Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Habari zenu wanajukwaa, baada ya kugundua kuwa mtu huyu imeshindikana kabisa kusahaulika ndani ya mioyo ya Watanzania na wasio Watanzania nimeona nianzishe uzi ambao utagusa pande zote yani wale wanaodhani alikuwa Rais bora na wale wanaodhani hakuwa Rais bora.

Ikumbukwe kwamba tangu amefariki mtu huyu imepita takribani miezi sita na siku kadhaa mpaka hapa ninapoandika huu uzi, sasa naomba wale Magufulians waseme kwanini wanadhani huyu alikuwa Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na watoe sababu za kusema hivyo pia wale wanaodhani hakuwa Rais bora watoe sababu zao.

Ndugu zangu nimelazimika kuanzisha huu uzi kutokana na kile ninachokiona kwamba jina la Magufuli sasa limekuwa kama dini mana unapomponda tu kama pembeni yako kuna mfuasi wake basi hawezi kukuacha salama.

Hii imepelekea kutokea mikanganyiko na sintofahamu kwenye majukwaa mbalimbali inafikia kipindi unakuta mada haihusiani na Magufuli lakini uzi unaharibika kwa sababu ya u-Magufuli vs u-Anti Magufuli.

Sasa ndugu zangu tusiendelee kuharibu nyuzi za watu, kama una dukuduku lako kuhusiana na kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kuongoza Tanzania basi weka hapa dukuduku lako au maoni yako juu ya mwamba huyu yaweke hapa jamii ifahamu ni kwa namna gani kiongozi huyu alikuwa mzuri au mbaya.

Nianze na mimi binafsi msimamo wangu juu ya JPM, ni kwamba namuona kama Icon na benchmark ya viongozi waliopo na watakaokuja kwasababu zifuatazo

1. Muanzilishi wa Tanzania mpya. JPM alikuwa kiongozi mwenye uthubutu wa kuwakaripia viongozi wote walio chini yake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba iwe ni viongozi wa kuteuliwa na yeye mwenyewe au wa kuchaguliwa basi viongozi walitii, ilikuwa ni utaratibu kwa viongozi wa Tanzania waliochini ya Rais kikatiba kujiamulia mambo watakavyo wao ikibidi hata kukaidi maagizo yanayotolewa na Rais, hii ilipelekea huko nyuma nchi yetu kupoteza muelekeo lakini chini ya JPM maagizo yakawa yanafuatwa na kasi ya utendaji ikawa kubwa kuwahi kutokea Tanzania.

2. Kiongozi mkweli daima. Mtu huyu alikuwa ni moja kati ya binadamu wachache wakweli, alikuwa mwanasiasa pekee asiyejuwa kuongopa, ilifika mahali akajiingiza kwenye mgogoro na wanasiasa wenzake ndani ya CCM kwakuwa wengi wao hawakuzoea ukweli, JPM akisema hili hapana basi juwa kwamba halitatokea au akisema hili linawezekana basi juwa hivyo, hakuwa mtu wa kupepesa macho, alikuwa na uwezo wa kuongea ukweli hadharani pasipo kuficha ficha kitu chochote, hii ikapelekea viongozi waliokuwa wanaendekeza siasa majitaka kumuogopa kwani mzee yule hakuwa akijali kama unatokea CCM au upinzani.

3. Msimamo mkali. Chini ya JPM tuliona Tanzania yenye msimamo na isiyoyumbishwa na mtu yeyote au taifa lolote lile liwe na uchumi mkubwa au mdogo, hii ikapelekea Tanzania kufahamika zaidi kimataifa na duniani kote.

4. Kiongozi mwenye maono. Hayati JPM alikuwa ni kiongozi mwenye maono, hili liko wazi kwani maono yake hasa kwenye nyanja za kiuchumi ndio zikapelekea nchi yetu kuingia uchumi wa kati kabla ya muda uliokusudiwa, hii ilitokana na maono na jitihada zake kuhakikisha nchi yetu inajitegemea kwa kuanzisha miradi iliyoonekana haiwezekani lakini chini ya uongozi wake ikawezekana, pia maono yake yalijidhihirisha hata kwenye ugonjwa ulioikumba dunia kwa sasa ugonjwa wa Corona, nchi nyingi duniani zimeanza kutumia theories alizozitoa Hayati JPM.

5. Kiongozi mwenye ushawishi. Hayati JPM alikuwa na karama ya ushawishi mbele ya jamii, alikuwa na uwezo wa kusema jambo fulani na jamii nzima ikakubaliana naye kwa asilimia kubwa, kiukweli kabisa hata leo hii JPM akiamka na akasema watanzania wachanje basi believe me dawa za kuchanja hazitatosha, hii ni kutokana na imani kubwa aliyojiwekea mbele ya jamii kwakuwa watanzania waliamini kwamba JPM ana upendo wa dhati kwa wananchi wake na hawezi kuwarubuni kwa namna yoyote ile.

6. Mtu wa Mungu. Licha ya mapungufu yake kibinaadamu lakini ni ukweli usiopingika kwamba JPM alikuwa ni mtu wa Mungu, siku zote za uongozi wake hakuacha kumtegemea Mungu na hili alilifanya hadharani kwa kumtaja Mungu popote alipoenda na watu wake wakaribu wanasema mzee yule ulikuwa ni utaratibu wake kumtanguliza Mungu mbele.

7. Kipenzi cha wengi. Ukiacha mitandao ambao kuna wachache wanaomsema vibaya Magufuli ni dhahiri shairi kwamba hayati alipendwa na wengi, hii ilijidhihirisha pale alipofariki, umati uliojitokeza haukuwahi kutokea na sidhani kama utatokea kwa siku za karibuni, sio kwamba walioenda kumuaga walienda kukejeli bali waliguswa haswa, vilio kila pembe ya waagaji na kila sehemu mwili ulipoenda, hii inathibitisha ni jinsi gani watanzania walimpenda kiongozi wao.

Yako mengi ya kumuelezea Magufuli lakini itoshe kwa haya niliyoyaandika kumuelezea, mengine niwaachie ninyi wenzangu karibuni.
Sisi tulishmsahau umetukumbusha wewe. Nani akae amkumbuke muuaji kama yule?Tunashukuru Mungu kwa kutuondolea balaa kubwa
 
Tofauti na kuwapiga vita mapunga, mafisadi, vyeti feki, vibaraka, wanafki na mahujumu uchumi, uko na sababu gani ya kumchukia JPM uloitoa hapa? Lissu hata leo akija afisa yeyote mzalendo mwenye kuviishi viapo vyake lazima amshughulikie wala haitaji amri ya Amiri jeshi mkuu, vivyo hivyo kwa mjinga yeyote atayeenda kinyume na maslahi mapana ya Taifa lazima apotezwe, haki za ushoga ndo unazozitaka? ajira tushasema huko juu, hii ni nchi yetu sote hakuna alokuwa bora zaidi ya mwingine, hakuna ongezeko la mishahara na pesa ikaenda kujenga reli itayotumiwa na wote wafanyakazi na wakulima..tuliridhika.
Uliridhika wewe na baba yako.
 
Ujasiri ni ni ule uwezo wa kusimamia na kupambania unachokiamini bila kujali wala kuhofia chochote.

Huu uwezo watz wengi hawana na Magu alijitahidi sana kuuchochea.

Kwamba PM alidanganya hilo ni lake yeye kama yeye halihusiani na mada.
Sasa hawataki hawa waja, wanaoamini katika Magufuli wanatoa sababu hawa wengine wanaenda kinyume na thread inavyotaka, tatizo la hawa jamaa mpaka wanaonekana ni kituko ni pale wanaposhindwa kutetea hoja wanabaki kutoa maneno ya kashfa ambayo hayasaidii na wala hayawezi kuondoa ukweli kwamba Magufuli ndiye aliyeanzisha Tanzania mpya kwa kufanya mambo mengi ndani ya muda mfupi mfano:

Ujenzi wa vituo vya afya vingi kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa barabara kilometers nyingi kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa mabwawa makubwa ya umeme kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa madaraja ya kuvunja rekodi kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa meli kubwa na vivuko kila mahali.

Ujenzi na ukarabati wa shule nyingi.

Ujenzi wa na ukarabati wa Airports na ports nyingi kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa miji mipya mfano Dodoma.

Uunganishaji umeme kwa wananchi kwa asilimia kubwa kuwahi kutokea.

Upelekaji maji vijijini kwa kasi kubwa kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa barabara za kisasa flyovers na interchanges.

