Watanzania tuna moyo mzuri lakini wahuni na wageni wanatumia hali hiyo kutuibia kutuumiza na kututawala

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
WATANZANIA TUNA MOYO MZURI LAKINI WAHUNI
Nchi yetu ya Tanzania ni kisiwa cha amani Duniani,hili ni tokeo la malezi mema ya Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,siasa ya ujamaa na kujitegemea ilitufanya tuwe waungwana na wastaarabu,Ahsante Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Leo Tanzania ndio nchi pekee katika bara la Afrika inayoheshimika kwa kutunza amani na utulivu,Tanzania ndio nchi pekee barani Afrika ina utulivu wa uhakika na watu wenye moyo mzuri,na ndio nchi pekee barani Afrika inawatu waungwana na wastaarabu,Uungwana na ustaarabu wetu ndio umetufanya tuendelee kuwa kisiwa cha amani na utulivu,na hiki ndio kielelezo cha werevu.

- Mabepari na Makabaila yanaingia katika nchi ya Waungwana na Wastaarabu.

Watanzania sisi ni waungwana sana na wastaarabu sana aisee,Uungwana wetu na ustaarabu wetu usiokifani siufananishi na chochote kile ila ni moyo mzuri wa kiwango hasa, Uungwana wetu na ustaarabu wetu ni advantage kubwa sana kwa watesi na waonevu,hakuna kitu kinawapa nguvu watesi kama uungwana na ustaarabu wa Watanzania,moyo wetu mzuri umewatajirisha wageni wengi waliokuja Tanzania huku sisi Watanzania tukibaki masikini kwa kuuza karanga mtaani na kutambiana uswahilini kwa kupika mboga ya nyama na kuwacheka wanaokula maharage kila siku na wengine wakishinda na mlo mmoja kwa siku,Baniani mmoja aliwahi kuniambia alikuja Tanzania akiwa na begi lenye shati na suruali moja na dola mia moja mfukoni,akapokewa na Mtanzania mmoja akampeleka Wizarani kama mwekezaji akapewa tender na sasa hivi ni bilionea, anasema mtaa ukiwa na baniani mmoja basi mtaa mzima unakuwa tajiri lakini shida moja Watanzania wanaomba ruhusa kila siku ya kwenda msibani leo kafa mjomba,kesho shangazi,bibi,babu akimaliza wote anaanza tena shangazi,mjomba,bibi wa babu na bibi mzaa baba.

Upole wa Watanzania,moyo mzuri umewafanya raia wa kigeni waliokuja kama wataalam kuhonga sehemu mbalimbali kuongezewa vibali kuendelea kukaa Tanzania, wanasema hapa Tanzania ndio mahali peke hata ukimuonea Mtanzania utapata chawa Mtanzania atakaekusifia, Mkenya mmoja tulikuwa tunakula kwenye mgahawa, alivyomaliza kula Mama muuza akamwambia wewe nenda nakujua utalipa kesho,yule mkenya alishangaa sana akasema mimi ni mkenya naweza toka hapa na usinipate tena,huyu mkenya akasema ninyi Watanzania hamtaweza hamjui kazi na hamtaweza biashara sababu "you have a good heart"! Kenya hamnaga huruma ofisini ufanye kosa wana"kusuck" saa hiyo hiyo hakuna kuoneana huruma huku ukiharibu kazi, ndio maana Wakenya wengi mpaka leo wanapenda sana Magufuli,alikuwa ukiharibu anakutoa saa hiyo hiyo ili nchi iende mbele,

Nikiwa masomoni nchini Kenya shule moja inaitwa Muguga miaka ya 90,tukitoka prepo nikakuta mkikuyu na mkamba wanapigana nikaenda kugombelezea wakaacha kupigana wakaanza kunipiga mimi,nilikimbia na kujifunza uzalendo mkubwa walionao Wakenya, kwenye jambo lao wanalopigania hawataki waingiliwe hadi haki na usawa vipatikane, nikafahamu Kenya nchi ya kibepari na Wakenya wale uhuru waliupigania hawakupewa na hii imepelekea kushape kizazi cha kenya kwenye fikra kuliko sisi waatanzania,mkenya hata mtu wa kawaida anajiamini na anajua haki zake na yuko tayari kuzipigania ila mtanzania ni muungwana sana na mstaarabu kiasi cha kuruhusu haki yake kuiacha iende ikiwa jambo liko ndani ya uweza wake lakini atakuambia anamwachia Mungu, point hapa sio kuisifia sana Kenya hapana still wanamatatizo yao kama rushwa, ukabila, kiwango chao cha maendeleo hakija pishana sana na Tanzania,ila jambo ambalo nauhakika nalo wakenya sio watu wa kukubali wawe masikini hata kwa rasilimali ndogo ambazo Mungu amewajaalia ila watanzania licha ya rasilimali nyingi ambazo Mungu ametujaalia wageni mabebari na Makabaila yanakuja kuzichukua na sisi tunamwachia Mungu,je Mungu hakutupa wajibu juu ya rasilimali alizotujaalia!?

- Je ni kweli Ujamaa umeleta Upole ulisababisha Watanzania kuibiwa rasilimali zao?

Jibu ni hapana tukirejea nchi ya China,kinachowezekana nchi nyingine huenda ikawa vigumu kufanya kazi nchi nyingine bila mabadiliko,huenda ni kweli system ya nchi ambayo ina mali ya kutosha (natural resources..) wakati wa Mwalimu Nyerere, Watanzania walikuwa sio wasomi sana wala sio wachapakazi na watu wa kujituma huenda,Ujamaa ulikuwa best suited,(au Social Democracy) Naamini Mwalimu alipendelea Ujamaa kwa namna uchumi kuwa privately owned lakini state inakuwa na uangalizi mzuri as well as kutoa kodi ambayo inaweza ikatoa huduma kwa majority kama Nordic Countries. Kwa nchi kama Marekani mfumo wa Ujamaa ni vigumu kufanya kazi kwa nchi kama marekani ambao watu ni wengi na ni vigumu kwa state kuchukua huu mzigo wa kuwaangalia watu kama ilivyo kwa Nordic countries.

China wana mfumo wao wa Ujamaa ambao ni tofauti na sehemu nyingine..., Uingereza ni mabepari ingawa (health care) huduma za jamii ni bure tofauti na America ambapo huduma za afya sio bure...Utaona kwamba ile free market ya Hayes ni tofauti na America wanachokifanya ambacho ni Keynes kwamba state inaingilia hapa na pale na kuinject funds na kufanya bail-outs za hapa na pale ambazo zinafanya watu hata wasiogope kutumbua pesa ambazo sio zao wakijua kwamba kosa likifanyika state itaingilia kati na kuwasaidia...Hivyo basi Ujamaa wakati wa Mwalimu ulikuwa ni bora ambapo tulikuwa hatugawi maliasili zetu kuliko sasa tunavyozigawa bure (this has nothing to do na mfumo wowote wa kisiasa bali ni ujinga wetu ulimbukeni na tamaa za kikundi cha watu wachache)

Ujamaa unakupa kuridhika kama hakuna dira na maono kwamba ni vigumu kufanya kazi kwa nchi za kibepari sababu kutokuwa na ushindani wa kutosha kwenye Ujamaa kunafanya watu kubweteka na quality inapungua na watu kutokujali (Hii ni Mali ya Umma na Umma ndio sisi,wacha tuenjoy) lakini kwenye soko huria ushindani unashusha bei na kufanya product kuwa nzuri zaidi (wakati apple anakuja na iphone mwingine anakuja na kitu kingine kizuri zaidi...) n.k.Lakini kwa Tanzania we dont really need ubepari ku-thrive na kutokana na watu wetu ambao wengi wanahitaji welfare (social democracy huenda inafaa zaidi). We have nothing to loose tuna mtaji wa kutosha wa madini na maliasili nyingi na kwa population yetu udhibiti unaweza ukatunufaisha wote..., (hata Gaddaffi aliweza kwa Libya kutokana na utajiri wa nchi yake kulingana na idadi ya watu wake.) Hii inawezekana tu kama Tanzania itapata viongozi sahihi kwa wakati sahihi,nazungumzia Kiongozi kama Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Hayati Edward Moringe Sokoine na Hayati Daktari John Pombe Magufuli.

Nimalizie kwa tafakuri Jadidi,Ni afadhali wakati wa Uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na dira au ndoto ya kutaka kututoa sehemu moja na kutupeleka mahali fulani kuliko sasa ambapo nchi haina itikadi wala dira,kwa nini nasema hivi? Katiba tuliyonayo inasema wazi nchi hii ni ya Ujamaa na kujitegemea, lakini tunachoshuhudia sasa kikiendelea ni ukoloni mamboleo kwa gia ya uwekezaji na utandawazi ambao Mwalimu Julius Nyerere aliukemea sana,tulisikia kuuzwa kwa bandari kwa mkataba wa milele,kama ni kweli basi rasilimali za taifa zinaporwa kama hazina mwenyewe na mbaya zaidi tunaolalamika bado ni masikini vilevile kama ambavyo Mwalimu Julius Nyerere alituacha.Sasa lipi bora la umaskini wa kijamaa wakati wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo Mwalimu Nyerere alitaka wote tuwe matajiri ama wote tuwe masikini au Ubebari wa hivi leo uliokithiri na umaskini kwa mwananchi mmoja mmoja wenye moyo mzuri,lipi bora kuleta wawekezaji huku wananchi walio wengi wanapata mlo mmoja kwa siku? huku wakiwa hawana uhakika wa kupata huduma muhimu kama elimu, afya, maji safi, nishati n.k? Mwalimu Julius Nyerere alisema" Ni afadhali kuwa masikini huru kuliko kuwa tajiri mtumwa?

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

- Bachelor of business administration in International business.

- Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-

- Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Back
Top Bottom