Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Huna akili kabisa wewe, ushawahi huwafikiria wakulima wasokuwa na vyeti vya kuajiriwa sehemu? unahisi nchi hii ni ya wasomi pekee? hizo ajira unazozungumzia za kada ya afya unamaanisha alikosea kujenga hospitali? leta takwimu hapa utoneshe kabla ya JPM tulikuwa na hospitals ngapi za wilaya zilizojengwa baada ya uhuru na ulinganishe na zilizojengwa na JPM pekee ndani ya miaka mitano, ulitaka aajiri watu ndani ya miaka mitano sawa na miaka yote ya uhuru? huna kitu kichwani, wanaowatuma wangojee shoo.
Sibishani na punguani
 
Hhhhhhh...muuza ngada na shog.a leo anauwezo wa kutambua nani punguani, maisha yanaenda kasi sana..asompenda Magufuli ni teja, mwenye vyeti feki, fisadi, shoga, kibaraka wa mabeberu, mwendawazimu....
Mkuu sitaki ban maana umekuja tu kukata mauno
 
Magu alishindwa ku balance mambo yake. Siku zote unapokuwa kiongozi usitake kuwa mtawala.

Kuna tofauti kati ya kiongozi na mtawala. Sasa Magu alijiona mtawala kama absolute monarchy fulani kama Kim Jong Un. Aliamua alilotaka bila kujali miongozo mbali mbali iliyopo kama katiba n.k

Alichukia sana mtu yeyote alieenda kinyume nae (aliempinga) au alietaka kumshauri. Na hili limesababisha akaua watu na kutesa wengine. Kesi zakubambikiwa kila siku. Wenye hela wote walitingishwa.

Japo kuna mazuri mengi pia aliyafanya kama kuwa na msimamo na kutekeleza miradi kadhaa bila kusua sua na uchapakazi mtimilifu lakini alishindwa kujua kuwa katika nafasi aliyokuwepo lazima kuwe na watu ambao hawatakubaliana nae. Hivyo alipaswa kujua kuwa lazima akosolewe na kushauriwa.

Pia ni rais ambae alikuwa anapenda maendeleo ya vitu na sio watu. Ndio maana yeye alikuwa kila siku ni miradi na uzinduzi wa miundombinu tu. Mara madaraja mara barabara, reli n.k.

Alishindwa kutambua kuwa 'standard' way ya kupima maendeleo ni kuangalia GDP per capita. Yani uchumi wa mtu mmoja mmoja.

"GDP per capita measures the economic output of a nation per person. It seeks to determine the prosperity of a nation by economic growth per person in that nation."

Ni ajabu sana unakuta serikali inanunua ndege, inajenga miundombinu kibao lakini hali za watu ni tete wengi per capita income ni chini ya dola moja. Hivi mtu ambae hana uhakika wa kula au kuvaa anaweza kwenda kupanda ndege? Ndio maana ATCL inajiendesha kwa loss.

Ilitakiwa focus ingekuwa kwenye per capita income ili watu wakishakuwa na hali nzuri wanafanya manunuzi biashara zinakuwa serikali inapata kodi na mzunguko wa hela unakuwepo. Baada ya hapo serikali inafanya hizo projects na zinakuwa na tija kwa wananchi na serikali kwasababu watu wata afford kuzitumia kwasababu wana hela.

Tatizo mzee aligoma kushauriwa. Sijawahi kufikiri kuwa nchi hii hatuna wataalamu wa uchumu wenye uwezo wa kumshauri rais. Hata sisi ma laymen tunaobumba bumba tunaweza kuona concepts za kiuchumi rahisi kama hizi.
Chalii yangu hakika umenena jambo la msingi Sana
Siku zote wataalamu wanashauri Ili nchi iendelee inapaswa ijenge mifumo imara sio kujenga viongozi imara,
Mfumo ukiwa imara hata mtu awe kilaza ataweza kuongoza nchi
Na ikaenda vema tu!

Tunahitaji mfumo imara sio viongozi imara ambao wanapita tu ila mfumo utadumu daima!
 
Naona anti - Magufuli hawana point zozote zaidi ya kutukana na Jazba, nazidi kujifunza vizuri kuwa Magufuli kafanya mazuri mengi, japo ni binadamu alikuwa na mapungufu yake. Mungu amrehemu Huyu mwamba.
Vipofu na misukule wa Lumumba wanaonaga Point basi?
Nyie ni kushangilia tu Kama mazombi onesha fact uliyoitoa hapa zaidi ya mipasho tu!
 
Ukweli daima unauma sana, waambieni wanaowatuma kwamba wajipange sana, tena sana vinginevyo watapotea kabisa kwa ramani ya siasa nchini, wapeni salamu akina "marope" pia wanaotaka kuuza TANESCO.
Hao ndo wanaojua maana ya uongozi siyo yule chizi
 
Hivi points zote zinazotolewa kuhusu Magufuli aliyofanya huzioni wewe? Au umemiss kutukana tu... maana ndio mnachoweza
 
Habari zenu wanajukwaa, baada ya kugundua kuwa mtu huyu imeshindikana kabisa kusahaulika ndani ya mioyo ya Watanzania na wasio Watanzania nimeona nianzishe uzi ambao utagusa pande zote yani wale wanaodhani alikuwa Rais bora na wale wanaodhani hakuwa Rais bora.

Ikumbukwe kwamba tangu amefariki mtu huyu imepita takribani miezi sita na siku kadhaa mpaka hapa ninapoandika huu uzi, sasa naomba wale Magufulians waseme kwanini wanadhani huyu alikuwa Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na watoe sababu za kusema hivyo pia wale wanaodhani hakuwa Rais bora watoe sababu zao.

Ndugu zangu nimelazimika kuanzisha huu uzi kutokana na kile ninachokiona kwamba jina la Magufuli sasa limekuwa kama dini mana unapomponda tu kama pembeni yako kuna mfuasi wake basi hawezi kukuacha salama.

Hii imepelekea kutokea mikanganyiko na sintofahamu kwenye majukwaa mbalimbali inafikia kipindi unakuta mada haihusiani na Magufuli lakini uzi unaharibika kwa sababu ya u-Magufuli vs u-Anti Magufuli.

Sasa ndugu zangu tusiendelee kuharibu nyuzi za watu, kama una dukuduku lako kuhusiana na kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kuongoza Tanzania basi weka hapa dukuduku lako au maoni yako juu ya mwamba huyu yaweke hapa jamii ifahamu ni kwa namna gani kiongozi huyu alikuwa mzuri au mbaya.

Nianze na mimi binafsi msimamo wangu juu ya JPM, ni kwamba namuona kama Icon na benchmark ya viongozi waliopo na watakaokuja kwasababu zifuatazo


1. Muanzilishi wa Tanzania mpya. JPM alikuwa kiongozi mwenye uthubutu wa kuwakaripia viongozi wote walio chini yake kwa mamlaka aliyopewa kikatiba iwe ni viongozi wa kuteuliwa na yeye mwenyewe au wa kuchaguliwa basi viongozi walitii, ilikuwa ni utaratibu kwa viongozi wa Tanzania waliochini ya Rais kikatiba kujiamulia mambo watakavyo wao ikibidi hata kukaidi maagizo yanayotolewa na Rais, hii ilipelekea huko nyuma nchi yetu kupoteza muelekeo lakini chini ya JPM maagizo yakawa yanafuatwa na kasi ya utendaji ikawa kubwa kuwahi kutokea Tanzania.

2. Kiongozi mkweli daima. Mtu huyu alikuwa ni moja kati ya binadamu wachache wakweli, alikuwa mwanasiasa pekee asiyejuwa kuongopa, ilifika mahali akajiingiza kwenye mgogoro na wanasiasa wenzake ndani ya CCM kwakuwa wengi wao hawakuzoea ukweli, JPM akisema hili hapana basi juwa kwamba halitatokea au akisema hili linawezekana basi juwa hivyo, hakuwa mtu wa kupepesa macho, alikuwa na uwezo wa kuongea ukweli hadharani pasipo kuficha ficha kitu chochote, hii ikapelekea viongozi waliokuwa wanaendekeza siasa majitaka kumuogopa kwani mzee yule hakuwa akijali kama unatokea CCM au upinzani.

3. Msimamo mkali. Chini ya JPM tuliona Tanzania yenye msimamo na isiyoyumbishwa na mtu yeyote au taifa lolote lile liwe na uchumi mkubwa au mdogo, hii ikapelekea Tanzania kufahamika zaidi kimataifa na duniani kote.

4. Kiongozi mwenye maono. Hayati JPM alikuwa ni kiongozi mwenye maono, hili liko wazi kwani maono yake hasa kwenye nyanja za kiuchumi ndio zikapelekea nchi yetu kuingia uchumi wa kati kabla ya muda uliokusudiwa, hii ilitokana na maono na jitihada zake kuhakikisha nchi yetu inajitegemea kwa kuanzisha miradi iliyoonekana haiwezekani lakini chini ya uongozi wake ikawezekana, pia maono yake yalijidhihirisha hata kwenye ugonjwa ulioikumba dunia kwa sasa ugonjwa wa Corona, nchi nyingi duniani zimeanza kutumia theories alizozitoa Hayati JPM.

5. Mtu wa Mungu. Licha ya mapungufu yake kibinaadamu lakini ni ukweli usiopingika kwamba JPM alikuwa ni mtu wa Mungu, siku zote za uongozi wake hakuacha kumtegemea Mungu na hili alilifanya hadharani kwa kumtaja Mungu popote alipoenda na watu wake wakaribu wanasema mzee yule ulikuwa ni utaratibu wake kumtanguliza Mungu mbele.

6. Kipenzi cha wengi. Ukiacha mitandao ambao kuna wachache wanaomsema vibaya Magufuli ni dhahiri shairi kwamba hayati alipendwa na wengi, hii ilijidhihirisha pale alipofariki, umati uliojitokeza haukuwahi kutokea na sidhani kama utatokea kwa siku za karibuni, sio kwamba walioenda kumuaga walienda kukejeli bali waliguswa haswa, vilio kila pembe ya waagaji na kila sehemu mwili ulipoenda, hii inathibitisha ni jinsi gani watanzania walimpenda kiongozi wao.

Yako mengi ya kumuelezea Magufuli lakini itoshe kwa haya niliyoyaandika kumuelezea, mengine niwaachie ninyi wenzangu karibuni.
Aliheshimu Demokrasia
Chaguzi zilikuwa za Haki na Huru
Wapinzani Walifanya Mikutano yao bila KAMATA kamata ya Polisi
Wabunge 19 Wasio kuwa na Chama Walivuliwa Ubunge Wao


Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Vipofu na misukule wa Lumumba wanaonaga Point basi?
Nyie ni kushangilia tu Kama mazombi onesha fact uliyoitoa hapa zaidi ya mipasho tu!
Tofauti na kuwapiga vita mapunga, mafisadi, vyeti feki, vibaraka, wanafki na mahujumu uchumi, uko na sababu gani ya kumchukia JPM uloitoa hapa? Lissu hata leo akija afisa yeyote mzalendo mwenye kuviishi viapo vyake lazima amshughulikie wala haitaji amri ya Amiri jeshi mkuu, vivyo hivyo kwa mjinga yeyote atayeenda kinyume na maslahi mapana ya Taifa lazima apotezwe, haki za ushoga ndo unazozitaka? ajira tushasema huko juu, hii ni nchi yetu sote hakuna alokuwa bora zaidi ya mwingine, hakuna ongezeko la mishahara na pesa ikaenda kujenga reli itayotumiwa na wote wafanyakazi na wakulima..tuliridhika.
 
Ukweli daima unauma sana, waambieni wanaowatuma kwamba wajipange sana, tena sana vinginevyo watapotea kabisa kwa ramani ya siasa nchini, wapeni salamu akina "marope" pia wanaotaka kuuza TANESCO.
Mkuu umepiga mlemle..mitaa.hira kweli hii mijitu, wametumwa kupima kina cha maji, "kigogo" wanahangaika sana, tunawafahamu na dawa iko jikoni.
 
