Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,510
- 4,224
Ama kweli, ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Huu ndiyo uhalisia wa hali zilivyo katika nchi hizi mbili.
Ukiachilia mbali swala la mfumuko wa bei, nina uhakika endapo haya yanayotokea katika shirika la TANESCO na kutesa wananchi kwa migao ya umeme kila kona lingetokea kwa majirani zetu, tayari baadhi ya watu wangeshawajibishwa na umma. Achilia mbali maji, huduma za afya, elimu, miundombinu, ulambaji asali n.k.
Lakini cha kushangaza, Watanzania wako busy na kusifu na kuimba mapambio ya kupongezana kana kwamba sasa Tanzania ni New York kubwa 😄.
Ni mwendo wa kupongezana na kusifiana tu! Tanzania mbele kwa mbele! Note: Kuna wanaoponda ila kupanda bei maharage ni mfano tu, hapa nazungumzia kupanda bei bidhaa kiujumla, pamoja na mambo mengine ya hovyo yanayoendelea kama migao ya umeme, maji n.k.