BCom ya UDOM mashaka matupu - Department Haina Majibu

Kwanini tatizo lisitatuliwe? Hivi chuo kikubwa kama hicho , majengo ya kutisha halafu elimu duni maana yake nini? Mgt inashindwa nini kutafuta ufumbuzi? Tunataka quality education na siyo mradi degree tu za bila viwango, fanyieni kazi haraka hilo tatizo acheni siasa siasa zenu
 
Wewe umeorodhesha maBcom mengi na unasema 1 ndiyo yenye matatizo alaf hauitaji ni ipi kati ya hizo,ni afadhali nimuamini mtoa uzi kuliko wewe maana unatoa habari nusu nusu,na hausemi kwa nini hiyo Bcom.1 ina matatizo.

haujaelewa kwa sababu maana ipo ndani ya maeleza na sijaiandika peupe kama ukisoma hiyo post na kuunganizha na mleta uzi ungenielewa. Kwa kifupi ni hiyo b.com account.
 
kuna watu wanaongea vitu alafu hawana ufahamu navyo,ni vyema mkauliza kisha kabla ya kutupia post,udom kama udom hakuna kozi inayoitwa bcom,na department ya business studies ilichokuwa inataka ni udom kuwa exmpted,kuwa exempted mana ake wahitimu(hususan wa bcom accounting)kuanza na module E Badala ya module A,na NBAA hawakukataa kukisajili bali kiliwaambia wafate syllubus yao na ndo mana utaona(2012/2013) account & finance ya udom imekuwa ya kibaba zaidi,na hivi sasa chuo kimekuwa exempted na kuna wana kibao wa udom washalamba iyo Module E wanafukuzia F,kwa iyo ushauri wangu watu tusiropoke ropoke mambo tusiyoyajua,mnatuharibia sokoni ni vyema muwaache wenye kujua waongee mambo haya,na kama kuna mtu ana mashaka na account ya udom atafute wadhamini itungwe pepa yoyote anayotaka ikatungwe popote kule afu tukae ubaoni man 2 man.
 
ninachojua ni kwamba wanafunz wa udom wanaanzia module E na rafiki zangu wengi teyari wameshagraduate huko NBAA walisoma Bcom accounting udom na kwa taarifa ni kwamba mkuu wa department sio tena Njiku kwa sasa ni mwingne anaitwa Mwakapala yeye ana kiwango chake cha elimu ni ngazi ya master
 
Mitihani imejaa clues tupu!wahadhiri bado wachanga sana!kina profesa osa-ki wawekeni vijana sawa!
 
Imefahamika kuwa, pamoja na kusajiliwa na TCU, kozi ya BCom inayotolewa na UDOM haitambuliwi na bodi za wataalamu (Professional Bodies kama NBAA, NBMM etc).
Hilo bado halijathibitishwa kwa kozi nyingine ukiacha BCom.
Habari za kuaminika kutoka NBAA zinasema UDOM bado hawakidhi 'vigezo' vya kutambulika japo haikutanabaishwa kwa wazi vigezo ni vipi.
Imeelezwa kuwa NBAA walikuwa na vyuo viwili vinavyoomba kutambulika (UDOM na St.John), lakini ilipitisha uamuzi wa kukitambua St.John na kukikataa UDOM.
Department inayohusika na BCom walipojaribu kuulizwa kuhusu hilo swala walisema, "hawajui". Vilevile, mkuu wa hiyo idara (anayefahamika kwa jina la Anna Njiku) amekuwa mara kadhaa akikata simu za wanafunzi waliomaliza wanaoulizia hilo suala.
Zaidi ya yote, idara hiyo imeelezwa kusambaza taarifa za uongo kwa wanafunzi wa BCom walioko chuoni kuwa tayari wamepata usajili. Mpaka sasa wanafunzi hao wanafikiri mambo yao ni mazuri, huku bodi zikithibitisha tofauti.
Taarifa kutoka NBAA zinaeleza kuwa, wao wanatambua Diploma ya biashara itolewayo na CBE ni bora kuliko BCom itolewayo na UDOM. Watu waliomaliza hiyo Diploma wameruhusiwa kuanzia ngazi ya module C, lakini watu toka UDOM wameambiwa wao ni ngazi ya module B.
SWALI: Je, waajiri wataendelea kuwachukua wahitimu waliokataliwa na professional bodies?

Ngoja engmtorela mtetezi wa UDOM akusikie.
 
Mnaniacha hoi na masomo ya biashara!yaani hamtambuliki mpk mpitie NBAA na PSPTB,wakati Geology,education,wildlife,molecular biology,economics,statistics ukimaliza unapeta2.
Ushauri kwa wanaopenda kuajiriwa especially waliosoma PCB,CBG soma livestocks,agric,pharmacy etc. adv.math e.g EGM,PCM,PGM etc.haina haja ya kubanana ktk accounts,procurement.soma B.A STATISTICS au MONITORING&EVALUATION,hautasumbuka sana kupata ajira.usiangalie majina ya kozi.UHASIBU,PROC. kila mtu anakimbilia,matokeo yake hadi uje utambulike ufanye mitihani mingiiii!
 
mnaniacha hoi na masomo ya biashara!yaani hamtambuliki mpk mpitie nbaa na psptb,wakati geology,education,wildlife,molecular biology,economics,statistics ukimaliza unapeta2.
Ushauri kwa wanaopenda kuajiriwa especially waliosoma pcb,cbg soma livestocks,agric,pharmacy etc. Adv.math e.g egm,pcm,pgm etc.haina haja ya kubanana ktk accounts,procurement.soma b.a statistics au monitoring&evaluation,hautasumbuka sana kupata ajira.usiangalie majina ya kozi.uhasibu,proc. Kila mtu anakimbilia,matokeo yake hadi uje utambulike ufanye mitihani mingiiii!

hujielewi kweli wewe , hata engineers wana erb, lawyers wana school of law
 
Back
Top Bottom