa.

Kwa Sababu hiyo ilikataliwa, Je Mahakama inajiuliza Je Mahakama inazuiwa? Mahakama Inazingatia Hoja zote za Utetezi na Upande wa Mashtaka. Hakuna Ubishi Kwamba suala la Detention Register Ililetwa kwa ajili ya Utambuzi na Shahidi Alishindwa Kujenga Misingi ya Kielelezo hicho.

Na Kwamba Kukataliwa kwake halikuwa imelifikisha Mwisho Shauri hilo, kama ambavyo Nimeeleza katika Sheria Kesi, Ili Mahakama Iweze Kufikia Maamuzi Ilikuona Kama Issue ya Estoppel inahusika lazima Mahakama Ione kama yanafanana, Katika Context na Substance yake.

Jaji: Katika Shauri Mbali lipo Mbele ya Mahakama hii Utolewaji wa Kielelezo hicho hata Kama Kingepokelewa Isingefika Mwisho. Kielelezo hicho Kilikuwa bado lazima kitolewe na Shahidi ambaye ni Competent. Kama Kupokelewa hakuweziKufikia Mwisho wa Shauri lake.

Mahakama Inaona kwamba Issue ya Estoppel haiwezi Kuwepo, Suala linalobakia ni Kuwepo au Kutowepo Kwa DISPOSAL ORDER. Mahakama Imeelekezwa Kutumia Kifungu cha 353 na Mwongozo wa Mahakama. Na Kwamba Mahakama Imeelekezwa Kwamba bila a Kuwepo Kwa DISPOSAL ORDER, Basi Utolewaji Wa Barua ya Naibu Msajili hakuwezi Kuhalilisha Suala hilo.. Mahakama Imezingatia Hoja zote. Mahakama Inaona kwamba zuala Zima La Upokelewaji wa Kielelezo Mahakamani, Ni Kwa Mujibu wa Sheria, Na Baada Ya Kielelezo Kupokelewa inabaki kuwa Chini ya Mahakama

Jaji: Imeelezwa Vizuri Kwenye Mwongozo wa Mahakama, Mahakama Imefuata kifungu 353(3) kinasema Kwamba Bila Kuathiri Kifungu cha Kwanza nza, Mahakama ikiona Inafaa, Kitu ambacho Kimetolewa Mahakamani kitolewe Na Kurudishwa Mahakamani Kwa Ushahidi.

Kwa Masharti itakayokuwa imeweka. Ni wazi Kwamba Kumbe Kielelezo Kinapokuwa Christmas ni ya Mahakama, Kwamba pale Kielelezo Kinapokuwa Kinatoa Kinapswa Kitolewa kwa Amri ya Mahakama, Nakubaliana na Upande wa Utetezi, Na Kwamba Mahakama inapokiwa imekipokea Kielelezo hicho haihusiki na Kutunza Kielelezo hicho, Ni Jukumu la Hakimu Mfawidhi na Naibu Msajili. Mwongozo Unasema Kwamba watamteua atakaye tunza. Kanuni inampa Naibu Msajili na Hakimu Mfawidhi Uwezo wa Kudhibiti Vielelezo.

Jaji: Kwamba Naibu Msajili ana jukumu ya Kukagua Register ya Vielelezo. Kwa kusudi la Kujiridhisha, Lakini Suala la Kutoa Kielelezo Mahakamani, Sura ya Nne inasema Kwamba Utoaji wa Vielelezo Unafanyika Mwisho Baada ya Shauri Kufika au Rufaa Kukata Katika Shauri hilo

Kama Mwenendo wa Jinai Unavyosema, Ni Msimamo Wa Sheria Kama ambavyo Mahakama Iliamua Katika kesi ya SIAYO, Vielelezo vinatakiwa Vitoke ambapoa Shauri LIMEFIKA Mwisho, Kwamba KATIKA MWONGOZO sehemu Ya Nne inasema Kwamba

Pamoja na Kanuni hiyo Kielelezo Kinaweza Kutoka Mapema Wakati Shauri linaendelea, Kama ambavyo Kifungu cha 353(1), Kwamba Mahakama itatoa Amri ya Kuachiwa kwa Kielelezo, Mpaka Pale Mahakama Itakapokuwa unahitaji Kielelezo hicho.

Mahakama inaweza Kutoa Amri ya Kutoa Kielelezo Pale ambapo Shauri LIMEFIKA Mwisho au Rufaa imefika Mwisho. Mahakama Katika Amri yake inayohusu Disposal Order inahusu Kama Kielelezo Kurudi kwa Mwenyewe, Kielelezo Kiharibiwe, Au Kurudi Serikalini

Jaji: Mahakama U+itasema kwamba ni Kielelezo Gani kiharibiwe Kila Mwisho Mwezi,, Na Mwisho ni kwamba pale ambapo Kielelezo Kinatakiwa kuharibiwa Notisi utolewe Siku 30 kabla kwa Mshtakiwa, Ofisi ya Upelelezi, ofisi ya Mwanasheria. Hiyo ndiyo namna Kielelezo Kinapswa Kitolewe

Mahakama hii inakubaliana na Upande Wa Utetezi kwamba Naibu Msajili hana Mamlaka ya Kutoa Kielelezo, Mamlaka yake ni Kusimamia pale Kielelezo Kinapokuwa Kwenye Chumba Cha Kielelezo. Kusimamia Utolewaji au Kuharibiwa kwa Kielelezo hicho.

Jaji: Kwa namna hiyo basi ni Kweli Kwamba Kielelezo hakiwezi Kutolewa pasipo Amri ya Mahakama. Hata hivyo Mahakama inatakiwa Ijielekeze Katika Sheria Kesi hiyo. Mahakama inatakiwa Kusema Kwamba Kielelezo Kurudi Kwa Mwenyewe, au Kiharibiwe, au Kurudishwa Serikalini

Mahakama haina Mamlaka ya Kutolea Amri nje ya Kazi hizo Juu. Barua ilivyoandikwa Kwa Naibu Msajili Haikuwa imeeleza Mambo hayo hapo Juu. Mahakama Ina maoni kwamba halikuwa Muafaka kwa Kutolea Amri ya kuteketeza

Lakini Naibu Msajili ametajwa Kwamba ana uwezo wa Kutunza Kielelezo, Na Kwamba Kielelezo Kinacho takiwa kwa kesi zaidi ya Moja au Mahakama Moja, Mahakama zaidi ya Moja. Kutokana na hali hiyo basi ni wazi Siyo Kila wakati Kwamba Kila Wakati Kielelezo Kinapokuwa Kutumika Kinatakiwa

Kiwe na Amri ya Mahakama, Kwamba Kinaweza Kutumika Kwa Kesi au Mahakama Zaidi ya moja bila Amri ya Mahakama, Kwamba Naibu Msajili atakuwa ananoti kwenye Register yake Movement ya Kielelezo hicho, KIELELEZO SIYO LAZIMA PAWE NA AMRI YA MAHAKAMA.

Jaji: Nimeona Kwamba Siyo lazima Kielelezo hicho kuwa na Amri ya Mahakamani, Kwa sababu hiyo naitupilia Mbali Sababu zote tatu za Mapingamizi ya Kuzuia Kielelezo hicho, NATOA AMRI

Mawakili wa pande zote mbili Wanasimama na Kukaa

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Kufuatilia Maamuzi ya Mahakama naomba Sasa Shahidi aruhusiwe Kuendelea Kutoa Ushahidi Wake

Jaji: Upande wa Utetezi Kuna Hoja yoyote

Kibatala: Hakuna, Endelea

Jaji: Kwa Mujibu wa Utaratibu Kielelezo Kinatakiwa Kisomwe

Wakili wa Serikali: tunaomba sasa tupewe P2 ilishahidi aweze Kusoma

Jaji: Tunaomba Shahidi asome Maeneo ambayo ni Relevant tu

Mallya: Sawa tu

Wakili wa Serikali: Ushahidi wako umesema tarehe 07 August 2020 ulipokea Watuhumiwa walioletwa na Kingai na ACP jumanne, Twende Kwenye eneo ulilowaingiza na utusomee

Shahidi: amemaliza kukifafanua Kitabu cha Mahabusu

Wakili wa Serikali: Mtu huyu aliyetolewa alirejea Saa ngapi

Shahidi: Saa 5 na Dakika 6

Wakili wa Serikali: anaonekana namba Ngapi

Shahidi: Namba 401

Wakili wa Serikali: Wakati anaingia hii mara ya Pili, Alikuwa na Hali gani

Shahidi: Physical Condition ni Good

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuingia Tarehe 07 August 2020 saa Tano, ni lini tena alitoka

Shahidi: alitoka tena Tarehe 08 August 2020, Majira ya Sa 4 na Dakika 05 Asubuhi

Wakili wa Serikali: nani alimtoa

Shahidi: Inspector Mahita

Wakili wa Serikali: Sababu za Kumtoa

Shahidi: Nje kwa Upelelezi

Wakili wa Serikali: Mtu Mwingine uliyepokea ni nani

Shahidi: Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: anasema Entry namba Ngapi

Shahidi: 393

Wakili wa Serikali: aliingizwa Saa ngapi

Shahidi: 07 August 2020, Saa 12 na Dakika 9

Wakili wa Serikali: baada ya kumuingiza ni lini alitoka tena

Shahidi: 07 August 2020 Saa 11 na Dakika 11

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Kitabu kuna Entry ya Lesheni

Shahidi: Leseni Supply anatakiwa apewe Asubuhi Mchana na jioni, Kwa Mujibu wa Kitabu Mtuhumiwa amepewa Chakula Asubuhi, Mchana na Jioni

Wakili wa Serikali: Taarifa za Kwenye Kitabu ni za Kituo gani Shahidi Taarifa za Central Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Watu hao uliowapokea hapa Mahakamani Wapo?

Shahidi: Wapo kwenye Kizimba cha Washtakiwa

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama yupi ni yupi

Shahidi: hawa wawili wa Kati kati, Wapili kutoka Kulia ni Adam na huyu Mwingine ni Mohammed Abdilah Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Uliwapokea wapi

Shahidi: Dar es Salaam, Central

Wakili wa Serikali: Lini

Shahidi: Tarehe 07 August 2020

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna Serikali swali lingine kwa Shahidi, Tumemaliza Examination In-chief

Nashon Nkungu: Shahidi Unafahamu Kwamba Washtakiwa Wanasema hawajawahi Kuonana na wewe na hawajawahi Kufika Central Da es Salaam?

