Bei ya Cement yapanda

Bei ya Cement yapanda

Tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi
Eti Kodi kwa maendeleo ya nchi!!!

Nchi gani?

Hii nchi tunalipishana Kodi za kuumizana wakati hao watawala wanaishi bure kwa kila kitu. Hadi magari wanaagiza zero km na yanapita bure bandarini,alafu sisi wa chini tunaagiza vigari vya 2008 IST na vitz,Kodi zaidi ya gari.

Wanapandisha cement Kodi wakati wao wanaishi bure hawalipii chochote.

Tunalipa Kodi alafu wao wanaitafuna bila huruma!!
 
"Kumbe ni buku tu"..?

Wanaochukua mzigo kubwa ndio wanaojua ukibwa wa hiyo buku.

Chukua hiyo buku, halafu fanya kama unanunua mifuko 200 au zaidi.

Kwenye shughuli za ujezi hata Tsh 500 ni kubwa sana, labda kama unajenga kaburi.
Sawa tuu,kipato kikubwa unachangia sana shida Iko wapi?

Bado sh.100 ya mafuta inakuja
 
Bado na mafuta ya magari yanapanda pia..

Kwani wakati Serikali inasema itaongeza hizo bei Bungeni nyie mlikuwa mnajua itakuaje labda? Watanzania ni watu wa ajabu sana
Kule Bungeni tumepeleka Wawakilishi wasioweza kututetea.

Hii Nchi hata turudishe kodi ya Kichwa lakini maendeleo yataishia kusemwa midomoni mwa Wanasiasa tu lakini sio kuonekana field.

Viongozi wanatafuna hii Nchi kwa Ufisadi
 
🤣🤣🤣🤣😂😂 we dogo kuna wakati huwa sikuelewi, hasa tokea suala la dp lije!
Mimi nina misimamo tofauti katika mambo, usipate tabu kunielewa. nasapoti uwekezaji wa Bandari, lakini sisapoti kuongeza makodi na matozo ya Mwigulu na Zungu.

Na huwa na speak my mind na kupenda mijadala, kuliko kuwa na heard mentality kama Wanyamapori.
 
Taarifa iliyosambazwa na Uongozi wa kiwanda cha cement cha Dangote , inaeleza kwamba sababu za kupanda kwa Bei ya cement ni ongezeko la kodi ya serikali kwenye bidhaa hiyo .

Taarifa yao hii hapa .

View attachment 2674532
Bidhaa nyingi muhimu ziliadimika wiki hii madukani, maana zilifungiwa kusubiri bei mpya kuanzia kesho tarehe moja July

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo haliwezekani ndugu
Watawala hawa wasiokuwa na huruma na Wananchi wao ndio watatupush tu uprise na kuwatoa kwa nguvu.

Sasa hivi wanapanga kutuibia kura uchafuzi ujao.

Baada ya ule mpango wa Serikali ya nusu mkate Lissu alipougomea.
 
Huyo Mnyiramba kamteka huyo Mama kila kitu anamwambia Hewala hajuikama anakivizia kiti.
 
Watawala hawa wasiokuwa na huruma na Wananchi wao ndio watatupush tu uprise na kuwatoa kwa nguvu.

Sasa hivi wanapanga kutuibia kura uchafuzi ujao.

Baada ya ule mpango wa Serikali ya nusu mkate Lissu alipougomea.
😳 Eeeh eti nini? Relief inapatikana kirahisi ukifungua moyo, come commander eeh alipogomea Nusu mkate ikawaje sasa, maana hiyo itasaidia kua na Msingi halali na wenye logic kua na ujasiri wa kuwa front kuwang'oa watu mamlakani,
 
😳 Eeeh eti nini? Relief inapatikana kirahisi ukifungua moyo, come commander eeh alipogomea Nusu mkate ikawaje sasa, maana hiyo itasaidia kua na Msingi halali na wenye logic kua na ujasiri wa kuwa front kuwang'oa watu mamlakani,
Sisi CHADEMA hatutaki kuhongwa viti Bungeni tunataka Katiba Mpya ndio tuingie kwenye Uchaguzi ambao ni huru na wa haki na kama CCM itatushinda kihalali tutawapongeza.
 
Hizi Kodi wanazotukamua utasikia siku si nyingi CAG akisema kuna Mabilioni yameibiwa na serikali ya CCM, Bunge la CCM Mahakama za CCM Mapolisi wa CCM na hata JW.

No hate no Fear.
 
Back
Top Bottom