Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,487
- 2,344
Kutokana na kauli ya Makonda inaonekana wazi ilililenga Bunge, kuwa limechangisha fedha kwa jina la Timu ya Taifa ila hazijafika.
Binafsi nilijiuliza sana, haya mahaba ya wabunge kwa Taifa Stars yametoka wapi, yameanza lini? Kumbe kulikuwa na posho.
______________
HARUFU YA UFISADI
Kama pesa hazikufika ina maana walizitumia wabunge. Spika anasema KWA WABUNGE 65 WALIPUNGUKIWA 200M, tukigawanya ina maana kila mbunge alipungukiwa Tsh. 3,100,000. Nauli ya kwenda Cairo na kurudi haizidi Tsh. 1,700,000 kwa kichwa, swali ni kuwa walihitaji zaidi ya Tsh. 3,100,000 kwa kichwa za kazi gani?
Labda Makonda arekebishe kauli kuwa hiyo taasisi ilipeleka fedha nusu hapo tutaelewa kidogo
Heche kaongeza utata zaidi
Heche anasema wabunge wote walioenda walitoa hela zao wenyewe. anasema kama spika alichangisha michango yeye Hana hizo taarifa.
Alikua akihojiwa efm sports hq
Kama Spika alichangisha pesa ambazo wabunge hawajapewa kwa mujibu wa heche wala Timu haijapewa kwa mujibu wa Makonda, je fedha hizi zimetumika kufanya nini, ziko wapi?
MH. SPIKA MAJIBU TAFADHALI