Shahidi: Sifahamu Kama Wanasema hivyo

Nashon: Unafahamu kuhusu Station Diary

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: na ni Duty ya CRO

Shahidi: Sahihi

Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba Kupatiwa Exhibit P2

Nashon: ni Sahihi Kabisa kwamba Askari anayekuja na anayetoka lazima wasainishane kwenye Station Diary

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: ni sahihi Kwamba inatajwa kwamba Nimemkabidhi, pamoja na Silaha na Majina ya Mahabusu

Shahidi: Nafahamu kwamba nitakwa la Kisheria

Nashon: na Kutaja Watuhumiwa na mali

Shahidi: Kwenye suala la Watuhumiwa sijafahamu

Nashon: uoni kwamba Station Diary Ingekuwa ya Muhimu Kuwepo Mahakamani

Shahidi: Siyo ya Umuhimu

Nashon: Pale Kituo cha Central Police Dar es Salaam, palikuwa na Askari Wengine wakati Wakina Kingai wanatoka MOSHI

Shahidi: Ndiyo palikuwa na Askari Wengine

Nashon: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Katika Askari Waliokuwepo Kituoni Hapakuwa na Askari Wengine ambao wangewachukua Maelezo Watuhumiwa?

Shahidi: Sikusema

Nashon: Je ulipata Kufahamu kama Kuna Ndugu au Wakili Waliokwepo wakati wanachukuliwa Maelezo

Shahidi: Hapana

Nashon: Je, kuna Ndugu au Mawakili walikuja kuwatembelea Washitakiwa

Shahidi: Hakuna

Mallya: Kwamba Kwa Madai yako ulikuwa Central Siku ya 07 August 2020

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwamba Wakati huo ulikuwa umefanya Kazi kwa Muda gani

Shahidi: Mwaka 2014 Mpaka 2020

Mallya: Pale CRO Ulikaa mara ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Mallya: Kwa hiyo Ulishawahi Kufanya Kazi za General Duties Mara kadhaa

Shahidi: Sahihi

Mallya: Kwa huo Mwezi wa Saba pia Ulikaa pale CRO

Shahidi: Ndiyo, lakini Sikumbuki Mara ngapi

Mallya: Umesema Ushawahi Kufanya kazi Central, Nitafuti e Sehemu Nyingine Kwenye hicho Kitabu ambapo ukishawahi Kufanya Majukumu hayo

Shahidi: Tarehe 02 August 2020

Mallya: Mheshimiwa Jaji Utaangalia Wakati Unafanya Uamuzi Kwenye Serial Namba 184

Mallya: Wakati Unaandika wakati wa Kumtoa Mtu, Sababu inakuwa kweli au lah

Shahidi: Wakati amemtoa

Mallya: interest yangu Entry inayomuhusu Mshitakiwa Wa Pili, Wakati anamtoa aliandika nini

Shahidi: Nje kwa Upelelezi

Mallya: Jumanne anasema kwamba alimtoa Kwa sababu ya mahojiano, we umeandika sababu ya upelelezi

Shahidi: Ndiyo mahojiano ni sehemu ya upelelezi Mallya Kwa hiyo ni kitu kimoja, hicho

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Soma hapa na hapa..

Shahidi: NJE KWA UPELELEZI, NJE KWA MAHOJIANO

Mallya: Sasa ni kitu Kimoja

Shahidi: Hapana, Upelelezi ni Broad na Mahojiano ni Specific

Mallya: Kwa Uelewa kwako Wewe Maana yake nini

Shahidi: Mchakato unaotumika Kuanzia Kesi Imefunguliwa Mpaka Pale inapofikishwa Mahakamani

Mallya: Walikwambia Wanawatoa kwa Jambo gani

Shahidi: Mmoja kwa ajili ya Upelelezi na Mmoja kwa ajili ya Mahojiano

Mallya: aliyemtoa Mshitakiwa wa 3 ni nani

Shahidi: Inspector Mahita

Wakili wa Serikali: OBJECTION Kuhusu Utaratibu, unampomhoji Mtu, Basi Inukuliwe Maneno sahihi, Wakili azuiliwe Kuweka Maneno kwa Shahidi ambaye hayupo huku

Kibatala: OBJECTION tulishawahi Kuweka Utaratibu humu kwamba Objection itafanyika kwa Majibu siyo Maswali

Jaji: Una Kifungu cha Sheria Kinacho Kataza hilo

Wakili wa Serikali: naomba Dakika 1

Wakili wa Serikali: Sijakipata Kifungu Moja kwa Moja ila Mheshimiwa Jaji unapokuwa unamuhoji Shahidi Kwamba Fulani Alishasema kifu fulani hairuhusiwi na wewe unajua hilo

Jaji: Kanuni za cross Examination inasemaje

Mallya: Maswali ambayo yanamdhalilisha Shahidi, Maswali anayoulizwa Shahidi hapa hayamlengi Shahidi

Mallya: Sababu alizomtoa Mtuhumiwa Mahabus Central Ni pamoja na Kwenda Kumpiga

Shahidi: Hapana kwa ajili ya Upelelezi

Mallya: Ulikutwa na Diary hapa Mahakamani, na Jaji akasema wewe ni VIOLATOR

Shahidi: Mheshimiwa Jaji, Entry Namba 396 sababu ya Kumtoa, Tarehe na Muda na Mtu aliyemtoa Mtuhumiwa no. Tofauti na Kalamu iliyotumika au Mwandiko wangu uliotumika Kumuingiza Mtuhumiwa.

Mallya: Ulipata Kueleza Mahakamani?

Shahidi: Hapana

Mallya: Vifupi Vya Maneno kwenye Detention Register Mnaandika wenyewe au Ni kwa Mujibu wa Sheria

Shahidi: Mujibu wa PGO

Mallya: Ngoja nikuonyeshe PGO, naona DAR ES SALAAM kwamba CDS ni nini.

Shahidi: Inawekezakana ni Chuo Cha Polisi

Mallya: nakuonyesha Vituo Vya Polisi Vyote Tanzania na Vifupi Vyake Nionyeshe Walipo andika CENTRAL ni CDS

Shahidi: Anakodoa kwa Muda mrefu..

Mallya: nimetafuta sijaona, Sijui kama utapata Muda wa Kutosha

Shahidi: Mimi sijaona humu

Mallya: Sasa sisi ili tuamini kwamba hiki kitabu kitoke DSM Polisi Central tulitaka tuone kiandikwe ni POLICE CENTRAL DAR ES SALAAM au Kifupi Chake, Kwa Sababu kuna Kimoja Hakipo Sahihi

Shahidi: Detention Register ipo sahihi

Mallya: mie nataka nijue Kipi Hakipo Sahihi

Jaji: sasa katika ya PGO na DETENTION REGISTER kipi Kipo sahihi

Shahidi: siwezi Kusema Kwamba PGO Haipo sahihi

Jaji: Swali ni Kwamba Kipi hakiko sahihi

Shahidi: Hakuna ambacho Hakipo Sahihi

Mallya: Sasa Kuna Diary yako ulikamatwa nayo Mahakamani

Shahidi: sijakamatwa nayo

Shahidi: Niliandika Siku ya Kwanza kuja Kutoa Ushahidi Tarehe 20 September

Jaji: Ndiyo Siku uliyoandika

Shahidi: Hapana Kabla ya Siku ya Kuja Kutoa Ushahidi

Mallya: Kwa Uwezo wa Pale Central na rasilimali zake Ukoje

Shahidi: Hayo sasa Watakuwa Kuzungumzia watu wa Utawala

Mallya: Kwa Ufahamu Wako wewe Ukishawa Kuishiwa Karatasi Pale Central za Kuandikia Maelezo

Shahidi: Hapana

Dickson Matata: Nitakuhoji Maswali Machache Kutokana Maelezo uliyoyatoa Hapa Mahakamani, Kutokana ana Wateja wetu Kupinga kwamba hawakuwa hi Kuandika Maelezo na hawajawahi Kufika Central Dar es Salaam. ulisema Kituo chako Cha Kwanza Kuanza Kazi ni wapi

Shahidi: Msimbazi

Matata: Msimbazi ipo wapi

Shahidi: Wilaya ya Kipolisi Kariakoo

Matata: Kuna sehemu yoyote ulitaja Kiongozi uliyewahi Kufanya naye kazi Pale Msimbazi

Shahidi: Sijazungumzia

Matata: Ukiachana na Kutaja Majina yako na Force Namba zako, Kuna Ushahidi wowote Umeonyesha kwamba Uliwahi Kufanya kazi Central Police Dar es Salaam

Shahidi: Ndiyo nimeleta Detention Register Yenye Muandiko wangu Mimi

Matata: Kuna Kitu chochote umeleta Mahakamani mabpo kwa Kuangalia DR tunaweza Kusema huu ni Mwandiko wako

Shahidi: Kimya

Matata: twende sasa Kwenye DR, Mheshimiwa Jaji namuonyesha Kuanzia Entry namba 393

Matata: Nenda tarehe Saba, Kuna Sahihi yako hapo Kwenye hizo Entry?

Shahidi: Hakuna

Matata: Kuna sehemu Yoyote yenye Force Namba yako hapo?

Shahidi: Hakuna

Matata: nikisema Mtu yoyote anaweza Kuandika, kilichoandikwa hapa nitakuwa nakosea

Shahidi: utakuwa unakosea

Matata: Kuna Kitu Kingine chochote kinachoonyesha kwamba Detention Register Imetoka Polisi Central Dar es Salaam Na siyo Mbweni

Shahidi: Kitu Pekee ni hiyo CD

Matata: ni sahihi Kwamba Mwaka huu Ndiyo umeanza Kufanya kazi Oysterbay Polisi

Shahidi: Ndiyo Mwaka huu

Matata: Pale Central Mmesema Mnatumia CD. Je, Oysterbay Mnatumia nini?

Shahidi: OB

Matata: hiyo OB inatoka inatokana na nini

Matata: PGO namba 05 ndiyo inazungumzia Vifupisho Vya Vituo Vya Polisi. Hebu Soma haoa

Shahidi: Oysterbay Inasema ni OYB

Matata: Kuna Kitabu au Mwongozo Umekuja nao hapa Unaonyesha Oysterbay ni OB na siyo OYB?

Shahidi: Hapana

Shahidi: Kimya

Kibatala: ile Diary Uliyo kuwa nayo Kwenye Kizimba, sehemu Mahususi ambazo zinahusika na Kesi hii zimeingia Kama Kielelezo Cha Mahakama namba 1

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Siku hiyo ulikuwa wapi

Shahidi: Sikumbuki nilikuwa wapi

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Vitu vilivyochukuliwa kwenye Diary Yako vinahusiana na Kesi hii na Ushahidi wako Shahidi: Ndiyo Vinahusiana

Kibatala: na Unafahamu Kwamba Mahakama Imechukua Kurasa Kwenye Diary Yako Kabla ya wewe Kuja Kutoa Ushahidi Leo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Ulifafanua kwa Jaji Wakati wa Kuongozwa na Wakili wa Serikali Kwamba Kuna Kidhibiti namba Moja Mule Kuna 1,2,3 na Maana yake ni nini

Shahidi: sijafafanua

Kibatala: kwa sababu hujafafanua, Je unafahamu Kwamba ulifafanua wakati wa Re Examination

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Basi Kama hufahamu, mkijaribu tutasimama

Kibatala: Shika Kielelezo namba P1 Muonyeshe Mheshimiwa Jaji, Ni wapi Pameandikwa CENTRAL POLICE STATION DAR ES SALAAM

Shahidi: Hakuna

Kibatala: kwa hiyo ili Mahakama iijue Kwamba Kielelezo hiki Ni Cha Central lazima iingie Kwenye Details za Ndani

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mojawapo ya Vifaa kazi Vya Utambuzi ni PGO

Shahidi: Ndiyo PGO

Kibatala: Kingine kipi

Shahidi: miongozo ya Jeshi la Polisi huwa Inatolewa

Kibatala: Ni lini umefahamu Kwamba Unakuja Kutoa Ushahidi wa Kesi Ndogo ya Mohammed Ling'wenya

Shahidi: Sikumbuki Tarehe, ila kama Siku 13 Nyuma

Kibatala: Toka unapokea Summons, ni lini Ulifanya Maandalizi ya Kuleta Muongozo

Shahidi: sijaleta Muongozo

Kibatala: Kuna Mtu yoyote alikuzuia kuleta

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kingine ni Kitu gani

Shahidi: Police auxiliary Act

Kibatala: Kifungu gani

Shahidi: Kimya

Kibatala: Katika Kielelezo P1 hapo Katikakati ni nini hicho

Shahidi: Mheshimiwa Jaji ni pini iliyodondokea kwa Bahati Mbaya katika Ukurasa unaowahusu Washtakiwa hawa

Kibatala: Ulifafanua kuhusu hiyo pini

Shahidi: SiKufafanua

Kibatala: hiyo tarehe 07 August 2020 ulipokea Zamu kutoka kwa nani na nani

Shahidi: aliyepokea Zamu ni Afande Fatuma

Kibatala: Kwahiyo wewe humfahamu hata Askari Mmoja kati ya wale uliowapokea

Shahidi: Siwakumbuki

Kibatala: Ulipotoka Duty uliwakabidhi Askari nani na nani

Shahidi: aliwakabidhi Afande Fatuma, miye siwajui

Kibatala: Imakama Maana yake nini

Shahidi: Miye sikumbuki

Kibatala: Kuna Mpango Kazi Unaonyesha Askari Fulani anakaa wapi na nani anaenda wapi

Shahidi: Ndiyo upo

Kibatala: na wewe Mpaka Unakuja Kutoa Ushahidi, hujaleta sehemu ya Mpango kazi

Shahidi: Kimya

Kibatala: Unamfahamu Mtu anaitwa Lembrus Mchome

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: anasema Kwamba Mwaka Jana Mwezi wa Tano Ulimpokea Oysterbay Polisi Ukiwa CRO

Shahidi: Simkumbuki

Kibatala: ana sababu gani za kukusingizia

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: hiyo Siku ya tare 07 August 2020, Wakati Unampokea Mohammed Abdilah Ling'wenya alikuwa na Karatasi yoyote

Shahidi: Sikumkuta na Chochote

Kibatala: Wakati Unaongozwa ulipata Kuzungumzia Kuhusu Seizure Certificate

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Je Exhibit zinatunzwa wapi kama Mtu akikutwa navyo

Shahidi: Kwa Mtunza Vielelezo

Kibatala: Walikuongoza Kuzungumzia Kuhusu Vielelezo vya Mohammed Ling'wenya

Shahidi: Kimya

Kibatala: Mtunza Vielelezo anaitwa nani

Shahidi: Sikumbuki ni Siku Nyingi sana

Kibatala: ulisema Mohammed Ling'wenya alichukuliwa Maelezo Kwenye Ofisi ya OCS, umesema kwa Jaji nani alifungua Mlango

Shahidi: Sikusema Kibatala: Ulimweleza Jaji Kuwa OCS alikuwepo wapi

Shahidi: Sikusema

Kibatala: nani alikuwa Custodian wa Detention Register

Shahidi: mimi

Kibatala: Wakati unasema Ulimsindikiza ASP Jumanne, ulisema Detention Register Ulimuachia nani

Shahidi:

Kibatala:
Kuna sehemu nilisikia Unasema Ulitambua Barua ya Naibu Msajili kwa Sababu ya Sahihi yake, we Unaifahamu Sahihi ya Naibu Msajili?

