Bashe amlipua Membe

Bashe amlipua Membe

Mkuu jifunze kufikiri kwanza kabla ya kuandika humu JF.

Tuko hapa kujadili hoja yake na sio personal issues.

Ununio Islamic Seminary ina husika vipi na hoja ya Bashe?

labda angesoma PUGU SEMINARY ndio kwake angekua bora watu wa aina hiyo skuzote wao hua ni IVYO CHA MUHIM NI KUMSAMEHE BURE ajui nini atendalo
 
Ili CCM ife kifo cha ASILI, hakuna JIWE litaachwa kusimama juu ya JIWE lingine. Kwasababu NGUZO kubwa inayokiongoza chama hiki ni FITINA na RUSHWA tunazozishuhudia waziwazi sasa. Hili linatokana na mfumo wa kinafiki na mitandao/makundi waliojitengeneza wenyewe. Sasa kila kundi linajiona lipo juu na hakuna linalotaka kujishusha. Walianza kwa uchaguzi wa Urais, wakaingia kwenye chaguzi zao za ndani ambao sasa ndiyo SUMU yao kubwa waliojitengenezea.


umesema kweli bro....................lakini.....dah hivi wadhani watanzania wamekomaa kisiasa hata kwa level hii ndogo ya kuona udhaifu wa CCM kweli. Nina wasiwasi na watanzania wenzangu............
 
wamarekan ni kina nani kwa ufahamu wako huo mdogo?

Acha chuki zako za kibaguz zisizo na mcng, kama angekuw haramia kuna sbb gan ya kutokukamatwa na vyombo vya dola? na hilo jina umelipata wapi kama cyo kwa wamarekani?
 
msomali huyo angalieni asije geuza tz ikawa kama somalia, wao wamezoea bunduki alias al shababu


mumeanza ukabila!tukiulizana wote tutajikuta hamna mwenye asili ya nchi hii ,tujadili hoya tusijadili mtu,mipaka waliweka wakoloni.
 
Duh! hii balaaa! halafu baada ya kutifuana watashikana mikono na kuimba. kidumu Chama cha Mageuziiiiiiiiiii.....watu: kidumuuuuuuuuuuuuuuu
 
Kibaraka wa Lowassa mkubwa huyu,wacha wasagane wenyewe Magamba kwa Magamba.
 
‎"Kwa maslahi ya chama chetu, kwa maslahi ya nchi yetu Membe ni hatari kama ukoma".... By Hussein Bashe; 2012.



Kwa maslahi mapana ya nchi EL ni hatari zaidi na ni janga kwa taifa! Mungu ibariki Tanzania!
 
70522_100001601868505_7816183_n.jpg


BASHE AMTAJA MEMBE KUHUSIKA KUANDAA VIPEPERUSHI VYA KUMHUJUMU RAIS KIKWETE

Alipoulizwa kama yeye ni kibaraka wa Lowassa, Bashe alikana, lakini alisema anamuunga mkono kwa kila jambo analofanya.
“Mimi sio kibaraka wa Lowassa, lakini atagombea urais mwaka 2015, nitampigia kampeni na nitampa kura yangu kwani ni mwanasiasa mvumilivu, mzalendo na kama asingekuwa mvumilivu ni wazi kwamba nchi ingekuwa katika sura nyingine, hata mimi nimejifunza mambo mengi kutoka kwake,” alisema.


Source: Tanzania Daima

.............. Hivi huyu Bashe ni nani katika nchi hii! au ndo yale yale ya kambare wote wana ndevu, hakuna mdogo wala mkubwa ........ maana kila akiongea neno linakuzwa sana............... sasa kama analazimisha kututafutia Rais ajaye atakuwa anakosea............ asitulazimishe

 
kanusu mbona umekaa jikoni sana? Lete hapa sebuleni, si ulisema utakuja kumalizia stori yote hapa?
 
Last edited by a moderator:
Namkubali kwa sababu sio mnafiki, mahali alipo anakiri yupo hapo- wengi wa wanasiasa wetu huwezi kujua ana msimamo gani au anaunga mkono nini/nani!!! mmojawao akiwa ni "namba 1"

Hivi lowassa alishatangaza nia ya kugombea urais?
 
wacheni siasa za makundi ccm yetu inakataza makundi watu wawili wa chama kimoja alafu kupingana ni hatari unampa adui mwanya wa kukuingia bila kujijua
 
salaam wana Bodi wote
Hongereni wana CCM kwa kufanya Mkutano wenu Mkuu huku kukiwa na mazingaombwe lukuki.

Naomba nimuongelee Bwana Hussein Bashe. Mwaka 2008 aligombea Umakamu mwenyekiti (UVCCM) na Beno Malisa akashindwa. Tena kwa mbinu kwani nilikuwa mmoja wa wajumbe wa mkutano Mkuu. Bashe alishindwa baada ya Mwenyekiti wa CCM kushawishi uongozi kubadili Ratiba ya Mkutano na kura kupigwa baada ya Hotuba ya Ufunguzi na si kesho yake kama ratiba ilivyovyokuwa isaema. Bwana bashe akakimbia Dodoma akiwa yeye na Bw. Nape, Rostam Azizi na wengine wengi baada ya matokeo kuvuja usiku wa saa 8.00.

Baada ya Mapacha watatu (R.A,E.L na A.C) kushambuliwa sana kwa tuhuma za Ufisadi na CCM kuanzisha slogan ya kuvuana Magamba Bwana Bashe akawa wakili kwenye media kwa kuwalinda na pengine kuwatetea na hata kuwajibia baadhi ya mambo (kwa Mfano Bashe alimjibia Rostam Kuhusu Uhusiano kati ya Caspian na Richmond) kuwashambulia kwenye media kina NAPE, SITA, MWAKYEMBE, MENGI nk. kuhusu tuhuma za Richmond na Ufisadi kupitia kampuni ya New Habari Coperation.kumbuka kuwa Nape NNauye ndiye aliekuwa wakala wa kuhesabu kura za Bashe 2008.

Bwana Bashe akagombea Ubunge nzega kupitia CCM wakamwambia sio Raia wa Nchi hii wakammwaga na mpaka leo hakuna lolote lilisomwa na Wizara ya mambo ya Ndani kuhusu Uraia wa Bashe. Haya tena akaomba NEC nako CCM wakamtosa. Anatajwa kuwa mtoa Rushwa kwenye uchaguzi wa UVCCM Leo anasambaza Vipeperushi vya kumpinga Mwenyekiti wao.

Kuna mambo mengi tu; Swali huyu Kijana CCM haimtaki, Lakini pia sio Raia kwenye hii nchi anafanya nini? Anaitakia nini CCM wakati imeonyesha kumkataa? Kwa nini anampinga Kikwete Uswahiba na kina beno waliokuwa wapinzani wake 2008 umeanza lini na uadui na kina membe Nape ,Sita waliokuwa wanambeba 2008 umeanza lini.

my Take: kama huyu kijana Chama chake Hakimtaki, Uraia wake ni Magumashi lakini bado anapata coverege kubwa kiasi hiki mi naona lipo Tatizo USALAMA WA TAIFA INGIENI KAZINI. Huyu mtu sie kabisa. Nahofia yasije yakawa ya yule waziri mhindi alikufa akaenda kuzikwa canada. Siku E.L akiwa Rais huyu Bwana atakuwa waziri wa Ulinzi msipoangalia.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom