Bei ya Nishati ya Mafuta Kenya Yaendelea kupaa kama Ndege Vita

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,715
Ndugu zangu Watanzania,

Sasa nitaanza kueleweka naposema kila wakati humu jukwaani kuwa Rais samia anachapa kazi,anafanya kazi kwa ajili ya watanzania,anatubeba kisera katika kuhakikisha hatupati maumivu ya kupanda kwa gharama za maisha, kwa kuchukua hatua mbalimbali za kisera. Kuusema ukweli siyo kujipendekeza au Kusaka uteuzi au fadhira kutoka kwa mamlaka.

Sasa huko kenya kwa sasa ni kulia kwa kwikwi na kububujikwa kwa machozi,kutokana na kupanda kwa nishati ya mafuta ambako hakujawahi kushuhudiwa katika Historia ya Taifa hilo ambalo kwa sasa linaihofia sana Tanzania ya Rais samia kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania unaoendelea kwa sasa.

Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na petrol Nchini kenya( EPRA)imetangaza bei mpya ya nishati ya mafuta inayoonesha kupanda kwa bei ukilinganisha na bei ya mwezi uliopita,Ambapo sasa liter moja ya petrol itauzwa shilingi 217.39 kutoka shilingi 211.64 mwezi uliopita, Diesel itauzwa sasa kwa shilingi 205.47 kutoka 200.99 mwezi uliopita na mafuta ya Taa yatauzwa kwa shilingi 205.06 kutoka 202.61 mwezi uliopita.

Ifahamike ya kuwa shilling moja ya kenya ni sawa na shilingi 16.77 za kitanzania. Hivyo liter moja ya petroli inayouzwa shilingi 217.36 kwa kenya ni sawa na shilingi 3646.93 kwa Tanzania, Dieseli inayouzwa 205.47 kwa kenya ni sawa na 3445.75 fedha za kitanzania wakati mafuta ya Taa yanayouzwa 205.06 kwa shilingi za kenya ni sawa na shilingi 3438.85 pesa za kitanzania. Hivyo unaweza ukaona ni namna gani hali ni mbaya kwa upande wa nchi hiyo ya kenya ambayo baadhi ya watu hapa jukwaani kwa ulimbukeni wao hupenda kuichukulia kama nchi ya kuigwa,wakati kiuhalisia kwa sasa chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais samia Tunaipita kwa kasi ya upepo.

Hapo kitu kinachopaswa kieleweke ni kuwa bei hizo zipo hivyo baada ya serikali ya kenya kuweka Ruzuku ya Billion 1.76 fedha za kenya.Bila hivyo hali ingekuwa mbaya zaidi ya kusaga meno na kulia. Kwa kuwa bila Ruzuku petroli ingeuzwa kwa 220.43, Dieseli 217.11 na mafuta ya Taa kwa 214.66 fedha za kenya ,Ambapo kwa fedha za Tanzania ni sawa na 3696.61 kwa petroli, 3640.93 kwa Diesel na 3599 kwa mafuta ya Taa.

Sababu zilizotajwa za kupanda kwa bei hizo na mfumuko huo wa bei ni kushuka kwa thamani ya shilingi ya kenya dhidi ya dollar ya marekani ambayo ndio inayotumiwa katika manunuzi,Nchi za OPEC kupunguza uzalishaji wa mafuta,vita ya urais na ukraine n.k.

Kwa hiyo watanzania tuendelee kuelewa kuwa serikali yetu chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais samia inafanya kazi kubwa sana na ya kizalendo sana katika kuhakikisha kuwa watanzania hatuelemewi na mzingo wa gharama za maisha.ndio maana serikali yetu imekuwa ikichukua Hatua mbalimbali za kiuchumi kuhakikisha kuwa tunapata ahueni ya maisha. Ikumbukwe na kueleweka ya kuwa siyo dhamira wala lengo la Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania kuona watanzania tukiumia au kupata maumivu kwa jambo lolote lile, serikali ya Rais samia ipo kwa ajili ya kutupatia Matumaini,kutupa faraja, kutuwezesha,kutushika mikono, kutuinua,kutuvusha katika hali ngumu,kutupatia Tabasamu,kutuondoa katika umaskini na pia kutupatia nuru kila uchwao.

Zinapojitokeza changamoto ndogo ndogo tujitahidi kuwa wavumilivu,watulivu na wenye subira wakati serikali yetu inaendelea na kazi ya kutatua changamoto husika,tusiwe watu wa kulalamika sana,kupiga kelele zisizo na msingi na kupotoshwa na watu wenye chuki binafsi na serikali yetu na Rais wetu mpendwa.tukumbuke ya kuwa siyo wote wanaofurahia namna tunavyofanya vizuri kiuchumi na kupata maendeleo na mafanikio chini ya uongozi wa Rais samia,wapo wanaotamani ashindwe na asifanikiwe,hivyo tusiwape nafasi ya kumdhoofisha na kumkwamisha Rais wetu mpendwa.Tumuunge mkono Rais wetu na tumtie nguvu na moyo na kumpa faraja ya kusonga mbele.yote afanyayo ni kwa ajili yetu watanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Kwann umeichagua Kenya kujilinganisha nayo?

Unajua kuna nchi hazina bandari wala reserves za mafuta na bei iko Chini kabisa ya mafuta? Kwann usijilinganishe na hizo
 
Acha kuhamisha magoli ndugu yangu.nyie si ndio huwa mnashinda humu jukwaani kupotosha na kusema hali ya kenya ni nzuri na hakuna habari za mfumuko wa bei wala gharama kubwa za maisha?
 
Unaweza ku quote comment yangu au uzi wangu niliposema hivyo?
 
Blah blah blah, siku utakayo kuja kutambua kuwa ni kwa nini 1kshs =17Tshs, ndio uje tujadili mkuu, na pia siku utakayo kuja kujitambua kuwa 217 SIO Sawa na 3600 njoo tujadili hapa, unafikiria why hapa Tanzania tusinunue mafuta kwa Lita moja 217 ths?,na tunatumia 3600ths kupata Lita moja?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Sasa nitaanza kueleweka naposema kila wakati humu jukwaani kuwa Rais samia anachapa kazi,anafanya kazi kwa ajili ya watanzania,anatubeba kisera katika kuhakikisha hatupati maumivu ya kupanda kwa gharama za maisha, kwa kuchukua hatua mbalimbali za kisera. Kuusema ukweli siyo kujipendekeza au Kusaka uteuzi au fadhira kutoka kwa mamlaka.

Sasa huko kenya kwa sasa ni kulia kwa kwikwi na kububujikwa kwa machozi,kutokana na kupanda kwa nishati ya mafuta ambako hakujawahi kushuhudiwa katika Historia ya Taifa hilo ambalo kwa sasa linaihofia sana Tanzania ya Rais samia kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania unaoendelea kwa sasa.

Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na petrol Nchini kenya( EPRA)imetangaza bei mpya ya nishati ya mafuta inayoonesha kupanda kwa bei ukilinganisha na bei ya mwezi uliopita,Ambapo sasa liter moja ya petrol itauzwa shilingi 217.39 kutoka shilingi 211.64 mwezi uliopita, Diesel itauzwa sasa kwa shilingi 205.47 kutoka 200.99 mwezi uliopita na mafuta ya Taa yatauzwa kwa shilingi 205.06 kutoka 202.61 mwezi uliopita.

Ifahamike ya kuwa shilling moja ya kenya ni sawa na shilingi 16.77 za kitanzania. Hivyo liter moja ya petroli inayouzwa shilingi 217.36 kwa kenya ni sawa na shilingi 3646.93 kwa Tanzania, Dieseli inayouzwa 205.47 kwa kenya ni sawa na 3445.75 fedha za kitanzania wakati mafuta ya Taa yanayouzwa 205.06 kwa shilingi za kenya ni sawa na shilingi 3438.85 pesa za kitanzania. Hivyo unaweza ukaona ni namna gani hali ni mbaya kwa upande wa nchi hiyo ya kenya ambayo baadhi ya watu hapa jukwaani kwa ulimbukeni wao hupenda kuichukulia kama nchi ya kuigwa,wakati kiuhalisia kwa sasa chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais samia Tunaipita kwa kasi ya upepo.

Hapo kitu kinachopaswa kieleweke ni kuwa bei hizo zipo hivyo baada ya serikali ya kenya kuweka Ruzuku ya Billion 1.76 fedha za kenya.Bila hivyo hali ingekuwa mbaya zaidi ya kusaga meno na kulia. Kwa kuwa bila Ruzuku petroli ingeuzwa kwa 220.43, Dieseli 217.11 na mafuta ya Taa kwa 214.66 fedha za kenya ,Ambapo kwa fedha za Tanzania ni sawa na 3696.61 kwa petroli, 3640.93 kwa Diesel na 3599 kwa mafuta ya Taa.

Sababu zilizotajwa za kupanda kwa bei hizo na mfumuko huo wa bei ni kushuka kwa thamani ya shilingi ya kenya dhidi ya dollar ya marekani ambayo ndio inayotumiwa katika manunuzi,Nchi za OPEC kupunguza uzalishaji wa mafuta,vita ya urais na ukraine n.k.

Kwa hiyo watanzania tuendelee kuelewa kuwa serikali yetu chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais samia inafanya kazi kubwa sana na ya kizalendo sana katika kuhakikisha kuwa watanzania hatuelemewi na mzingo wa gharama za maisha.ndio maana serikali yetu imekuwa ikichukua Hatua mbalimbali za kiuchumi kuhakikisha kuwa tunapata ahueni ya maisha. Ikumbukwe na kueleweka ya kuwa siyo dhamira wala lengo la Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania kuona watanzania tukiumia au kupata maumivu kwa jambo lolote lile, serikali ya Rais samia ipo kwa ajili ya kutupatia Matumaini,kutupa faraja, kutuwezesha,kutushika mikono, kutuinua,kutuvusha katika hali ngumu,kutupatia Tabasamu,kutuondoa katika umaskini na pia kutupatia nuru kila uchwao.

Zinapojitokeza changamoto ndogo ndogo tujitahidi kuwa wavumilivu,watulivu na wenye subira wakati serikali yetu inaendelea na kazi ya kutatua changamoto husika,tusiwe watu wa kulalamika sana,kupiga kelele zisizo na msingi na kupotoshwa na watu wenye chuki binafsi na serikali yetu na Rais wetu mpendwa.tukumbuke ya kuwa siyo wote wanaofurahia namna tunavyofanya vizuri kiuchumi na kupata maendeleo na mafanikio chini ya uongozi wa Rais samia,wapo wanaotamani ashindwe na asifanikiwe,hivyo tusiwape nafasi ya kumdhoofisha na kumkwamisha Rais wetu mpendwa.Tumuunge mkono Rais wetu na tumtie nguvu na moyo na kumpa faraja ya kusonga mbele.yote afanyayo ni kwa ajili yetu watanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Pilipili ya shamba yakuwashia nini ya mambo ya mafuta kenya huko wewe yanakuhusu nini..
 
Back
Top Bottom