Battle: Pacome Zouzoua vs Aziz Ki nani ni engine ya Yanga?

Jan 31, 2024
42
119
Japokuwa wote ni wachezaji wa Yanga na wote wanafanya kazi nzuri katika klabu yao ila wewe kama shabiki wa Yanga unaona nani asipokuwa uwanjani timu ina struggle sana kupata matokeo.

Karibuni kwa mawazo wana JF.
 
Ngoja nikusaidie, sababu umeamua kutumia analogy ya engine.

engine ili iweze kufanya kazi, inahitaji mafuta yaunguzwe, oxygen ya kusaidia kuungua na kiwashio(ignition). So diarra ni mafuta, bacca ni oxgen na aucho ni ignition. So, hao watatu ndio unaweza sema, engine ya Yanga.
 
Kwa mtu ayejua mpira atakubaliana na Mimi kua ukimtoa diarra, aucho na Ibrahim bacca.... Automatically utakua umebomoa timu....

Haya nyinyi wa azizi k na pacome endeleeni
Mpira unaujua vizuri mkuu hasa hasa Aucho Yanga hii ya sasa ni Aucho na Aucho ni Yanga jamaa analeta utulivu mkubwa sana kwenye timu na kiungo kati ya beki na washambuliaji..bravo Kwa mtazamo mzuri
 
Kwa mtu ayejua mpira atakubaliana na Mimi kua ukimtoa diarra, aucho na Ibrahim bacca.... Automatically utakua umebomoa timu....

Haya nyinyi wa azizi k na pacome endeleeni
Ulichokiongea ni kwel kabisa ...tukianza na diara anajua sana kucheza na kuzipanga beki zake na mabake wanapo kosea yupo Shap ku fanya maamuzi

Bacca uyu jamaa ni beki na nusu yan..bacca haimbwi sana sababu n mzawa tunamchukulia poa ila jamaa anajua sana kuficha makosa ya wenzake kama jana kipind cha kwanza Lomalisa alikuwa anafanya makosa mengi ila bacca alikuwa anaokoa nafasi

Khalid Aucho (doctor) uyu jamaa ni fundi na nusu yeye ndio anafanya wakina pacome Max na aziz waonekane yeye ndio anaamua Yanga wachezaje uwanjani yeye ndio anaamua sasa tupooze kasi na sasa tuongeze kasi anawavuruga sana kati

KWANGU AUCHO NDIO ROHO YA YANGA
 
Yanga akikosekana AZIZ KI hata upatikanaji wa Magoli huwa mgumu. To me, Pacome na Aziz bora aziz awepo uwanjani, huwa anaamua sana game na mbele timu itembee vipi.
 
Mpira unaujua vizuri mkuu hasa hasa Aucho Yanga hii ya sasa ni Aucho na Aucho ni Yanga jamaa analeta utulivu mkubwa sana kwenye timu na kiungo kati ya beki na washambuliaji..bravo Kwa mtazamo mzuri
Basi katika mechi ya nusu fainali ya nyumbani apewe Khaled Aucho iwe "Aucho Day"
 
uimara wa Young Africans unaanzia kwa watu watatu, Djigui Diara, Ibrahim Bacca, Khaleed Aucho, sifa za hawa jamaa huwa ni rahisi kusahihisha makosa ya wenzao pale wanapokesa, kitu kingine Aziz Ki uwepo wake uwanjani kunafanya timu iwe na faida kwa kuwa ana uwezo wa kufunga kwa mipira iliyokufa, anaweza kufunga kwa open space, tukija kwa Pacome huyu ni kiungo mshambuliaji ambaye kwa miaka mingi Young Africans hawakuwahi kuwa nae, huyu Pacome sifa yake kuu ni mchezaji anayenyumbulika pindi awapo uwanjani huwezi jua kuwa anacheza namba ipi, ana uwezo wa kukaba, ana uwezo wa kutengeneza nafasi na ana uwezo wa kufunga pia, kwa hiyo kwa mtazamo wangu kila mmoja ni bora kulingana na majukumu yake yanamtaka afanye vitu gani? VIVA Young La Africans, from Qurter final to Semi Final CAF Champion League. PAMOJA TUNAWEZA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom