KERO Barua ya wazi kwa Shabiby bus

KERO Barua ya wazi kwa Shabiby bus

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Bila sisi Watanzania kubadilika na kuchukua hatua hakuna ambacho tutafanya zaidi ya maumivu moyoni!

Kama unayo risiti na mzigo wako umepotea,Tafuta Mwanasheria waburuze mahakamani,hiyo risiti ndiyo ushahidi wenyewe!

Kama hiyo Barua ilikuwa muhimu maana yake wamekukwamisha na kukupotezea muda,Hapo itabidi wakulipe fidia ya kukupotezea muda!,Wapeleke mahakamani hao Wapumbavu Ili angalau wanaweza kuacha uzembe,Haya mambo ya Kuwa kila Jambo tunalalamika sidhani kama yatatusaidia!
Mahakama hizi hizi ambazo wanatoa Maamuzi ya kesi Kwa kupewa maelekezo na siyo Kwa misingi ya Kisheria?
 
Bila sisi Watanzania kubadilika na kuchukua hatua hakuna ambacho tutafanya zaidi ya maumivu moyoni!

Kama unayo risiti na mzigo wako umepotea,Tafuta Mwanasheria waburuze mahakamani,hiyo risiti ndiyo ushahidi wenyewe!

Kama hiyo Barua ilikuwa muhimu maana yake wamekukwamisha na kukupotezea muda,Hapo itabidi wakulipe fidia ya kukupotezea muda!,Wapeleke mahakamani hao Wapumbavu Ili angalau wanaweza kuacha uzembe,Haya mambo ya Kuwa kila Jambo tunalalamika sidhani kama yatatusaidia!
Sasa mahakamani ni kupeleka kesi ya ngedere kwa nyani, hakuna haki.
 
Wabongo hawajui kabisa customer service.
Hizo niishara za management dhaifu, wafanyakazi hujibu wateja wanavyojisikia wao, baadaye kampuni hupoteza wateja na kufa.

Popote ambapo ni sehemu ya huduma ukiona kuna ujinga ujinga wa namna hiyo, basi uongozi ni dhaifu.
 
Esther hata kwa mawe siitaki, kama mara 3 hivi Esther kwenda Rombo reporting time saa 9 alfajiri bus inaondoka saa 1:15 asubuhi, chaaa
Ndio tabia yao
Esther hata kwa mawe siitaki, kama mara 3 hivi Esther kwenda Rombo reporting time saa 9 alfajiri bus inaondoka saa 1:15 asubuhi, chaaa
Ndio walivyo hao kwa ruti zao nyingi. Ubabaishaji kwenye suala la kuzingatia muda pamoja na lugha tata za makondakta. Inahuzunisha sana.
 
Nilisikia Abood ndio kimeo kumbe na Shabiby pia... basi mitihani hii.. So Kampuni bora ya waaminifu ni Tahmeed pekee
 
Kwenye suala la usafirishaji wabongo bado hatuwezi. Haya makampuni yote ya mabasi ni upumbavu mtupu wanafanya kwenye kusafirisha vifurushi na bahasha. Kuna basi walinipotezea EFD Receipt ikabidi tukubaliane nisafirishe mizigo yangu bila kunichaji mpaka nifidie gharama za kuprint receipt nyingine. Walinielewa kwa sababu nilikuwa nasafirisha mizigo karibu kila siku. Angekuwa mteja mwingine wangekataa. SCANDNAVIA itakumbukwa milele.
 
utawaona wabaya Shabiby ila shida ni wahudumu na uwezo wao wa kutatua shida umeishia hapo.
Shabìby ndiye mmiliki, hawezi kujitenga na lawama.
Kama ana watumishi wasio na nidhamu maana yake hata yeye hana nidhamu.
 
wadada wengi kwenye haya makampuni ya mabasi wana nyodo, dharau na jeuri.

Ni chanzo cha kupunguza thamani ya uaminifu kwa wateja wao
 
Hizo niishara za management dhaifu, wafanyakazi hujibu wateja wanavyojisikia wao, baadaye kampuni hupoteza wateja na kufa.

Popote ambapo ni sehemu ya huduma ukiona kuna ujinga ujinga wa namna hiyo, basi uongozi ni dhaifu.

Bongo nzima ni dhaifu. Hii kila mtu anajua. Huwezi compare service za bongo na nchi zingine.

Hapo bado hujaongelea taasisi za serikali. USA unaweza tuma barua hata WH na ukajibiwa ila bongo namba za simu na barua pepe za taasisi ni kama mapambo tu hazijibiwi hata siku moja. Nchi ya kipumbavu sana hii.
 
Huduma katika haya ma bus ya mikoani, kampuni nyingi bado hazijaweza kutoa kiwango kinachostahili, na kinachowafelisha wanachukua watu ambao hawana weledi kutokana na malipo madogo, matokeo yake ndo hayo. Nlishawai safirisha Taa kutoka Dsm to Mbeya na kampuni moja ya bus, kufika mbeya taa 9 zimevunjika kumbe kwenye kupakia mizigo waliweka mizigo mingine juu yake , na nliwaambia pale ofsini kwao wakati nalipia ule mzigo kuwa zile ni taa na kwenye box kwa nje nikaandika KIOO kama taadhari ili katika kupanga mizigo wapange kwa uangalifu lakini bado wakafanya huo uzembe. Nlirudi ofisini kudai fidia majibu yao ndo yalinichosha. Walisema mzigo wenye vitu vya kuvunjika wanasafirisha kwa dhamana ya mteja hivyo hawahusiki na uharibifu wowote

Note: Taa moja ilikua inagharimu 70k × 9 = 630k ikawa imepotea kirahisi hivo
Hili nimeshindwa kulivumilia roho inaniwaka moto .
Ndugu na ushahidi unao mpaka leo ?
Baada ya majibu hayo ulichukua hatua gani ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom