BAWACHA yamtaka Polepole amtaje aliyempiga Lissu risasi

BAWACHA yamtaka Polepole amtaje aliyempiga Lissu risasi

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
17,564
Reaction score
27,633

Swali gumu la BAWACHA kwa Polepole, "Tutajie pia waliompiga Lissu risasi, tunakushukuru kwa mambo mengi unayotuambia"

===

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Taifa, Sharifa Suleiman, amemshambulia vikali aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Taifa na Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, akimtaka kutoa ukweli kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, badala ya ‘kujifanya’ mtetezi wa haki.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Sharifa amesema anashangazwa na kauli za hivi karibuni za Polepole zinazokosoa chama tawala na kutetea viongozi wa CHADEMA, ikiwemo kesi inayomkabili Lissu kwa tuhuma za uhaini.

“Ninashangazwa na Humphrey Polepole ambaye mara zote amekuwa akisema ‘tuwakatae wahuni’, leo hii amekuwa akimpenda Tundu Lissu na kujifanya kumtetea. Kama kweli una nia njema na unakiri ulishiriki maamuzi mengi wakati wa Magufuli, basi toka hadharani utuambie nani aliyempiga risasi Lissu,” amesema Sharifa.

Sharifa ameongeza kuwa, Polepole hawezi kudai kuungana na Watanzania wanaopinga dhuluma wakati akiwa sehemu ya waliokuwa wakihujumu CHADEMA kipindi cha nyuma.

“Usitupake mafuta nyuma ya chupa. Tunajua ulishiriki maamuzi makubwa dhidi ya chama chetu. Watanzania wakusamehe? Sawa, lakini kwanza sema ukweli- nani aliyempiga risasi Tundu Lissu. Vinginevyo, tuwapuuze wahuni, tuwakatae wahuni, kwa sababu wahuni bado wako kazini,” amesisitiza.

Humphrey Polepole, ambaye hivi karibuni alijiuzulu nafasi ya Balozi wa Tanzania nchini Malawi na kuvuliwa hadhi ya ubalozi, amekuwa akitoa matamko makali dhidi ya CCM na Serikali, akisisitiza umuhimu wa haki, demokrasia na kutaka kesi ya uhaini dhidi ya Lissu iondolewe.

https://www.instagram.com/p/DNzsl3Xaoy9/comments/?hl=en
 
Mla mla leo mla jana kala nini? Na ndiyo maana Polepole katanguliza kuomba msamaha hadharani kwa kushiriki kwake mambo ambayo hayafai - katubu na tumemkubalia.

Kwa sasa HOJA mezani ni nani na kwa
nini database 3 zinasomana?? Ya CCM, NEC na NIDA. Na je tushukue hatua gani kabla ya tarehe 20 Oct.

Tuangalie tunachomokaje hapa tulipo na hii ndiyo hoja iliyo mbele yetu.
 
Kwenye hili, nimekuwa na mashaka ya siku myingi sana ndani ya chama changu cha Chadema

Kama tu chama kinaweza kuwa na viongozi mamluki wa CCM kwa kupewa kitu kidogo kukihujumu chama?

Hata hili la kuhujumiana wao kwa wao kwa kupewa kitu kidogo inawezekana kabisa kwa hao waliokuwa mamluki kutoka ccm

Siamini kilichotokea huku mwiahoni mwishoni kisa tu mtu kapigwa chini uongozini ati anaamua kumyuti utazani hakuwahi kuwa kiongozi wa wa juu kabisa kwenye chama
 
Slow ana objective aliyopewa, hawezi kutoka nje ya hiyo.

Wataalamu wa mambo ya kijeshi wanasema Slow ni ile kitu inaitwa "advance party" au "foward detachment". Ametangulia kuandaa mazingira ya kimedani na kisaikolojia.

Kwamba the "main body" is yet to arrive. Ukifika wakati huo sote tutakuwa kwenye mindset moja juu ya wahuni.
 
Mla mla leo mla jana kala nini? Na ndiyo maana Polepole katanguliza kuomba msamaha hadharani kwa kushiriki kwake mambo ambayo hayafai - katubu na tumemkubalia.

