BAVICHA yamtaka Makamu wa Rais kuomba radhi kwa kusema uongo kuhusu Maji ya Maiti na Samaki Kanda ya Ziwa

Mwenyekiti wa Bavicha , ambayo ni Taasisi bora kabisa ya vijana barani Africa , John Pambalu , akizungumza na vijana wenzake huko Geita kwenye vikao vya ndani , bila kumung'unya maneno wala kuona aibu , amemtaka Makamu wa Rais wa Tanzania Mh Philipo Mpango , kujitokeza hadharani na KUOMBA RADHI KUTOKANA NA KUTELEZA KWA ULIMI WAKE NA KUONGEA UONGO KUHUSU MAJI YA MAITI KUTUMIKA KUHIFADHIA SAMAKI wanaovuliwa Ziwa Victoria .

Pambalu amedai kwamba ni muhimu sana kwa Makamu wa Rais kuwapigia magoti wananchi , kwa vile kauli yake ile iliyopingwa na bunge la Tanzania imepunguza ama kuua kabisa soko la Sangara , Sato na dagaa wa Mwanza , huku njia pekee na fupi sana ya kurudisha Soko la samaki hao duniani ni kwa Makamu wa Rais kusimama hadharani na kukiri kwamba alikurupuka .
Ulivyo mwongo na mwenye kiherehere mpaka dagaa? Kwani dagaa wanahifadhiwa au waanikwa? Mwongo ni mwongo tu na njia yake ni fupi
 
Na kansa nayo itawachagua wana ccm wenyewe?.Hili jambo linahitaji majibu sahihi ila tatizo nikwamba tuko kwenye nchi ambayo hatujielewi.Litaenda litaisha kimya kimya ila watakaoendelea kuumia ni wananchi wote bila kubagua itikadi za vyama.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
EEeeehnHeee, mkuu wangu 'gigabyte', liishe na kupita mara ngapi?
Hiyo sasa imebaki ni historia tu ya kusimulia kwamba kulikuwepo na habari kama hiyo iliyosemwa na Makamu wa Rais!

Tupo kwenye hali mbovu kabisa kiutawala.

Hata Makamu wa Rais mwenyewe hana hamu tena ya kulizungumzia, au kufuatilia nini kimefanyika baada ya kufyatuka kwake.

Na kwa vile ni jambo la kibiashara, na hii serikali ni ya wafanya biashara, si ajabu Makamu wa Rais akaonywa asiropoke tena hadharani!

Wewe waone tu watu kama akina Erick Hamisi, bila shaka wanajutia kwa nini hawakujuwa mapema!
 
Back
Top Bottom