Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,392
- 39,495
Na. M. M. Mwanakijiji
KLH News
Daima Macho Hatulali mpaka kijulikane!
Jengo jipya la Bunge Dodoma!
Bunge letu limetukanwa hadharani. Nilisubiri kwa hamu kuona kama kuna mwandishi, mbunge au kiongozi yeyote wa Tanzania ambaye atapaza sauti yake na kupiga kelele kufuatia taarifa kuwa kuna mikataba iliyotiwa saini na vyombo vya Tanzania ambayo inakataza Bunge (wawakilishi wa watu) kuihoji, kuingalia au hata kuipitia mikataba hiyo.
Hivi karibuni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA) alitaka serikali iulete Mkataba wa uendeshaji wa Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro ulioipa kampuni ya KADCO kazi hiyo kwa malipo ya Dola 1000 (ndiyo, elfu moja) kwa mwaka wakati kampuni hiyo inapata karibu Dola 5000 kwa siku toka KLM. Bw. Kabwe alitaka wabunge wapewe nafasi ili waweze kuusoma na kuelewa ni kitu gani kilichokubaliwa ndani ya mkataba huo. Hata hivyo Naibu Waziri wa Miundo Mbinu Dr. Maua Daftari alisema kuwa kipengele cha 30.4 cha mkataba huo kinaifunga serikali na mbia wake, Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO), kutoa habari kwa mtu yeyote ambaye si mhusika wa moja kwa moja kwenye utekelezaji wa mkataba huo. Kwa mujibu wa Dr. Daftari na ilivyonukuliwa na gazeti mojawapo nchini wabunge si wahusika wa moja kwa moja na mkataba huo, badala yake serikali itaendelea kuwawakilisha.
Hapo sasa ndipo naona ya kuwa Bunge letu limetukanwa hadharani. Kinachoudhi na kukera ni kuwa Wabunge wa CCM na wale wa Upinzani wamekubali maelezo ya Dr. Daftari bila upinzani wa kina wa hoja ya kuwa wao hawana haki ya kupewa maelezo na ikibidi kupitia mikataba hiyo wao wenyewe. Ni sawa na mtu kuambia umedondosha kitu na unapobongoa anakupiga teke na wewe unageuka na unapotaka kulalama anasema hauna haki ya kulalama! Serikali si wawakilishi wa wananchi kwa kuchaguliwa!! Na Serikali siyo wawakilishi wa Bunge! Bunge ni wawakilishi wa watu na ni Bunge linalotunga sheria ambazo serikali inafuata!! Ni Bunge pekee lenye uwezo wa kumuita mtu yeyote binafsi au kama kampuni na kutaka wapewe maelezo yoyote ambayo ni kwa maslahi ya Taifa.
Kama ni kweli Bunge letu halina uwezo wa kuhoji mikataba ya serikali na kuiitaka mikataba hiyo iletwe na itazamwe na Wabunge wenyewe basi Bunge letu lina udhaifu mkubwa wa kisheria na kiutendaji. Hebu fikiri kwa dakika chache kuwa kitengo, au wakala fulani wa serikali anaingia mkataba na kampuni fulani kufanya jambo fulani, mkataba huo kwa sababu fulani unazua utata, basi Kamati ya Bunge (kwa niaba ya Bunge) wanataka kuona na kuusoma mkataba huo halafu kiongozi wa serikali anawaambia It is none of your business! Haikuhusu! Ndugu zangu, kama hilo si tusi la rejareja basi ni tusi la nguoni!!
Ninachosema ni hivi:
a. Bunge kwa kutumia huu mfano huu wa KADCO lidai nafasi yake ya kisheria kwa kulazimisha mkataba huo uletwe kwa Wabunge na uangaliwe! Vinginevyo wakikubali kipengele hicho kisimame kama alivyodai Dr. Daftati basi watarajie mikataba mingi itawekwa kipengele kama hicho ili kuzuia vyombo vya serikali kupata nafasi ya kuangalia mikataba hiyo. Sijali hasa kama watu binafsi wakikatazwa kuangalia lakini ikifikia kuwa hata Wawakilishi wa wananchi wananyimwa fursa ya kuangalia mikataba na hivyo kulinda maslahi ya wananchi basi Bunge letu ni butu na lililobweteka!
b. Kama hakuna sheria inayoipa nguvu Bunge kuangalia mkataba wowote unaoingiwa na mtu, chombo, idara, wakala n.k chochote cha Kitanzania iwe ya serikali, au binafsi basi sheria hiyo itungwe mara moja ili kulinda maslahi ya Taifa, mali za Taifa na haki za wananchi! Katika sheria hiyo (kama haipo) ni lazima iwekwe wazi kuwa hakuna mkataba wowote utakoingiwa chombo chochote cha kitanzania (vya umma au binafsi) katika ardhi ya Tanzania au utakavyohusisha vyombo tanzu vyake ndani au nje ya Tanzania vitakavyokataza moja kwa moja au kwa kuashiria (directly or implicitly) kuwa Bunge halina uwezo wa kuiangalia mikataba hiyo kwa sehemu au yote (partially or totally). Mkataba wowote utakaokuwa na kipengele hicho mkataba huo utakuwa umepotoka na umetenguka (null and void).
c. Bunge lipewe nguvu ya kuwaita wale wote wanaoiingiza serikali katika mikataba wakati wa majadiliano na kuwahoji kwanini walikubali vipengele fulani viingizwe kwenye mikataba hiyo. Watu wanaoshiriki katika majadiliano ya mikataba kwa upande wa serikali wawe wanaweza kuitwa kutoa maelezo chini ya kiapo ya kwanini waliingia mikataba fulani. Na kama watu hao wataonekana kufanya hivyo kwa kujinufaisha au kuidhulumu serikali, basi Mwanasheria Mkuu apewe mamlaka ya kuwafungulia mashtaka ya kuihujumu serikali. Lengo liwe ni kuhakikisha kuwa wale wote wanaoaminiwa na serikali kufanya majadiliano basi wanafanya hivyo wakiwa na lengo moja na moja tu nalo ni kuhakikisha kuwa Mikataba inanufaisha kwa kiwango cha juu zaidi (maximum level) serikali au kitengo husika bila kunyima kwa haki faida kwa upande wa pili wa mkataba kwa kiwango cha juu wanachoweza kupata.
Hivyo basi, wabunge wetu walirudie jambo hili (la KADCO na KIA) na kulazimisha makampuni na wizara kuuleta mkataba huo kwao ama sivyo wanaanza kujenga mazoea mabaya (bad precedent). Wabunge wetu licha ya vyama vyao wasikubali kuburuzwa na serikali kwa kupewa maelezo dhaifu yasiyo na kichwa wala mguu yanayotolewa na mawaziri au manaibu waziri wanapojibu maswali Bungeni!!! Ama sivyo, iko siku badala ya kupigwa bongoa tutajikuta tumepigwa dafrau!!!