Ndugu zangu watanzania wote mnaomiliki magari hizi ni bei mpya kupata new motor vehicle lecence pamoja na registration za magari pale TRA Bei imepanda kwa asilimia 95%.
Hivi kweli tutafika, mafuta ya gari yamepanda, motor vehicle license nayo imepanda, nasikia na umeme umepanda kutoka 240,000/= mpk 560,000. KWELI HAYA NDIO MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?
ENGINE CAPACITY (0 - 500)
Utalipia shilling 50,000/=
Na Penalty yake ni sh. 30,000/=
ENGINE CAPACITY IKIWA 501 - 1500
Utalipia shiling 80,000/=
Penalty yake ni sh. 42,000/=
ENGINE CAPACITY IKIWA 1501 - 2500
Utalipia shilling 150,000/-
Na penalty ni shiling 60,000/=
ENGINE CAPACITY IKIWA NI 2501 - 5000
Utalipia shilling 330,000/=
Penalty ni shilling 105,000/=
ENGINE CAPACITY IKIWA NI 5001 AND ABOVE
Utalipia shilling 175,000/=
Penalty itakuwa ni sh. 66,000/=
Nadhani hapo mtakuwa mmenipata.
Sijui Bajaj yangu ina uwezo gani!
Watanzania tumenyamaza mfumuko wa bei unapanda hivi? Hakuna namna ya kuepusha? Bei ya Service Lines imepanda zaidi ya mara mbili, Bei ya Leseni imepanda hivyo, bei za vyakula juu mara mbili, bei za internet zimepanda juu kabisa zaidi ya mara nne.
Tutaendelea kuumia hivi hadi lini? Hakuna suluhu? Mishahara ambayo watanzania waliahidiwa kufikia Novemba itakuwa imepanda (Sekta binafsi) sasa nayo haina dalili za kupandishwa na imepigwa kalenda hadi mwakani, kwanini bei za vitu hivi zisingeanza kupanda baada ya kipato cha mwananchi wa chini kupanda?
Hivi tunaelekea wapi? Mnajua kuwa kupanda kwa leseni za vitu hivi vya moto (motor vehicles) kutapelekea kupanda kwa nauli?
Nauli ya daladala iliyokuwa Tshs 150/= mijini (Kipindi cha mwaka mmoja unusu uliopita enzi za Ben) sasa kimefikia Tshs 350/= na kwa mwendo huo kitafikia Tshs 500/= punde. Nauli ya Taxi (town trips) iliyokuwa Tshs 1,000/= kipindi cha Ben sasa ndani ya mwaka mmoja unusu hivi imefikia Tshs 3,000/- na kwa kuongezeka kwa gharama za leseni utasikia ghafla taxi kwa town trips wanafikia Tshs 6,000/= Mche (mchi?) wa sabuni ya kipande uliokuwa Tshs 250/= kipindi cha Mkapa umefikia Tshs 800/=! Chumba cha kupanga (uswahilini) ambacho kilikuwa ni Tshs 10,00/= kwa mwezi sasa kimefikia Tshs 30,000/= [Kumbuka mshahara haujapanda!] Masikini Tanzania... Oh, my country
Hivi nini hatma ya mtanzania? Masuala haya yanaumiza kichwa na kukatisha tamaa juu ya tuelekeako. Soko la ajira limeachwa linaenda ovyo, waajiri wanalipa wanavyotaka na huku wakikwambia ni soko huria. Soko huria limekuwa si huria tena, hakuna mamlaka ya kulidhibiti. Gharama za maisha zimepanda kuliko kiwango ambacho kinatarajiwa!
Am totally confused!
1. Itasaidia kupunguza ajali barabarani kwa kuondoa madereva wazembe
2. Itaongeza pato la serikali
3. Itasaidia Mazingira na afya zetu
Kusema kweli sirikali ya huyu muungwana imebadili kabisa mfumo wa maisha ya Wadanganyika, kutoka 'bad' kwenda 'worse'. Tunamlaumu Mkapa kuwa kaiba, lakini afadhali maisha yalikuwa na nafuu kuliko ya muungwana, kwani ndani ya miaka miwili tu ya utawala wake maisha yamekuwa hayashikiki. Kila kitu bei juu! Tumejadili sana suala hili katika mada fulani hapo kwenye contribution ya 1.9% ya madini katika uchumi wa taifa. Nadhani hadi kufikia mwaka 2010 lita ya petroli tutanunua hadi 10,000 kwa mwendo huu.
Tufanye nini sasa?