Barua ya wazi kwa Waziri wa Elimu na Rais wa Chama cha Skauti Tanzania: Mgogoro wa Kikatiba unaoendelea kwenye chama

jointscout5

New Member
Mar 18, 2016
1
0
BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA AMBAYE NI RAIS WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA MANTIKI YA MGOGORO WA KIKATIBA SKAUTI

Salaam kwako Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, rais wa chama cha Skauti Tanzania.

Napenda kuchukua nafasi hii kuelezea yangu machache kuhusu fukuto linaloendelea hivi sasa katika Chama cha Skauti Tanzania.

Kinachoendelea hivi sasa ni mogogoro
wa Kikatiba ulioanzishwa na viongozi wenyewe, ulianza tarehe 13/01/2022 kusikika minong’ono kupitia kurasa za mitandao ya kijamii hasa mtandao wa “WhatsApp” wa simu za kiganjani katika makundi mbalimbali ya Skauti, minong’ono hiyo ilihusu Skauti Mkuu kutenguwa nafasi ya Kamishna Mkuu, ukimya wa mfukuto huo ulizimwa
na Kamishna Mkuu tarehe 14/01/2022 majira ya usiku alipojitokeza kwa umma na
kuelezea kuwa ni jaribio la kutaka kumtengua nafasi yake lakini limeshindikana kwa kufuata Katiba ya Chama cha Skauti ya mwaka 2017, Ibara ya 10.6.1(v) ‘Skauti Mkuu kwa mapendekezo ya Bodi ya Taifa anaweza kutengua uteuzi wa Kamishna Mkuu’

(A) Hoja Kupinga: Kamishna Mkuu alikataa utenguzi huo kwa madai ya kwamba;

i. Kutengua nafasi ya Kamishna Mkuu ni mchakato ambapo Skauti Mkuu lazima apate mapendekezo kutoka kwa Bodi ya Taifa (Baada ya mapendekezo hayo inabaki kuwa hiyari yake kukubali ama kuyakataa)
sasa kwa hili Skauti Mkuu hakupata mapendekezo yoyote kutoka katika Bodi.

Kwamba; Skauti Mkuu hakushirikisha Bodi impe hayo mapendekezo ibaki hekma, busara na weledi wake ayakubali au ayakatae hayo mapendekezo na kubwa Zaidi bodi haipo kwa maana imeisha muda
wake;

ii. Bodi ya Taifa imeisha muda wake (Katiba Ibara ya 6.13(i) ‘Each
member elected by the general Assembly is elected for a period of three (3) years and can be re-elected once. After two continuous terms, a retiring member shall only be eligible for re-election after a lapse of three (3) years. However, two third of its members shall be retained at
every term of election’ (Katiba ya tafsiri ya Kiswahili ina mapungufu ya kifungu hiki imenilazimu kwenda katika toleo mama na kunukuu kifungu kama kilivyo)

Kwamba; Bodi iliundwa kwa kuchaguliwa na Mkutano Mkuu uliofanyika 23-24 Februari 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa, katika Viwanja vya Bunge Dodoma, hadi kufikia Februari 2021 muda wake wa miaka mitatu ulikuwa umeisha.

(B) Hoja Utii: (Kanuni ya Skauti ya Saba (7) “Skauti ni mtiifu”) Wapo wanaosema kuwa Kamishna Mkuu angetii utenguzi wa aliye mteua na kumtaka afuate taratibu nyingine ikiwa kukata rufaa kwa rais wa Chama (Waziri mwenye dhamana).

Kwamba; Aidha Kamishna Mkuu aliitengua kanuni hiyo ya saba (7) kwa kutumia
Kanuni ya kumi (10) “Skauti ni safi katika mawazo, maneno na matendo”. Ambapo kimsingi Skauti Mkuu angeweza kuitumia na kuepusha mgogoro huu. Katiba inampa mamlaka Skauti Mkuu kumteua Kamishna Mkuu, Ibara ya 10.4.1(v) “Kumteua Kamishna Mkuu akishauriana na Bodi ya Taifa na Kamati Tendaji ya Taifa” hapa ina dhihirika wazi kuwa kumteua Kamishna Mkuu ni mchakato na kumtenguaalikadharika vivyo hivyo ni mchakato.

(C) Sababu kwanini ni mgogoro wa Kikatiba. Tuchukulie KWA MFANO Kamishna Mkuu amekubali utenguzi wa nafasi yake na Skauti Mkuu amemkaimisha Naibu Kamishna Mkuu nafasi ya Kamishna Mkuu, ifahamike kuwa Kamati Tendaji inakaa madarakani kwa muda wa miaka mitatu (3),

Kipindi cha kutumikia Kamati Tendaji, rejea katiba Ibara ya 7.3(i) na P.O.R
kifungu cha 51.3 “Each member shall be appointed for a term of three years and
as per provisions stated in the Adult in Scouting Policy.”

Hoja: Kwa kuwa Kamati Tendaji hudumu kwa miaka mitatu (3), wajumbe wa Kamati
Tendaji hii waliteuliwa Januari 2019 hadi kufikia Januari 2022 muda wao umefikia ukomo wa miaka mitatu, lakini kwa kuwa Naibu Kamishna Mkuu aliteuliwa na kuapishwa Desemba 2018 hadi kufikia Desemba 2021 muda wake ulikwisha malizika, hivyo basi hakuna uharali wa yeye kuweza kushikilia nafasi ya kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu.

Kwamba; Bodi muda wake umeisha na Kamati Tendaji muda wake umeisha,
isipokuwa Makamishna Wakuu Wasaidizi watatu (3) tu muda wao bado
upo kikatiba, ambao ni:-

1. Kamishna Mkuu Msaidizi wa Hati na Usajili (nafasi yake iliuishwa mwezi Mei 2021 kutoka nafasi ya Maafa na Ukoaji kwenda Hati na Usajili)

2. Kamishna Mkuu Msaidizi wa Maendeleo ya Jamii na Vyuo (aliteuliwa mwezi Agosti 2021 kutoka Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana)

3. Kamishna Mkuu Msaidizi Maafa na Uokoaji (aliteuliwa mwezi Novemba 2021 kutoka Kamishna wa Wilaya ya Ubungo)
Kwa hali ilivyo sasa Skauti Mkuu hana mamlaka yoyote kikatiba kumteua Kamishna Mkuu miongoni mwa Makamishna Wakuu Wasaidizi waliobakia kwa kuwa uteuzi wa Kamishna Mkuu ni mchakato unaoshirikisha Bodi ya Taifa na Kamati Tendaji ambapo Bodi haipo imemaliza muda wake na Kamati Tendaji haina akidi (Katiba Ibara 7.8) inayokubalika kikatiba.
 
Back
Top Bottom