Bei Mpya Ya Motor Vehicle License

Domo Kaya

JF-Expert Member
May 29, 2007
531
59
Ndugu zangu watanzania wote mnaomiliki magari hizi ni bei mpya kupata new motor vehicle lecence pamoja na registration za magari pale TRA Bei imepanda kwa asilimia 95%.

Hivi kweli tutafika, mafuta ya gari yamepanda, motor vehicle license nayo imepanda, nasikia na umeme umepanda kutoka 240,000/= mpk 560,000. KWELI HAYA NDIO MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?

ENGINE CAPACITY (0 - 500)
Utalipia shilling 50,000/=
Na Penalty yake ni sh. 30,000/=

ENGINE CAPACITY IKIWA 501 - 1500
Utalipia shiling 80,000/=
Penalty yake ni sh. 42,000/=

ENGINE CAPACITY IKIWA 1501 - 2500
Utalipia shilling 150,000/-
Na penalty ni shiling 60,000/=


ENGINE CAPACITY IKIWA NI 2501 - 5000
Utalipia shilling 330,000/=
Penalty ni shilling 105,000/=

ENGINE CAPACITY IKIWA NI 5001 AND ABOVE
Utalipia shilling 175,000/=
Penalty itakuwa ni sh. 66,000/=

Nadhani hapo mtakuwa mmenipata.
 
Sijui Bajaj yangu ina uwezo gani!

Watanzania tumenyamaza mfumuko wa bei unapanda hivi? Hakuna namna ya kuepusha? Bei ya Service Lines imepanda zaidi ya mara mbili, Bei ya Leseni imepanda hivyo, bei za vyakula juu mara mbili, bei za internet zimepanda juu kabisa zaidi ya mara nne.

Tutaendelea kuumia hivi hadi lini? Hakuna suluhu? Mishahara ambayo watanzania waliahidiwa kufikia Novemba itakuwa imepanda (Sekta binafsi) sasa nayo haina dalili za kupandishwa na imepigwa kalenda hadi mwakani, kwanini bei za vitu hivi zisingeanza kupanda baada ya kipato cha mwananchi wa chini kupanda?

Hivi tunaelekea wapi? Mnajua kuwa kupanda kwa leseni za vitu hivi vya moto (motor vehicles) kutapelekea kupanda kwa nauli?

Nauli ya daladala iliyokuwa Tshs 150/= mijini (Kipindi cha mwaka mmoja unusu uliopita enzi za Ben) sasa kimefikia Tshs 350/= na kwa mwendo huo kitafikia Tshs 500/= punde. Nauli ya Taxi (town trips) iliyokuwa Tshs 1,000/= kipindi cha Ben sasa ndani ya mwaka mmoja unusu hivi imefikia Tshs 3,000/- na kwa kuongezeka kwa gharama za leseni utasikia ghafla taxi kwa town trips wanafikia Tshs 6,000/= Mche (mchi?) wa sabuni ya kipande uliokuwa Tshs 250/= kipindi cha Mkapa umefikia Tshs 800/=! Chumba cha kupanga (uswahilini) ambacho kilikuwa ni Tshs 10,00/= kwa mwezi sasa kimefikia Tshs 30,000/= [Kumbuka mshahara haujapanda!] Masikini Tanzania... Oh, my country

Hivi nini hatma ya mtanzania? Masuala haya yanaumiza kichwa na kukatisha tamaa juu ya tuelekeako. Soko la ajira limeachwa linaenda ovyo, waajiri wanalipa wanavyotaka na huku wakikwambia ni soko huria. Soko huria limekuwa si huria tena, hakuna mamlaka ya kulidhibiti. Gharama za maisha zimepanda kuliko kiwango ambacho kinatarajiwa!

Am totally confused!
 
Ndugu zangu watanzania wote mnaomiliki magari hizi ni bei mpya kupata new motor vehicle lecence pamoja na registration za magari pale TRA Bei imepanda kwa asilimia 95%.

Hivi kweli tutafika, mafuta ya gari yamepanda, motor vehicle license nayo imepanda, nasikia na umeme umepanda kutoka 240,000/= mpk 560,000. KWELI HAYA NDIO MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?

ENGINE CAPACITY (0 - 500)
Utalipia shilling 50,000/=
Na Penalty yake ni sh. 30,000/=

ENGINE CAPACITY IKIWA 501 - 1500
Utalipia shiling 80,000/=
Penalty yake ni sh. 42,000/=

ENGINE CAPACITY IKIWA 1501 - 2500
Utalipia shilling 150,000/-
Na penalty ni shiling 60,000/=


ENGINE CAPACITY IKIWA NI 2501 - 5000
Utalipia shilling 330,000/=
Penalty ni shilling 105,000/=

ENGINE CAPACITY IKIWA NI 5001 AND ABOVE
Utalipia shilling 175,000/=
Penalty itakuwa ni sh. 66,000/=

Nadhani hapo mtakuwa mmenipata.