Tofauti na kuwapiga vita mapunga, mafisadi, vyeti feki, vibaraka, wanafki na mahujumu uchumi, uko na sababu gani ya kumchukia JPM uloitoa hapa? Lissu hata leo akija afisa yeyote mzalendo mwenye kuviishi viapo vyake lazima amshughulikie wala haitaji amri ya Amiri jeshi mkuu, vivyo hivyo kwa mjinga yeyote atayeenda kinyume na maslahi mapana ya Taifa lazima apotezwe, haki za ushoga ndo unazozitaka? ajira tushasema huko juu, hii ni nchi yetu sote hakuna alokuwa bora zaidi ya mwingine, hakuna ongezeko la mishahara na pesa ikaenda kujenga reli itayotumiwa na wote wafanyakazi na wakulima..tuliridhika.
haaaaaaaa
Aisee kweli wewe ni mzigo Kuna msukule wowote pale Lumumba anamuweza Tundu Lissu Kwa hoja?
Acha kuchekesha jukwaa Aisee hivi ni nani yule aliyepewa mashtaka ya kubumba zaidi ya 50 mwaka 2017 ?
Mlimuweza basi?
Si ndio yule yule aliyepangua mashtaka yote mbaka kesi ikaendeshwa mbaka night na Judge akatupilia mbali mashtaka uchwara na mawakili wa serikali wakaumbuka!
Unajua kilichofuatia Ni Nini?

Mtu pori jiwe aliwatuma vikaragosi wampige risasi area D pale Dodoma na kumuandalia mazishi kwa hotuba ya kinafiki ya kumsifia ila ajabu jamaa mbaka Leo yupo hai ila dhalimu alishatangulia Chattle Mabatini!

Lissu mlimshindwa mahakamani,
Mkamshindwa Kwa bunduki

Leo unatuambia Nini wewe msukule wa jiwe?
 
haaaaaaaa
Aisee kweli wewe ni mzigo Kuna msukule wowote pale Lumumba anamuweza Tundu Lissu Kwa hoja?
Acha kuchekesha jukwaa Aisee hivi ni nani yule aliyepewa mashtaka ya kubumba zaidi ya 50 mwaka 2017 ?
Mlimuweza basi?
Si ndio yule yule aliyepangua mashtaka yote mbaka kesi ikaendeshwa mbaka night na Judge akatupilia mbali mashtaka uchwara na mawakili wa serikali wakaumbuka!
Unajua kilichofuatia Ni Nini?

Mtu pori jiwe aliwatuma vikaragosi wampige risasi area D pale Dodoma na kumuandalia mazishi kwa hotuba ya kinafiki ya kumsifia ila ajabu jamaa mbaka Leo yupo hai ila dhalimu alishatangulia Chattle Mabatini!

Lissu mlimshindwa mahakamani,
Mkamshindwa Kwa bunduki

Leo unatuambia Nini wewe msukule wa jiwe?
Hehe..akili za kupumliwa kisogoni na faru John bhana, mwambie aje nchini asiongelee space "majukwaa" yako wazi.
 
Hehe..akili za kupumliwa kisogoni na faru John bhana, mwambie aje nchini asiongelee space "majukwaa" yako wazi.
hata akija mna Cha kumfanya kwenye mahakama
Zaidi ya kutumia ubabe wa kijinga tu mummalizie Kwa risasi
Hamna hoja tunawajua nyie mahakamani ni weupe na watupu Sana hata PGO zinawashinda pimbi nyie ni zero brain!
 
japo mi yule mzee alinipiga hela. kwangu mimi alikuwa. 50/50. mzur na mbaya. na cwez kumlaum anaemsifia wala kumlaumu. coz kila mtu na tafsir yake. ni vigum mtu kumshawish mtu ambae amefilisiwa au ndugu yake aliuwawa na serikali yake kumpenda kama ilivyo vigum kwa aliyetoka akapiga maisha wakat wake akamponda.
lakn ukibalance stor utakuta Mzee alikuwa mtawala mzur na ila alikosa baadhi ya vitu muhm vya uongoz.
ila nataman kaela kangu alikochukua kwenye duka langu la kubadilishia hela wanirudishie jaman daa.
 
89. ....................90. ...................... 91. ..............................................92. USHINDI WA KISHINDO WA KURA ZA KWENYE MABEGI. 93. ............................................94...............
 
Back
Top Bottom