Makamo wa Rais aombe radhi Watanzania.Mwenyekiti wa Bavicha , ambayo ni Taasisi bora kabisa ya vijana barani Africa , John Pambalu , akizungumza na vijana wenzake huko Geita kwenye vikao vya ndani , bila kumung'unya maneno wala kuona aibu , amemtaka Makamu wa Rais wa Tanzania Mh Philipo Mpango , kujitokeza hadharani na KUOMBA RADHI KUTOKANA NA KUTELEZA KWA ULIMI WAKE NA KUONGEA UONGO KUHUSU MAJI YA MAITI KUTUMIKA KUHIFADHIA SAMAKI wanaovuliwa Ziwa Victoria .
Pambalu amedai kwamba ni muhimu sana kwa Makamu wa Rais kuwapigia magoti wananchi , kwa vile kauli yake ile iliyopingwa na bunge la Tanzania imepunguza ama kuua kabisa soko la Sangara , Sato na dagaa wa Mwanza , huku njia pekee na fupi sana ya kurudisha Soko la samaki hao duniani ni kwa Makamu wa Rais kusimama hadharani na kukiri kwamba alikurupuka .
Pia CDM itafute mbadala wa Pambalu maana kiti kimempwaya,Hasikiki, Hana mvuto Kwa wananchi Kwa nafasi hiyo.
Nimemsikia Mbowe Juzi akilalamikia bavicha, nadhani ni wasaa wa Pambalu kukaa pembeni kubeba uwajibikaji.
Mungu ibariki CDM, Mungu ibariki TANZANIA.
Ameeeen.