Monday, 13 June 2011 07:59 newsroom
NA STEPHEN BALIGEYA, DODOMA
Wabunge wanne wa NCCR-Mageuzi nao wametangaza kuacha kupokea posho hizo, wakisema zipelekwe kwenye fungu la 74 la fedha za maendeleo, ambalo ni maalumu kwa ajili ya mkoa wa Kigoma. Wana-NCCR hao wakiongozwa na David Kafulila (Kigoma Kusini), wameshauri posho wanazolipwa wabunge na watumishi wengine wa serikali, zikatwe kodi ili kuchangia pato la taifa. Wakizungumza na Uhuru kwa masharti ya kutotajwa majina gazetini ili kuepusha mgogoro, baadhi ya wabunge wa CHADEMA wamedai hakuna makubaliano yaliyofikiwa kutaka wabunge wa chama hicho kuzikataa posho hizo. Kwa mujibu wa wabunge hao, kilichoelezwa na Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA kuhusu kauli ya Zitto Kabwe, si azimio lililofikiwa na chama kwa ajili ya utekelezaji. Wabunge hao wa CHADEMA walisema wanachofahamu ni kuwa, hakuna mbunge wa chama hicho aliyeshinikizwa kutopokea posho hizo ambazo ziko kisheria. "Hapa ieleweke kuwa tumejadili suala hilo, kama unavyojua mawazo ya wengi, wapo waliokubali na waliokataa. Hakuna muafaka uliofikiwa kuwa tukatae posho, bali kama mbunge mmoja mmoja akitaka na afanye hivyo, ndiyo maana Zitto katoa uamuzi binafsi," alisema mbunge huyo. Alisema iwapo ungekuwa uamuzi wa pamoja, kungekuwa na utaratibu wa namna fedha hizo zitakavyotumika, lakini kwa kuwa ni hiari ndiyo maana Zitto kazielekeza kwenye mfuko wake wa Kigoma Initiative Development (KDI). Mbunge mwingine wa viti maalumu wa chama hicho, alisema Mbowe amejichanganya alipokuwa akiunga mkono hoja ya Zitto kwa kudai hilo ni azimio la CHADEMA. Alisema haina mantiki kwa mbunge kukataa posho za vikao na baadae kuelekeza fedha hizo ziwekwe kwenye mfuko wa maendeleo ambao anaumiliki.
"Ungewekwa utaratibu maalumu kwamba fedha hizi tunaziweka kwenye mfuko wa maendeleo wa jimbo, na tuhakikishe zinatekeleza miradi iliyokusudiwa. Ukisema utazitumia wewe hapa unakuwa unadanganya watu, kwani usipotekeleza hakuna wa kukuwajibisha," alisema.
Kafulila kwa upande wake akizungumza na waandishi wa habari jana alisema wameandaa barua ambazo leo wataziwasilisha kwa Spika wa Bunge Anne Makinda na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo.
Alisema wanataka fedha hizo zipelekwe kwenye fungu linalohusu mkoa wa Kigoma ili kuharakisha miradi ya maendeleo. Wabunge wote wa chama hicho wanatoka mkoa huo.
"Lazima ieleweke kuwa mbunge anapata malipo ya aina tatu, moja ni mshahara wa mwisho wa mwezi, mbili ni pesa ya kujikimu kwa siku akiwa nje ya jimbo na tatu ni posho ya kikao wakati anahudhuria Bunge ambayo ni sh. 70,000 kwa siku," alisema.
Kafulila alisema wanapinga kulipwa posho ya vikao vya Bunge kwa kuwa wanalipwa posho ya kijikimu, hivyo wanalipwa mbili zinazofanana.
"Mbunge yuko Dodoma anapewa posho ya kujikimu kwa kuwa yuko nje ya jimbo, lakini bado akihudhuria kikao analipwa, huu ni mwingiliano na matumizi mabaya ya fedha za umma, lazima posho ya kikao iondoke, maana huwezi kulipwa posho mara mbili," alisema.
Mbunge mwingine wa chama hicho, Felix Mkosamali (Kasulu Mjini), alisema licha ya kuandaa barua, wanajipanga kuwasilisha hoja binafsi bungeni kutaka kufutwa kwa posho za vikao ili kupunguza mzigo kwa walipa kodi wa Tanzania.
"Tutawasilisha hoja binafsi na wakikataa kuipitisha, itakuwa fursa kwa wananchi kutambua watu waliowatuma wanawaza kitu gani na wataamua cha kufanya," alisema.
Aliwashauri wabunge wengine kuitazama hoja hiyo na kuijadili kwa mtazamo tofauti ili kusaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali.
Spika Anne alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi akisema amepokea barua ya Zitto, lakini Bunge litaendelea kumpatia fedha hizo kupitia akaunti yake ya awali na ataamua kwa kuzipeleka.
"Ni kweli Zitto ameandika barua akitaka fedha zake zipelekwe KDI, lakini hatutafanya hivyo kwa kuwa Bunge halina mamlaka ya kuingilia matumizi ya fedha za mbunge. Sheria ndiyo inayosema, hatubadilishi," alisema.
Monday, 13 June 2011 07:59 newsroom
NA STEPHEN BALIGEYA, DODOMA
U AMUZI wa baadhi ya wabunge kutangaza kuacha kupokea posho za vikao vya Bunge umezidi kuwagawa, huku wale wa CHADEMA wakimgeuka Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Mkuu uchonganishi utaacha lini? CCM KAZI IPO!UAMUZI wa baadhi ya wabunge kutangaza kuacha kupokea posho za vikao vya Bunge umezidi kuwagawa, huku wale wa CHADEMA wakimgeuka Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.Wabunge wanne wa NCCR-Mageuzi nao wametangaza kuacha kupokea posho hizo, wakisema zipelekwe kwenye fungu la 74 la fedha za maendeleo, ambalo ni maalumu kwa ajili ya mkoa wa Kigoma. Wana-NCCR hao wakiongozwa na David Kafulila (Kigoma Kusini), wameshauri posho wanazolipwa wabunge na watumishi wengine wa serikali, zikatwe kodi ili kuchangia pato la taifa. Wakizungumza na Uhuru kwa masharti ya kutotajwa majina gazetini ili kuepusha mgogoro, baadhi ya wabunge wa CHADEMA wamedai hakuna makubaliano yaliyofikiwa kutaka wabunge wa chama hicho kuzikataa posho hizo. Kwa mujibu wa wabunge hao, kilichoelezwa na Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA kuhusu kauli ya Zitto Kabwe, si azimio lililofikiwa na chama kwa ajili ya utekelezaji. Wabunge hao wa CHADEMA walisema wanachofahamu ni kuwa, hakuna mbunge wa chama hicho aliyeshinikizwa kutopokea posho hizo ambazo ziko kisheria. Hapa ieleweke kuwa tumejadili suala hilo, kama unavyojua mawazo ya wengi, wapo waliokubali na waliokataa. Hakuna muafaka uliofikiwa kuwa tukatae posho, bali kama mbunge mmoja mmoja akitaka na afanye hivyo, ndiyo maana Zitto katoa uamuzi binafsi, alisema mbunge huyo. Alisema iwapo ungekuwa uamuzi wa pamoja, kungekuwa na utaratibu wa namna fedha hizo zitakavyotumika, lakini kwa kuwa ni hiari ndiyo maana Zitto kazielekeza kwenye mfuko wake wa Kigoma Initiative Development (KDI). Mbunge mwingine wa viti maalumu wa chama hicho, alisema Mbowe amejichanganya alipokuwa akiunga mkono hoja ya Zitto kwa kudai hilo ni azimio la CHADEMA. Alisema haina mantiki kwa mbunge kukataa posho za vikao na baadae kuelekeza fedha hizo ziwekwe kwenye mfuko wa maendeleo ambao anaumiliki.Ungewekwa utaratibu maalumu kwamba fedha hizi tunaziweka kwenye mfuko wa maendeleo wa jimbo, na tuhakikishe zinatekeleza miradi iliyokusudiwa. Ukisema utazitumia wewe hapa unakuwa unadanganya watu, kwani usipotekeleza hakuna wa kukuwajibisha, alisema.Kafulila kwa upande wake akizungumza na waandishi wa habari jana alisema wameandaa barua ambazo leo wataziwasilisha kwa Spika wa Bunge Anne Makinda na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo.Alisema wanataka fedha hizo zipelekwe kwenye fungu linalohusu mkoa wa Kigoma ili kuharakisha miradi ya maendeleo. Wabunge wote wa chama hicho wanatoka mkoa huo.Lazima ieleweke kuwa mbunge anapata malipo ya aina tatu, moja ni mshahara wa mwisho wa mwezi, mbili ni pesa ya kujikimu kwa siku akiwa nje ya jimbo na tatu ni posho ya kikao wakati anahudhuria Bunge ambayo ni sh. 70,000 kwa siku, alisema.Kafulila alisema wanapinga kulipwa posho ya vikao vya Bunge kwa kuwa wanalipwa posho ya kijikimu, hivyo wanalipwa mbili zinazofanana.Mbunge yuko Dodoma anapewa posho ya kujikimu kwa kuwa yuko nje ya jimbo, lakini bado akihudhuria kikao analipwa, huu ni mwingiliano na matumizi mabaya ya fedha za umma, lazima posho ya kikao iondoke, maana huwezi kulipwa posho mara mbili, alisema.Mbunge mwingine wa chama hicho, Felix Mkosamali (Kasulu Mjini), alisema licha ya kuandaa barua, wanajipanga kuwasilisha hoja binafsi bungeni kutaka kufutwa kwa posho za vikao ili kupunguza mzigo kwa walipa kodi wa Tanzania.Tutawasilisha hoja binafsi na wakikataa kuipitisha, itakuwa fursa kwa wananchi kutambua watu waliowatuma wanawaza kitu gani na wataamua cha kufanya, alisema.Aliwashauri wabunge wengine kuitazama hoja hiyo na kuijadili kwa mtazamo tofauti ili kusaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali.Spika Anne alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi akisema amepokea barua ya Zitto, lakini Bunge litaendelea kumpatia fedha hizo kupitia akaunti yake ya awali na ataamua kwa kuzipeleka.Ni kweli Zitto ameandika barua akitaka fedha zake zipelekwe KDI, lakini hatutafanya hivyo kwa kuwa Bunge halina mamlaka ya kuingilia matumizi ya fedha za mbunge. Sheria ndiyo inayosema, hatubadilishi, alisema.Source: Gazeti Kongwe la UHURU, Juni 13, 2011CDM Kazi ipo!!!
nikisoma hapo kwenye red tu nimeshamaliza kila kitu. asante mkuu kwa taarifa.