Beating the Drum on One Side: Confusing the People on Both Sides

Beating the Drum on One Side: Confusing the People on Both Sides

Inferiority complex at work, Nyerere alikuwa na nia njema kutokuruhusu hayo mnayoyataka.. Kwanini waislamu kote duniani ndio wanahangaika, eti 'holy war'..kama dini yenu inaweka wazi kwamba asiyekubaliana na uislamu auwawe, sasa huo si udikteta..
 
Wanajamvi,
Mimi haikunipitikia wakati ule kama iko siku ilm ile nilosoma
chuoni yaani madrasa itakuja kunifaa mimi na jamaa zangu.

Hivi sasa kuna watu wamerudi na matusi...

Maalim Haruna alikuwa akisema, "Mtu hatukani ila pale anapokuwa
kahamaki.

Ukiona hivyo basi muache hadi ghadhabu zake zimepoa ndipo
ikiwa unaona ipo haja ukaendelea na mnakasha."

Nimemueleza Lusungo historia ya 1947 - 1954 kilipitika nini katika
maisha ya Abdul kuja kuunda TANU 1954.

Katika kisa hiki nikawaleta wazalendo wawili muhimu katika
kuwaelewa wanasiasa waliokuwapo baada ya WW2 - Chief Kidaha
Makwaia na Julius Nyerere na vipi waliingiliana na Abdul Sykes
katika kutafuta uongozi wa kuwavusha Waafrika kuelekea kuunda
TANU na kudai uhuru.

Sikutegemea matusi na kejeli.
Nilitegemea mnakasha utanoga kwa maswali zaidi...
 
'islam' means 'peace'.where is that peace..penye nia pana njia na penye mwislam asiyejielewa kuna vita..wakristu, wabudha, wapagani n.k ndio wanahubiri na kutenda 'amani'..
 
Shida yako kubwa hutaki kutoka kwenye box, sasa twende taratibu,
Kwani Maji Maji walipigana na Waingereza?
Unaedandia treni ni wewe mswahili kwa sababu unashupaa na makosa aidha ya kiherufi lakini hili swala langu hujalijibu, nimeuliza hivi

Mohamed Said anaamini Juhudi za kupigania uhuru wa Tanganyika zilifanywa na Waislamu, je unakubaliana na hili?.

Nipo Pembeni kwenye mkeka hapa nachoma mahindi nakusubiri

Mie nimekuuliza swali linakuwa gumu sana kwako kujibu? Kwanza jibu swali langu halafu ulete hayo yako, ndiyo raha ya mnakasha, au unaonaje?

Jee, Mau Mau walipigana na Mjerumani?
 
'islam' means 'peace'.where is that peace..penye nia pana njia na penye mwislam asiyejielewa kuna vita..wakristu, wabudha, wapagani n.k ndio wanahubiri na kutenda 'amani'..

OK tumekusoma.

Jee, Mau Mau walipigana na Wajerumani?
 
Lusungo,
Unafikiri sawasawa na mimi siwezi kukulaumu kwa hilo.
Mantiki inaweza ikaangushwa na kitu kingine.

Ungejua kadi za TANU zilivyogawiwa ungelijua na kwanini Abdul mkubwa
kapata kadi na. 3 na Ally mdogo kadi yake ni na. 2.

Kadi ya Nyerere ilikuwa lazima iwe na. 1 kwa heshima yake kama rais
wa TANU.

Kadi zile zilinadiwa.
Mwenye dau kubwa anatangulia kuchukua kadi.

Hukuyajua haya.
Ndipo nikasema nakuwia radhi na mantiki si inakuwa sawa muda wote.


Ahsante MS

Ninachokupendea ni kwamba huna jazba na unaelewa nini unafanya...

Unaelewa takwa la MTU na unajitahidi kutimiliza...

Sisi wengine humu hatuingii kwaajili ya Kejeli au matusi tunataka elimu na fafanuzi zitakazoondoa contradictions ktk mind set zetu.

Ahsante kwa muda wako.
 
Lusungo,
Hili jina linanikumbusha marehemu mdogo wangu Ibrahim.

Alikuwa na rafiki yake anaitwa Joseph Lusungo akipiga trumpet
NUTA Jazz miaka ya 1970.

Urafiki wao ulikuwa katika kucheza draft na walikuwa na barza
yao.

Ibrahim alichukua 1st prize best student in Chemistry miaka 3
mfululizo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Lusungo nae pia kesha tangulia mbele ya haki.

Ahsante kwa yote kaka.
 
Mkuu Mohamed Said

Hoja alizotoa Prof. Karim Hirji zinazima madai yako yote unayotoa sehemu mbalimbali juu ya kile unachokiita "kuonewa kwa waislam Tz". Hisia za UDINI ndio zinakuongoza. Na kwa jinsi hii ni ngumu kushawishi umma wenye kuweza kupambanua ukweli ni upi. Hoja zako ziko bias sana hata mtoto wa primary atatambua wewe ni MDINI. Ndiyo, wewe ni mdini kwa sababu unafungamanisha hali mbaya za waislam hapa nchini kuwa ni matokeo ya "mfumo Kristu" kitu ambacho si kweli. UNAWAGAWA WATANZANIA.

ACHA MARA MOJA.
Tehe! tehe! tehe!
Du! sina mbavu!!!!!
 
OK tuekusoma.

Jee, Mau Mau walipigana na Wajerumani?

Tatizo lililokutokea hivi punde la kuandika tuekusoma badala ya tumekusoma, naam linaweza kua limemtokea Prof Hirji badala ya kuandika Maji Maji akaandika Mau Mau.

Hata Mohamed Said hajishupalia hilo, kwa nini sasa usiende kwenye swali langu
 
Last edited by a moderator:
Mie nimekuuliza swali linakuwa gumu sana kwako kujibu? Kwanza jibu swali langu halafu ulete hayo yako, ndiyo raha ya mnakasha, au unaonaje?

Jee, Mau Mau walipigana na Mjerumani?

Hapana alipigana na Muingereza, sasa zamu yako
 
Mkuu turudi zetu kwa Matola huku hupawezi

Mkuu nafahamu sipawezi ila nahitaji kupaweza ili nijue...

Kutopaweza dawa yake si kukimbia ila kutujitahidi kupaweza...

Sikuingia hapa kukejeli laa... Nimeingia ili nijue na kwa bahati nzuri ndugu MS anaweza mjuvya MTU.
 
Last edited by a moderator:
Kama mwathirika mmojawapo wa hii lugha nimejitahidi kulisoma hili andiko na limenipa mwanga zaidi.
Ubabaishaji umekuwa mwingi Tanzania mpaka wanaibuka waandishi na analysts wababaishaji kati masuala nyeti kabisa ya kitaifa. Na kibaya zaidi wapo waliojipenyeza mpaka kwenye nafasi za kufanya maamuzi wanaowasujudia hawa watafiti wababaishaji na wenye malengo yao maalumu.
Asante sana Prof. Hirji kwa kujariju kurudisha mambo katika mstari.
 
Prof. Karim Hirji ameandika kisomi sana,hajabeba jazba za kidini. Hivi ndivyo namna wasomi wanavyotakiwa kujitofautisha na walalamishi.

As the author of the article being discussed, I would like to make a few important corrections and points:

1. There was an unfortunate typographic error; in haste I wrote Mau Mau instead of Maji Maji. I apologize
for this error on my part.
2. The version of my article on this website is an INCOMPLETE VERSION. THE FINAL SECTION INCLUDING
THE CONCLUSION HAS BEEN CUT OFF. SO THE FORUM MEMBERS HAVE NOT GOT THE FULL STORY. I
HAVE SENT THE FULL VERSION TO THE MODERATOR. PLEASE READ IT.
3. My main aim is not to contest historic details but to expose an erroneous way of thinking.
4. I am not pro-Christian, pro-Muslim, pro-Hindu etc. but simply pro-Tanzania who wishes to see
mutual harmony and tolerance between all religions, creeds, races, ethnicities, etc.
5. As I write in my conclusion, I regard Mohamed Said as a key intellectual voice in our society
who needs to be heard.
6. But if anyone including him promotes flawed views, we should be free to criticize them.
7. Let us discuss important issue affecting our nation in a brotherly sisterly spirit. Otherwise, if we
fight among ourselves on narrow grounds, only the enemies of the nation and exploiters of the
common person will benefit.

Prof. Karim Hirji
 
Hoja ipi ya kujibiwa? Hirji ka criticize, kaulizwa maswali mawili tu, hajajibu mpaka sasa au wakala wake KVM hajajibu, kakwepa.

Mimi binafsi nimeonesha mapungufu ya maandiko ya Hirji ambayo hakuna aliyekuja na jibu, kuna mmoja tu kaja kasema hizo data kweli za kufikirika. Unajuwa hiyo maana yake nini kisomi? maana yake criticism ya Hirji yote inafaa itupwe kwenye garbage bin.

Lakini ili tuwape wengi faida na darsa, tutauendeleza mnakasha tartiiiiibu tuwape darsa, nnauhakika wengi wenu mtafaidika, maana mnaonesha kuwa wengi wenu hamko katika kiwango cha usomi wa kuweza kukabiliana na minakasha ya kisomi na hii ni fursa yenu kujipatia mawili matatu.

Professor Hirji, kwa kushindwa kuelewa tu Mau Mau na Wajerumani ni kama mbingu na ardhi na akaandika hivyo katika hizi pumba zake anaonesha kuwa ni Professor bogus (with all due respect).

Na hilo la kukiri kwake kuwa ana criticize kwa kutumia "hypothetical... data..." ndiyo kama nilivyokueleza awali, na laiti ingalikuwa kaileta hii criticism kwenye jopo la wasomi na kuna Mwenyekiti, Mwenyekiti tayari angeshamwambia "shut up, seat down and listen to other scholars".

Nawahurumia sana wanafunzi wanaofundwa na "Professor" kama huyu Hirji, hakuna zaidi bali wanajazwa ujinga tu.

Mash'kuura yaa ukh'y FF.

Hata mimi naingia wasi wasi na huo U-Profesa wake isije kuwa kama ule wa Maji Marefu.

Mwenye CV yake jamani naomba tafadhwali aiweke hapa. Tusije pata dhunuub kwa dhan'na.

 
Tatizo lililokutokea hivi punde la kuandika tuekusoma badala ya tumekusoma, naam linaweza kua limemtokea Prof Hirji badala ya kuandika Maji Maji akaandika Mau Mau.

Hata Mohamed Said hajishupalia hilo, kwa nini sasa usiende kwenye swali langu

Mau Mau na maji maji na typo ya kukosa kuchapa herufi moja wapi na wapi?

Nataka ujibu wewe, achana na Hirji, hana jipya. Mau Mau walipigana na Mjerumani?
 
Kama mwathirika mmojawapo wa hii lugha nimejitahidi kulisoma hili andiko na limenipa mwanga zaidi.
Ubabaishaji umekuwa mwingi Tanzania mpaka wanaibuka waandishi na analysts wababaishaji kati masuala nyeti kabisa ya kitaifa. Na kibaya zaidi wapo waliojipenyeza mpaka kwenye nafasi za kufanya maamuzi wanaowasujudia hawa watafiti wababaishaji na wenye malengo yao maalumu.
Asante sana Prof. Hirji kwa kujariju kurudisha mambo katika mstari.

Mau Mau walipigana na Mjerumani?
 
mie nimekuuliza swali linakuwa gumu sana kwako kujibu? Kwanza jibu swali langu halafu ulete hayo yako, ndiyo raha ya mnakasha, au unaonaje?

Jee, mau mau walipigana na mjerumani?

na omba msamaha wenu. Haata profesa anaweza kufanya kosa la kitoto. Maana yangu ilikuwa
maji maji lakini kwa haraka niliandika mau mau.
Lakini kosa dogo kimoja kama hilo haliwezi kupindua logic na ukweli wa makala mzima.
Ni wale ambao hawataki kufikiria mambo kwa kiundani ndiyo watayanganganyia makosa madogo
madogo.

Prof. Karim hiri
 
Nani alipigana na Muingereza? hivi hata kuandika sentensi kamili mnashindwa? hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Hahaha we mama nachelea kusema uwezo wako wa kuargue mambo ni mdogo,

kfhirji ameshaomba radhi kwa alichoandika Mau Mau badala ya Maji Maji, ambao hatujashikwa na Dini tukakuambia ni makosa madogo madogo,

Sasa punde tu wewe mwenyewe umekosea badala ya kuandika Tumekusoma, ukaandika tuekusoma.

Mbona Banzi lililopo jichoni kwako inakua ngumu kuliona?

Bado hujajibu Swali langu, nmekuuliza hivi

Mohamed Said anaamini Uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa na Waislamu, Je unakubaliana na hilo.

Nimejibanza Hapa mtaa wa Uhuru karibu na duka la mshihiri huku nikila kashata baada ya kuchoma mahindi kwa muda sasa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom