Barua: Zitto akataa posho za vikao

Barua: Zitto akataa posho za vikao

Wanajamii angalieni sana ujanja wa wanasiasa.zito katoa kwa mkono wa kulia na kuchukua kwa mkono wa kushoto.angepeleka kwenye halmashauli ya jimbo lake na sio ngo.
 
............
Kwanini ZITTO atukuzwe wakati AMEBUNI UTARATIBU MWINGINE WA KUTUMIA POSHO YAKE KUPITIA KDI ?????? Wenzake wanafanya wajibu wao moja kwa moja wakati Zitto anapitishia posho yake KDI. Anatuchezea mchezo wa pwagu na pwaguzi(Sitaki nataka)

Tofauti ya zitto na hao wengine ni kuwa ziito ameonyesha kuwa hzio pesa hawatakiwi kupewa wabunge. hao wengine uliowataja hawakuwai wala kuthubutu i kukataa kuongezewa posho sababu wao wanajua wakipewa posho kubwa basi ndo watazidi kuwa miungu watu.

Kuna tofauti ya mtu kusema huu mshahara ni mkubwa umezidi kwa elfu 30,000 na mwingine ambaye hajasema kama mashara anapata si mkubwa lakini akatoa 30,000 na kusaidia watu bila kusema kama mshahara ni mkubwa.

Wabunge wengi wanatamani wapate zaidi ya kile wanachoapata sasa ili wawasaidie wanchi na waonekane wao ndo wanatatua matatizo. Zitto kaenda mbali zaidi kasema hizo pesa haziitaji huruma ya mbunge kusaidia watu wake . Amsema hizo pesa sio stahili zao wabunge . Umeonona
tofauti hapo????!!!!!!



 
Nina wasiwasi na Zitto kutaka posho yake waipeleke katika taasisi ya Kigoma Development Initiative.Inaweza kuwa anakataa posho mkono wa kulia kumbe anapokea mkono wa kushoto kwa fedha hizo kumrudia yeye tena.We have to be keen on that my friends.Pia Slaa angeandika barua naye kutaka mshahara wake wa kifisadi aliolazimisha chama chake kimlipe upunguzwe, maana anahubili asioyatenda.
 
Nimesoma vizuri post zote hapa, nimepata somo moja kwamba maendeleo kwa mtz ni ndoto. Kweli Zito ni jasiri ingawa wapo wengine waliofanya kama yeye. Jamani tujenge moyo wa kusaidia wenzetu wenye shida sio kupinga kila kitu. Hii kauli yake ni sumu kwa wabunge wa ccm. Wanakigoma wanabahati kuwa na mbunge kama Zito
 
Nina wasiwasi na Zitto kutaka posho yake waipeleke katika taasisi ya Kigoma Development Initiative.Inaweza kuwa anakataa posho mkono wa kulia kumbe anapokea mkono wa kushoto kwa fedha hizo kumrudia yeye tena.We have to be keen on that my friends.Pia Slaa angeandika barua naye kutaka mshahara wake wa kifisadi aliolazimisha chama chake kimlipe upunguzwe, maana anahubili asioyatenda.
Ama kweli.....nilidhani JF ni uwanja wa thinktank kumbe kinganga!
 
zitto amefanya kitu kizuri sana ambacho watanzania wengi kwasasa tunahitaji viongozi kama zitto.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa msimamo wake kuhusu kutaka posho za vikao zifutwe nchi nzima zikiwemo za wabunge.

Chadema wamedai kuwa, posho hizo zikifutwa, jumla ya Sh bilioni 900 zitaokolewa kwa mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cha chama hicho mjini Dodoma leo , Mwenyekiti wa chama hicho na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alisema kwa sasa bajeti ya nchi imeelemewa na mzigo mzito wa posho ambazo fedha zake ni nyingi kuliko mishahara ya watumishi wote nchini.

“Tunachosema sisi ni kwamba suala la kufutwa kwa posho za vikao si la Zitto (Naibu Katibu Mkuu Kabwe Zitto) bali ni msimamo wa chama chetu, na hatuzungumzii posho za wabunge pekee, la hasha tunataka posho za vikao nchi nzima zifutwe ili kunusuru matumizi mabaya ya fedha za Serikali,” alisema Mbowe.

Amesema, wanapinga suala la watumishi kulipwa posho kwa sababu vikao vinavyofanywa ni sehemu ya kazi ya watumishi hao hivyo hawapaswi kulipwa tena posho kwa kazi waliyoajiriwa lakini kwa sasa suala hilo limekua nchi nzima na kuwa kama ugonjwa.

“Hata sisi wabunge tunalipwa mishahara, lakini tukija tena hapa kwenye vikao vya Bunge ambako ni sehemu ya kazi yetu tunayolipiwa mishahara tunalipwa tena posho, huu ni wizi wa fedha za umma,” amesema Mbowe.

Ametoa mfano kuwa yeye mwenyewe na fedha za posho anazolipwa kuwa akiingia bungeni awe amezungumza au la hulipwa posho na iwapo ikitokea Spika wa Bunge Anne Makinda akataka kukutana na Kamati ya Uongozi ambayo ni mjumbe pia hulipwa posho ambapo pia siku hiyo ikitokea tena Kamisheni ya Bunge ikakutana hulipwa tena posho.

Aliyaita malipo hayo kama matumizi mabaya ya fedha za Serikali ambayo husababisha watumishi wengi wa umma wakimbilie zaidi kwenye vikao na semina badala ya kufanya kazi.

“Utakuta kuna kikao cha Maendeleo ambapo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, watendaji na wakuu wa idara wanakutana kujadili suala la maendeleo, kikao hicho kitajaa watendaji wote wakisubiri posho wakati hiyo ni sehemu ya kazi, Chadema tunaamini kuwa iwapo posho itatolewa hata watumishi watabaki maofisini kufanyakazi,” alisema.

Alitahadharisha kutokumuhusisha Zitto binafsi na hoja hiyo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya umma kwa kuwa ni hoja ya chama na inamuhusu kila mwanachama wa chama hicho ambapo aliongeza kuwa hoja hiyo itajadiliwa na kufafanuliwa vizuri katika bajeti ya Kambi ya Upinzani inayotarajiwa kuwasilishwa wiki ijayo.

Amesema uamuzi wa Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kuandika barua kwa Katibu wa Bunge kuomba posho zake zipelekwe kwenye mfuko wa jimbo, umetokana na tafsiri potofu zilizozushwa dhidi yake juu ya suala hilo la posho za vikao.

Amesema, iwapo suala la kulipana posho linatokana na mishahara ya watumishi kuwa midogo, alishauri mishahara hiyo iongezwe ili kuziba pengo hilo ambalo linasababisha fedha nyingi za Serikali kupotea.

Kuhusu suala la yeye (Mbowe) na wabunge wengine wa Chadema kuendelea kupokea posho za vikao vya Bunge, alisema hilo halimzuii wala kuwazuia wabunge hao wasizungumzie hoja hiyo kwa kuwa hata kama wasipochukua posho hizo haitosaidia.

“Ni sawa na sasa hivi mimi ni kiongozi wa kambi ya upinzani naendeshwa na gari aina ya V8 ambalo ni la gharama kubwa, haitosaidia kutokulitumia kwa kuwa tayari limeshanunuliwa na lipo,”

Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo hadi pale suala hilo litakapowasilishwa bungeni.

Pamoja na chama hicho, Chama cha Mapinduzi (CCM) pia jana kilikutana ambapo Katibu wa Wabunge wa chama hicho, Jenister Mhagama alisema walikuwa wakijadili masuala ya chama yanayohusiana na Bunge ambayo maazimio yake hayatolewi kwa vyombo vya habari.
 
Mheshimiwa Mbowe,

Suala si mishahara midogo kwani wanaofaidika na posho ni wakubwa ambao tayari wana mishahara mikubwa kulinganisha na KCC na marupurupu kibao.

Hii kansa inatakuwa kupatiwa tiba haraka sana.
 
Hapa kuna watu wanaogopa Zitto kafanya overtake kwa kasi ya ajabu, nina hakika kwa hili la Zitto huko chamani hakukaliki. Kuna watu wanataka alwayz kizuri kionekane kufanywa na wao, wako tayari hata kufuta kazi nzuri aliyeifanya mwingine ikiwa tu wanaona kwa kazi ile jamaa atapata sifa.

