Roberto Olveira: Pacome alinifukuzisha kazi Simba

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
Kocha wa zamani wa Club ya Simba Robertihno Olveira, Akizungumza kutoka Brazili, Robertinho alieleza kama alitimuliwa kutokana na matokeo ya mechi yake ya mwisho dhidi ya Yanga basi ubora wa Pacome ulichangia kwa asilimia kubwa kuondoka katika klabu hiyo.

Alisema Pacome ni kiungo ambaye anacheza soka la kisasa sana akiwa na kasi, ya kwenda lango la wapinzani pia anacheza kwa ajili ya timu sio kutafuta ustaa.

“Sitaki kuingia kwenye siasa za nani bora kati ya Chama na Pacome, kwani nawaheshimu wote ni wachezaji wenye akili kubwa, lakini Pacome bado atabaki katika kumbukumbu isiyofutika kwangu kwa namna alivyotupa shida kwenye mechi ya mwisho,” alisema Robertinho na kuongeza;

“Naona moto ule ameendelea na kama ataendelea hivi ataendelea kusumbua kwenye ligi ya Tanzania na Afrika, napenda sana uchezaji wa Pacome kwa kuwa ni kiungo. Uwepo wa Pacome Yanga umemrahisishia kazi Aziz KI kwa kuwa timu nyingi zitamwangalia zaidi yeye na wakati Yanga ina wachezaji wengine hatari kama Aziz.”

Mastaa hao wa Yanga wanaofahamika kwa ubora wao,wote wakitokea timu moja ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast, licha ya kuzungumziwa na kocha huyo lakini wamekuwa na wakishikilia rekodi ya mabao.

Aziz KI mpaka sasa ndie anaongoza kwa ufungaji Ligi Kuu akiwa na mabao 10 na kutokana na ubora wao kuna uwezekano mkubwa wa viungo hawa kufunga zaidi mpaka mwisho wa msimu. Yanga itakuwa ugenini Ijumaa, Tarehe 8 Machi kusaka alama tatu dhidi ya Namungo, ikiwa ni mechi ya 17 ya ligi wakiwa na jumla ya pointi 43 katika michezo 16 waliyokwisha kucheza.
 
Ngoma wamemsajili wao, wamemsajili Saido, walimrudisha Chama, wenzao wamemchukua Pacome na Maxi ila shida na lawama wakamtupia Robertinho.

Na kwa Simba ile ya jana dhidi ya Prisons, mwisho wa msimu hii timu itafumuliwa yote tena, na itakuwa Simba mbovu zaidi kuliko hii ya sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom