Najua katika hili zogo wapinzani wetu wamepata cha kusema, wamepata upenyo wa kupumulia, wanakesha wakiomba dua kwamba Chadema ipasuke ili wapate kupona.
Ninatoa rai kwa wanachama wengine wote kwamba hili saga liwe fundisho kwa kila mtu ili baadae asije akathubutu kuanzisha, kushiriki, kufadhili ama kushabikia uasi na usaliti ndani ya chama.
Natumaini viongozi wangu wakuu watakuwa makini kufuatilia haya yote yanayojiri hapa na kuchukua hatua stahiki kwa haraka iwezekanavyo kwa ajili ya mustakabali mwema wa chama chetu. Na kwakweli ninawasihi wawe wakali zaidi katika kulishughulikia suala hili ili hapo mbeleni pasitokee tena mtu awaye yeyote akafikiria kufanya uasi ama usaliti ndani ya chama hata kama atakuwa analipwa fedha nyingi kiasi gani.
Ndugu yangu Mwita Maranya: Hao nao wanatuhumiwa kwa njia moja au nyingine au hujasikia Makamu Mwenyekiti(moja ya viongozi wakuu) akitishia kurejesha kadi ya chama.