Ununuzi wa ndege nyingi kuliko awamu yoyote.

Usimamizi uliotukuka wa rasilimali mfano madini na kwa mara ya kwanza madini yakaanza kuleta faida mpaka sasa tunavyoongea ndiyo sekta yenye mchango mkubwa katika uchumi wa nchi, hii haijawahi kutokea kabla yake.

Kurudisha nidhamu kazini kwa watumishi wa umma, hili wala sihitaji kulitolea ufafanuzi.

Ujenzi wa miundombinu ya reli, haijawahi kutokea Tanzania ikajenga reli kwa pesa yake hata Nyerere alishindwa.

Na mengine mengi, sasa hizo ni hoja zinazohitaji mtu makini wa kuzipinga kwamba si kweli na hawezi kutokea mtu huyo mana huo ndio ukweli yani hizo ni facts huwezi kuzipinga, na kama yupo mtu wa kuzipinga hizo facts atokee apinge kwa hoja pasipo matusi, hicho ndicho kinachowakosesha raha hawa Anti-Magu.
 
Habari zenu wanajukwaa, baada ya kugundua kuwa mtu huyu imeshindikana kabisa kusahaulika ndani ya mioyo ya Watanzania na wasio Watanzania nimeona nianzishe uzi ambao utagusa pande zote yani wale wanaodhani alikuwa Rais bora na wale wanaodhani hakuwa Rais bora.

Ikumbukwe kwamba tangu amefariki mtu huyu imepita takribani miezi sita na siku kadhaa mpaka hapa ninapoandika huu uzi, sasa naomba wale Magufulians waseme kwanini wanadhani huyu alikuwa Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na watoe sababu za kusema hivyo pia wale wanaodhani hakuwa Rais bora watoe sababu zao.

Ndugu zangu nimelazimika kuanzisha huu uzi kutokana na kile ninachokiona kwamba jina la Magufuli sasa limekuwa kama dini mana unapomponda tu kama pembeni yako kuna mfuasi wake basi hawezi kukuacha salama.

Hii imepelekea kutokea mikanganyiko na sintofahamu kwenye majukwaa mbalimbali inafikia kipindi unakuta mada haihusiani na Magufuli lakini uzi unaharibika kwa sababu ya u-Magufuli vs u-Anti Magufuli.

Sasa ndugu zangu tusiendelee kuharibu nyuzi za watu, kama una dukuduku lako kuhusiana na kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kuongoza Tanzania basi weka hapa dukuduku lako au maoni yako juu ya mwamba huyu yaweke hapa jamii ifahamu ni kwa namna gani kiongozi huyu alikuwa mzuri au mbaya.

Nianze na mimi binafsi msimamo wangu juu ya JPM, ni kwamba namuona kama Icon na benchmark ya viongozi waliopo na watakaokuja kwasababu zifuatazo
emoji116.png
emoji116.png

1. Muanzilishi wa Tanzania mpya. JPM alikuwa kiongozi mwenye uthubutu wa kuwakaripia viongozi wote walio chini yake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba iwe ni viongozi wa kuteuliwa na yeye mwenyewe au wa kuchaguliwa basi viongozi walitii, ilikuwa ni utaratibu kwa viongozi wa Tanzania waliochini ya Rais kikatiba kujiamulia mambo watakavyo wao ikibidi hata kukaidi maagizo yanayotolewa na Rais, hii ilipelekea huko nyuma nchi yetu kupoteza muelekeo lakini chini ya JPM maagizo yakawa yanafuatwa na kasi ya utendaji ikawa kubwa kuwahi kutokea Tanzania.

2. Kiongozi mkweli daima. Mtu huyu alikuwa ni moja kati ya binadamu wachache wakweli, alikuwa mwanasiasa pekee asiyejuwa kuongopa, ilifika mahali akajiingiza kwenye mgogoro na wanasiasa wenzake ndani ya CCM kwakuwa wengi wao hawakuzoea ukweli, JPM akisema hili hapana basi juwa kwamba halitatokea au akisema hili linawezekana basi juwa hivyo, hakuwa mtu wa kupepesa macho, alikuwa na uwezo wa kuongea ukweli hadharani pasipo kuficha ficha kitu chochote, hii ikapelekea viongozi waliokuwa wanaendekeza siasa majitaka kumuogopa kwani mzee yule hakuwa akijali kama unatokea CCM au upinzani.

