Barua ya wazi kwa Mzee Jakaya Mrisho Kikwete: Hivi wakati unaweka ndani Masheikh wetu ulikuwa unafikiria nini?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,654
2,000
Mzee Jakaya!

Shikamoo mzee, nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Naomba nikupe taarifa tu kuwa jela kuna Masheikh zaidi ya 150 , na wengi wao waliwekwa ndani kipindi cha utawala wako. Hivi mzee ulikuwa unafikiria nini kwa mambo haya?

Ninafahamu kuwa wewe personally siyo mtu mbaya, na nimekuwa nikiamini sana kuwa una utu sana ndani yako. Na kwa kweli umetenda mambo mengi mazuri sana kwa nchi yetu, ikiwemo miundo mbinu, kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi vyuo vikuu, masilahi ya watumishi, ajira na demokrasia na mambo mengi tu.

Lakini kuna jambo moja huwa linanitazi sana mzee wangu. nalo linahusu HAKI, Hivi wakati serikali yako inachukua uamuzi wa kuwaweka ndani waja hawa na watumishi wa "MUUMBA MBINGU NA NCHI" ulikuwa ukifikiria nini haswa?

Masheikh wa uamsho walikaa ndani kwa miaka zaidi ya saba, serikali yako ndiyo iliiyowaweka ndani kwa kesi ya Ugaidi, serikali yako ikashindwa kuthibitisha ugaidi wao mahakamani, na serikali zilizofuata nazo zikashindwa kuthibitisha ugaidi wao kwa muda wa miaka yote hiyo nane. Mwishowe DPP akafuta kesi bila kutoa sababu, yaani akasema hana nia ya kuendelea na kesi hiyo. Hivi Mzee wetu Jakaya, unafahamu vizuri kuhusu Mwenyezi Mungu anavyosema kwenye Qur'an juu ya watu wasiotenda haki katika ardhi?

Mheshimiwa Jakaya, Jana Sheikh Ponda amekwenda Magerezani kuonana na Masheikh wengine ambao walikamatwa mwaka 2013 wakati wewe ukiwa rais, na mpaka leo serikali haijathibitisha tuhuma zao za Ugaidi. Mzee wangu hivi kweli ulifanya fair kwa waja hawa wa Mwenyezi Mungu?.

Bila shaka umesomasoama masuala ya dini ya kiislamu, unajua vizuri kisa cha nabii Yusufu kuwekwa gerezani kwa kosa ambalo wala hakulifanya, Je umewahi kujiuliz Dhimma uliyo nayo mbele ya Mwenyezi Mungu kwa hili jambo la kuwaweka ndani Watumisha wa MWINGI WA REHMA bila haki?

Mzee naamini wewe ni mtu mwenye access na Rais Samia, nakuomba kwa heshima na taadhima tumia nafasi hii ya access uliyonayo kumuomba Rais Samia afute kesi na awaachie huru masheikh hawa watumishi wa MWINGI WA REHMA.

Mzee Jakaya, ulichowafanyia waja hawa wa Mwenyezi Mungu siyo sawa, Nakuomba ufanye jitihada zako kurekebisha hili suala!

Nikukumbushe tu, miongoni mwa hawa uliowaweka ndani katika utawala wako bila ushahidi, miongoni mwao wamo waliokupigania sana kisiasa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, wakati huo ulikuwa na hali mbaya sana mbele ya Dr Slaa , mzee kumbuka hilo!

Wako katika Ujenzi wa Taifa
Missile of the Nation!
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
10,062
2,000
Bwana "Kombora la Taifa" labda nikwambie tu, kuna wakati mambo ya Dola na usalama wa nchi huwa ni magumu sana kuyaletea ushabiki.

Wangekuwa ni viongozi wa CDM tungesema. JK ni CCM anakandamiza CDM, wangekuwa ni wakristo tungesema JK Muislamu anakandamiza Ukristo, wale ni masheikh wa kiislam na JK ni muislam naamini lipo jambo ambalo kuna wakati raia hatupaswi kuhoji bali kuamini tu Dola inatenda sawa kutulinda.

Wale wahuni wa mkulanga, Tanga na kule kibiti wengine informers wao na supplier + coordinators wao tulikuwa tunaishi nao mtaani kuwatarget na kuwatia mkononi ni kazi ya Dola kimyakimya.

Si ajabu leo hii ukiwekewa hadharani ya bwana mabunduki pale french embassy unaweza kustaajabu lakini inabaki kuwa taarifa za dola.

Kupatikana kwa Osama Bin laden na kuuwawa kulitokana na taarifa kutoka kwa mtoto mchunga kondoo kule tora bora wakati tena mambo yameshapoa. U-smart wa akili wa wale USA uliwafanya kutomdharau yule dogo na baadaye kuishia kumtesa guatanamo kupata proper lead.
 
Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
12,247
2,000
Nikukumbushe tu, miongoni mwa hawa uliowaweka ndani katika utawala wako bila ushahidi, miongoni mwao wamo waliokupigania sana kisiasa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, wakati huo ulikuwa na hali mbaya sana mbele ya...

