Nimekumbuka Polisi walikuja kijijini kwetu, tena walikua wamekuja kufanya msako was wawindaji holela, coz kijijini kwetu kupo karibu na msitu mnene, ila sio hifadhi.
Basi walivyofika wakafikia kwa mtendaji was kijiji, wakapokelewa, walivyomaliza mazungumzo yao, wakaambiwa kuna vijana fulani hao ndio hodari was kuwinda wanyama pori bila kibali wala ruhusa,
Sasa walivyofika kwa kijana m1 hawaku mkuta muhusika, ila walimkuta mzazi wake, yaan baba ake, katika kuhoji baba anagoma kutoa ushirikiano, si wakaanza kumpiga yule baba, acha wambaluzee, wanashangaa anageuka cobra, asiwaumize nini, polisi wawili walifia hospital ya mkoa, kwa kuchelewa matibabu, toka palee, heshima na adabu.
Waajiriwa was serikali wakija kijijini kwetu wanaishi kwa tahadhari..kwetu uchawi unanunuliwa tena kwa grade, ni bei yako tu.