Based ON True story

Based ON True story

Kuna kipindi miaka ya nyuma nilipataga deal la kuua mbwa koko wasio na wenyewe wanaozurura mtaani kwa kutumia bunduki

Siku ya kwanza ilienda vizuri niliua mbwa 47 kwenye vitongoji viwili siku iliyofuata yule afsa mifugo akaniambia leo ni jumapili tutatembelea mabucha nikakwambia sawa by saa 12 asubh tukaanza kupita bucha moja baada ya jingine

Tulipita mabucha kama matatu ukweli nililenga mbwa zaid ya 15 waliokuwa wanazurura kwa kuokota mifupa na finyango za nyama zilizodondoka chini.

Bucha la nne hapa ndipo nilipoona tukio la ajabu tumefika tu na byke jamaa akapaki mbali kidogo tukasogea pale buchani kwa miguu taratibu ....niliangaza macho eneo la pale buchani nikaona mbwa kama watatu bs nikatarget wa kwanzia nikapiga kuja kupiga wapili loooh akanguka chini na milio mkali gafla akabadilika na kuwa bibi kizee huku akilia kwa uchungu na akafia palepale huku mdomo wake na mikono ikiwa imechafuka mafuta na midamu kibao haikuwa hallucinations na nilikua sjanywa pombe hii ilinishangaza sana inawezekana vipi mbwa kubadilka na kuwa binadamu?

Ilikua ni tukio la kustajabisha sana pale buchani baadhi ya raia wakaanza kuongea chini chini huyu ni bibi flani tunamjua na ni mchawi mkubwa tukawauliza leo alikuwa hapa buchani wakajibu hapana dah afsa alipiga simu police na kuripot tukio.

Ikabidi nistop lile deal aise.
Walikulipa shilingi ngapi kwa kila mbwa uliyemdedisha?Na huyo bibi ulivyomuua walikupa shilingi ngapi?
 
Hiyo ni sayansi na teknolojia ya binadamu ya kwanza ya binadamu zamani binadamu alitegemea nguvu kutoka kwenye miti na wanyama, lakini sasa hivi anategemea nguvu kutoka kwenye madini, alafu leo anaiita teknolojia! Kama Akili Mnemba (AI) ni matokeo ya kuweka mabilioni ya nyaya kwenye mashine ili kurahisisha mahesabu, kinachotumika pale si ni madini ya mawe silicon na quartz? Sasa, je, mawe yanaweza kufikiria? Mbona hata aliyetengeneza AI mwenyewe anashangaa alipata maono afanye vile ila alichotengeneza kimekuwa na UWEZO usio wakawaida ,Hata maisha tunayoishi sasahivi ni uchawi sema tushazoea mazingira....hata zamani wachawi walikuwa wanaoteshwa au mtu tu anakuwa na wazo maono analifanyia kazi akishafanikisha anawafundisha wengine basi utaaramu huo unasambaa Dunia nzima,vivyo hivyo hata kwa Hawa wachawi wakisasa tunaowaita wanateknolojia mtu analala ghafla anapata aidia anaanza kuoneshwa michoro atumie madini gani hatimaye anapata shauku anafanyia majaribio hatimaye kitu linakuwa kamili akishafanikisha basi anafundisha wengine utaaramu unaenda Dunia nzima sema sasa hivi yameshakuwa majanja yana weka patent
 
Back
Top Bottom