Yanga vs Simba; Yanga ni Mamelodi

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
Rekodi imeandikwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam leo tarehe 5 Nov 2023,timu Bora barani Afrika, Yanga imeifunga timu bora ya Simba magoli 5-1, katika mchezo ulioonyesha ubora wa timu ya Yanga ukifanana na ubora wa Mabingwa wa Afrika mwaka 2016 timu ya Mamelodi Sundowns,

Timu ya Yanga inayocheza boli la pasi za kati zinazoonana na kufika kwa mlengwa,Yanga inayochezea mpira na kuwa laini kama mlenda ikiwa na mafundi viungo Aziz Ki,Pacome Zouzoua,Max Nzengeli na Mudadhir Yahya iliweza kutawala dimba la kati na kufanya Simba ionekane kama Mtibwa Sugar ya Manungu,Turiani ama Mashujaa ya Kigoma, Yanga ikiwa na golikipa bora barani Afrika Djigue Diarra,walinzi madhubuti Dickson Job, Kwasi Yaoyao,Khalid Aucho, Lomalisa na Mshambuliaji asiyeonekana lakini akipata boli anakuweka Kennedy Musonda.

Technically, Simba walitakiwa kukubali kuwa Yanga wana kiwango bora haijawahi kutokea na wanaweza kumfunga yeyote kati ya klabu bora za Afrika kwa sasa iwe Wydad, ama Al Alhy, iwe Esperance ama Mamelodi Sundowns,Simba walichotakiwa kufanya leo wangecheza compact football kupunguza idadi ya magoli,sasa wao wakacheza open football na kuacha mianya kwa combination ya Pacome,Aziz Ki na Max Nzengeli, nakujikuta wanaaibishwa, Simba walikuwa wanaona aibu kubana uwanja kwa sàbabu walijiona wakubwa yaani timu kubwa iliyoshiriki African Super League bila kuzingatia kiwango cha Yanga kwa sasa ambapo kama Yanga ingalikuwepo kwenye African Super League basi Fainali ingechezwa Yanga vs Mamelodi Sundowns.

#SinaShakaNaYangaMsimuHuu.
 
Rekodi imeandikwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam leo tarehe 5 Nov 2023,timu Bora barani Afrika,Yanga imeifunga timu bora ya Simba magoli 5-1,katika mchezo ulioonyesha ubora wa timu ya Yanga ukifanana na ubora wa Mabingwa wa Afrika mwaka 2016 timu ya Mamelodi Sundowns,

Timu ya Yanga inayocheza boli la pasi za kati zinazoonana na kufika kwa mlengwa,Yanga inayochezea mpira na kuwa laini kama mlenda ikiwa na mafundi viungo Aziz Ki,Pacome Zouzoua,Max Nzengeli na Mudadhir Yahya iliweza kutawala dimba la kati na kufanya Simba ionekane kama Mtibwa Sugar ya Manungu,Turiani ama Mashujaa ya Kigoma,Yanga ikiwa na golikipa bora barani Afrika Djigue Diarra,walinzi madhubuti Dickson Job,Kwasi Yaoyao,Khalid Aucho,Lomalisa na Mshambuliaji asiyeonekana lakini akipata boli anakuweka Kennedy Musonda.

Technically, Simba walitakiwa kukubali kuwa Yanga wana kiwango bora haijawahi kutokea na wanaweza kumfunga yeyote kati ya klabu bora za Afrika kwa sasa iwe Wydad, ama Al Alhy, iwe Esperance ama Mamelodi Sundowns,Simba walichotakiwa kufanya leo wangecheza compact football kupunguza idadi ya magoli,sasa wao wakacheza open football na kuacha mianya kwa combination ya Pacome,Aziz Ki na Max Nzengeli,nakujikuta wanaaibishwa, Simba walikuwa wanaona aibu kubana uwanja kwa sàbabu walijiona wakubwa yaani timu kubwa iliyoshiriki African Super League bila kuzingatia kiwango cha Yanga kwa sasa ambapo kama Yanga ingalikuwepo kwenye African Super League basi Fainali ingechezwa Yanga vs Mamelodi Sundowns.

#SinaShakaNaYangaMsimuHuu.
Igweeeeeee,
 
Hawa wakulialia bado wanatesa na 5g maana kila kukicha wakiona jezi ya njano au kgjani wanajificha, wakisikha sauti ya Ally kamwe wanazima radio, wakiingia mtandaoni yupo manara yaani mpaka wasemeee. Yanga ya 5g noma tunanenepa wao wanakonda.
 
Back
Top Bottom