Kwa sasa HOJA mezani ni nani na kwa
nini database 3 zinasomana?? Ya CCM, NEC na NIDA. Na je tushukue hatua gani kabla ya tarehe 20 Oct.

Tuangalie tunachomokaje hapa tulipo na hii mdiyo hoja iliyo mnele yetu.
Ameomba msamaha kwa kuyasema yote mabaya waliofanya?, Hivi ndugu wa akina Ben saa 8, Rwanda na wengineo wanamuelewa?, baada ya kupambania Tanzania kama nchi, anapambania CCM yake iliyojaa uozo miaka dahali...
 
Slow ana objective aliyopewa, hawezi kutoka nje ya hiyo.

Wataalamu wa mambo ya kijeshi wanasema Slow ni ile kitu inaitwa "advance party" au "foward detachment". Ametangulia kuandaa mazingira ya kimedani na kisaikolojia.

Kwamba the "main body" is yet to arrive. Ukifika wakati huo sote tutakuwa kwenye mindset moja juu ya wahuni.

hii unayosema hapa, nimeisikia pia leo kwa wale wanyetishaji wa "za ndaaaaaani" kabisa!
 
Slow slow yupo makini sana katika kulipua mabomu yake, Upande wa Jiwez hataugusa sana maana huko ndiko alikopewa shavu.
Politically ni poor strategy akirudi sana huko.

Kwanini?
To effectively destroy Sa100's regime, people must see how she has critically betrayed her predecessor's (JPM) seemingly praiseworthy track record in leadership viz-a-viz cracking down on corruption, uzembe wa watumishi wa umma, plus building once more a unique sense of nationalism.

Who knows maybe wahuni wale wale ndio wanahusika na lile tukio pia.

Time will tell.
Nadhani kwa mtazamo wa Polepole, mzalendo (JPM) is somehow more justified kutenda alichotenda kuliko kiongozi anayeonekana kutenda hivyo kwa maslahi binafsi au ya kundi fulani la wachache.

The end justifies the means?!
 
Huyo mama aache ujinga , huenda isije ikatokea tena nafasi kama hii katika historia ya siasa za Tanzania. Hii ndiyo saa ya CHADEMA kujitathmini, kujifunza kutokana na makosa ya zamani, na kuonyesha kwamba ni chama mbadala kinachoweza kuaminiwa na wananchi.

Huyo mama anachofanya ni kuharibu, inapaswa wamtumie Polepole kufika wanapohitaji, wakishafika hayo ya Lissu yatafahamika tu, ni mambo madogo sana, kuna kesi watu wanahukumiwa baada ya miaka 20 tukio kutokea... tumieni akili sio hisia.. kwa hio wakimjua aliyempiga Lissu risasi leo hii watafanya nini kama dola haipo mikononi mwao?
 
View attachment 3452694

Swali gumu la BAWACHA kwa Polepole, "Tutajie pia waliompiga Lissu risasi, tunakushukuru kwa mambo mengi unayotuambia"
Haya ndiyo majibu ya hoja zake; na wewe umekuwa msemaji wa BAWACHA tokea lini.

Mwanzo nilikuchukulia kuwa mtu mwenye akili inayojitegemea kumbe ni kundi lile lile la Genge la Samia; wengi wao nawaita ni "Mizoga" kwa maana maslahi yao yako juu ya maslahi ya taifa hili.
 
1. Enzi za Mkapa, alikimbia nchi kwa kutetea wachimbaji wadogo waliofukiwa hai mgodini.

2.....akapigwa risasi.

3. Baada ya kusema kuhusu makaa ya mawe, akapewa kesi ya uhaini

Tukuulize ww Stuxnet ni nani hao?
'Stuxnet' ni mmoja wa "mizoga" muhimu inayotumiwa na Genge la Samia kueneza mifarakano katika jamii ili waendelee kubaki madarakani.
Mwanzo alijificha ficha asijulikane anasimamia wapi hasa, sasa mambo yamaekuwa mazito imelazimu ajitokeze mbele kumpambania Samia na Genge lake.

Huyu hana tofauti yoyote na hao akina Tlaatlaah, Voicevariable na takataka nyingine zilizomo humu JF; kazi yao kubwa ikiwa ni kupindisha na kuchafua mijadala inayo husu ukombozi wa taifa hili.
 
Back
Top Bottom