Basi la Kampuni ya Arusha One lapata ajali daraja la mto Wami

Basi la Kampuni ya Arusha One lapata ajali daraja la mto Wami

Uhuni wa madereva,hilo daraja jembamba hivyo yatapitaje mabasi mawili kwa pamoja?Hao Madereva naona walikuwa wamelewa pombe
 

Unaweza ukamkamata dereva ukamtandika bakora mpaka akajikojolea.​
 
MWAKA 1996 OCTOBER TULIPATA AJALI MBAYA SANA HAPA AIR MSAE ILIGONGANA NA TAYASSAR. MAISHA YA WATU WENGI YALIANGAMIA.
 
Hata private drivers mkuu, si ajabu kumwona mtu anaendesha huku anajibu SMS, au mwingine anaangalia hata movie kwenye simu.
Sasa hao nao ni shida nyingine,siku hizi polisi akikuona unacheza na simu wakati wa kuendesha gari unakula fine hapo hapo.
 
Halafu kwenye mto kuna mamba,viboko na samaki hatari sana
 
Hili daraja ningekuwa la kwanza kufikiria kulijenga kabla hata ya flyover za mjini, sijui kama tuna takwimu lakini nina uhakika sehemu hii ni kati ya sehemu zinaongoza kwa ajali nchini. Watanzania wengi wamepoteza Maisha hapa kuliko usumbufu wa kuwahi airport uliokuwa unafanyika makutano ya Tazara. Wakati umefika serikali itupie jicho hili eneo. Huwezi kupita hapo hata siku moja bila kukuta gari limepata ajali au kukuta mabaki ya vioo yenye kuashilia kutokea kwa ajali. Hebu tuanze kuweka kipaumbele kwenye Maisha ya wananchi kwanza. Mwananchi lives matter...
 
MwenyeziMungu asante kwakuwaokoa watu wako bila Neema yako hapo watu wangepoteza maisha yao, pia tunaomba tunusuru sisi watu wa kaskazini maana ndio njia yetu ya kwenda nyumbani zetu hilo daraja liko kama mtego ni ngumu sana mtu kuamini kwamba Hilo daraja lipo hivyohivyo kabla Tz haijapata uhuru😐😶
 
IMG-20180829-WA0014.jpg
IMG-20180829-WA0013.jpg
Sina hakika imetokea lini na nini chanzo but hapa ni daraja la Wami,hili basi limeponea chupu chupu kuzama mtoni,kusema ukweli hapa ni Mungu tu ndo katenda miujiza ya kunusuru viumbe wake hakuna namna ya kumsifu dereva wala nini,ni Mungu tu.
Ifike mahali sasa Serikali nayo ichukue hatua ya kujenga daraja la kisasa sio hadi msikie siku watu wamekufa ndio muanze kuhangaika....kulikua na haja gani ya kwenda kujenga uwanja wa ndege Chato ambao hauna umuhimu wowote kwa sasa na mnaacha kushughulikia hili daraja ambalo wakazi wa mikoa yote ya Kaskazini na nchi ya Kenya wanalitegemea, tusiwe wagumu wa kufikiri.
 
Back
Top Bottom