Bei ya Cement yapanda

Bei ya Cement yapanda

Hii mbaya sana..., ila...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Mbona Unatuchanganyia habar mkuu
 
Imagine VP ni mchumi, FM(Finance minister) ni mchumi, wameshindwa hata kumshauri huyo nanihii kweli?

Hii maana yake ni kuwa, hata kodi ya pango(biashara na makazi) zitaongezeka. Hawaoni namna wanavyoumiza raia wao?
 
"Kumbe ni buku tu"..?

Wanaochukua mzigo kubwa ndio wanaojua ukibwa wa hiyo buku.

Chukua hiyo buku, halafu fanya kama unanunua mifuko 200 au zaidi.

Kwenye shughuli za ujezi hata Tsh 500 ni kubwa sana, labda kama unajenga kaburi.
Halafu hiyo mifuko inapelekwa mbali
 
Upuuzi wa hali ya juu wanshindwa kukusanya kodi huko wanakuja kumtwika mzigo mwananchi

Hakuna kitu sipendi kama bidhaa za ujenzi kuongezewa tozo au kodi

Hapo tutegemee pia bei za tofali kupanda
Serikali ina uwezo wa kukusanya kodi ila tatizo ni Siasa na wanasiasa.

TRA walitangaza mwaka huu kuwa kuanzia mwezi March Machinga wote na biashara zote zilizo Kariakoo lazima ziwe na EFD, kwenye utekelezaji

Siasa zikaingilia,CCM wakaiagiza Serikali isitishe, Rais S.Hasani akaagiza MoFin wafute ikafutwa.

TRA wanasema walipakodi Tz ni milioni 4 pekee kati ya Milioni 20 wenye uwezo wa kulipa.
Na kati ya hao wenye TIN ni 1.6mil tu, sasa angalia huo mzigo hapo.
Imebidi sasa wawekeze nguvu katika kila mtu alipe
 
Hizi kodi zinaenda kuporwa tu kama ripoti ya CAG Kichere inavyosema, na badala ya Serikali ya CCM kufhibiti uporaji wao wanazidi kutuongezea mzigo wakati pipa linamatobo na wao wenyewe ndio wamekinga na kuchota.
 
Serikali inachukua 600k kwa tani 30 za cement. Huu ni unyang’anyi kabisa. Bei kesho kwa dsm haitakuwa 17k kwa mfuko itakuwa 18k.
Mbona Cement Dar zinauzwa kwa 13700-14500

Baada ya ongezeko itakuwa 14700-15500
 
Serikali ina uwezo wa kukusanya kodi ila tatizo ni Siasa na wanasiasa.

TRA walitangaza mwaka huu kuwa kuanzia mwezi March Machinga wote na biashara zote zilizo Kariakoo lazima ziwe na EFD, kwenye utekelezaji

Siasa zikaingilia,CCM wakaiagiza Serikali isitishe, Rais S.Hasani akaagiza MoFin wafute ikafutwa.

TRA wanasema walipakodi Tz ni milioni 4 pekee kati ya Milioni 20 wenye uwezo wa kulipa.
Na kati ya hao wenye TIN ni 1.6mil tu, sasa angalia huo mzigo hapo.
Imebidi sasa wawekeze nguvu katika kila mtu alipe
Ndio tunarudi kulekule wameshindwa kukusanya kodi kwa kuendekeza siasa
 
Wanachosahau wanasiasa wanapoamua kuongeza Kodi,Anaeumia Ni mtumiaji sio mfanyabiashara

Angalia Apo dangote kaweka wazi kua itaongezeka buku kila mfuko

Maana ake hiyo Tsh 20 kila kilo inalipwa moja kwa moja na mlalahoi

KWA tafsiri hiyo
Hii tuite Ni TOZO YA CEMENT, sio kodi
Sababu wengi hawalipi kodi hivyo inapelekwa kwenye bidhaa kila mtu aumie kwa njia yake
 
Back
Top Bottom