KERO Bei za vyakula kwa wasafiri ni kubwa

KERO Bei za vyakula kwa wasafiri ni kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mm hua nasafiri na package ya Korosho, Kuniuzia chips kavu za baridi 5000 ni sawa na utapeli.

Note: Mambo hua yanaharibika nikisafiri na wanawake
 
Muda ufikapo utataja hadi hoteli ama maeneo yenye gharama kubwaaa
 
Haya mambo ya kushindilia misosi mizito safarini ni kutaka kujipa usumbufu unaoepukika. Ingekuwa mabasi yana vyoo ndani ingekuwa freshi kulakula safarini. Misosi ya mahotelini yanakoenda mabasi ni ghali kinyama, wakati kuna biskuti, karanga na maji/juisi kidogo inatosha kutuliza njaa kuliko kununua msosi ghali alafu ubanwe na haja kubwa wakati kituo cha kusimama ni mbali, unaweza kujinyea na kusababisha kero ndani ya basi kwa harufu mbaya ya kinyesi, ukibanwa na mkojo unaweza kujitoa aibu ukakojolea chupa kuliko kubanwa na mavi hakuna kujitoa ufahamu, ni aibu kubwa
 
Yaani mbea Dar ni lazima ule?nunua vitu vikavu kausha ukistuka makambako hii hapa wakae na michipsi yao
Kuna watu akisafiri lazima ale njiani hata kama ni Dar Moro.. Kuna watu wakisafiri afikapo lazima ahangaike kutafuta mwanamke wa kulala nae!
 
Tuzifahamu hizo hoteli njia zote kuanzia dar to moshi/arusha, dar to mwanza, musoma, bukoba, dar to iringa, mbeya, maana asubuhi umepata chai lazima ubanwe na mkojo kukojoa ni korogwe au mombo kama unaenda moshi/arusha. Unakojoa morogoro mpaka shinyanga kama unaenda mwanza. Ukitoka moshi kukojoa/kunya ni babati. Safari usiwe makulakula sana utapata shida ya kujisaidia kituo na kituo na umbali mrefu sana. Unakula chakula ghali safarini halafu unaishia kufedheheka pindi ukibanwa na haja zote mbili. Kumekuwa na visa vingi sana vya abiria kufedheheka kwa kutokwa na haja bila kutaka. Kuficha aibu wengine huzingizia ni wagonjwa baada ya haja kuwatoka kwa kushindwa kujikaza hadi wafike kituo cha kujisaidia chooni
 
Biskuti na juisi nimemaliza kila kitu kitendo cha kuuziwa ndizi moja buku wakati nikiwa mbingu ndizi nne jero niliona ni utapeli.
Chips kavu 7k ***** ungese saana
 
Unaposafiri kuwa muangalifu sana na abiria jirani yako anayekulakula njia nzima kila akiona msosi/matunda, maji, juisi, mahindi, huyo lazima atabanwa na haja tu, akijinyea utalazimika kuikimbia siti yako uliyekaa naye jirani, uko radhi usimame kuliko kuvumilia harufu kali ya kinyesi. Ule chakula ghali safarini halafu ulete shida ndani ya basi ni aibu
 
Kitu pekee natumia safarini ni kahawa au chai basi. Kula kula hovyo mzee kuna siku utatia aibu 😄
 
Unakuta umepanda basi high class VIP, mnapelekwa kwenye hizo hoteli za misosi ghali, abiria wanatitia misosi mizito, mbeleni basi linaanza kunuka mavi ndani na hamjui aliyekunya ni nani. Kumbe kuna abiria kajinyea na ameshindwa kujibana mpaka kituo cha kujisaidia, hasa haya mabasi ya masafa marefu yana vituo vichache sana vya kujisaidia, ndio kwenye hizo hoteli za misosi ghali
 
Kuna nyama tulikula mkata alooh ile nyama ilikuwa tamu mix mafuta futa aseeh nikisafr awamu hii sjui itakuwepo bado,, njia ya Dsm Tanga vyakula sio vibaya sana vipo kawaida
 
Kumekuwa na bei kubwa/ghali sana ya vyakula kwa wasafiri nchini. Sehemu ambazo magari yanapeleka abiria kula yamekuwa yakitoza gharama sana za vyakula, Wahusika walifuatilie hili, watu wanaumia sana.

Watanzania ni kama hakuna wa kuwasaidia kiuongozi na kiutawala.
viongozi/watawala wako bize kuwadhibiti Wadai haki,
 
Back
Top Bottom