Shahidi: Siyo Familiar Sana

Kibatala: Wakati Barua hii inasainiwa ulikuwepo

Shahidi: Sikuwepo

Kibatala: Wakati Mnapeana Barua hii Sisi tulishirikishwa?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji sehemu gani katika hii Barua umesaini Kwamba Ulipokea wewe

Shahidi: sijasaini

Kibatala: nilisikia Kuna sehemu Walikusainisha Je Umekuja na hicho Kitabu Ulichosaini

Shahidi: Hapana

Kibatala: Soma hii Barua ilivyoandikwa Kwa naibu Msajili, Kuna Jina lako

Shahidi: Hapana

Kibatala: Sasa Naibu Msajili alijuaje wewe unahitaji Kielelezo

Shahidi: Sijui yeye

Kibatala: Soma kwenye Barua Mlipeana Kielelezo gani

Shahidi: TP 1

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kwa Mujibu wa Jaji Mkuu, Vielelezo Vyote vinatakiwa kuanza na P na siyo TP

Kibatala: Unajua kwa nini tulipinga hii Barua Kupokelewa

Kibatala: tulipinga Mahakama Kuitwa kama Shahidi Kibatala: kwa Ruhusa Ya Mahakama, kesi Inayomuhusu Mohammed Ling'wenya, alitolewa Nje kwa nini

Shahidi: Kwa Upelelezi

Kibatala: Eleza Sasa ni Wapi ulifafanua kwamba Nje kwa Upelelezi ina Manisha nini

Shahidi: Sikumbuki

Shahidi: Kimya

Kibatala: Nje kwa Upelelezi na Nje kwa Mahojiano ni sawa

Shahidi: Hazifanani lakini ni Kitu Kimoja

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kidhibiti Kinatakiwa kijielezee chenyewe

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Kuna PPR namba, Mueleze Mheshimiwa Jaji Maana yake nini

Shahidi: Kimya

Kibatala: Je Nakala ya Ling'wenya Ya Seizure Certificate for na fall Kwenye PPR namba

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ulitoa Ufafanuzi hapa Kwenye Kitabu Kuna DASH Kwenye PPR namba

Shahidi: Ndiyo ipo

Kibatala: Ulitoa Ufafanuzi Kwa Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba hii Detention Register inaishia lini

Shahidi: Tarehe 12 August

Kibatala: Kama Mke wa Ling'wenya alikuja Polisi Central Station alikuja Polisi Station, kwa Kitabu hiki angeambiwa yupo wapi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: kama Mke wa Ling'wenya Alikuja Central na haukumuona kwenye Daftari itakuwa nini?

Shahidi: Sijui

Kibatala: Nimesikia Kwamba Mnaulizana na Mallya kuhusu Mwandiko. Je, Ulitoa Kitu Kingine Chenye Mwandiko wako tuweze Kulinganisha?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Physical Condition ni sawa na Health Conditions?

Shahidi: ni Tofauti

Kibatala: Wakati unaweka Entry za Ling'wenya Kingai na Timu yake walikuwepo

Shahidi: Kingai alikuwa mbali ila timu yake walikuwepo

Kibatala: ulifanya Upekuzi Maungoni kwa Ling'wenya

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Nani alikwepo

Shahidi: Afande Fatuma

Kibatala: Kwa hiyo ni Ushahidi Wako Kwamba Ulifanya Upekuzi Wako Mbele ya Afande Fatuma

Shahidi: Ndiyo Nilifanya

Kibatala: Shahidi wako Mwingine ni nani

Shahidi: TIMU nzima iliyokuwa CRO

Kibatala: Majina ya Ling'wenya uliyapata Kutoka kwa nani

Shahidi: Kwa wao wenyewe

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kulikuwa na Alternative Facilities za Kuwasiliana na ndugu zake Ling'wenya?

Shahidi: Hapa Sijamwambia

Kibatala: Unaifahamu station Diary

Shahidi: Ndiyo PF 51

Kibatala: Umetoa hapa Mahakamani

Shahidi: Sijaja na Station Diary

Kibatala: ulitaja kwa Mheshimiwa Jaji Kwamba nani alikupa DR

Shahidi: Sikutaja

Kibatala: Ulitaja Mtu aliyekupa

Shahidi: Sikutaja

Kibatala: Kwani hii ni Mali yako au Mali ya Jeshi la Polisi

Shahidi: Mali ya Jeshi la Police

Kibatala: Entry ya Ling'wenya Ipo wapi

Shahidi: 392

Kibatala: Na Imeacha Kutumika lini

Shahidi: 12 August 2020

Kibatala: Fungua Entry namba 208.. Tarehe ngapi?

Shahidi: hapasomeki

Kibatala: Mie nakwambia Mwaka 2021

Shahidi: Hapana Hapasomeki

Kibatala: Miye na kwambia Mwaka 2021

Shahidi: Hapana Hapasomeki

Kibatala: Fungua tena Entry 114

Shahidi: 30 July 2021

Kibatala: Entry 113

Shahidi: Haisomeki

Kibatala: Fungua Entry namba 156, 03 August 2021

Kibatala: Unafahamu Kwamba hiki Kielelezo kinapimwa pia Kwa Uongo wake

Kibatala: Nakuonyesha Entry inayomuhusu Ling'wenya, Aliingia Saa 06:07hrs, Wakati anatoka 08:10, kuna au hakuna Hours?

Shahidi: Hakuna Hours

Kibatala: wakati Unaongozwa na Hila ulifafanua Shahidi Sikumbuki

Kibatala: Katika Entry ya Ling'wenya Kuna Dole Gumba, Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama Ulifafanua Kuwa Dole Gumba la Nani

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Mheshimiwa Jaji sina swali lingine naomba Kurudisha Kielelezo namba P2

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Tumekaa Mfukilizo tangu Asubuhi, Ikikupendeza tunaomba tupate Health Break Jaji Utetezi

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Sisi tunapinga, Tunapinga Tunahisi Muda huo utatumika Kumfundisha majibu Shahidi

Wakili wa Serikali: Hoja iliyotumika ni tuhuma Jaji: kasema ana wasiwasi tu

Wakili wa Serikali: Basi tunaomba tupate Health Break

Jaji: Wote tulikwepo humu ndani na Hasa Mimi, mimi napata Ugumu kumfungia Sehemu asifundishwe Majibu

Mallya: tusaidie, najitolea Kukaa naye na nitakula naye

Jaji: basi naelekeza Hilla, Mallya na Shahidi Mkae pamoja

Mallya: Pius Hilla tujawahi Kula pamoja

Jaji: basi Leo Mtakula pamoja kwa Amri ya Mahakama

Jaji: na Kama Watachukua Nusu saa basi Break iwe lisaa lizima

Jaji anatoka

Jaji amerejea

Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji, uwakilishi Upande wa Jamhuri Una marekebisho Kidogo

Tungeomba Mahakama Iridhie Kuwaingiza Kwenye Quorum Wakili wa Serikali Robert Kidando na Wakili wa Serikali Abdallah Chavula, Wengine tupo Kama tulivyo kuwa awali..

Wakili Peter Kibatala: Kwa Upande wa Utetezi Quorum ipo kama tulivyo kuwa awali na tupo tayari Kuendelea

Wakili wa Serikali, Pius Hilla: Shahidi Sasa Nitakuuliza Maswali Kwa ajili ya Ufafanuzi Kufuatiwa na yale waliyokuuliza Mawakili Wasomi

Wakili wa Serikali: Umeulizwa Kwamba Washitakiwa Wakana Kwamba Hawajafikishwa Central hebu fafanua hufahamu nini

Shahidi: sikuwa nafahamu kama, Lakini Mimi ndiye niliyewapokea na Nikawa Detain.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kuwa Supplied na Kielelezo Cha Mahakama.

Wakili wa Serikali: Shahidi Uliulizwa Swali hukusiana na hawa Watuhumiwa Kutolewa Nje, Kwa Mahojiano na Kwa Upelelezi, Ifafanulie Mahakama

Uliposema Kwamba Mahojiano ni sehemu ya Upelelezi

Shahidi: Upelelezi Unajumuisha Kuwa Mtuhumiwa alitolewa atahojiwa, atarekodiwa naninavyo fahamu Mimi Mahojiano ni pale Mtuhumiwa anapotolewa Nje Specific kwa kwenda Kuhojiwa

Wakili wa Serikali: Ukasema Kwa Kusoma Kuna Utofauti, Je Utofauti wake nini

Shahidi: Kwamba Mahojiano ni tofauti na Upelelezi lakini Mahojiano ni Sehemu ya Upelelezi

Wakili wa Serikali: Kuna Swali Mallya alikuuliza Kwamba Mahita aliwatoa watuhumiwa kwenda Kuwapiga, Ukasema Siyo Kweli, Je Ulimaanisha nini

Shahidi: Kwa sababu Afande Mahita hakumtoa Kwa Sababu ya Kumpiga na Kupiga siyo Sehemu ya Upelelezi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Maswali Mengi Mengi Kuhusiana na Abbreviation CDS na CD ukaonyeshwa na PGO Ukasema DR haina Makosa na PGO haina Makosa, Je Kule Central CD ni Kifupisho cha Neno gani

Shahidi: CD Kifupisho cha CENTRAL DAR ES SALAAM, haipatikani Kwenye Kifupisho cha Kituo chochote pale Tanzania Nzima WS: Uliulizwa pia Kuwa Kituo chako Cha Kazi Msimbazi na pia Kitu gani Kinathibitishwa Kwamba Ulifanya Central

Shahidi: Kwa hapa ni D. R ambayo Kifupisho chake uwezi kukioata Sehemu Yoyote Tanzania na Kwamba Mimi ndiye niliyejaza

Wakili wa Serikali: Ulionyeshwa Specific Kwenye Entry namba 393 Ukasema Hakuna Sahihi yangu wala Jina langu, Je Ni kitu gani Kitaonyesha wewe Umewahi Kufanya kazi Central

Shahidi: Entry Inaonyesha Mtuhumiwa alichukuliwa na Afande Kingai

Wakili wa Serikali: Nini Kinaonyesha Kwamba Ulikwepo Siku Ile

Shahidi: Uwepo Wa Mwandiko wangu

Wakili wa Serikali: Kwenye swali hilohilo Ujafafanua Kwamba Siyo Mtu yoyote anaweza a kuandika hicho kitabu

Shahidi: Siyo watu wote waweza...

Wakili wa Serikali: Jikite kwenye Entry namba 393

Shahidi: Siyo Mtu yoyote anaweza Kupata namba ya Kesi, Kupata details za Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali hapa kuhusiana na PIN kukutwa Katikati, Ukajibu kwamba HAIKWEPO. Ifafanulie Mahakama haikwepo Wakati gani

Shahidi: Wakati natoa Ushahidi Mara ya kwanza

Kibatala: OBJECTION swali lilikuwa alifafanua au hakufafanua..

Wakili wa Serikali: PIUS HILLA Mheshimiwa Jajiiye nilisikia Jibu la Pin haikwepo na Nataka Kufafanua

Jaji: alitoa hilo Jibu lakini wakili akasema halitaki

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Ukasema Huku fafanua, kwakuwa PIN ndiyo Umeonyeshwa Ieleze Mahakama ni Pin ya namna gani

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Ni Kipande cha Pin ipo Katikati katika Ukurasa WA Mohammed Ling'wenya, Ndiyo Maana Nika fafanua haikuwepo.. Mheshimiwa Jaji naomba Kupewa P1, (Barua).. Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha shahidi

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa hiyo Barua ni Kitu gani unaitambua

Shahidi: nilikuwa namkabidhi wa Detention Register

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Shahidi Ulicho kuwa unakabidhiwa kwa Mujibu wa hiyo Barua ni Kitu gani

Shahidi: Detention Register

Wakili wa Serikali: Lipo swali lingine Uliulizwa Kuhusiana na Physical Condition Na Ukasema Hakuna Entry ya Health Condition, Ukasema Kwenye D. R hakuna Sehemu ya Health Conditions ulikuwa unamaanisha nini

Shahidi: sehemu tuliokuwa tunatumia Physical condition Kuandika kwenye Detention Register

Wakili wa Serikali: aliuliza wakili kwamba Mtu aliye kutishia akiwepo atakuwa na hofu

Shahidi: Ndiyo aliuliza kwamba Mtu aliye kutishia akiwepo Tishio Kinaendelea? Nikajibu ndiyo

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu D. R Ukasema DR ni Mali ya Polisi, Ulimwambia kuwa Unamanisha nini

Shahidi: Nilienda Kumuomba Mkuu wa Kituo, Kwamba Natakiwa kutoa Ushahidi, akanisainisha kwenye Station Diary

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Hatuna Maswali

Jaji: Shahidi Nakushukuru Kwa Ushahidi Wak

Jaji: Kuna Shahidi Mwingine?

Wakili wa Serikali: Pius Hilla Kwa Leo Hatuna Shahidi Mheshimiwa Jaji, ambaye yupo tayari Kuingia Kwenye Kizimba cha Ushahidi, Tunaomba Usikilizwaji uhairishwe kwa Leo hadi Kesho Tarehe 23 November 2021 ambapo tutaleta Shahidi Mwingine

Jaji: Utetezi

Kibatala: hatuna pingamizi Mhe. Jaji ukizingatia na muda

Jaji: Kufuatia maombi ya hairisho Mahakama inahairisha mpaka kesho saa 3 asubuhi, upande wa mashtaka wanaelekezwa kuleta mashahidi, watuhumiwa wataendelea Kuwa chini ya magereza mpaka kesho asubuhi saa 3 Jaji anatoka
 
Jaji: Nimeona Kwamba Siyo lazima Kielelezo hicho kuwa na Amri ya Mahakamani, Kwa sababu hiyo naitupilia Mbali Sababu zote tatu za Mapingamizi ya Kuzuia Kielelezo hicho, NATOA AMRI
sawa muheshimiwa Jaji, kazi iendelee !!
 
Mapingamizi yote matatu Jaji Taganga kayakataa.

Kasema, eti kielelezo kilichopo chini ya mahakama si lazima kuwe na DISPOSAL ORDER kukitoa unless kesi iwe imemalizika na kielelezo hicho kitolewe kwa nia ya kukiharibu au kukirejesha serikali au kwa mwenyewe.

Hakuna haja ya kuwa na DISPOSAL ORDER ya kielelezo kilicho chini ya custody ya mahakama iwapo kielelezo hicho kinaendelea kutumika kwenye kesi inayoendelea ambayo hukumu yake haijatoka.

Mjadala unaendelea.
 
Kumbe ndo maana alikataa kufanya Ijumaa alikuwa na consultation kutoka Chamwino Ikulu. Angetumia hata sheria basi, kukataa hilo Pingamizi. Lakn hapo katumia mamlaka, bila kujua kwamba kuna siku maamzi haya, yanaweza kuathiri kesi nyingine, yatakapotumika kama Rejea.

Anyway, naamini mbele ya Safari haya maamzi ya influence pasipo ku-base kwenye Sheria, kanuni na taratibu yatafikia kikomo. Na hii kesi itawaumbua. Eee mwenyezi Mungu, katika hili tunakuomba usimame na Mwenye Haki.
 
Wanadamu bwana mbwembwe nyiiingi sote mwisho wetu ni kuoza na kunuka tu

1637321653808.jpg
 
Jamani Wenye busara hawapo wafute huu ujinga?? Muda na rasilimali fedha zinapotea bure mnatuchosha.
 
Mwanzooooni mwa kesi ilitoka lawama mawakiri wasomi wa Mbowe wamehongwa. Je, hayo ndiyo matokeo?
 
Back
Top Bottom