Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 104,121
- 183,966
Mwenyekiti wa Bavicha , ambayo ni Taasisi bora kabisa ya vijana barani Africa , John Pambalu , akizungumza na vijana wenzake huko Geita kwenye vikao vya ndani , bila kumung'unya maneno wala kuona aibu , amemtaka Makamu wa Rais wa Tanzania Mh Philipo Mpango , kujitokeza hadharani na KUOMBA RADHI KUTOKANA NA KUTELEZA KWA ULIMI WAKE NA KUONGEA UONGO KUHUSU MAJI YA MAITI KUTUMIKA KUHIFADHIA SAMAKI wanaovuliwa Ziwa Victoria .
Pambalu amedai kwamba ni muhimu sana kwa Makamu wa Rais kuwapigia magoti wananchi , kwa vile kauli yake ile iliyopingwa na bunge la Tanzania imepunguza ama kuua kabisa soko la Sangara , Sato na dagaa wa Mwanza , huku njia pekee na fupi sana ya kurudisha Soko la samaki hao duniani ni kwa Makamu wa Rais kusimama hadharani na kukiri kwamba alikurupuka .