3. Msimamo mkali. Chini ya JPM tuliona Tanzania yenye msimamo na isiyoyumbishwa na mtu yeyote au taifa lolote lile liwe na uchumi mkubwa au mdogo, hii ikapelekea Tanzania kufahamika zaidi kimataifa na duniani kote.

4. Kiongozi mwenye maono. Hayati JPM alikuwa ni kiongozi mwenye maono, hili liko wazi kwani maono yake hasa kwenye nyanja za kiuchumi ndio zikapelekea nchi yetu kuingia uchumi wa kati kabla ya muda uliokusudiwa, hii ilitokana na maono na jitihada zake kuhakikisha nchi yetu inajitegemea kwa kuanzisha miradi iliyoonekana haiwezekani lakini chini ya uongozi wake ikawezekana, pia maono yake yalijidhihirisha hata kwenye ugonjwa ulioikumba dunia kwa sasa ugonjwa wa Corona, nchi nyingi duniani zimeanza kutumia theories alizozitoa Hayati JPM.

5. Mtu wa Mungu. Licha ya mapungufu yake kibinaadamu lakini ni ukweli usiopingika kwamba JPM alikuwa ni mtu wa Mungu, siku zote za uongozi wake hakuacha kumtegemea Mungu na hili alilifanya hadharani kwa kumtaja Mungu popote alipoenda na watu wake wakaribu wanasema mzee yule ulikuwa ni utaratibu wake kumtanguliza Mungu mbele.

6. Kipenzi cha wengi. Ukiacha mitandao ambao kuna wachache wanaomsema vibaya Magufuli ni dhahiri shairi kwamba hayati alipendwa na wengi, hii ilijidhihirisha pale alipofariki, umati uliojitokeza haukuwahi kutokea na sidhani kama utatokea kwa siku za karibuni, sio kwamba walioenda kumuaga walienda kukejeli bali waliguswa haswa, vilio kila pembe ya waagaji na kila sehemu mwili ulipoenda, hii inathibitisha ni jinsi gani watanzania walimpenda kiongozi wao.

Yako mengi ya kumuelezea Magufuli lakini itoshe kwa haya niliyoyaandika kumuelezea, mengine niwaachie ninyi wenzangu karibuni.
MAGUFULI ALIKUA ANALENGO GANI NA HII NCHI.
Hapa ndio kwenye point.

Kwa mtu alie normal( hana mihemko (akiacha sababu zingine pembeni)) na mwenye upeo na akatumia akili tu yakuzaliwa hawezi kubeza jitihada za magufuli na serikali yake awamu ya tano.

Yani kabisaaa!!! Mtu huoni impact ya projects zilizoanzishwa kweli? Hapa utakua na upeo au uelewa wa mambo mdogo sana, Unafikilia leo tu, Hizo project ni process inayohitaji coordination ya hali ya juu kwahiyo lazima zitachukua muda kuzaa matunda.

Jipime upeo wako hapa; yani wewe ulitaka baada tu ya miradi kukamilika mapato yaanze kupanda hapohapo... kwa akili hiyo hauna tofauti na mtu aliyeandaa shamba akapanda mazao yake eti anatarajia kesho avune!? Ni impossible. Hivi vitu vina-phase, ndani ya hizo phase kuna stages tofauti tofauti lazima uwe na subira tu "mambo mazuri hayahitaji haraka"

Kwa kutumia mfano huo wa mazao hii miradi unaweza ukachukulia kama annual(vegetable) na perennial (fruit trees) crops. Sasa miradi iliyoanzishwa na Magufuli ni miradi dume(perennial crops) kama vile macadamia nut, minazi, parachichi mitiki, yaani ukiwekeza uku itakuchukua si chini ya miaka 5 kuanza kuvuna mavuno ya uhakika. Bado inatakiwa upambane na pests sasa hawa pests ndio tunapambana nao hapa.

Sasa miradi tulioizoea mingi ni kama annual crops tena horticultural one. Yaani baada ya miezi mitatu umevuna ila ubaya wake ni mazao hayadumu mda mrefu, perishable,

Sasa kwa hii miradi dume tunaenda kutengeneza ajira za kufa mtu kwasababu mazingira mazuri kwa wawekezaji yatakua ni yauhakika.

Kuna watu watakuja na porojo kibao hapa... yote ni kwasababu maslahi yao yaliguswa moja kwa moja, na kwanini yaguswe ni kwasababu hawakua wanastaili(wote tunajua sakata la vyeti fake, wafanyakazi hewa, ukwepaji kodi,mikataba mibovu, ufisadi).

Alafu vijana mnatumika sana kwenye siasa...inawezekana unajua au huju. habari ndio hiyo.
 
hakuna kijana anayetumika hapa wote tunaakili timamu Kama wewe unamkubali Mimi simkubali usiforce tufanane Arif!
 
Magufuli alikuwa ni mchapa kazi, asiyevumilia uvivu, mwenye vision, na mwenye kujiamini na kuamini uwezo Wa ngozi nyeusi katika kujitegemea na kujisimamia.
A free minded person,
Angalau nchi yetu iliyokuwa underdog for years ilipata heshima iliyostahili na ilitajwa kote duniani.
Alikuwa too much agressive kwa upinzani and especially while dealing with mediocrity,
Hakupenda ujinga kama mimi nisivyopenda incompetency, uvivu na ujinga.

Hapa I can rank the best presidents Tangu tupate uhuru

1. Mwalimu JK Nyerere
2. John P Magufuli
3. Benjamin Mkapa
4. Ally Hassan Mwinyi
5. Jakaya Kikwete
6. Samia Suluhu Hassan

NB. Tunahitaji kiongozi kama Magufuli, Huku mtaani watu Wa kawaida ambao ni over 99% ya Watanzania they miss him big time,
Duniani hatudumu milele, Apumzike kwa Amani.
We dini gani mkuu?
 
Matapeli na yaliyozoea vya kunyonga ndio yatamponda huyu mzee, wakati pia matoto yao aliyasomesha bure mpaka sasa yanasoma sababu yake.. Baba zao wakikosa pesa wanamsingizia jpm..

Angekuwepo sasa hivi vijiji vyote nusu vilivyobaki vingekuwa na umeme.. Kitu ambacho watangulizi wake kimewashinda. Yeye kafanya kwa muda mchache tu..
 
Alikua Mwizi aliyejificha kwenye kivuli Cha Uzalendo uchwara, Hii ilidhihirika pale alipokuwa waziri wa ujenzi baada ya kuchukua nyumba za Nation Housing maeneo ya upanga na Oysterbay na kuwapa ndugu,marafiki na hawara kwa janja janja za nyani
Yaani kiufupi ni alifoji document Kwa kuzuga kauza kumbe kajiuzia mwenyewe Kwa Bei ya maandazi!

Harafu Sasa alikataa kukaguliwa na CAG prof Assad upotevu wa zaidi ya Tsh trillion 1 zilizopotea kimagumashi na Kwa kutopitishwa na bunge,
Akamuundia zengwe CAG Kwa kumstaafisha chini ya kamati ya roho mbaya wakiongozwa na Kimbunga Jobo wa pale Makao Makuu ya Bunge!

Miradi ya Matrillion kupelekwa kijijini kwao Chato ikiwemo intanational airport ambapo haikuidhinishwa na bunge Wala kukaguliwa na mkaguzi Mkuu wa serikali yaani CAG

Naanza na hayo kwanza nakuja na povu la buku jero kumkandia Nduli Jiwe!
Keep waiting!
Kwenye nyumba za national housing Sisi hatujui nikiwa kigoma kata ya kamara daraja la lwiche akiwa waziri alisimamia kwa vitendo daraja lile na kulikuwa kuna ufujaji mkubwa wa vitu pale sitosahau alisismama Imara kwa watu wa kigoma watanielewa
Ila kwenye urais sote ni mashuhuda hata mipira ya miguu tunasema alijaribu
Ila kwa the late president mr Magufuli kwangu halujaribu bali aliweza
Rejea wakati akiikataa brbr ya kona ya bwiru kiloleli mpaka buzurugwa mwanza
 
Sasa hawataki hawa waja, wanaoamini katika Magufuli wanatoa sababu hawa wengine wanaenda kinyume na thread inavyotaka, tatizo la hawa jamaa mpaka wanaonekana ni kituko ni pale wanaposhindwa kutetea hoja wanabaki kutoa maneno ya kashfa ambayo hayasaidii na wala hayawezi kuondoa ukweli kwamba Magufuli ndiye aliyeanzisha Tanzania mpya kwa kufanya mambo mengi ndani ya muda mfupi mfano:

Ujenzi wa vituo vya afya vingi kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa barabara kilometers nyingi kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa mabwawa makubwa ya umeme kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa madaraja ya kuvunja rekodi kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa meli kubwa na vivuko kila mahali.

Ujenzi na ukarabati wa shule nyingi.

Ujenzi wa na ukarabati wa Airports na ports nyingi kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa miji mipya mfano Dodoma.

Uunganishaji umeme kwa wananchi kwa asilimia kubwa kuwahi kutokea.

Upelekaji maji vijijini kwa kasi kubwa kuliko Rais yoyote.

Ujenzi wa barabara za kisasa flyovers na interchanges.

Ununuzi wa ndege nyingi kuliko awamu yoyote.

Usimamizi uliotukuka wa rasilimali mfano madini na kwa mara ya kwanza madini yakaanza kuleta faida mpaka sasa tunavyoongea ndiyo sekta yenye mchango mkubwa katika uchumi wa nchi, hii haijawahi kutokea kabla yake.

Kurudisha nidhamu kazini kwa watumishi wa umma, hili wala sihitaji kulitolea ufafanuzi.

Ujenzi wa miundombinu ya reli, haijawahi kutokea Tanzania ikajenga reli kwa pesa yake hata Nyerere alishindwa.

Na mengine mengi, sasa hizo ni hoja zinazohitaji mtu makini wa kuzipinga kwamba si kweli na hawezi kutokea mtu huyo mana huo ndio ukweli yani hizo ni facts huwezi kuzipinga, na kama yupo mtu wa kuzipinga hizo facts atokee apinge kwa hoja pasipo matusi, hicho ndicho kinachowakosesha raha hawa Anti-Magu.
Siku zote wasiokuwa na hoja hukimbilia matusi.
 
Naanza na no 3
Sikatai miradi kupelekwa Chato kimkakati ila napinga kwanini miradi mingi iliyopelekwa Kule Ina bajeti kubwa kuzidi uhalisia wa eneo
Kingine mingi ya miradi hiyo haikukaguliwa na mkaguzi Mkuu wa serikali wala haikupitishwa na bunge
Kingine kandarasi ya miradi hiyo haikuwekwa wazi Kama sheria inavyotaka kua tenda itangazwe na Wazabuni wajitokeze wagombee tenda kisheria ila maajabu ikapewa kandarasi Mayanga Construction ambayo Kwa tetesi inadai ni kampuni iliyokua na mkono wa Jiwe!

Hilo swala unalichukuliaje?
Mzee tetesi peleka fb,hapa tunataka real fact
 
Magu alishindwa ku balance mambo yake. Siku zote unapokuwa kiongozi usitake kuwa mtawala.

Kuna tofauti kati ya kiongozi na mtawala. Sasa Magu alijiona mtawala kama absolute monarchy fulani kama Kim Jong Un. Aliamua alilotaka bila kujali miongozo mbali mbali iliyopo kama katiba n.k

Alichukia sana mtu yeyote alieenda kinyume nae (aliempinga) au alietaka kumshauri. Na hili limesababisha akaua watu na kutesa wengine. Kesi zakubambikiwa kila siku. Wenye hela wote walitingishwa.

Japo kuna mazuri mengi pia aliyafanya kama kuwa na msimamo na kutekeleza miradi kadhaa bila kusua sua na uchapakazi mtimilifu lakini alishindwa kujua kuwa katika nafasi aliyokuwepo lazima kuwe na watu ambao hawatakubaliana nae. Hivyo alipaswa kujua kuwa lazima akosolewe na kushauriwa.

Pia ni rais ambae alikuwa anapenda maendeleo ya vitu na sio watu. Ndio maana yeye alikuwa kila siku ni miradi na uzinduzi wa miundombinu tu. Mara madaraja mara barabara, reli n.k.

Alishindwa kutambua kuwa 'standard' way ya kupima maendeleo ni kuangalia GDP per capita. Yani uchumi wa mtu mmoja mmoja.

"GDP per capita measures the economic output of a nation per person. It seeks to determine the prosperity of a nation by economic growth per person in that nation."

Ni ajabu sana unakuta serikali inanunua ndege, inajenga miundombinu kibao lakini hali za watu ni tete wengi per capita income ni chini ya dola moja. Hivi mtu ambae hana uhakika wa kula au kuvaa anaweza kwenda kupanda ndege? Ndio maana ATCL inajiendesha kwa loss.

Ilitakiwa focus ingekuwa kwenye per capita income ili watu wakishakuwa na hali nzuri wanafanya manunuzi biashara zinakuwa serikali inapata kodi na mzunguko wa hela unakuwepo. Baada ya hapo serikali inafanya hizo projects na zinakuwa na tija kwa wananchi na serikali kwasababu watu wata afford kuzitumia kwasababu wana hela.

Tatizo mzee aligoma kushauriwa. Sijawahi kufikiri kuwa nchi hii hatuna wataalamu wa uchumu wenye uwezo wa kumshauri rais. Hata sisi ma laymen tunaobumba bumba tunaweza kuona concepts za kiuchumi rahisi kama hizi.
Ivi kipi kinapaswa kitangulie miundombinu bora kisha uchumi wa mwananchi Au uchumi wa mwananchi kisha miundombinu?

Ila navyofahamu Mimi miundo mbinu bora inamchango mkubwa kwa kipato cha mtu mmoja mmoja na inanishangaza tutaanzaje na uchumi wa mtu bila kuboresha vitu kama ivyo.

Nyuma ya miundo mbinu kuna manufaa makubwa ambayo yanaweza kulisaidia taifa kusonga mbele kiuchumi
 
MAGUFULI ALIKUA ANALENGO GANI NA HII NCHI.
Hapa ndio kwenye point.

Kwa mtu alie normal( hana mihemko (akiacha sababu zingine pembeni)) na mwenye upeo na akatumia akili tu yakuzaliwa hawezi kubeza jitihada za magufuli na serikali yake awamu ya tano.

Yani kabisaaa!!! Mtu huoni impact ya projects zilizoanzishwa kweli? Hapa utakua na upeo au uelewa wa mambo mdogo sana, Unafikilia leo tu, Hizo project ni process inayohitaji coordination ya hali ya juu kwahiyo lazima zitachukua muda kuzaa matunda.

Jipime upeo wako hapa; yani wewe ulitaka baada tu ya miradi kukamilika mapato yaanze kupanda hapohapo... kwa akili hiyo hauna tofauti na mtu aliyeandaa shamba akapanda mazao yake eti anatarajia kesho avune!? Ni impossible. Hivi vitu vina-phase, ndani ya hizo phase kuna stages tofauti tofauti lazima uwe na subira tu "mambo mazuri hayahitaji haraka"

Kwa kutumia mfano huo wa mazao hii miradi unaweza ukachukulia kama annual(vegetable) na perennial (fruit trees) crops. Sasa miradi iliyoanzishwa na Magufuli ni miradi dume(perennial crops) kama vile macadamia nut, minazi, parachichi mitiki, yaani ukiwekeza uku itakuchukua si chini ya miaka 5 kuanza kuvuna mavuno ya uhakika. Bado inatakiwa upambane na pests sasa hawa pests ndio tunapambana nao hapa.

Sasa miradi tulioizoea mingi ni kama annual crops tena horticultural one. Yaani baada ya miezi mitatu umevuna ila ubaya wake ni mazao hayadumu mda mrefu, perishable,

Sasa kwa hii miradi dume tunaenda kutengeneza ajira za kufa mtu kwasababu mazingira mazuri kwa wawekezaji yatakua ni yauhakika.

Kuna watu watakuja na porojo kibao hapa... yote ni kwasababu maslahi yao yaliguswa moja kwa moja, na kwanini yaguswe ni kwasababu hawakua wanastaili(wote tunajua sakata la vyeti fake, wafanyakazi hewa, ukwepaji kodi,mikataba mibovu, ufisadi).

Alafu vijana mnatumika sana kwenye siasa...inawezekana unajua au huju. habari ndio hiyo.
Umeongea point kubwa sana mkuu lkn hawa waja hawataweza kukupinga kwa facts cz hawana, ila wataishia kukutukana tu, hawa ndio wajuwaji wa mitandaoni.
 
Back
Top Bottom