Ben Kigaila: Nimekabidhi barua ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake kwa Spika saa 2:42 asubuhi!

Naibu katibu mkuu wa Chadema mh Benson Kigaila amesema amekabidhi barua ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake kwa Spika wa bunge leo saa 2:42 asubuhi

Barua amekabidhiwa Katibu muhtasi wa Spika kea dispatch

Source: ITV
Sitaarajii kusikia wakati huu kuwa kilicho kabidhiwa ni kipeperushi au kikaratasi kama maneno ya enzi Ileee,bila shaka Sasa itasomeka ni taarifa rasmi na barua ya kiofisi kati ya ofisi mbili tofauti na yenye vigezo vyote ya kiofisi🤔
 
Hii nguvu wanayotumia kadema dhidi ya covid 19 wangeitumia kulinda kura zao kwenye chaguzi wangekuwa na 70% ya wabunge na wawakilishi!
 
Hii nguvu wanayotumia kadema dhidi ya covid 19 wangeitumia kulinda kura zao kwenye chaguzi wangekuwa na 70% ya wabunge na wawakilishi!
Humaanishi eti eeh! Kwa yule nyamaume nani angelinda au kusogelea kituo Cha kupigia kura? Au ulikuwa hujakua miaka hiyo? Basi mwombe bibi Yako akusimulie hadithi ya mtu yule huenda ukawaonea huruma cdm.
 
Huyo nae namuonaga amekaa kinjaa njaa flani hivi . sema pia hanaga ushawishi kabisa.
 
Naibu katibu mkuu wa Chadema mh Benson Kigaila amesema amekabidhi barua ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake kwa Spika wa bunge leo saa 2:42 asubuhi

Barua amekabidhiwa Katibu muhtasi wa Spika kea dispatch

Source: ITV
Si mlishapeleka miaka miwili iliyopita- hii ya pili inahusu nini tena?
 
Nahisi wataeeka pingamizi la kimahakama kwa hati ya dharula wakipinga kuvuliwa uanachama Hadi kesi Yao ya msingi itakapotolewa uamuzi!
 
Jana mnyika aliandika kwenye Twitter yake kuwa hiyo barua ilishafika kwa spika.

Leo msaidizi wake anasema barua imefika leo.

Tuagize popcorn
 
Naibu katibu mkuu wa Chadema mh Benson Kigaila amesema amekabidhi barua ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake kwa Spika wa bunge leo saa 2:42 asubuhi

Barua amekabidhiwa Katibu muhtasi wa Spika kea dispatch

Source: ITV

Maajabu ya Tanzania sio quantifiable!Kwahiyo, huko nyuma walimuambia Ndugai kiubatili batili kwa mdomo tu (au kwa barua batili) kwamba Halima na wenzake sio wanachama tena wa CDM?
 
Haya mambo ya nchi wakati mwengine ni kizungu nkuti. Nimemsikia Katibu wa kwanza Baraza la Mapinduzi ZNZ Mzee Salim akiongelea kuhusu Muungano ulivyoundwa. Walikuja kutoka ZNZ
akiongoza na Rais Karume sr 1964 kwa mazungumzo na Mwl Nyerere. Huyu Katibu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi akatolewa kwenye Kikao na Mwl akaambiwa aende akanyoe ndevu akapewa gari na dereva ampeleke kunyoa. Kwa maneno yake, Babu wee niliporudi kikao kilisha isha tukatiwa ndani ya ndege tukarudishwa ZNZ. Rais Karume sr kakaa kimya hakuniongelesha siku ya tatu ndio anatuambia alilazimishwa.
 
Back
Top Bottom