Nakumbuka Mzee Mohamed Said aliwahi kueleza namna sheikh Ponda na wenzake walivyozunguka nchi hii kumpigania JK mwaka 2010........hii nchi dini na siasa zimejaa wasanii.
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,654
2,000
bwana "Kombora la Taifa" labda nikwambie tu...kuna wakati mambo ya Dola na usalama wa nchi huwa ni magumu sana kuyaletea ushabiki....
Kwa kisingizio cha ulinzi na usalama watawala wameumiza wengi bila haki. Na mara nyingi inatokana na viongozi kutafuta shortcut, hawataki kuinvest vya kutosha kwenye upelelezi, wanaamua tu kutia ndani watu bila ushahidi.

Kikwete ni muislamu, siijui level ya commitment yake kwa uislamu, lakini licha ya uislamu wake yeye pia ni mwanasiasa. Naamini yalipogongana maslahi yake ya kidini na ya kisiasa aliamua kuchagua upande wa kisiasa na madaraka. Na ushahidi huu wa kuwaweka ndani masheikh bila haki ni sehemu mojawapo tu ya abuse ya madaraka
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
50,844

Ukiwa kiongizi wa kisiasa huwezi kuwa na dini!
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,654
2,000
Jiandae kwa matusi toka kwa wagalatia,hapo Sasa watajifanya wapo pamoja na Samia kushinikiza hasiwaachie hao masheikh
Linapokuja suala kama hili wengi hapa JF huwa hawako sympathetic na Waislamu, sijui kwa nini!

Huwezi kuona hoja za Ulinzi na usalama zikiapply kwa kesi ya Mbowe, huwa tunaconclude kuwa Mbowe kaonewa. Ila kwa Masheikh huwa tunasema serikali "inalinda" nchi dhidi ya ugaidi
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
11,276
2,000
Mzee Jakaya, ulichowafanyia waja hawa wa Mwenyezi Mungu siyo sawa, Nakuomba ufanye jitihada zako kurekebisha hili suala!

Kuna mambo wengi ya kidhalimu Jakaya aliyafanya enzi ya utawala wake yakiwemo kuua watu, mfano ni jinsi alivyoamuru kuuliwa kwa mwandishi Mwangosi kule Iringa na baadae kumpandisha cheo Kiongozi wa operation ile! Watu wengi pia waliteswa kwa kusimamia HAKI akiwemo Dr. Ulimboka.

Huyu mkwere alikuwa Kiongozi dhalimu lakini mnafiki na aliwahadaa watu kwa kucheka Cheka!
 
Black belts

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
2,236
2,000
Linapokuja suala kama hili wengi hapa JF huwa hawako sympathetic na Waislamu, sijui kwa nini!

Huwezi kuona hoja za Ulinzi na usalama zikiapply kwa kesi ya Mbowe, huwa tunaconclude kuwa Mbowe kaonewa. Ila kwa Masheikh huwa tunasema serikali "inalinda" nchi dhidi ya ugaidi
Hapo akili kichwani mwako, serikali imeandaa Ushaidi dhidi ya ugaidi wa mbowe, hila mpk viongozi wa dini ya kikristo wanapinga kuwa sio kweli kasingiziwa, hila angekuwa wa upande mwingine ungesikia wanavyofurahi kuwa hajaonewa.
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
10,062
2,000
Linapokuja suala kama hili wengi hapa JF huwa hawako sympathetic na Waislamu, sijui kwa nini!

Huwezi kuona hoja za Ulinzi na usalama zikiapply kwa kesi ya Mbowe, huwa tunaconclude kuwa Mbowe kaonewa. Ila kwa Masheikh huwa tunasema serikali "inalinda" nchi dhidi ya ugaidi

Bwana "Kombora la Taifa" narudi tena kwako.

Hata kwa Mbowe, tunarudi palepale, mambo ya dola ni magumu sana na haijalishi nani yuko madarakani.... hatupaswi kushupaza shingo na kusema Mbowe sio gaidi au Mbowe gaidi. Bali tunaomtetea tupambane na data za kisheria kumtetea clearly with no doubt " wenye macho tutaona" wanaosema ni gaidi waje na clear evidence " wenye macho pia tutaona"

Kuna wakati sisi wananchi tunakuwa mashabiki sana na kujipa pande matokeo yake shida zinaanza, tusio mashabiki wa Sabaya tulishangilia tukasema serikali imetenda haki, waliomashabiki wa Sabaya wanasema ameonewa aim kumdhalilisha chuma na kuzima legacy... Hebu tuache kuwa mashabiki tuangalie mambo kiupana na kuzipa chance pande zote then tuhukumu..
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,654
2,000
Kuna mambo wengi ya kidhalimu Jakaya aliyafanya enzi ya utawala wake yakiwemo kuua watu, mfano ni jinsi alivyoamuru kuuliwa kwa mwandishi Mwangosi kule Iringa na baadae kumpandisha cheo Kiongozi wa operation ile !! Watu wengi pia waliteswa kwa kusimamia HAKI akiwemo Dr. Ulimboka.
Huyu mkwere alikuwa Kiongozi dhalimu lakini mnafiki na aliwahadaa watu kwa kucheka Cheka!!!
Hata Sheikh Ponda alikoswakoswa risasi kipindi cha Utawala wa Jakaya!
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,451
2,000
bwana "Kombora la Taifa" labda nikwambie tu...kuna wakati mambo ya Dola na usalama wa nchi huwa ni magumu sana kuyaletea ushabiki....

Wangekuwa ni viongozi wa CDM tungesema.JK ni CCM anakandamiza CDM, wangekuwa ni wakristo tungesema JK muislamu anakandamiza Ukristo....wale ni masheikh wa kiislam na JK ni muislam naamini lipo jambo ambalo kuna wakati raia hatupaswi kuhoji bali kuamini tu Dola inatenda sawa kutulinda...

Wale wahuni wa mkulanga, Tanga na kule kibiti wengine informers wao na supplier + coordinators wao tulikuwa tunaishi nao mtaani kuwatarget na kuwatia mkononi ni kazi ya Dola kimyakimya..
Si ajabu leo hii ukiwekewa hadharani ya bwana mabunduki pale french embassy unaweza kustaajabu lakini inabaki kuwa taarifa za dola.

Kupatikana kwa Osama Bin laden na kuuwawa kulitokana na taarifa kutoka kwa mtoto mchunga kondoo kule tora bora wakati tena mambo yameshapoa....usmart wa akili wa wale USA uliwafanya kutomdharau yule dogo na baadaye kuishia kumtesa guatanamo kupata proper lead..

Kupatikana Osama bin Laden ni mtoto mchunga kondoo? Wacheni kulisha watu matango pori kwa maslahi yenu:

IMG_20211025_101717_170.jpg

Manhunt for Osama bin Laden - Wikipedia

Ninakazia:

Pamoja na yote anaweza kulaumiwa JK pana watu wasiojulikana nyuma ya pazia. Hao ndiyo walio wachawi wetu:

Kama CCM siyo adui -- mchawi wetu ni nani?

Terms za reference ni mahsusi walipo.
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,654
2,000
Bwana "Kombora la Taifa" narudi tena kwako.

Hata kwa Mbowe, tunarudi palepale, mambo ya dola ni magumu sana na haijalishi nani yuko madarakani.... hatupaswi kushupaza shingo na kusema Mbowe sio gaidi au Mbowe gaidi.... bali tunaomtetea tupambane na data za kisheria kumtetea clearly with no doubt " wenye macho tutaona" wanaosema ni gaidi waje na clear evidence " wenye macho pia tutaona"...

Kuna wakati sisi wananchi tunakuwa mashabiki sana na kujipa pande matokeo yake shida zinaanza, tusio mashabiki wa Sabaya tulishangilia tukasema serikali imetenda haki, waliomashabiki wa Sabaya wanasema ameonewa aim kumdhalilisha chuma na kuzima legacy... Hebu tuache kuwa mashabiki tuangalie mambo kiupana na kuzipa chance pande zote then tuhukumu..
Kaka hata akina Hitler, Iddi Amin, Mobutu, Bokassa wote hao wanaweza kuja na hoja hizohizo za "tumefanya haya kwa sababu tuna ushahidi wa kiintelijensia kuwa hawa ni maadui wa Taifa". Hata hivyo hilo haliondoi unyama wao!
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
10,062
2,000
Linapokuja suala kama hili wengi hapa JF huwa hawako sympathetic na Waislamu, sijui kwa nini!

Huwezi kuona hoja za Ulinzi na usalama zikiapply kwa kesi ya Mbowe, huwa tunaconclude kuwa Mbowe kaonewa. Ila kwa Masheikh huwa tunasema serikali "inalinda" nchi dhidi ya ugaidi

nakuongezea na hii itafakari sana..

leo hii mashabiki wa Mbowe watakuja kuwatetea Masheikh ili wapate supporter dhidi ya Mbowe, ila zama zile hao hao wangekwambia serikali iko sawa waislamu magaidi hahahaha.... sorry for my reverse thinking..
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,815
2,000
Huu uzi wako unanitatiza, umekaa mkao wa segregation, na ubaguzi wa aina yoyote uwe wa rangi, dini, jinsia, kabila, itikadi za kisiasa lazima upingwe.

Kwako masheikh ni wa muhimu zaidi ya wengine wasio viongozi wa dini? wale wengine kule gerezani wasio viongozi wa dini watasemewa na nani?

Hii hoja yako imekuja vibaya, itatafsiriwa kumbe ndio maana huyu wa sasa akawaachia kwa sababu ni mwenzao halafu at the same time anawaweka ndani anaopenda yeye, huku akisema wazi wana ushahidi wa kufanya hivyo dhidi yao kwenye mahojiano yake na BBC wakati kila mmoja anajua ni kesi ya uongo.

Tuongee ukweli hapa, huwa unamtazamo wa kidini sana, ndio maana ulikuwa ukilia sana wakati ule waislamu wenzio hawapewi teuzi, lakini sasa wanapewa kwa spidi ya 5G umefunga mdomo wako kimya, watu wa aina yako wasipoangaliwa kwa makini wataleta sumu mbaya kwenye jamii yetu ambayo raia wake wote ni sawa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom