Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,497
- 51,090
Mzee Jakaya!
Shikamoo mzee, nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Naomba nikupe taarifa tu kuwa jela kuna Masheikh zaidi ya 150 , na wengi wao waliwekwa ndani kipindi cha utawala wako. Hivi mzee ulikuwa unafikiria nini kwa mambo haya?
Ninafahamu kuwa wewe personally siyo mtu mbaya, na nimekuwa nikiamini sana kuwa una utu sana ndani yako. Na kwa kweli umetenda mambo mengi mazuri sana kwa nchi yetu, ikiwemo miundo mbinu, kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi vyuo vikuu, masilahi ya watumishi, ajira na demokrasia na mambo mengi tu.
Lakini kuna jambo moja huwa linanitazi sana mzee wangu. nalo linahusu HAKI, Hivi wakati serikali yako inachukua uamuzi wa kuwaweka ndani waja hawa na watumishi wa "MUUMBA MBINGU NA NCHI" ulikuwa ukifikiria nini haswa?
Masheikh wa uamsho walikaa ndani kwa miaka zaidi ya saba, serikali yako ndiyo iliiyowaweka ndani kwa kesi ya Ugaidi, serikali yako ikashindwa kuthibitisha ugaidi wao mahakamani, na serikali zilizofuata nazo zikashindwa kuthibitisha ugaidi wao kwa muda wa miaka yote hiyo nane. Mwishowe DPP akafuta kesi bila kutoa sababu, yaani akasema hana nia ya kuendelea na kesi hiyo. Hivi Mzee wetu Jakaya, unafahamu vizuri kuhusu Mwenyezi Mungu anavyosema kwenye Qur'an juu ya watu wasiotenda haki katika ardhi?
Mheshimiwa Jakaya, Jana Sheikh Ponda amekwenda Magerezani kuonana na Masheikh wengine ambao walikamatwa mwaka 2013 wakati wewe ukiwa rais, na mpaka leo serikali haijathibitisha tuhuma zao za Ugaidi. Mzee wangu hivi kweli ulifanya fair kwa waja hawa wa Mwenyezi Mungu?.
Bila shaka umesomasoama masuala ya dini ya kiislamu, unajua vizuri kisa cha nabii Yusufu kuwekwa gerezani kwa kosa ambalo wala hakulifanya, Je umewahi kujiuliz Dhimma uliyo nayo mbele ya Mwenyezi Mungu kwa hili jambo la kuwaweka ndani Watumisha wa MWINGI WA REHMA bila haki?
Mzee naamini wewe ni mtu mwenye access na Rais Samia, nakuomba kwa heshima na taadhima tumia nafasi hii ya access uliyonayo kumuomba Rais Samia afute kesi na awaachie huru masheikh hawa watumishi wa MWINGI WA REHMA.
Mzee Jakaya, ulichowafanyia waja hawa wa Mwenyezi Mungu siyo sawa, Nakuomba ufanye jitihada zako kurekebisha hili suala!
Nikukumbushe tu, miongoni mwa hawa uliowaweka ndani katika utawala wako bila ushahidi, miongoni mwao wamo waliokupigania sana kisiasa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, wakati huo ulikuwa na hali mbaya sana mbele ya Dr Slaa , mzee kumbuka hilo!
Wako katika Ujenzi wa Taifa
Missile of the Nation!