DOKEZO Barua ya wazi Kwa Mkuu wa Trafiki

DOKEZO Barua ya wazi Kwa Mkuu wa Trafiki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2015
Posts
3,574
Reaction score
4,856
Barua ya wazi kwa mkuu wa Traffic Police

Kuna zoezi limefanyika Jumamosi ya tarehe 14.02.2026 - Jangwani Road na ni zoezi la dhuluma na kuibia wananchi ambao tayari wanaumizwa na mifumo kandamizi.

Afisa waliweka kamera na kusimamisha wenye magari mengi kwa kisingizio wanadaiwa fine. Mbaya zaidi wanakataa kurudisha leseni hadi ulipe fine ya kubambikiziwa.

Kwa mfano niliandikiwa fine kosa ambalo gari hiyo haikuwa barabarani siku hiyo na kuhusiana na leseni isiyofahamika kwangu wala familia yangu (kumbuka watoto ni wadogo chini ya umri) na kuhusiana na hali ya gari yaani car condition! Nilijaribu kumwelezea traffic lakini hataki kusikiliza logic.

Ajabu kuna wenye magari kama 6 walilalamika issue hiyo hiyo. Kuingia TMS ni wazi aliyefanya kosa anaonekana inaunganisha na hiyo leseni. Walichokifanya polisi waligeuza herufi moja na kutubambikizia fine ambayo ilijumuishwa na penalty kuwa zaidi ya 50k.

Kumbuka fine eti ni ya Januari mwaka huu tarehe ambayo haijakamilika siku 30. Plate CJY inageuzwa kuwa CUY kumwibia mwananchi wa kawaida. Kibaya hela hiyo nilikuwa naenda kumchukulia mtoto dawa zake.

Nimerudi nyumbani bila kutimiza jukumu hilo. Hii imeniuma sana. Je, kukosa uadilifu huu nani anausimamia au wanapigiwa makofi na kupewa hongera kwa makusanyo batili? Nani atanirudishia hela yangu??

Tafakari na kutenda haki kunahitajika afande.
 
Ushauri wangu ukishikwa fine kwanza angalia validity ya control number ya fine kupitia mfumo wa GePg. Mimi kwangu ilikuwa haijulikani wala haiexist.

Tambua namba yako ya leseni ya udereva kama inaakisi ile iliyopigwa fine kwa kutumia mfumo wa TMS ukiona leseni nyingine. Mimi nilipoingiza namba ya aliyepigwa fine nikakuta muda wakati mahali vinafanana na vya kwangu ili hali gari haitembeagi mchana ni asubuhi kazini inatoka usiku kurudi. Na niligundua herufi ya kati imepishana na yangu ya platenumber. Cha kustaajabisha dereve huyo ana fine karibu 7 zote hajawahi kulipa.

Zipo taarifa zisizo rasmi kwamba mfumo wa camera kutambua fine hapo katikati ulikuwa hauko vizuri kikazi.
 
Back
Top Bottom