Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Hivi umeandika haya ukiwa timamu kabisa au umelewa?
Yaani miaka 60 Toka uhuru wapinzani ndio walikua kikwazo?

Wewe na Jiwe akili zenu za ajabu Sana Aisee unatia aibu Kwa hiyo comment yaani am sure hata MATAGA pori watakuja kukupinga Kwa nguvu zote,
Haya Sasa zile ajenda zake za kuweka Bunge la kijani zilitimia unaona kinachotokea?

Mlisema hii nchi wapinzania ndio tatizo ndani ya kipindi kifupi tu Cha bunge la kijani kuhodhi bunge wao wenyewe wameshakiri nchi bila upinzani ni sawa na kutia maji kwenye Tenga

Aliyewaamisha kua upinzani unachelewesha maendeleo baada tu ya uchafuzi wa uchaguzi akaanza kuona aibu kubwa baada hata wale raia waliomuunga mkono nafsi kuwasuta waakanza vunja Hadi katiba kulazimisha kambi rasmi ya upinzani ndio wale wabunge Covid 19 kina Mdee
Tunaowaona wakitafuna Kodi zetu Kwa Ujinga wa mpuuzi Jiwe!

Ona hata aibu shame on you kuleta hoja dhaifu!
Hehehehee hoja dhaifu alafu unashindwa kuijibu, hilo ndo tatizo la Anti-Magu hamna sababu za msingi kabisa za kumkataa Magu hamna zaidi ya matusi basi.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Hehehehee hoja dhaifu alafu unashindwa kuijibu, hilo ndo tatizo la Anti-Magu hamna sababu za msingi kabisa za kumkataa Magu hamna zaidi ya matusi basi.
kwahiyo hapo juu ndio umejiona umeandika hoja ya maana kweli!
Bro umetia aibu tu Sana tu yaani mbaka hapo nimeamini wewe ulikua shabiki mjinga wa Jiwe
Na nyie ndio mliomponza Mzee wa watu mbaka akaumbuka!
 
06: Aliamsha hamasa ya watanzania ya kujiamini na kujiona kwamba wanaweza.
Naunga mkono hoja mkuu wangu na aliamsha morale ya kufa mtu,alifanya watu wajiamini hata kusema uongo mbele za Umma bila hata chembe aibu mfano ni Pale
Kassim Majaliwa Kassim aliposimama mbele ya mimbari ya msikiti kule Njombe na kuwatangazia Watanzania Kwa ujasiri uliotukuka kwamba Rais ni mzima na anachapa kazi
Wakati kiuhalisia alikua hoi bin Mfu!
Huo ni ujasiri wa ajabu na kujiamini kulikopitiliza

Na Bado yupo anahudumu hata hakujiudhuru Kwa kuudanganya umma!

Only In Tz!
 
Hehehehee hoja dhaifu alafu unashindwa kuijibu, hilo ndo tatizo la Anti-Magu hamna sababu za msingi kabisa za kumkataa Magu hamna zaidi ya matusi basi.
Ukishakuwa tu mfuasi wa kundi sijui pro-magu sijui ant-magu unakuwa msukule.

Binadamu timamu aliye huru anatoa hoja, anapinga hoja ama anasapoti hoja.

Sasa ukisema hakutaka upinzani na akaweka chama chake ili asipate shida kujenga stigla george unaijua tafsiri yake au na wewe ni msukule?
 
kwahiyo hapo juu ndio umejiona umeandika hoja ya maana kweli!
Bro umetia aibu tu Sana tu yaani mbaka hapo nimeamini wewe ulikua shabiki mjinga wa Jiwe
Na nyie ndio mliomponza Mzee wa watu mbaka akaumbuka!
Sasa unapoanza kutoa matusi haitasaidia kuepuka ukweli [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ukishakuwa tu mfuasi wa kundi sijui pro-magu sijui ant-magu unakuwa msukule.

Binadamu timamu aliye huru anatoa hoja, anapinga hoja ama anasapoti hoja.

Sasa ukisema hakutaka upinzani na akaweka chama chake ili asipate shida kujenga stigla george unaijua tafsiri yake au na wewe ni msukule?
Anti-Magu wengi ni matusi tu mmeajaaliwa.
 
Wewe unaweza kuniuliza swali mm wewe? Haya liko wapi hilo swali mbn silioni.
Ndio naweza kukuuliza ila wewe unaweza usijibu kama haitakupendeza.

Nimeuliza:

Sasa ukisema hakutaka upinzani na akaweka chama chake ili asipate shida kujenga stigla george unaijua tafsiri yake au na wewe ni msukule ilimradi usifie tu hata kama sifa zinamchafua?

Yafuatayo ni maneno yako post namba 101 ukimjibu dumas;

"So Magu alikuwa hapendi unafki unafiki na ndiyo maana hakutaka upinzani kabisa, upinzani wa Afrika unachelewesha maendeleo ya hili bara, utakuta nchi inahitaji kujenga stiglers gorge lakini upinzani unagoma, ukija kuchunguza kumbe wamelipwa vipesa na watu ili mradi usifanyike nchi iwe inaingiza majenereta kwa wingi."
 
Ukimtoa JKN my best pres,ni Hon Ben Mkapa...
Itatuchukua muda mrefu kupata kichwa kama hiki,alijenga taasisi imara ambazo zinafanya vizuri mpaka sasa.

Akifuatia kwa karibu na Hon JK. Mungu ampe afya njema,kipindi cha huyu baba maisha yalikua mazuri mno,pamoja na vyeti feki na kelele za upigaji ,lakini,
1.Aliajiri kila mwaka
2.Alipandisha madaraja wafanyakazi
3.Alijenga miundo mbinu bila majisifu yoyote
4.Uhuru wa kujieleza na kuchallenge serikali ulikua mkubwa.
5.Upendo miongoz mwa Watz ulikua mkubwa...no chuki kati ya CCM na upinzani(hoja zilihusika zaidi kuliko kuumizana)
Niishie hapo,Mungu aendelee kumlinda mh.JK..
 
Habari zenu wanajukwaa, baada ya kugundua kuwa mtu huyu imeshindikana kabisa kusahaulika ndani ya mioyo ya Watanzania na wasio Watanzania nimeona nianzishe uzi ambao utagusa pande zote yani wale wanaodhani alikuwa Rais bora na wale wanaodhani hakuwa Rais bora.

Ikumbukwe kwamba tangu amefariki mtu huyu imepita takribani miezi sita na siku kadhaa mpaka hapa ninapoandika huu uzi, sasa naomba wale Magufulians waseme kwanini wanadhani huyu alikuwa Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na watoe sababu za kusema hivyo pia wale wanaodhani hakuwa Rais bora watoe sababu zao.

Ndugu zangu nimelazimika kuanzisha huu uzi kutokana na kile ninachokiona kwamba jina la Magufuli sasa limekuwa kama dini mana unapomponda tu kama pembeni yako kuna mfuasi wake basi hawezi kukuacha salama.

Hii imepelekea kutokea mikanganyiko na sintofahamu kwenye majukwaa mbalimbali inafikia kipindi unakuta mada haihusiani na Magufuli lakini uzi unaharibika kwa sababu ya u-Magufuli vs u-Anti Magufuli.

Sasa ndugu zangu tusiendelee kuharibu nyuzi za watu, kama una dukuduku lako kuhusiana na kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kuongoza Tanzania basi weka hapa dukuduku lako au maoni yako juu ya mwamba huyu yaweke hapa jamii ifahamu ni kwa namna gani kiongozi huyu alikuwa mzuri au mbaya.

Nianze na mimi binafsi msimamo wangu juu ya JPM, ni kwamba namuona kama Icon na benchmark ya viongozi waliopo na watakaokuja kwasababu zifuatazo[emoji116][emoji116]

1. Muanzilishi wa Tanzania mpya. JPM alikuwa kiongozi mwenye uthubutu wa kuwakaripia viongozi wote walio chini yake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba iwe ni viongozi wa kuteuliwa na yeye mwenyewe au wa kuchaguliwa basi viongozi walitii, ilikuwa ni utaratibu kwa viongozi wa Tanzania waliochini ya Rais kikatiba kujiamulia mambo watakavyo wao ikibidi hata kukaidi maagizo yanayotolewa na Rais, hii ilipelekea huko nyuma nchi yetu kupoteza muelekeo lakini chini ya JPM maagizo yakawa yanafuatwa na kasi ya utendaji ikawa kubwa kuwahi kutokea Tanzania.

2. Kiongozi mkweli daima. Mtu huyu alikuwa ni moja kati ya binadamu wachache wakweli, alikuwa mwanasiasa pekee asiyejuwa kuongopa, ilifika mahali akajiingiza kwenye mgogoro na wanasiasa wenzake ndani ya CCM kwakuwa wengi wao hawakuzoea ukweli, JPM akisema hili hapana basi juwa kwamba halitatokea au akisema hili linawezekana basi juwa hivyo, hakuwa mtu wa kupepesa macho, alikuwa na uwezo wa kuongea ukweli hadharani pasipo kuficha ficha kitu chochote, hii ikapelekea viongozi waliokuwa wanaendekeza siasa majitaka kumuogopa kwani mzee yule hakuwa akijali kama unatokea CCM au upinzani.

3. Msimamo mkali. Chini ya JPM tuliona Tanzania yenye msimamo na isiyoyumbishwa na mtu yeyote au taifa lolote lile liwe na uchumi mkubwa au mdogo, hii ikapelekea Tanzania kufahamika zaidi kimataifa na duniani kote.

4. Kiongozi mwenye maono. Hayati JPM alikuwa ni kiongozi mwenye maono, hili liko wazi kwani maono yake hasa kwenye nyanja za kiuchumi ndio zikapelekea nchi yetu kuingia uchumi wa kati kabla ya muda uliokusudiwa, hii ilitokana na maono na jitihada zake kuhakikisha nchi yetu inajitegemea kwa kuanzisha miradi iliyoonekana haiwezekani lakini chini ya uongozi wake ikawezekana, pia maono yake yalijidhihirisha hata kwenye ugonjwa ulioikumba dunia kwa sasa ugonjwa wa Corona, nchi nyingi duniani zimeanza kutumia theories alizozitoa Hayati JPM.

5. Kiongozi mwenye ushawishi. Hayati JPM alikuwa na karama ya ushawishi mbele ya jamii, alikuwa na uwezo wa kusema jambo fulani na jamii nzima ikakubaliana naye kwa asilimia kubwa, kiukweli kabisa hata leo hii JPM akiamka na akasema watanzania wachanje basi believe me dawa za kuchanja hazitatosha, hii ni kutokana na imani kubwa aliyojiwekea mbele ya jamii kwakuwa watanzania waliamini kwamba JPM ana upendo wa dhati kwa wananchi wake na hawezi kuwarubuni kwa namna yoyote ile.

6. Mtu wa Mungu. Licha ya mapungufu yake kibinaadamu lakini ni ukweli usiopingika kwamba JPM alikuwa ni mtu wa Mungu, siku zote za uongozi wake hakuacha kumtegemea Mungu na hili alilifanya hadharani kwa kumtaja Mungu popote alipoenda na watu wake wakaribu wanasema mzee yule ulikuwa ni utaratibu wake kumtanguliza Mungu mbele.

7. Kipenzi cha wengi. Ukiacha mitandao ambao kuna wachache wanaomsema vibaya Magufuli ni dhahiri shairi kwamba hayati alipendwa na wengi, hii ilijidhihirisha pale alipofariki, umati uliojitokeza haukuwahi kutokea na sidhani kama utatokea kwa siku za karibuni, sio kwamba walioenda kumuaga walienda kukejeli bali waliguswa haswa, vilio kila pembe ya waagaji na kila sehemu mwili ulipoenda, hii inathibitisha ni jinsi gani watanzania walimpenda kiongozi wao.

Yako mengi ya kumuelezea Magufuli lakini itoshe kwa haya niliyoyaandika kumuelezea, mengine niwaachie ninyi wenzangu karibuni.
Magufuli nilichomkubali ni kutokuwabembeleza, kuwatia jambajamba na kuwatoa uharo watumishi wa umma na wengineo.

Ila nilikuwa simuamini anapopeleka pesa ni wapi, maana alibana kisenge.
 
Ndio naweza kukuuliza ila wewe unaweza usijibu kama haitakupendeza.

Nimeuliza:

Sasa ukisema hakutaka upinzani na akaweka chama chake ili asipate shida kujenga stigla george unaijua tafsiri yake au na wewe ni msukule ilimradi usifie tu hata kama sifa zinamchafua?

Yafuatayo ni maneno yako post namba 101 ukimjibu dumas;

"So Magu alikuwa hapendi unafki unafiki na ndiyo maana hakutaka upinzani kabisa, upinzani wa Afrika unachelewesha maendeleo ya hili bara, utakuta nchi inahitaji kujenga stiglers gorge lakini upinzani unagoma, ukija kuchunguza kumbe wamelipwa vipesa na watu ili mradi usifanyike nchi iwe inaingiza majenereta kwa wingi."
Umeona jinsi ulivyo mweupe kichwani, nilikuambia wewe huwezi kuniuliza mm swali [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Umeona jinsi ulivyo mweupe kichwani, nilikuambia wewe huwezi kuniuliza mm swali [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
sio hawezi kukuuliza swali mbona umeulizwa ila huna jibu zaidi za kuruka ruka tu bila hoja wewe ndio tafsiri ya kilaza halisi
Hakuna hoja uliyojibu kitaalamu tokea uanzishe sledi zaidi ya ushabiki wa kupumbavu!
 
Naunga mkono hoja mkuu wangu na aliamsha morale ya kufa mtu,alifanya watu wajiamini hata kusema uongo mbele za Umma bila hata chembe aibu mfano ni Pale
Kassim Majaliwa Kassim aliposimama mbele ya mimbari ya msikiti kule Njombe na kuwatangazia Watanzania Kwa ujasiri uliotukuka kwamba Rais ni mzima na anachapa kazi
Wakati kiuhalisia alikua hoi bin Mfu!
Huo ni ujasiri wa ajabu na kujiamini kulikopitiliza

Na Bado yupo anahudumu hata hakujiudhuru Kwa kuudanganya umma!

Only In Tz!
Ujasiri ni ule uwezo wa kusimamia na kupambania unachokiamini bila kujali wala kuhofia chochote.

Huu uwezo watz wengi hawana na Magu alijitahidi sana kuuchochea.

Kwamba PM alidanganya hilo ni lake yeye kama yeye halihusiani na mada.
 
sio hawezi kukuuliza swali mbona umeulizwa ila huna jibu zaidi za kuruka ruka tu bila hoja wewe ndio tafsiri ya kilaza halisi
Hakuna hoja uliyojibu kitaalamu tokea uanzishe sledi zaidi ya ushabiki wa kupumbavu!
Hebu niulize wewe hilo swali aliloniuliza.
 
Back
Top Bottom