Kusema kweli sirikali ya huyu muungwana imebadili kabisa mfumo wa maisha ya Wadanganyika, kutoka 'bad' kwenda 'worse'. Tunamlaumu Mkapa kuwa kaiba, lakini afadhali maisha yalikuwa na nafuu kuliko ya muungwana, kwani ndani ya miaka miwili tu ya utawala wake maisha yamekuwa hayashikiki. Kila kitu bei juu! Tumejadili sana suala hili katika mada fulani hapo kwenye contribution ya 1.9% ya madini katika uchumi wa taifa. Nadhani hadi kufikia mwaka 2010 lita ya petroli tutanunua hadi 10,000 kwa mwendo huu.
Tufanye nini sasa?
 
Hakuna suruhisho zaidi ya Wadanganyika kuwa na msimamo, Leo hii tunalalamikia mfumuko wa bei.. mwaka 2010 ukifika huyu muuza sura atatudanganya na tutamchagua.

Haya siyo maisha kwa kweli kipindi cha Mkapa ukiacha nyumbani shilling 5,000/= utakula mboga saba na juice juu, sasa hivi bila ya kuacha kodi ya meza 10,000/= chakula hakiliki. maisha yamekuwa ghali sana. sasa niambie kwa mwezi mtanzania wa kawaida anakula 8,000 x 30days = 240,000/= hiyo ni kula tu tena umejibana sana, bado hujapanda daladala, hujampa mtoto hela ya shule, hujanunua luku, hujamlipa house girl wako, na kodi inakusubiri. Mtanzania wa kawaida anapokea kiasi gani aweze kufanya yote haya jamani.

Mimi nadhani imefikia wakati Wadanganyika tuseme basi na tumechoka na maisha haya. Tunaburuzwa sana serikali (CCM) Imetumia pesa nyingi sana ktk kufanikisha kikao chao (NEC) cha kamati kuu.
 
Wandugu,

kwa ufupi asiyekuwa nacho hatakiwi kuwa nacho MILELE. Na mwenye nacho anatakiwa aendelee kuwa nacho MILELE!

Aaaaameeeeeen!
 
Sio feza nyingi,inaonyesha wengi hamjarudi nyumbani kwa muda mreeeeeeeefu,ndio mnaona hayo manamba na matamshi ayalingani na huko mliko mwambieni awape mahesabu kwenye dola mtaona huko mliko mnashida zaidi kuliko hapa bongo.
 
Kuna taarifa nyingine za kodi mbali mbali toka mamlaka ya mapato Tanzania, zinapatikana hapa, [media]http://www.tra.go.tz/documents/KODINA.PDF[/media]

Ni vizuri kuzipitia.
 
Du hata ca kusema sina maana hata sisi tuliokuwa tunadandia mtandao wa TTCL kwenye internet sasa bei ya kudownload imeongezwa kutoka Tzs. 50 kwa 1 MB kuwa Tzs. 300. Mwendeshaji mpya huyo kutoka Canada.

Na tunasubiri bei ya nauli ya treni tu iongezwe, maana mwekezaji mpya lazima ataongeza tu.
 
maisha kwa watanzania ni magumu sana,kwa hiyo viongozi wanachofanya ni kutafuta njia za mkato ilikutatua matatizo.ongezeko la hiyo kodi ni kutokana na kuongezeka kwa magari ktk jiji la dar hivyo kinachotokea ni kupandisha kodi ili kupunguza idadi ya magari barabarani.
Huu mimi nauita ni wizi tena ule wa mchana kweupe na ni ufisadi wa hali ya juu ambao hauwezi kuvumiliwa kabisa.Tumekuwa na kodi nyingi ambazo hazina manufaa kwa wananchi,serikali ilitakiwa kuimarisha kwanza public transport ndipo iweze kupunguza foleni kwa kupandisha kodi kama ilivyofanya.
Au ndio wanaongezea nauli ya jk iliaweze kusafiri bila matatizo.
Mwiba,maisha ya ulaya uwezi kufananisha na bongo hata kwa asilimia moja,kwetu ni jehanamu
 
