Which Civilians ? Kikwete, RA. We need to end this fckn hereditary successions...kila Siku ni mwinyi kikwete na wajukuu waje watutawale just to protect their Cake...ona sasa hivi familia ya Samia nayo ishaingiza wabunge wa familia 🗑️
Hata Museveni ni mwanajeshi, jeshi kakabidhi kwa mwanae.
Hata Salva Kiir ni mwanajeshi, anamtoa cheo mwanae anamuweka mume wa mwanae.
Nepotism haiishi tu kisa jeshi liko madarakani, mbona humohumo jeshini wanapelekana kozi na command watoto na ndugu wa maofisa, sasa wakipata madaraka makubwa zaidi si wanafanya yaleyale.
Hakuna utofauti wowote wa kitabia baina ya jeshi na wananchi ni kwamba tu jeshi lina sheria zinabana wanajeshi.
Unaona Israel ilivyo, raia na wanajeshi wana tabia zinafanana ndio maana nchi sometimes huwa inaongozwa na retired military officers na sometimes raia na tofauti hamna. Vilevile kwa Nigeria, hakuna utofauti wa tabia huwa unaonekana baina ya military juntas na tawala za kiraia ila tu tawala za kiraia huwa zinabanwa kama ambavyo Goodluck Jonathan alishindwa uchaguzi, au Musa Yar'Adua alivyofariki hakuna risasi ilirushwa au mtu kunyongwa.
Sasa huwezi kuwa na jamii mbovu kwa asili alafu eti jeshi pekee ndio liwe zuri ila polisi wabovu, wanasiasa wabovu, walimu wabovu, madaktari wabovu. Sasa hilo jeshi ni la mamluki au uzao uleule?
Kama hakuna control kwa utawala unategemea nini. Likiingia jeshi sahau kuhusu Lissu wala Polepole. Utasikia majina yaliyokuwa kambini ambayo hayajali lolote kuhusu good governance, uchumi, sheria, haki za binadamu. Yenyewe yanakariri utii no matter what, yaleyale ya Pakistan mkuu wa shirika la umeme alikuwa Major/Brigadier General wa mizinga, hajui lolote kuhusu nishati.