Kwa mwananchi wa kawaida asiyejua nini CDM/CCM anayewaza kesho atapata wapi chakula Zitto ni shujaa, ila kwa Mwananchi mwenye mawazo ya kesho mimi ndio nipigiwe magoti na kuitwa "Mheshimiwa" Zitto ni threat.

Na Chadema damu (I mean Chadema Chagga) hii ni threat kwao, dogo kafanya timing.
 
Ni kweli muheshimiwa Mbowe unachongea,wakubwa wanachukua posho wakati wakati WAALIMU wanakufa njaa na wakulima na watu wa chini
 
kamatieni hapo hapo walazimishwe ccm wasipate posho ndizo zinawapeleka bungeni. Watakimbia bungeni ccm maana kutaabika kwa chadema ni kawaida ni walalahoi waliozoea shida so posho ikiwezekana wazikatae. Hiyo ndilo goli zito kwa ccm
 
Zitto Congrats,

I must say that certainly, leadership is not an intangible: it's the ability to convince and inspire people to follow.

To me you are the pioneer of modern political pluralism; standard-bearer for social democracy, bulwark against oppression, a political agent of change who always acted with good authority, even if it was bound to bring you into conflict with others on the political map, A role model for those who want to be mentally young; forever sharp and hopeful.

A practical politician who still inspires the nation to believe in justice and not thuggrey. A true leader wants nothing more than to make people independent, as leaders in their own rights. Instead of trying to inebriate us with your rhetoric, a true leader reflects our own light back to us. A leader provides a new direction, inspiring us to abandon our old ways of doing things. When we are imbibed with our self-interests - be they infinitesimal or magnitude - a leader sends out a wake-up call, alerting us to seek the true priorities in life.

You remain one of the few Tanzanian politicians to find courage to step away from mindless inherited Obsurd loyalty when you thinks the principles you believe in are being betrayed. Let the others follow the suit
 
yeye mbona huko bungeni hakusema? aache kutufanya mapofu na kutaka kutuwini kisiasa kirahisi namna hiyo
Mkuu, umemfuatilia kweli? Hata bajeti ya upinzani mbona ina mapendekezo hayo? Sioni kama ni kutaka kujitia umaarufu. Haya tutakuja kuona faida yake hapo baadaye!
 
Nadhani kuna vitu viwili ambavyo ni lazima tuvitenganishe:

a. Malipo ya Posho mbalimbali
Nadharia ya posho kama posho siyo jambo geni katika utumishi uwe wa umma au wa binafsi. Hivyo kuna posho za safari, posho za hali ngumu n.k n.k Miongoni mwa posho hizo ni posho za vikao (sitting allowances). Kwa kadiri nilivyoelewa hadi hivi sasa na baada ya kuipitia barua ya Zitto, posho ambazo hakubaliani nazo ni hizo za vikao. Zitto HAJAPINGA posho zote. Sidhani kama kuna kiongozi anayeweza kupinga posho zote kwa watumishi wa umma na akawa mkweli kukubali kuishi kwa kutumia mishahara tu.

Endapo posho zote zitafutwa na uamuzi ukachukuliwa wa kuboresha mishahara na kila mtu akajua kuwa analipwa mshahara tu, UFUJAJI mwingine ambao wa fedha za umma hauwezi kutokea. Sitaki kuamini kuwa posho za vikao ndio zinatumika vibaya zaidi kuliko posho zingine. Japo wazo la kukataa posho za vikao ni zuri na limekuwepo muda mrefu na hasa kukosekana kwa mantiki zake kama Zitto anavyosema tukikubali hoja hiyo ilivyo (at face value) ni rahisi kukubali hoja nyingine dhidi ya posho nyingine.

- Posho za Hali ngumu (hardship allowances) - kila kazi ina ugumu wake iwe ni kutokana na essence ya kazi yenyewe au mazingira yake; kama hili ni kweli na mtu anaingia katika kazi ambayo ina ugumu kwanini alipwe posho ya ugumu wakati toka mwanzo alijua kuwa ni sehemu ya kazi?

- Posho ya kusafiri - kama serikali inamlipa mtu gharama ya kusafiri, kukodi chumba na matumizi kwanini imlipe tena posho zaidi ya gharama ambazo serikali inaingia? Kwa wale ambao tumefanya kazi kwenye taasisi mbalimbali kuna kitu hicho cha expense reports ambapo kutokana na nafasi yake ana kiwango cha juu anachoweza kutumia na kiasi chochote juu yake lazima kipitishwe na bosi wake na huyo bosi naye anakiwango cha kupitisha juu yake lazima iwe reviewed na watu walio juu na kuna masharti mazito sana ya kuhalalisha matumizi juu ya bajeti. Kama mtu analipwa mshahara kwa mwezi mzima na anasafiri kikazi (kusafiri ni sehemu ya kazi yake) kwanini alipwe posho hiyo?

- Posho ya kujikumu (living allowance) - posho hii hutolewa wakati mwingine kutegemeana na mtu yuko wapi. Nasimuliwa kwamba mbunge awapo dar kikazi na anapokuwa Dodoma analipwa posho tofauti ya kujikimu kwa siku. Kama mtu huyu analipwa mshahara na tayari serikali inamlipia gharama ya gari na mafuta kwanini apewe na posho ya kujikimu tena? Mshahara si ndio unatarajiwa kumfanya mtu aishi sasa kwanini anapewa pesa nyingine ya kujikimu nje ya mshahara wake?

Binafsi ningependa posho zote zifutwe na utaratibu wa reimbursement tu utumike na kwa mtindo wa checks and balances.


Hilo ni jambo la kwanza.

b. Kuelekeza pesa ziende wapi
Hili la pili nina tatizo ambalo wengine tayari wameshaligusia; kuelekeza pesa zilizokataliwa kwa taasisi ambayo yeye mbunge ameamua ipewe. Kwa juu jambo hili ni zuri lakini lina hatari yake. Hivi Mbunge akiamua kwamba posho yake fulani (mojawapo kati ya posho nyingi) asipewe bali ipewe shule fulani, mtu fulani, taasisi fulani n.k tunaweza kusema kuna tatizo? Sasa kama taasisi ina "noble cause" wengi hawawezi kuona lakini nani anaamua 'noble cause' ni nini? Kama mtu akiamua posho yake hiyo fulani apewe mtu wa pembeni kwa sababu yoyote ile nani atakataa? Kimsingi, ipo haja ya kufahamu kama kuna mipaka ya kisheria au utaratibu unaoongoza wale wanaokataa posho zao au wanaoamua posho ziende kwingine - nini mipaka ya maelekezo haya?

Kwa vile hili linatokana na Zitto kutaka kuonesha mfano wa kutozitumia posho hizi kwa manufaa binafsi (na hapa najumlisha manuffaa ya taasisi yoyote au mtu yeyote anayehusiana na Mbunge - for an obvious conflict of interests) njia pekee ya kuwa mfano mzuri ni kuagiza Bunge lifungue akaunti maalum (escrow account) ambapo wabunge wasiotaka fedha za posho zipelekwe fedha hizo hadi itakapoamuliwa zifanywe nini (zinaweza kurudishwa kwenye akaunti za taifa au kuingizwa katika Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo lake).

Wazo ni zuri kama wengi tunavyoliona lakini nadhani lina matatizo katika maeneo yote mawili.
 
ccm wamekataa kufuta posho, mara wakiona jambo hilo litawanufaisha chadema kisiasa, wataanza nao kusema posho zifutwe na wao ndo watasema wameasisi wazo hilo, ccm mapunga kweli wenyewe ni kufuata mkumbo tu. katiba walikataa kufanyiwa marekebisho walipoona cdm wamelishikia bango na wananchi wanawaunga mkono tayari wakasema ni hoja yao.
 
Zitto Congrats,

I must say that certainly, leadership is not an intangible: it’s the ability to convince and inspire people to follow.

To me you are the pioneer of modern political pluralism; standard-bearer for social democracy, bulwark against oppression, a political agent of change who always acted with good authority, even if it was bound to bring you into conflict with others on the political map, A role model for those who want to be mentally young; forever sharp and hopeful.

A practical politician who still inspires the nation to believe in justice and not thuggrey. A true leader wants nothing more than to make people independent, as leaders in their own rights. Instead of trying to inebriate us with your rhetoric, a true leader reflects our own light back to us. A leader provides a new direction, inspiring us to abandon our old ways of doing things. When we are imbibed with our self-interests - be they infinitesimal or magnitude - a leader sends out a wake-up call, alerting us to seek the true priorities in life.

You remain one of the few Tanzanian politicians to find courage to step away from mindless inherited Obsurd loyalty when you thinks the principles you believe in are being betrayed. Let the others follow the suit

Kumbe ndiyo maana mlikua mnaunda mtandao wenu ndani ya chama Unaandika kwa maneno mazuri ili kuwaaminisha watanzania ninyi ni watu wema kwanza,una tuhuma za kupanga kwenda Kenya kupanga mipango ya kulipa kisasi kwa Bonny Onyoni kwenye jimbo lake.Njoo hapa ujisafishe,huko Chadema mmejaa mafioso watupu mnatuharibia nchi.Mkafie mbali,wachawi wakubwa
 
1. Namkumbusha Zitto Kwamba NGO zinalipa kodi kuanzia this financial year... so peleka huko uongeze mfuko wa Mkulo.2. Nadhani halmashauri ya Jimbo lako inaongozwa na CDM sasa unaona je upeleke hiyo hela kwenye halmashauri isimamiwe vizuri na madiwani wako kuleta maendeloe jimboni mwako.3. Of course huo utani wa kutumia bunge la jamhuri kufanya kazi za money transfer achana nao... hiyo fanya mwenyewe mkuu... Hapa mbinu zako zimekwama .. at least you will learn kwamba watanzania sio mambumbu kiasi hicho! so nice try.
Wapiga kelele kama ninyi hamuwezi kukosa kujitokeza. Personally nam-support zito na nia yake njema ya kuwajali watu wengine, si hawa mafisi wa CCM waliojaa tamaa hadi ulimu unaning'inia nje.Na wataendelea kujitokeza sana kwenye vyombo vya habari kumpinga zitto maana wao kilichowapeleka bungeni ilikuwa ni posho pamoja na benefits zingine za kibunge. Ndo maana utawaona wanafanya kazi kama wako usingizini, wana support kila kitu pasipokujua consequences zake. Shame on you CCM Mp's
 
Maandishi yatusaidia sana kutunza kumbukumbu.Haya mapambano ya Zitto kupinga hii dhuluma,unyonyaji na wizi tunaonyeshwa yameanza tangu 2007 akiwa hana hata Miaka miwili bungeni nikwamba hapa alikuwa na Mwaka mmoja tu,Kuna Watu wengine hata Wabunge wenzake wanaona Kwamba Zitto ni Mnafiki hasa wale Wabunge wapya simply b'coz Zitto alishafaidika na hizi Ela katika Bunge lililopita ila kutokana na hii thread inatudhiirishia wazi kwamba Zitto anasimamia anacho kiamini na c Mnafiki hata kidogo mwanzoni alitumia aproach ya maneno na sasa ivi ameamua atumie hii aproach na Impact zake tunaziona wazi.
Keep it up Zitto.
 
UAMUZI wa baadhi ya wabunge kutangaza kuacha kupokea posho za vikao vya Bunge umezidi kuwagawa, huku wale wa CHADEMA wakimgeuka Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Wabunge wanne wa NCCR-Mageuzi nao wametangaza kuacha kupokea posho hizo, wakisema zipelekwe kwenye fungu la 74 la fedha za maendeleo, ambalo ni maalumu kwa ajili ya mkoa wa Kigoma. Wana-NCCR hao wakiongozwa na David Kafulila (Kigoma Kusini), wameshauri posho wanazolipwa wabunge na watumishi wengine wa serikali, zikatwe kodi ili kuchangia pato la taifa.

Wakizungumza na Uhuru kwa masharti ya kutotajwa majina gazetini ili kuepusha mgogoro, baadhi ya wabunge wa CHADEMA wamedai hakuna makubaliano yaliyofikiwa kutaka wabunge wa chama hicho kuzikataa posho hizo.

Kwa mujibu wa wabunge hao, kilichoelezwa na Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA kuhusu kauli ya Zitto Kabwe, si azimio lililofikiwa na chama kwa ajili ya utekelezaji
. Wabunge hao wa CHADEMA walisema wanachofahamu ni kuwa, hakuna mbunge wa chama hicho aliyeshinikizwa kutopokea posho hizo ambazo ziko kisheria.

"Hapa ieleweke kuwa tumejadili suala hilo, kama unavyojua mawazo ya wengi, wapo waliokubali na waliokataa. Hakuna muafaka uliofikiwa kuwa tukatae posho, bali kama mbunge mmoja mmoja akitaka na afanye hivyo, ndiyo maana Zitto katoa uamuzi binafsi," alisema mbunge huyo.

Alisema iwapo ungekuwa uamuzi wa pamoja, kungekuwa na utaratibu wa namna fedha hizo zitakavyotumika, lakini kwa kuwa ni hiari ndiyo maana Zitto kazielekeza kwenye mfuko wake wa Kigoma Initiative Development (KDI). Mbunge mwingine wa viti maalumu wa chama hicho, alisema Mbowe amejichanganya alipokuwa akiunga mkono hoja ya Zitto kwa kudai hilo ni azimio la CHADEMA. Alisema haina mantiki kwa mbunge kukataa posho za vikao na baadae kuelekeza fedha hizo ziwekwe kwenye mfuko wa maendeleo ambao anaumiliki.

"Ungewekwa utaratibu maalumu kwamba fedha hizi tunaziweka kwenye mfuko wa maendeleo wa jimbo, na tuhakikishe zinatekeleza miradi iliyokusudiwa. Ukisema utazitumia wewe hapa unakuwa unadanganya watu, kwani usipotekeleza hakuna wa kukuwajibisha," alisema.

Kafulila kwa upande wake akizungumza na waandishi wa habari jana alisema wameandaa barua ambazo leo wataziwasilisha kwa Spika wa Bunge Anne Makinda na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo.

Alisema wanataka fedha hizo zipelekwe kwenye fungu linalohusu mkoa wa Kigoma ili kuharakisha miradi ya maendeleo. Wabunge wote wa chama hicho wanatoka mkoa huo.

"Lazima ieleweke kuwa mbunge anapata malipo ya aina tatu, moja ni mshahara wa mwisho wa mwezi, mbili ni pesa ya kujikimu kwa siku akiwa nje ya jimbo na tatu ni posho ya kikao wakati anahudhuria Bunge ambayo ni sh. 70,000 kwa siku," alisema.

Kafulila alisema wanapinga kulipwa posho ya vikao vya Bunge kwa kuwa wanalipwa posho ya kijikimu, hivyo wanalipwa mbili zinazofanana.

"Mbunge yuko Dodoma anapewa posho ya kujikimu kwa kuwa yuko nje ya jimbo, lakini bado akihudhuria kikao analipwa, huu ni mwingiliano na matumizi mabaya ya fedha za umma, lazima posho ya kikao iondoke, maana huwezi kulipwa posho mara mbili," alisema.

Mbunge mwingine wa chama hicho, Felix Mkosamali (Kasulu Mjini), alisema licha ya kuandaa barua, wanajipanga kuwasilisha hoja binafsi bungeni kutaka kufutwa kwa posho za vikao ili kupunguza mzigo kwa walipa kodi wa Tanzania.

"Tutawasilisha hoja binafsi na wakikataa kuipitisha, itakuwa fursa kwa wananchi kutambua watu waliowatuma wanawaza kitu gani na wataamua cha kufanya," alisema.

Aliwashauri wabunge wengine kuitazama hoja hiyo na kuijadili kwa mtazamo tofauti ili kusaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali.

Spika Anne alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi akisema amepokea barua ya Zitto, lakini Bunge litaendelea kumpatia fedha hizo kupitia akaunti yake ya awali na ataamua kwa kuzipeleka.

"Ni kweli Zitto ameandika barua akitaka fedha zake zipelekwe KDI, lakini hatutafanya hivyo kwa kuwa Bunge halina mamlaka ya kuingilia matumizi ya fedha za mbunge. Sheria ndiyo inayosema, hatubadilishi," alisema.

Source:
Gazeti Kongwe la UHURU, Juni 13, 2011

CDM Kazi ipo!!!
 
Back
Top Bottom