Nashindwa kuelewa kama bado ile KASUMBA {as said by Mwl.Nyerere} bado ss Watanzania tunao jiita Wadanganyika bado tunayo au ni kwamba tunajiendekeza?
Tumekua na vichwa viguu kuelewa au kupambanua mambo,hapa naona mto maada alilenga hali ngumu ya maisha ktk caurse ya mfumuko wa bei inayo leta kupanda kwa bei ya kila kitu kwa mtanzania mwenye mshahara wa kawaida.
Lakini hapo hapo tuna changany mambomawili kwa wakti mmoja kwa kulinganisha hali ilivyo kua hapo nyuma say mieze 24 iliyopita.Kwa maana nyingine utwala wa Bwn.Mkampa kulinganisha na Ndugu Kikwete,Naomba tuweke base ya mazungumzo au discussion hii ili tuje na conclusion ya maana na ya ukweli n a sio kua na Kasumba ya kuamini tuombiwayo na na wanayoytaka yawe hivyo.
Kwanza Ngugu mtoa maada na wachangiaji mliotangulia lazima tuelewe,NYUMBA HAIJENGWI BILA YA KUWEKA MSINGI, hapa ni na maana maatatizo au hili tatizo tulilo nalo sasa sio salwa la kumlaumu huyu Muungwana kwani yy ameichukua nchi tayari na matatizo yake ikiwemo huu UFISADI ambo ndio root ya kila ulionalo leo.Ukitaka jenga nyumba lazima uanze na msingi! msingi wa tatizo hili umejengwa miaka 6-7 nyuma kabla ya muungwana haja pewa nafasi ya kuuza sura.Mkapa ndio aliweka Msingi wa haya yote.Nakumbuka Mwl.wangu Economics shule alisema "Factor moja ya uchumi sio kama shoti ya umeme kwamba ukiwasha switch hapo hapo utaona cheche,ila it takes time mpaka impact ije kuwa revealed"
Chukua Epoch ya vipindi vya utawala wa hao waheshimiwa na otaona nini ninacho jalibu kupigia mstari,na kama kweli lazima tuwe na msingi ili tujenge jumba basi kimtazo kwa angle hii ni dhahili kwamba The beloved Mkapa ndio kiini cha tatizo.
Kama mtakumbuka au vile ijulikanavyo mwanzoni kabisa wa kipindi cha tatu cha utwala wa nchii hii Ilielezwa kwamba Raisi Mkapa ameilithi nchi ikiwa na mzigo kumkubwa wa MADENI ya NNJE amboyo wametokana na utawala mbovu wa MZEE RUKSA,natuliambiwa hii nikutokana na misingi mibovu ya uchumi wa zama za mzee yule. Tulikubaliana na hili pale tulipo takiwa kufunga mikanda kwa ajiri ya kuruhusu serikari kukusanya pesa za kulipa madeni hayo ambayo yanaendelea kulipwa mpaka leo hii,kiasi cha kuambiwa siku chache zilizo pita ili kilipa deni lote watanzania wote mpaka watoto wao walipe laki 4 na wale Watz walio nnje kila mmoja alipe sijui dola ngapi!
Sasa ni misingi ile ile Mibovu ya Bwn Mkapa kama ilivyo kuwa kwa bwana Ruksa iliyo letelea kufikia hapa tulipo.INFLATION ya kufa mtu unajikuta mwananchi wa kawaida unabeba mizigo ya serikari.So please Ndg.Dk stop bealeving on divine ruler sababu hakukuwepo na hakutokuwepo kama mtaendelea kujidanganya wenyewe ya afadhali ya furani...!Mm naita hiyo kasumba nnjooni kwenye dinia ya ukweli na anzeni kufocus baada ya kuamini muuambiwayo.Tuliweka misingi ya hayo huko nyuma sasa ndio nyumba inakaribia kwisha.
Sitaki nieleweke kama na jaribu kumtetea huyu bwana Muungwana NO! ila still kama anataka kuwa serious na kubadili hii hari anayo chance kwani ni muda mchache tu toka amepata nafasi ila yy na aliye tangulia are from the same ZOO sitoshaangaa akiwa ndio walewale.
Ni mawazo tu...!
 
Sijui Bajaj yangu ina uwezo gani!

Watanzania tumenyamaza mfumuko wa bei unapanda hivi? Hakuna namna ya kuepusha? Bei ya Service Lines imepanda zaidi ya mara mbili, Bei ya Leseni imepanda hivyo, bei za vyakula juu mara mbili, bei za internet zimepanda juu kabisa zaidi ya mara nne.

Tutaendelea kuumia hivi hadi lini? Hakuna suluhu? Mishahara ambayo watanzania waliahidiwa kufikia Novemba itakuwa imepanda (Sekta binafsi) sasa nayo haina dalili za kupandishwa na imepigwa kalenda hadi mwakani, kwanini bei za vitu hivi zisingeanza kupanda baada ya kipato cha mwananchi wa chini kupanda?

Hivi tunaelekea wapi? Mnajua kuwa kupanda kwa leseni za vitu hivi vya moto (motor vehicles) kutapelekea kupanda kwa nauli?

Nauli ya daladala iliyokuwa Tshs 150/= mijini (Kipindi cha mwaka mmoja unusu uliopita enzi za Ben) sasa kimefikia Tshs 350/= na kwa mwendo huo kitafikia Tshs 500/= punde. Nauli ya Taxi (town trips) iliyokuwa Tshs 1,000/= kipindi cha Ben sasa ndani ya mwaka mmoja unusu hivi imefikia Tshs 3,000/- na kwa kuongezeka kwa gharama za leseni utasikia ghafla taxi kwa town trips wanafikia Tshs 6,000/= Mche (mchi?) wa sabuni ya kipande uliokuwa Tshs 250/= kipindi cha Mkapa umefikia Tshs 800/=! Chumba cha kupanga (uswahilini) ambacho kilikuwa ni Tshs 10,00/= kwa mwezi sasa kimefikia Tshs 30,000/= [Kumbuka mshahara haujapanda!] Masikini Tanzania... Oh, my country

Hivi nini hatma ya mtanzania? Masuala haya yanaumiza kichwa na kukatisha tamaa juu ya tuelekeako. Soko la ajira limeachwa linaenda ovyo, waajiri wanalipa wanavyotaka na huku wakikwambia ni soko huria. Soko huria limekuwa si huria tena, hakuna mamlaka ya kulidhibiti. Gharama za maisha zimepanda kuliko kiwango ambacho kinatarajiwa!

Am totally confused!

Tell me about it invisible,
Kuna watu wanadai kuwa miaka miwili haitoshi kujadili mwelekeo wa sasa lakini hali ya maisha inatisha!

I am confused too and angry
 
Mimi naona hivyo viwango vipya sio vikubwa ukilinganisha na aina za magari na watu wenyewe wenye uwezo wa kumiliki magari hayo.

Hasira yangu ni kwamba hivi hela hazienda kwenye matumizi ya busara kuendeleza barabara na njia nyingine za kuinua uchumi wetu; watu wajanja wachache watajenga nyumba zao mikocheni na mbezi beach...
 
..matumizi makubwa = kupandisha kodi!

..matumizi makubwa = kuomba misaada!

..matumizi makubwa = kuua uchumi tartiibu!
 
Tena naona bado tuna-charge kidogo sana,

Kila mwaka kila mwenye gari na alipe yafuatayo:

1.Vehicle Inspection Charges - Traffic department ianzishe centre mbali mbali za kufanyia hii inspection ambako kila mwaka magari yatakuwa yanakaguliwa na kulipia huko.

2.Kila mwenye gari na alipie kila mwaka hiyo Moto vehicle license.

3. Kwa gari ambalo litashindwa ku-meet the standards they should pay more na wahakikishe gari linafanyiwa maintenance ili liwe worthy barabarani kabla halijaruhisiwa kurudi barabarani

4.Serikali iimarishe Public Transport.........this is very important

5.Utoaji wa leseni za madereva uwe computerised na kuwe na data base ya madereva wote............mwenye kukutwa na makosa mawili ....driving license yake iwe suspended kwa mwaka or two depending na aina ya kosa..............na mtu akikutwa anandesha bila ya leseni (wakati anayo).......basi apigwe faini ya $500 akishindwa atumikie kifungo miezi sita (6)..........ambaye hana leseni kabisa atumikie kifungo pamoja na faini $500.

6.Toa marupurupu kwa jeshi letu la Polisi kama vile maofisa wa Idara nyingine nyeti wanavyopata

7. Ongeza parking charges iwe kuanzia TShs 1000 mpaka 3000 depending na maeneo.....mfano itengenezwe parking lot kubwa sehemu kama jangwani mtu akipaki pale jangwani alipe TShs 1000....akienda mjini kati alipe TShs3000

Wakati huu serikali inapohangaika na congestion solution.....vile vile inge-impose hayo ninayoyapendekeza hapo juu................thats should be the practice kwa sababu

1. Itasaidia kupunguza ajali barabarani kwa kuondoa madereva wazembe
2. Itaongeza pato la serikali
3. Itasaidia Mazingira na afya zetu

serikali wakihitaji msaada wa mawazo zaidi ktk hii ishu contact Ogah through JF
 
1. Itasaidia kupunguza ajali barabarani kwa kuondoa madereva wazembe
2. Itaongeza pato la serikali
3. Itasaidia Mazingira na afya zetu

LoL,

Kaka ingekuwa inafanyika hivi mbona hakuna wa kupigia kelele? Mwenye kumiliki gari hili si tatizo kubwa kwa Tz, tatizo kubwa ni kuwa wale wanaomiliki magari ya kusafirisha abiria ama mizigo watabamiza raia si kawaida. Upo nipo, wanajibu "Ni biashara huria"
 
Unajua ni Invisible

Ubinafsi wa mapato na mawazo ndio unaotuua siku zote na wananchi kwa ujumla wake hutaabika.............

the same way kama watu wanavyonunua share ktk mashirika mbali mbali, ndivyo ambavyo nasi Tanzania ktk sector ya transport tulitakiwa tufanye, unda makampuni solely walau mawili au matatu kwa ajili ya Transportation..............., na iandaliwe policy kabisa ya kwamba Transporation vessels should meet THESE STANDARDS a, b, c in the company formed (very simple....), kwa hiyo makampuni yatakayo anzishwa yatakuwa na kazi ya kuhakikisha those standards are met (whatever the case may be). unaondoa ukiritimba wooote wa vipanya na vurugu za main transport stations nchini.

mfano rahisi tuliona Scandinavia Buses............watu wanatakiwa kuunganisha nguvu na kuform shirika kama hilo.....ambalo kutokana na share yako ndivyo utakavyopata faida.....na hakuna kinachopotea (interms of faida) hata ungekuwa unaoperate kivyako!!....then kunakuwa na utaratibu mzuri wa Timetables etc etc........

TRUST ME Invisible this one works perfectly..........uliza sehemu yeyote yenye system ya PublicTranspotation inayofanya kazi sawasawa watakuambia thats the idea

Tukiwa serious (Serikali)............mambo mengi tutayakokotoa

Contact Ogah through JF kama unahitaji msaada wa mawazo zaidi ya hapo
 
NOTE:
tena hilo wazo la parking lot pale jangwani na sehemeu nyingine.........serikali wala haihitaji kutumia pesa yake hata senti moja...................serikali tangaza zabuni za aina ya BOT (Build Own Transfer) then serikali you just collect revenue thats all
 
Kusema kweli sirikali ya huyu muungwana imebadili kabisa mfumo wa maisha ya Wadanganyika, kutoka 'bad' kwenda 'worse'. Tunamlaumu Mkapa kuwa kaiba, lakini afadhali maisha yalikuwa na nafuu kuliko ya muungwana, kwani ndani ya miaka miwili tu ya utawala wake maisha yamekuwa hayashikiki. Kila kitu bei juu! Tumejadili sana suala hili katika mada fulani hapo kwenye contribution ya 1.9% ya madini katika uchumi wa taifa. Nadhani hadi kufikia mwaka 2010 lita ya petroli tutanunua hadi 10,000 kwa mwendo huu.
Tufanye nini sasa?

Service expenditure serekali imekuwa kubwa kuliko uzalishaji, maana kila kukicha Transfer za Viongozi iwe ubalozi etc, na matumizi mengine ya safari bila kufanya tathimini ya faida na hasara ya ya kitendo hicho, watu wataserma oh in the long run , but any investment policy should go in the following basis long term return inakwenda na long term investment, short term results in kwenda na short term investment, eg eg transfer za watu muhimu zinatakiwa kuwa planed maybe 3 to 5 years, sio mwaka moja then mtu anahamishwa, then hata creation za position kama mawaziri na deputy, sasa matokeo yake tuna establishment kubwa ambayo haiendani na hali ya uchumi wetu.
 
Nyie mnachekesha sana, hivi mnategemea hawa wajamaa wafanye nini wakati wana li-serikali likubwa, wanapenda matanuzi, halafu hawana muda wa kufikiri kubuni na kupanua tax base-mnataka hizo watoe wapi? Si lazima wawakamue haohao walio nacho wachache. Tena hii haina athari kabisa kwa sababu wananchi vijijini hawaigusi, wala hawajui hicho kitu ni kitu hasa wakati wao hata mkokoteni hawana!

Tutalalamika sana hadi tutakapochukua hatua madhubuti za kukitoa hiki chama. Wakati tukisubiri basi ndiyo hivyo: bora maisha kwa kila mtanzania!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom