BBC waianika Tanzania tena!

BBC waianika Tanzania tena!

My be research yako ulikuwa unaifanyia baa,na mlivyozoea kutuandikia habari za kugoogle sidhani kama ulifika field wewe.
Inawezekana kabisa hakufanya vizuri hiyo research yake au mtazamo wake uko tofauti na wengi tunavyojua kuhusu child labour.
 
Yaani wewe ni journalist kumbe hata upeo huna kabisa....hujui hata maana ya child labour..hata wanaouza mayai chalinze ni child labour hata kama ni mitaji yao...jielimishe usije jidharaulisha tena

Haya sasa matusi! Suala la ajira mererani kwa watoto si kubwa wala la kulazimishwa. Kuna watoto nilibaini wamefiwa wazazi wote. Hao wanaingia pale kuchakuachakua kama ilivyo sehemu nyingine. Ninachokataa ni kile cha kuonesha kama child labour ya pale ni jambo lililobarikiwa na vyombo husika au na matajiri wa migodi.
 
Matusi hayasaidii. Mimi nimesema nyoka hawazami. Wanaokoteza mabaki nje tu
Pale kuna vyama kama arema na tamida vinazuia watoto kuzama. Walioko nje ni kawaida kama ilivyo kwenye fukwe ambako kuna watoto wengi au ktk masoko.

Manyerere mimi sijaenda huko na kukaa miezi miwii kama wewe lakini nakuhakikishia BBC hawajakurupuka na wala hawatumiwi na hao uliowataja. Just wait and see. By the way, hao watoto wakiokota huko nje kama unavyodai bado kuna kwenda shule kweli hapo? Juzi juzi msomali wa nyara zetu za taifa alikuwepo huko lakini sikumbuki hili kusemwa kama moja ya changamoto-Thanks to BBC for surfacing this crucial matter maana naona future ya watoto wa walalahoi imeachwa ikatumbukie shimoni bila msaada wowote.
 
Baada ya kufanikiwa kwenye pembe za ndovu, BBC wametukung'uta tena. Safari hii ni kwenye madini ya tanzanite. Wanadai tanzanite inachimbwa na watoto. Wameweka video ya "the gemstone mined by child labour". Huu utakuwa ni mkakati wa makaburu wa tanzaniteone ambao mara zote wameutangazia ulimwengu kuwa tanzanite yao pekee ndiyo halali maana haichimbwi na watoto. Hili ni pigo jingine kwa ndugu zetu wanaotegemea tanzanite kuendesha maisha yao.

Manyerere Jackton huwa ni mhariri nchumia tumbo ngoja watuanike maana ninyi wahariri wa Tanzania mnaogopa kuandika mambo kama hayo, suala la watoto kuchimba madini lipo sehemu nyingi nchi hii hebu nenda Mkuyuni na Matombo Morogoro utajiaonea mwenyewe
 
Baada ya kufanikiwa kwenye pembe za ndovu, BBC wametukung'uta tena. Safari hii ni kwenye madini ya tanzanite. Wanadai tanzanite inachimbwa na watoto. Wameweka video ya "the gemstone mined by child labour". Huu utakuwa ni mkakati wa makaburu wa tanzaniteone ambao mara zote wameutangazia ulimwengu kuwa tanzanite yao pekee ndiyo halali maana haichimbwi na watoto. Hili ni pigo jingine kwa ndugu zetu wanaotegemea tanzanite kuendesha maisha yao.

kwani ni uongo haichimbwi na watoto?? point hapa ni tanzanite kuchimbwa na watoto.....startv washaonesha sana documentary fupi ya watoto wa mererani, mbona hio hukuwahi kuizungumzia au kwasababu hii ni bbc?
 
Manyerere mimi sijaenda huko na kukaa miezi miwii kama wewe lakini nakuhakikishia BBC hawajakurupuka na wala hawatumiwi na hao uliowataja. Just wait and see. By the way, hao watoto wakiokota huko nje kama unavyodai bado kuna kwenda shule kweli hapo? Juzi juzi msomali wa nyara zetu za taifa alikuwepo huko lakini sikumbuki hili kusemwa kama moja ya changamoto-Thanks to BBC for surfacing this crucial matter maana naona future ya watoto wa walalahoi imeachwa ikatumbukie shimoni bila msaada wowote.
Hivi kwa maono yako kuna serikali ya kuwasaidia hawa watoto? Nani awapeleke shule? Hata marekani haijaweza na ndiyo maana inao wasiojua kusoma wala kuandika. Kama kujifungua tu hatuwezi kugharimia, hiyo shule na chakula serikali itaweza? Wale watoto wanatafuta kuishi. Hawawezi kufia ndani ilhalu kuna kuchakuachakua mchanga ili wapate kula.
 
Matusi hayasaidii. Mimi nimesema nyoka hawazami. Wanaokoteza mabaki nje tu
Pale kuna vyama kama arema na tamida vinazuia watoto kuzama. Walioko nje ni kawaida kama ilivyo kwenye fukwe ambako kuna watoto wengi au ktk masoko.

Uchimbaji siyo lazima ubebe sululu hata ukichekecha au kubeba viroba vya mawe nawe ni mshiriki hapo inaonesha jinsi ulivyo na uelewa mdogo wa shughuli za madini.
 
Wewe Manyerere utakua ulifanya utafiti huu ukiwa kifua wazi, wale watoto wanaowaokotea kuni na kuwabebea silaha waasi waitweje? Child labour kaisome vizuri tena uunganishe na haki za msingi za mtoto ndo urudi.
 
Baada ya kufanikiwa kwenye pembe za ndovu, BBC wametukung'uta tena. Safari hii ni kwenye madini ya tanzanite. Wanadai tanzanite inachimbwa na watoto. Wameweka video ya "the gemstone mined by child labour". Huu utakuwa ni mkakati wa makaburu wa tanzaniteone ambao mara zote wameutangazia ulimwengu kuwa tanzanite yao pekee ndiyo halali maana haichimbwi na watoto. Hili ni pigo jingine kwa ndugu z wanaotegemea etu tanzanite kuendesha yao.[/p] maisha

Yeye anahisi kuchimba mpka waingie ndani ya shimo labda.
 
The Boss, hujui kitu. Watoto wapo nje wanaokota tu. Hakuna anayeingia shimoni. Nimekaa miezi miwili pale sikuona mtoto "nyoka" akizama chini. Wanaozama ni wana-apollo.

Kaka we much as wanatakiwa wawe shule na kwingineko kwenye manufaa kwa umri na ustawi wao hilo si sahihi

We unasema wanaokota tu as if wewe wako ungewaruhusu wakaokote!!!!!!

Hakuna zimwi bora hapo! !!!!!
 
Haya ni matokeo ya sera za kipuuzi za hao hao waingereza na mabepari wenzake. Walituhadaa tukaamini ubepari ndiyo jibu. Kwa mtindo huu, kama mtoto, ama hana wazazi na qalezi, au anao lakini hawana uwezo, lazima aingie kwenyw hii mnayoona ni child labour. Hali si mbaya kama bbc wanavyouaminisha ulimwengu. Hili ni la dunia nzima.
 
Manyenyere kwa kutetea visivyowezekana sijui anavizia ukuu wa wilaya kutoka kwa mkuu wa kaya na dk zenyewe hizi za majeruhi
 
Kweli mkuu huyu jamaa cku izi hana msimamo coz nakumbuka aliandika ngorongoro (ncaa) kwa ufisadi wao wasomaji tukafuatilia kaahidi kupitia gazeti lake la jamhuri kuna dada mdogo anamilik maghorofa manzese tusubiri habari mara du mpaka leo hatujaiona mpaka nimeacha kusoma kigazeti chake nahisi alipewa chumba kimoja afanyie biashara! Uandishi unataka ethics na integrity dont promise what is beyond your scope mkuu. Ujanja ujanja c suluhisho walk ur words tutakuamin, kuthamini na kukufuata co blah blah kama siye ni watoto hapa

manyerere jackton huwa ni mhariri nchumia tumbo ngoja watuanike maana ninyi wahariri wa tanzania mnaogopa kuandika mambo kama hayo, suala la watoto kuchimba madini lipo sehemu nyingi nchi hii hebu nenda mkuyuni na matombo morogoro utajiaonea mwenyewe
 
Haya ni matokeo ya sera za kipuuzi za hao hao waingereza na mabepari wenzake. Walituhadaa tukaamini ubepari ndiyo jibu. Kwa mtindo huu, kama mtoto, ama hana wazazi na qalezi, au anao lakini hawana uwezo, lazima aingie kwenyw hii mnayoona ni child labour. Hali si mbaya kama bbc wanavyouaminisha ulimwengu. Hili ni la dunia nzima.

Mkuu hbii mambo ya sera mbaya tuliletewa na kama hayo ni old stories tangu enzi za SAP yaani tunalalama kama vile sisi ni "tabula rasa" kabisaaaa.......hatuna ubongo wala akili......????!!!!

Haya tumegundua mbaya nini kinafanyika kurekebisha!!!?????

Hilo la mzazi kukosa uwezo nalo ni la kulalamikia watu wa nje wakati wazazi wengine wanachukua posho ya siku kubwa kuliko mshahara wa mzazi mwingine kwa mwezi....huu nao ni ushauri wa nje!!!?????

Hali ya ustawi wa watoto yaweza kuwa mbaya kuliko ilivyooneshwa na BBC mkuu, kama hatukubali uwepo wa shida ni vipi tutaanza kushughulikia???????!!!!!
 
Baada ya kufanikiwa kwenye pembe za ndovu, BBC wametukung'uta tena. Safari hii ni kwenye madini ya tanzanite. Wanadai tanzanite inachimbwa na watoto. Wameweka video ya "the gemstone mined by child labour". Huu utakuwa ni mkakati wa makaburu wa tanzaniteone ambao mara zote wameutangazia ulimwengu kuwa tanzanite yao pekee ndiyo halali maana haichimbwi na watoto. Hili ni pigo jingine kwa ndugu zetu wanaotegemea tanzanite kuendesha maisha yao.
===================================

jana nimeiona hiyo habar,kwanza tusianze kuwasingizia makaburu,bbc wameonesha kinachoendelea,la pili ajira kwa watoto hapa Tanzania zipo,mashamban,migodini,mbona kila jambo tunakimbilia kusingizia?kwa sababu suala la NYOKA kule mereran ni la muda,a ILO imeshawai kutoa ripot za child labor in Tanzania,kwa miaka ya nyuma,me nnayo hiyo report ukipenda nipe e-mail nikutumie leo,ifike wakat tusisake mchawi jaman,
 
Back
Top Bottom