Bei ya Cement yapanda

Bei ya Cement yapanda

Sawa tuu si wameounguziwa kwingineko..

Mkoani tunanunua cement 17,000-19500 so sie tulizoea..

Mwisho umeambiwa hela inatakiwa wanafunzi wakapewe mikopo wasome hakuna njia mbadala
Kwa hiyo itapanda kwa buku tena hapo

Kuna matumizi mabaya ya kodi zinazokusanywa na ukusanyaji wa kodi umekithiri rushwa na ukwepaji wa kodi

Mwisho wa siku ndo hizi tozo tunabebeshwa sisi ili kufidia

Kumbuka hii haimwathiri mwenye kiwanda wala mfanyabiashara wa jumla na rejareja hata kidogo ni wewe mtumiaji wa mwisho ndiye unabebeshwa mzigo wa hiyo buku
 
Kwa hiyo itapanda kwa buku tena hapo

Kuna matumizi mabaya ya kodi zinazokusanywa na ukusanyaji wa kodi umekithiri rushwa na ukwepaji wa kodi

Mwisho wa siku ndo hizi tozo tunabebeshwa sisi.

Kumbuka hii haimwathiri mwenye kiwanda wala mfanyabiashara wa jumla na rejareja hata kidogo ni wewe mtumiaji wa mwisho unabebeshwa mzigo wa hiyo buku
Ndio
 
Kwenye uchumi ongezeko la buku ni hela kubwa sana

Dangote 42.5 Truck semi hubeba mifuko 600 bei ilikuwa ni 15,000 ulikuwa unaagiza kwa 9,000,000/=

Sasa hivi baada ya serikali kuongeza 1000 ni 16,000 ukiagiza semi ni 9,600,000/=

Hii cement ya Dangote 42.5 ndio huwa inatumiwa sana na viwanda vya kutengeneza tofali

Mtengeneza tofali naye ataongeza bei ya tofali ili kufidia hizo buku buku

Mtumiaji wa mwisho mwananchi akisema aanze ujenzi akienda kununua matofali anakuta bei iko juu akinunua na cement anakuta bei imepanda

Mambo ya Hon. Dr. Nchemba hayo
Yani Mwigulu Badala awapandishie Gharama ya bia walevi anapandisha bei kwenye ujenzi.

Hawa wachumi hewa wa nchi hii
 
Kule Bungeni tumepeleka Wawakilishi wasioweza kututetea.

Hii Nchi hata turudishe kodi ya Kichwa lakini maendeleo yataishia kusemwa midomoni mwa Wanasiasa tu lakini sio kuonekana field.

Viongozi wanatafuna hii Nchi kwa Ufisadi
Mkuu, wa leo sio wawakilishi wa Wananchi tena bali ni Wawakilishi wa Serikali. Wawakilishi wa Wananchi walikuwa zamani akina G55.
 
Mkuu, wa leo sio wawakilishi wa Wananchi tena bali ni Wawakilishi wa Serikali. Wawakilishi wa Wananchi walikuwa zamani akina G55.
Sahihi Mkuu, ndiyo maana wameshindwa kututetea Wananchi wenzao
 
Mbona Cement Dar zinauzwa kwa 13700-14500

Baada ya ongezeko itakuwa 14700-15500
Unaongelea bei ya cement ipi hiyo mkuu. Dangote na twiga plus bei ya awali ilikuwa 16000 kwa mfuko. Hizo za 14000 ni lucky, nyati, diamond na nyinginezo
 
Fikiria mtu anakula bure, analala bure, anaendesha bure, karibia 100% ya maisha yake anaishi bure kwa kutegemea watu fulani wampe, lakini hao wanaompa ili aishi vizuri anazidi kuwakandamiza.

Hivi waliobuni mifumo ya kuongozwa na siasa ni nani kama sio upumbavu? There mofos are so selfish.
Siasa ni nzuri Sasa changamoto inakutana na malimbukeni. Ndio maana hoja ya leaders are born Ina mashiko
 
Hivi kwa Afrika Mashariki,Kuna nchi yenye gharama kubwa za vifaa vya Ujenzi kama Tanzania?

Sio Gharama ya vitu tu bali TANZANIANS are most taxed people in the world!! Kila mahala ukipita ni Kodi kodi tu !! Serikali haiangalii kabisa upande wake wa matumizi yasiyokuwa na tija badala yake inafurahia kuwaumiza wananchi wake kwa matumizi ya kijinga! Maendeleo hayaji kwa kuwaumiza wananchi kwa kodi ovu!

Juzi wanatangaza kwa bashasha eti ile Ndege iliyokamatwa Ulaya imerudi nchini lakini hawasemei kiasi gani cha kodi ya Wananchi imetumika kukomboa ile Ndege kutokana na ubovu wa mikataba wanayoiingiza nchi sababu ya ujinga wao!!
 
Nimeona pia taarifa ya Mbeya cement, nayo imeonesha hilo ongezeko la shilingi 1,000 kwa kila mfuko wa saruji.

Yaani pamoja na ugumu huu wa maisha wameamua ku impose mzigo mwingine wa kodi kwa Raia wake 🙌

=======
Ingekuwa Nchi nyingine zinazoejielewa mfumko huu wa maisha ingekuwa tiketi ya Viongozi hao wakuu na Serikali yao kuondoshwa madarakani
Elimu haijatusaidia. Pia watz ni waoga
 
2020? Angalia usahihi
Niko sahihi 2020 nilikuwa Mwanza , na hiyo ndio bei tuliyokuwa tunachukulia mfuko wa cement (Twiga plus) kwa bei ya rejareja. Kipindi hicho cement zilidimika sana mikoni.
 
Bei ya cement ilipanda 2021 baada ya kifo cha magufuli

Niko sahihi 2020 nilikuwa Mwanza , na hiyo ndio bei tuliyokuwa tunachukulia mfuko wa cement (Twiga plus) kwa bei ya rejareja. Kipindi hicho cement zilidimika sana mikoni.
 
Back
Top Bottom