Bashe amlipua Membe

Bashe amlipua Membe

Usiangalie hoja kwa kumwangalia mtoa hoja. Angalia mantiki ya hoja na ujumbe unaobebwa na hoja inayotolewa. Namkumbuka Membe kwa uchambuzi wake wa habari za Kitine na mke wake akiwa kwenye matibabu Marekani. Aliandika kwa uchambuzi wa kiina sana, lakini kumbe nyuma ya pazia alikuwa na ajenda ya siri kumwingiza iKULU rafiki yake JK.Aliona Kitine angekuwa kikwazo kwa JK, AKAONA LAZIMA amwondoe kwa njia yoyote ile. Akafanikiwa kwa kuwa watu hawakumfahamu vizuri. Leo JK naye anataka kulipa fadhira kwa kumwingiza Membe Ikulu.
Inawezekana hoja ya Bashe ina ukweli. Katika kitabu chake cha Tujisahihishe JK Nyerere anasema ukweli usipuuzwe kwa kuangalia anayeusema kama ni kichaa au anatoka kamasi puani. Ukweli hata usemwe na nani una kawaida wa kujilipizia.
Usomali wa Bashe hauondoi ukweli wa Membe kuwa mnafiki kama kweli ni mnafiki
 
je ni mwana Ccm gani ambaye si mshirikina? Uchawi na majini ndio nguzo ya chama
 
Yatatimia lini maneno ya unabii huu? na nini dalili za utimilifu wake??

Babkey kasema hivi "Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama" nadhani hii inaweza kuwa ndio utimilifu wake !

 
Nchi inayoongoza kwa press conference za kujibu hoja zisizo na tija kuliko nchi nyingine wakati walikuwa wanauwezo wa kukaa na kuelezana ukweli, tunahitaji Taifa la kuvumialiana pale mtu anapokuwa na hoja tofauti na wewe maana itapunguza haya mambo ya kuita waandishi kwa ufafanunuzi, nilichojifunza taasisi nyingi watu huchukiana kisa wana mitazamo tofauti na ndio maana tuna shuhudia haya kila siku watu wanashindana kwenyeye vyombo vya habari hawafanyi mambo mengine. TUNASUBIRI UTUPAKULIE MAANA NI HAI YETU KUFAHAMU THOUGH WANABOA (na waandishi wetu hawatoki bure hapa)

Hivi ni kweli kwamba CCM tayari imekufa ! Eee bana eee! Duh ! Kweli hujafa hujaumbika , yaani mtu kama Bashe naye anaweza kufanya press conference kwa ajili ya ccm !
 
Hivi ni kweli kwamba CCM tayari imekufa ! Eee bana eee! Duh ! Kweli hujafa hujaumbika , yaani mtu kama Bashe naye anaweza kufanya press conference kwa ajili ya ccm !
Ndio kaka hujui ? CDM ndio wenye nguvu,CCM KUSHNEY ! , huoni MADIWANI wamepiga bao CDM 22 CCM 5,Alafu BASHE nikweli ni mwepesi ndio sababu kule NZEGA kura ya maoni za Ubunge alikuwa wa mwisho,wa kwanza alikuwa ni KIGWANGALA WA PILI SELELII NA WA MWISHO BASHE,we kichwa , me nakukubali unatisha lazima una Phd, andelea kutumia MAKALIO kufikiria.
 
Huyu Bashe si ndo yuko Dodoma na akina Fred Lowasa na Beno Malisa wakimpigia chapuo Lowasa awe mwenyekiti wa CCM hatimaye awe rais? Kwahiyo ni vita tu ya urais, hamna kitu hapa.

Anayepigiwa chapuo la Uenyekiti si Lowassa ni Karume
 
Hussein Bashe ni nani ndani ya CCM mpaka press conference yake ituumize kichwa?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
70522_100001601868505_7816183_n.jpg


BASHE AMTAJA MEMBE KUHUSIKA KUANDAA VIPEPERUSHI VYA KUMHUJUMU RAIS KIKWETE

Alipoulizwa kama yeye ni kibaraka wa Lowassa, Bashe alikana, lakini alisema anamuunga mkono kwa kila jambo analofanya.
“Mimi sio kibaraka wa Lowassa, lakini atagombea urais mwaka 2015, nitampigia kampeni na nitampa kura yangu kwani ni mwanasiasa mvumilivu, mzalendo na kama asingekuwa mvumilivu ni wazi kwamba nchi ingekuwa katika sura nyingine, hata mimi nimejifunza mambo mengi kutoka kwake,” alisema.


Source: Tanzania Daima
 
Hiyo ni vita ya makundi, Bashe lazima aseme hivyo maana asiposema ataambiwa ni yeye aliyeeandaa.
 
70522_100001601868505_7816183_n.jpg


BASHE AMTAJA MEMBE KUHUSIKA KUANDAA VIPEPERUSHI VYA KUMHUJUMU RAIS KIKWETE

Alipoulizwa kama yeye ni kibaraka wa Lowassa, Bashe alikana, lakini alisema anamuunga mkono kwa kila jambo analofanya.
"Mimi sio kibaraka wa Lowassa, lakini atagombea urais mwaka 2015, nitampigia kampeni na nitampa kura yangu kwani ni mwanasiasa mvumilivu, mzalendo na kama asingekuwa mvumilivu ni wazi kwamba nchi ingekuwa katika sura nyingine, hata mimi nimejifunza mambo mengi kutoka kwake," alisema.


Source: Tanzania Daima

ukweli ndio utakaoliweka huru taifa hili, maana utawasaidia wananchi kujua mbivu na mbichi!
 
Back
Top Bottom